Tanzania secures 1.8tri/- loans from China for construction Road 230 km and pipeline gas mtwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania secures 1.8tri/- loans from China for construction Road 230 km and pipeline gas mtwara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Rais Jakaya Kikwete Akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hui Liangya

  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akipeana Mkono na Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu alipomtembelea ikulu, Dar es Salaam.
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha ikulu Jijini Dar es Salaam jana Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu
  --
  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatano, Septemba 5, 2012, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hui Liangya kuhusu masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam mara tu baada ya Mheshimiwa Liangya kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu katika Tanzania kama sehemu ya ziara ya nchi za Afrika, viongozi wote wawili wameeleza kuridhishwa kwao na hali na ustawi wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Rais Kikwete ametumia nafasi ya ziara hiyo ya Mheshimiwa Liangya kuishukuru China kwa michango yake katika jitihada za maendeleo za Tanzania.


  Amesema Rais Kikwete: "Jamhuri ya Watu wa China imetusaidia mengi katika jitihada zetu za maendeleo kuanzia kwenye ujenzi wa Reli ya TAZARA, ujenzi wa Uwanja wa Taifa, ujenzi wa Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar Es Salaam, ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, na ahadi ya kusaidia kuanzisha Benki ya Kilimo Tanzania. Kwa hakika Jamhuri ya Watu wa China imetusaidia mengi na tunaishukuru sana."


  Rais Kikwete pia ameitaka China kuendelea kuisaidia Tanzania hasa katika maeneo ya jinsi ya kuongeza kasi ya uchumi. "Tunataka kwa kweli kujifunza kutoka mifano ya mafanikio ya marafiki zetu wa karibu kama China. Hivyo, bado tunaendelea kusisitiza ushirikiano wa China katika kuanzisha na kuendesha maeneo maalum ya uzalishaji –Special Economic Zones "


  Naye Mheshimiwa Liangya amemwambia Rais Kikwete kuwa China itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania ambao umekuwa unashamiri tokea ulipoanzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Tse Dung.


  Mheshimiwa Liangya amesema kuwa undani wa miradi yote ambayo China inasaidia katika Tanzania ungejadiliwa kwenye mkutano kati yake na Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika baada mchana wa jana


  Kiongozi huyo wa China pia ameisifu Serikali ya Mheshimiwa Kikwete kwa uamuzi wake wa kuanzisha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na kuongeza kuwa mpango huo umeandaliwa kwa umakini mkubwa. "Nawapongezeni kwa uamuzi wenu wa busara wa kuanzisha tena Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Ukitekelezwa vizuri unaweza kusukuma kwa kasi zaidi maendeleo ya nchi yetu."


  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.

  5 Septemba, 2012

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kila baada ya Miezi Miwili Viongozi wa Kichina Wanazuru Tanzania... HII INATISHA TAIFA LETU...
   
 3. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kuna mtu aliweka hapa uzi wa dawa za kulevya akimuhusisha mtoto wa mkuu kukamatwa huko China, hebu utafiti uanzie hapo
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Hapo mwisho kwenye statement ya kiongozi wa uchina,ni makosa ya kiuandishi ama ni kitu gani?je alimaanisha kusema maendeleo kwenye "nchi yenu"?
   
 5. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Hakupaswa kuwa mgeni wa Kikwete huyo bali mgeni wa Pinda. JK usikabe hadi penati
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Waliotoa taarifa ni ikulu, kama kawaida ni kosa la walioandaa taarifa/tamko.

  Inawezekana pia kuwa "lost in translation".
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Huo uzi sijauona,umehamishwa ama umefutwa?
   
 8. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu hata mimi nautafuta sana
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  mods ni waoga xana. cjuwi wamekula sumu gani? kuna sehem huo uzi umemwagwa kama njugu na watu wanausaula kama mitumba ya ilala-boma.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo kumbe haujafutwa?ebu nielekeze pahala ulipo mkuu.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  ngoja kukuche vzuri niombe ruksa kwa mamodz ya kuubandka kama yule jamaa aliomba ruksa ya kuweka pcha za wauwaji wa marehemu mwangosi. nikisepeshwa mnitetee.
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Hiyo habari source yake ni wapi?
   
 13. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hivi karibuni tutaanza kuwa na watunza bustani na watumishi wa ndani wachina kwa jinsi mambo yanavyoelekea halafu kibaya zaidi hatuna mikakati zaidi ya kupiga siasa wageni wanakuja kuchuma shamba la bb wanahamishia kwao,uzi wa madawa naona mods wameufuta ila too late ushasambaa kila kona sahv watu washaanza kurushiana kwenye emails zao hadi mabarabarani ushaanza kugawiwa
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,343
  Likes Received: 19,522
  Trophy Points: 280
  huyu rais hajui hata majukumu yake nina imani hana kazi za kufanya ... Huyu si angetakiwa akutane na kina bilal ama pinda sasa jk naye kujichukulia majukumu yya mwenzake ndio nini?
   
 15. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Wewe google tu utauona, siunalijua jina la huyo mtoto wa raisi ambaye ni tajiri na utajiri wake haujulikani ulikotokea
   
 16. Mtuflani

  Mtuflani JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 323
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Upo kwenye group la facebook "CHADEMA VS CCM"
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  jason bourne.!
   
 18. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umeona eenh!!

  Nami imenishitua sana. Kama mtu anaweza kuwatamkia wazi namna hii halafu bado mnaendelea kumchekea. Aibuu!!

  Ni kweli inajulikana kuwa China kama yalivyo mataifa ya Ulaya na America yapo kwa maslahi yao zaidi. Lakini anapowaambia wazi namna hii amekudharau sana wewe uliyemuhitaji.
   
 19. s

  sanjo JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Shamba la bibi. Hakuna tofauti na Mangungo vizazi vijavyo vitatulaumu sana kwa u Mangungo huu.
   
 20. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pamoja na uliyosema, kautafute ule uzi wa Ridhiwan Kikwete na kashfa ya Madawa ya Kulevya ambao nafikiri ulipewakichwa "JK auza ncha kumwokoa Ridhiwan asinyongwe"
   
Loading...