Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,491
- 19,323
Wakuu heshima zenu,
Hapa JF pamekuwa mahali penye uchambuzi yakinifu wa masuala yote.
LEO naleta hoja hii wakuu:-
Tuwachambue na kuwatathmini Marais wa awamu zote nne za uongozi hapa Tanzania.
Uchambuzi na tathmini hiyo ifanywe kulingana na mtu apendavyo au aonavyo, kijumla au jambo specific ila kwa heshima na nidhamu kubwa kwa wakuu wetu.
NYERERE,
MWINYI,
MKAPA,
KIKWETE.
Hao ndio reflection ya Watanzania. Roughly 25% ya Watanzania wana tabia za Kinyerere kujiamini kuwa wana uwezo wa kila jambo na kama wakiharibu basi ni kwa sababu ya watu wengine. Robo moja ina tabia za Kimwinyi za kutaka mambo yanyooke bila wao kufanya lolote, na ile sehemu 0.25 wana tabia za Kimkapa za kutaka kila kizuri wakimiliki kwa njia yoyote hata kama itabidi waue mtu ili kukipata. Sasa waliobaki ni wabababishaji tu wakiwa na tabia za Kikikwete za kutembelea majirani wakati wanapojua kuwa huko msosi uko mezani.