Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 57,750
- 92,175
Kuna baadhi ya mambo mtu unayaangalia kisha unajiuliza hivi kweli sisi ni Taifa la Tanzania au la wapi na watu gani?
Yanayotokea sasa kwenye maeneno haya hapa yanadhihirisha kuwa sisi si wamoja hatuna umoja na tumejaa Unafiki, Sifa na Kiburi
Yanayotokea sasa kwenye maeneno haya hapa yanadhihirisha kuwa sisi si wamoja hatuna umoja na tumejaa Unafiki, Sifa na Kiburi
- Yanayotokea Zanzibar ni kama vile yanatokea nchi ya Jirani, Ni aibu na fedheha kubwa sana, Bara wako kimya hakuna anayethubutu kunyanyua hata mdomo, hakuna ushwari wowote ule, tuliona hata viongozi wa Dini juzi kwa umoja wao walikemea haki ile. Tuliache hilo
- Hebu tuangalie hili la kukamatana na kufungana, aliwahi kujisemea Marehemu Baba yetu Nyerere kuwa Katiba yetu iko loose sana kiasi kwa ikitokea siku tukipata Rais mwenye hila hila za chini kwa chini tutaumia, Tujiandae kuumia. Hatuwezi kuwabagua Vijana wetu as if wao si sehemu ya Taifa hili, tukawakamate na kuwafunga kisha???? Ndio wamepata kazi. Hivi kweli Rais alifanya Cost-Benefit Analysis? Utawalipa watu watakaowakamata, Utawaweka ndani (mafuta ya magari/malori ya kwasafirishia), Chakula chao wawapo gerezani, matibabu n.k. Je mzigo wote huo nani atabeba? Serikali? Hahahahaahaaaaa
- Ukanda unaoendelezwa chini kwa chini si wa kupuuzia hata kidogo, kulikua na balancing ya Appointment za Nafasi, Kinachoendelea kwa sasa ni kwamba kwa wale ambao hawakuumuunga Mkono (si conclusion) au walioonekana kuchagua chama kingine kwa wingi ndio hao wamenyimwa hata kutoa Wakuu wa Mikoa, haya ni maneno yapo na yanazungumzwa. Ni hatari kwa Taifa kuendeleza mbegu hii imeee na kustawi, ikistawi sana tutashindwa kuing'oa.
-
Mbona hujazungumzia udini ambao kila post humu jamii forum lazima ukute watu wanaongelea dini zao