Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Kuna utaratibu wa kuexport madini na tozo au kodi za serikali.

Kuna hela kibao hapo serikali itapata.
Mfumo mbovu wa kijamaa huo. Mtu kachimba madini kwa jasho lake halafu serikali inaingilia mauzo yake. Halafu hiyo serikali haina uwajibikaji wowote, imejaa wezi na mafisadi wanaofuja jasho la wananchi.
 
Ndiyo tunarudi pale pale kwamba tuna mfumo mbovu wa kijamaa. Marekani hiyo watu wa kawaida wamechimba dhahabu wameuza kiholela wakatajirika na wakajenga nchi, sisi hata ardhi haturuhusiwi kumiliki.
Marekani walikuwa hawachimbi kwenye ardhi ya serikali. Ardhi ya Marekani ilikuwa na mgogoro sana baada ya kunyang'anya kutoka kwa wahindi wekundu enzi za wild west, ambayo ndiyo enzi iliyokuwa na uchimbaji wa dhahabu sana. Siyo kweli kuwa umiliki wa ardhi marekani ni huru sana kama unavyosema, kuna sheria zake pia, na kuna kodi kubwa ya ardhi ambayo mmiliki analipa serikalini.
 
Kwani sisi hatuna migogoro ya ardhi ambayo yote inamilikiwa na serikali? Huko Marekani waliochimba kiholela hata kama siyo kwenye ardhi ya serikali, wamejenga nchi yao na kuleta maendeleo. Sisi tumeng'ang'ania mfumo wa kijamaa mbovu.
 
Una chuki na mfumo wa kijamaa lakini mfumo huo haupo Tanzania leo, ulifutika Tanzania tangu mwaka 1987 kabla mfumo wa ukomunist katika nchi za Urusi, Poland, Rumania na nyingizeo haujavunjika lakini wao leo wana amendeleo kuliko sisi. Mfumo huo huo wa serikali kumiliki raslimali za nchi kama ardhi na madini ndio unaotumika China leo lakini wao wameendelea kuliko sisi. Usilalamikie mfumo wa ujamaa kwa Tanzania kukosa maendeleo, tatizo la maendeleo ni sisi wenyewe, siyo mfumo wa Ujamaa; in fact wakati wa ujamaa tulikuwa na maendeleo kidogo kuliko leo.

Unatakiwa utambua kuwa leo sisi ni wajinga sana tunaojidharau wenyewe hata kuhisi kuwa hakuna la maana tunaloweza kufanya, tunaishia kujidharau wenyewe tu kama wewe unavyofanya sasa; sisi ni wavivu tusiojituma mpaka tusimamiwe, tusiposimamiwa basi hakuna loloite tutakalofanya zaidi ya kupiga soga tu kuongelea mpira wa jana au kikao cha harusi wakati tukiwa kazini; sisi tunapenda sana kumiliki vitu vikubwa vilivyo nje ya uwezo wetu hadi kutusabisha ama kuwa wezi au kuishi kwa kukopakopa. Tabia hizo ndiyo recipe ya hali ya maendeleo Tanzania. Ni tabia ambazo zimeenea kuanzia serikali kuu hadi maisha ya mtu mmoja mmoja.
 
Unasema ujamaa haupo wakati sura ya kwanza ya ilani ya uchaguzi ya CCM inasema nchi imejengwa kwa misingi ya ujamaa na kujitegemea na CCM itailinda na kuidumisha hiyo misingi? Mfumo mbovu wa ujamaa bado upo.

Ukisema China wameendelea kwa mfumo wa ujamaa siyo kweli, waliifungua nchi yao wakawaita wawezekaji wa nchi za kibepari ndiyo wakachomoka. Halafu unajua Wachina wangapi waliteketea enzi za Mao Zedong? Zaidi ya Wachina milioni 38 walikufa.
 
Naona kama huielewi dunia hii bali unaongea nadharia tupu ya kujitungia tu. Usidhani kama China eti ilifungua nchi yao wakawaachia wawekezaji wajifanyie wanavyotaka kama unavyodhani. Jinsi China ilivyofungua kuwaita wawekezaji ndiyo hivyo Tanzania pia tuliwata wawekezaji. Ila China ilibaki na mashirika yake ya umma umma, na mojawapo ya masharti kwa wawekeaji kuruhusiwa kufanya biashara zao ndani ya China ilikuwa ni lazima washirikiane na wawafundishe wachina. Tofauti yake Tanzania tukauza mashirika yote ya umma wala hatukuwa na mpango wa kufanya wawekezaji hao walisadie Taifa; tuliwapa tax holidays za ajabu. Baada ya miaka kama kumi tu, wachina wakaanza kuendeleza mashirika yao kwa kutumia technology waliyojifunza kutoka kwa wawekezaji na kuanza kukataa bidhaa zilizozalishwa na wawekezaji hao. Sisi baada ya muda mfupi tu mashirika yote ya umma yakafa tukawa wategemeaji zaidi wa nje, na mpaka leo tunaendelea kubembeleza wawekezaji miaka yote 35 iliyopia tunalia na ujamaa tu.

Makampuni na mashirika yote makubwa unayoyajua kutokea China ni ya serikali; mifano michache ni kama vile kampuni ya TV ya Hisense, kampuni ya kutengeza ndege ya COMAC, Benki kubwa sana inaylipia miradi mingi ya ujenzi wa majumba na miundoa mbinu ya CCB ni mali ya serikali, Kampuni ya reli ambayo ndiyo imetengeza zile high speed train ya CR ni mali ya serikali, Migodi yote ya madini China ni mali ya serikali. Makampuni yote makubwa ya kutengeza magari kama SAIC, Dongfeng, FAW, Chang'an, BAIC,GAC na mengine mengi sana ni mali ya serikali, China bado wanaendelea na ukomunist twao tu, hakuna chama cha upinzani China, bali ni chama cha kikomunist tu, kuipinga serikali au kum[pinga rais China ni kosa la jinai.Sasa sijui undhani tofauti yao na ujamaa ni ipi.

Kwa nini hutaki kukubali kuwa Tanzania hatuna kisingizio bali ni sisi wenyewe? Hata Rwanda sasa hivi wanatupita standard of living wakati walichinjana sana miaka 28 tu iliyopita. Tunataka vya ulaini mno, tukisimamiwa kufanya inavyotakiwa tunalia na udikteta, tukiachiwa tujifanyie bila kusimamiwa tunaharabu hadi kukwama na wengine kama wewe kuanza kulaumu ujamaa uliokufa miaka 38 iliyopita; solutiona yetu ya haraka huwa ni kutembeza bakuli duniani na kutafuta mikop[o. China mtu akishikwa kwa rushwa, wizi wa mali ya umma, au madawa ya kulevya anayongwa; sisi kwetu tutamchekea tu na kumwona "mtu wa misheni town."

Wachina waliokufa kipindi cha mao hawana uhisnao wowote na kuendelea kwa china au kutokuendelea kwa Tanzania.
 
Wachina huo ukomunisti wameufuata tangu 1920s kwa nini haukuleta maendeleo tangu enzi hizo? Kwa nini walichelewa na mpaka watu zaidi ya milioni 38 walikufa? Mpaka walivyokubali mabepari waje kuwekeza ndiyo maendeleo yamekuja tena yamekuja haraka sana.

Kama unafikiri udikteta na ukomunisti ni njia ya maendeleo, nchi kama Korea Kaskazini ingekuwa na maendeleo kuliko ndugu zao wa Korea Kusini. Watu ni wale wale, utamaduni ni ule ule lakini upande uliofuata huo udikteta na ukomunisti watu wanakufa njaa na upande unaoufuata ubepari na demokrasia una maendeleo.

Ujamaa tulionao ni mfumo mbovu lakini bado tunaung'ang'ania. Tunahangaika kutafuta wawekezaji lakini hatuwezi kupata wawekezaji wengi kama walioenda kuijenga China.
 
Kweli Mambo haya yanaleta sintofaham.kwa upande wangu
1653635590605.jpg
ni Bora ningeishi Kama huyu Dada hukoooo.sio poa aseee......nikiwa Sina habar na mtu
 
Mwisho wa nchi kuacha kugeuzwa shamba la bibi yako, pale miccm yote mtakapo kufa wote ila mkiwa madarakani ni ngumu Sana mzee
CCM wakifa wote si ndio nchi itakuwa imekufa?. CCM wafe wote halafu abaki nani kutawala nchi?.
P
 
Wanabodi,

Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", na Leo ni kuhusu uzalendo wa kujitolea kuisaidia serikali yako na nchi yako, pale unapoona imeshindwa na inahitaji msaada, je tutaendelea kufanywa Shamba la Bibi Hadi Lini?.

Tanzania tunaendelea kufanywa Shamba la Bibi Hadi Lini?.
Wasalaam

Paskali​

Hili ni bandiko la zamani nililouliza, Tanzania tutaendelea kufanywa ni shamba la bibi hadi lini?.
Jana ripoti ya CAG imetoka, na kuonyesha kuwa kumbe Tanzania bado imeendelea kufanywa ni shamba la Bibi!, ila zamani tulikuwa tunafanywa Shamba la bibi na wageni wanaukuja na kujivunia rasilimali zetu watakavyo, na kujiondokea zao, lakini sasa ni Watanzania wenyewe tena wenzetu kwenye mamlaka, ndio wanatupiga!. Tutaendelea kufanywa ni shamba la bibi hadi lini?
P
 
Hili ni bandiko la zamani nililoulizwa tutaendelea kufanywa ni shamba la bibi hadi lini?.
Jana ripoti ya CAG imetoka, na kuonyesha kuwa kumbe Tanzania bado imeendelea kufanywa ni shamba la Bibi!. Tutaendelea kufanywa ni shamba la bibi hadi lini?
P
Hadi tukiamua kuwatoa CCM madarakani na kubadili mfumo wa Utawala.

Kubadili Mfumo wa Utawala hadi pale tutakapoweka misingi imara ya miongozo.

Sasa ili yote yaweze kufanikiwa lazima turudi kwenye kuwatoa CCM madarakani.

Je, tupo tayari kuwatoa CCM madarakani?
 
Mpaka Ccm ipokonywe madaraka
 
Let's assume it's true CCM iondolewe madarakani, lakini hatujaiondoa CCM madarakani ni lazima tuwe na mbadala wa CCM!. Swali ni tuitoe CCM madarakani, halafu aje nani?.
P
 
Back
Top Bottom