Tanzania: Salamu zangu kwa wakuu na watawala wa nchi wawanyanyasao wanyonge. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Salamu zangu kwa wakuu na watawala wa nchi wawanyanyasao wanyonge.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Radio Producer, Sep 3, 2012.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  1. Sauti zao wanyonge hazikusikilizwa kabisaa! Walijenga magorofa ya mabilioni ya fedha, wakala kwa starehe hawakuwakumbuka wanyonge hata kwa tone moja la maji na kipande cha mkate. Hapa napo mbingu siyo rahisi. Dini iliyosafi ni kuwaona wajane na yatima........

  2. Katika ulimwengu wa leo ni dhahiri makanisa mengi yameingiwa na mdudu mchafu. Nimeona madhehebu mengi duniani, lakini wamwabuduo Mungu aliyemkuu ni wachache mno.
  Wachungaji wengi wameyageuza makanisa kuwa hospital au clinic kila siku wakiombea wagonjwa ili wapate sadaka wajinufaishe katika maisha yao. ole wenu maana ile siku KUU i karibu nanyi aibu yenu itakuwa kubwa!

  Naona wito wangu u karibu na Mungu yu karibu kutimiza neno lake. ALL IN ONE THE NEXT GENERETAION MINISTRY FOR REAL SALVATION.

  Kanisani ni sehemu ya kujifunza neno la Mungu na miujiza ni ziada ya utimilizfu wa Mungu.

  3. Fahari ya kila mtu ni AMANI moyoni mwake. Nayo amani KUU hutoka kwake pekee aliyeumba mbingu na nchi. Asikudanganye mtu AMANI pekee inatosha maana hata neno la Mungu limesema: MTAONGOZWA KWA AMANI

  4. Katika safari za hapa duniani ziwe za maisha au safari za kutembelea zimepewa utii kwa mwanadamu. Leo ukikosea njia na kwenda kulala katika mistu minene kesho ukiamka unaruhusiwa kuitafuta njia yako ulioiacha ukaendelea na safari mpaka mwisho. Hata kama ukikosea ukafika sehemu isiyo sahihi hakuna shida yote yapo juu yako utarudi tena.

  Macho yangu yamejaa machozi, roho yangu inaniuma sana kwani nimewaona wanadamu wengi katika njia iendayo upotevuni yaaani kuzimu hawajarudi tena. USIJIDANGANYE UKIFA HUWEZI TENA KURUDI AU KUITAFUTA NJIA YAKO TENA NI HUKUMU MOJA KWA MOJA. USIUCHEZEE WAKATI HUU.

  5. Niseme nini juuya NEEMA kuu niliyopewa na Mungu? Wakuu wa nchi na watu mbalimbali wamefichwa neema hiyo KUU, na kamwe hawaoni wala kusikia. Nakuja kugundua kuwa kumbe mimi ndiye MKUU katika hao wakuu, unajua kwasababu gani?>>>>NIMEMPOKEA BWANA YESU KATIKA ROHO NA KWELI.

  6. Wote waliofanikiwa wamewahi kushindwa vibaya nakufanya makosa mengi katika safari yao ya kuelekea kwenye mafanikio. hivyo basi, usikate TAMAA kwa sababu ya kushindwa kwako jana. Inuka katika jina la Yesu ufanye tena...

  7. Hakuna aliye na dhamira na nguvu baada ya kifo. Amtesaye mwenzake kwasasa siku apotezayo uhai hutumbukia katia ulimwengu asiouzowea na nguvu zake zote hufunikwa kabisa wala asiweze kusema chochote.

  Hebu jiulize hapo ulipo, ghafla umepata shida ambayo imeondoa uhai wako, kufumba na kumbua uko ulimwengu mwingine utafanyaje?-MPOKEE BWANA YESU KATIKA ROHO NA HAKI.

  8. Usiuache mguu wako usogezwe wala uteswe, yeye alaye katika raha na zinaa zake mwenyewe hujiwekea hazina ya mavuno yake mwenyewe. Jenga hazina yako kwa wema wako mwenyewe kwani ndiyo hiyo utakayoivuna mwisho wa safari.

  9. Roho zao wanyonge waliokatizwa maisha yao na wenye nguvu na fahari zipo juu zimesubiri siku iliyo KUU ambapo haki itatoka kwake PEKEE aliyeziumba mbingu na chi. Tenda wema kwa watu wote utavuna fahari siku ya kiama.

  Nawasalimu katika Jina la Bwana Wetu Yesu Kristo.
  Kanisa la ALL in ONE wanawasalimia.
  RADIO PRODUCER
   
Loading...