Tanzania sasa inahitaji Katiba mpya kuliko muda wowote ule!

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
839
1,000
Ukisikiliza hotuba ya JPM ya kumwapisha Mama Anna Mghwira kuwa RC wa Kilimanjaro. Hapo utagundua huyu rais anapandikikiza chuki kwa jamii na kuona kwamba huyu rais anachukulia upinzani ni uadui badala ya changamoto. Na anaikumbatia katiba ya sasa kwa ajili ya matakwa yake binafsi badala ya taifa. Kama ni kweli ni mtu anajali kwamba taifa linatakiwa lijengwe kwa misingi bora ya utawala, basi kipaumbele chake kingekuwa ni kuhakikisha katiba mpya iliyowagharimu watanzania mabilioni ya pesa inapatikana. Kama angekuwa na uchungu wa jinsi gani pesa za watanzania zitapotea hovyo katiba pia ingekuwa kipaumbele chake lakini amekana kabisa! Na sababu moja ni wazi kwa nini hataki katiba mpya ni kile alichokieleza kwenye hotuba ya kumwapisha Anna Mghwira. KWAMBA: Anataka awe na mamlaka ya kupita kiasi kwamba kusiwe na sheria ya kumbana hata kama kakosea yaani ni UDIKTETA. Katika hotuba hiyo kasema na nukuu:

''Kwa sababu huwezi kumteua mtu kumpeleka bungeni akawe anakusema halafu huna mamlaka ya kumtoa'' ''Sasa mimi nawateua hawa kwenye nafasi ambazo nina mamlaka ya kuwatoa wakati wowote''

Kauli hizi zinaonyesha jinsi gani huyu rais ana vitisho na ni mkandamizaji wa uhuru wa hoja binafsi. Yeye anataka mtu yeyote anayemteua lazima akubaliane na yeye kwa lolote lile hata kama ni baya la sivyo atamtoa madarakani. Na ndiyo maana mpaka sasa anashindwa kumteua jaji mkuu kwa kuhofia kwamba akishamteua hatoweza kumtoa yeye kijinga kijinga. Hii ni hatari kubwa kwa demokrasia na pia inawashusha ari watendaji na ni katiba mbovu inayompa madaraka hayo. Kwani mbona JK alimteua Mh. James Mbatia wa NCCR-Mageuzi kuwa mbunge? Na hakumpangia kitu cha kusema bungeni? Na Mbatia aliendelea kuishutumu serikali kwenye mambo tofauti na hasa mfumo wa elimu. Na serikali ya JK haikuona ni tatizo wala uadui.
Lakini Rais Magufuli yeye anataka asipingwe na mtu yeyote iwe wa upinzani au wa ndani ya CCM. Na toka achukue madaraka amekuwa anatoa kauli hizi mara kwa mara za vitisho na dharau. Halafu kauli zake hazina weledi na za kijichanganya, anavyodai kwamba eti watu hawamwelewi eti kauli ya kusema yeye hawachagui wapinzani aliitoa Zanzibar. Sasa Zanzibar ni ncji ingine?? Kama yeye anawateuwa anaodai 'wapinzani' kwa niaba ya watanzania kwa nini sasa asimwache pia Dr.Shein kufanya kazi na maalim Seif katika serikali moja kwa manufaa ya wazanzibari?? Huu ni unafiki wa hali ya juu. Neno 'Tanzania' haliwezi kuwepo bila kuijumuisha Zanzibar. Sababu yeye siyo rais wa Tanganyika bali rais wa jamhuri ya muungano.

Wakati sasa umefika wa watanzania kusimama kidete bila kujali itikadi ya vyama na kudai KATIBA MPYA.
 

nyikila

Member
Jan 23, 2017
22
45
heshimu mamlaka iliyopo huwezi kumsema rais hivyo kama ni ushauri peleka sehemu husika
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,506
2,000
Huyo JPM alishatamka kuwa katika kampeni zake hakuwahi kutamka kuwa atakapoingia madarakani atashughulikia Katiba mpya!

Tafsiri ya hiyo ni kuwa Katiba mpya siyo kipaumbele chake.........

Yeye anatamani Katiba hii ya sasa iendelee daima kwa kuwa imempa yeye Rais madaraka ya 'mungu/mtu'
 

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
1,684
2,000
Safi sana. I wish 1 day vijana wote tuwe na mawazo +ve kama haya. Lakikn wachumia tumbo watakuja kuimwagia mapovu thread yako na kumtetea huyo wamuaminiye.
 

idaz

JF-Expert Member
Sep 1, 2013
1,010
2,000
Vijana na watz kwa ujumla ni watu wa kipekee duniani...waoga na wanafki hakuna mfano duniani,wanaona maovu,wanalia kimya kimya.
 

Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,946
2,000
Mm ninaamini kadri siku zinavyosonga mbele watu wanazidi kuondoa uoga na ukiangalia na kufikiria sababu ya kuziba watu midomo utapata jibu yakuwa raia sio waoga tena. Mwogope mtu ambaye mdomo wake anaufungua akiwa ndani ya blangeti ndo shida zake anaziwazisha
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,383
2,000
Mie nilijua watanzania tunatakiwa kujituma na kusaidia serikali sasa kuliko wakati wowote kumbe katiba
 

kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,584
2,000
Yaani viongozi wanajiona wao ni miungu watu. Katiba ibara ya 8 inasema mamlaka ya Serikali yabatokana na wananchi. Sisi wananchi ndio tunaotaka Katiba mpya na viongozibwajue hilo na walitekeleze
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom