Tanzania Presidents: Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete

Kwanza kabisa napenda kumpongeza Nyerere alituletea Uhuru Haikuwa kazi rahisi,aliweka miko ya uongozi,kaanzisha viwanda vingi,katoa elimu bure na afya ilikuwa bure,alipinga masharti ya IMF na Benki ya dunia

Pili: Mwinyi kafungua milango ya uchumi kwenye awamu yake ya uongozi lakini yeye kawa chanzo cha rushwa na ufisada kama huelewi zana ya ruksa na chukua chako mapema

Tatu: Mkapa - kaboresha miundo mbinu yetu,lakini na yeye alikumbatia wala rushwa

Nne:Kikwete - Tulimkubali mheshimiwa lakini maneno mengi kuliko vitendo,anachagua viongozi kwa kufuata urafiki ni hatari kwa watanzania anaowaongoza sasa tunaelewa nini kinaendelea

Mwisho Mwalimu Nyerere alituwekea misingi imara ya upendo,amani,umoja na mshikamano,
I salute you Mwalimu.

Elisante Yona
 
Nyerere: Uhuru wa kujadiliana (freedom of speech) ulikuwa mdogo, wananch walikuwa wanasikiliza one man show, aliweza kuwaunganisha watanzania kwa hofu na nguvu, vijiji vya ujamaa vilileta umaskini (sera ya wote tuwe maskini), utajiri wa halali ulionekana kama dhambi, elimu ya sekondari ilikuwa "kuchaguliwa na siyo kufaulu" ubaguzi katika nafasi mbalimbali za uongozi..dhambi hii inakula nchi mpaka leo

Mwinyi: Uhuru mpana zaidi, fursa nyingi za kusoma na kufanya biashara, wezi na watu wasiowaaminifu walishindwa kuthibitiwa, serikali ilikosa pesa, mpole kupita kiasi kushughulikia wahalifu...

Mkapa: yuko focused, aliweza kusimamia jambo lolote hata kama siyo popular, mjeuri shule nyingi zilijengwa, sekondari ilikuwa kufaulu siyo kuchaguliwa, kuabudu wazungu na kuingiza nchi kwenye mikataba mibovu

JK: msafiri, chaguo la mungu, matumaini mengi, too much expectation. ametoa freedom of speech, uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo sana, weak politician. amewashughulikia mafisadi kwasababu ya donors pressure! anaabudu wazungu

My take: Mwinyi and Mkapa were better than JKN and JK

Heshima kwako Tumain,

Nimekuelewa mkuu Tumain lakini kwenye hayo maandishi ya Blue umeharibi kabisa.Tanzania haijawahi kupata kiongozi wa hovyo kama Bwana Mkapa kabinafsisha mabenk yetu kwa wazungu kwa fedha kiduchu,kapalilia ufisadi kila mahali.EPA,Meremeta na nk ni matunda ya Bwana Mkapa muzee huyu anastahili kwenda segerea.
 
I beg to differ,
Mkapa na baraza lake la mawaziri walitaka perfomance kwenye taasisi za kibenki wakataka ushauri kutoka wataalamu WB wakamsahuri hicho alichofanya. note nimesema ana weakness ya kuabudu wazungu akaingizwa mkenge

Mkapa akipelekwa segerea tutaandamana kwasababu makosa mengine ni kibinadamu na tunastahili kwenda mbele siyo kuangalia nyuma...jamaa kwa hulka yake ni mjeuri lakini siyo sababu tosha kumpeleka huko
 
Jamani kamtizamo kangu kuhusu hawa jaaa nafikiria kwamba hata elimu ya nyota kinamba inalenga shabaha yake. Kama nililetewa wote niwape madaraja, Nyerere nampa NO 1 kama kipindi chake. Japo wakati wake tulikuwa maskini wa kitupwa potelea mbali utu ulikuwepo na uzalendo wa kuilinda heshima ya utaifa wetu kwa gharama yeyote. Mwinyi nae nampa daraja la pili kama kipindi chake. Yeye alifanikisha hata matonya kuwa na laki mfukoni japo serikalini kulipauka. Serikali sii zaidi ya watu wake na bila watu hakuna serikali. Hongera Mwinyi kwa kulitambua hilo. Mkapa yeye nampa daraja la tatu kama kipindi chake cha 3 aliimarisha uchumi wa serikali kuu kwa kuzinyanganya ngawira mwinyi alizowamwagia raia. Ila kipindi chake cha pili ktk urahisi alidokoa kutoka ktk hazina ya nchi yeye na wasaidizi wake. NO yake ya 3 kinyota inanena makuu kuliko ya mwinyi ila kaipaka matope kwa udhaifu wake mwenyewe tena mwishoni mwa kipindi. Kikwete yeye nampa daraja la nne sawa na kipindi chake. Amejaribu kuimarisha mahusiano ya watanzania na dola mfano wa jeshi la polisi kuwa karibu na watu, maofisi kujitambua kwamba huduma wanazotakiwa kutoa kwa umma sii ombi bali ni wajibu tena kwa wakati muafaka. Tatizo lililo kwa kikwete ni kwamba haya yote kayafanya kwa njia ya kujipendekeza kulikosababisha makundi yanayohasimiana milele. Pili kawa rais mwoga wa maamuzi magumu kuliko wote waliomtangulia. Na mwisho ana dalili za ku-mind hata mambo ya kitoto. KIKWETE BADO ANA MDA TOFAUTI NA WATANGULIZI WAKE JE ATAWEZA KUJIREKEBISHA??
 
Mhh,
Mambo makubwa.
 
Nyerere- Kimo cha kati, maji ya kunde,mwembamba
Mwinyi-Mfupi,mng'avu,si mwembamna sana wala si mnene
Mkapa-Mfupi, mnene,mweusi
Kikwete-Mrefu, si mwembamba wala si mnene,mweupe

wote ni ma hand some kasoro mmoja
 
And what do all these leaders have in common? They were members of CCM. Kwa hiyo kupitia wao tunaweza kuona nguvu na mapungufu ya chama tawala kwa nyakati tofauti. Sawa mtu ndiye ana shikiria uraisi lakini party politics play are big role in what the president does and can achieve.
 
nyerere- kimo cha kati, maji ya kunde,mwembamba
mwinyi-mfupi,mng'avu,si mwembamna sana wala si mnene
mkapa-mfupi, mnene,mweusi
kikwete-mrefu, si mwembamba wala si mnene,mweupe

wote ni ma hand some kasoro mmoja

lol! Good for a laugh but body build and attractiveness do not run the country. Uraisi siyo umodel au mashindano ya umiss. Kinacho takiwa ni performance, performance & performance!
 
Wa kwanza: Alitutoa matongotongo na akaweka misingi utawala bora, alikuwa mkali
kwa mambo ya kijinga kijinga, aliwatimua wote waliokuwa na akili wakati
huo ( Babu, Kambona etc) alitaka kufanya kazi na watu wenye itikadi
moja. alitaka watanzania tuendelee as a group kwamba hakuna
mabwana na watwana. Aliongoza kwa mifano na matendo,hakuiba
hata ndururu moja ya mtanganyika. Mali asili aliziacha ili kizazi kijacho kifaidi
wakati watanganyika wana upeo wa kuona mbali. Aliipenda tanzania kwa
moyo wote kuliko hata kina makongoro, Si sura tu aliyokuwa nayo nzuri
bari pia moyo wake mweupe usiyo na kinyongo kwa wale
wanaomwamini - wasiomwamini hakuwaamini pia. Alikuwa mcheshi na
alikuwa na uwezo wa KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU. Malecela na
Lowassa wanamkumbuka kwa uongozi wake uliotukuka.

Wa pili: Jamaa alipoingia tu, akafungua milango yote, serikali yake ikakosa pesa,
ikawa inakopa kwa mafisadi, kipindi hiki ndo wahindi walianza kufanya
dili chafu na serikali. alikuwa weak sana na first lady ndo alikuwa
kiongozi wa nchi - wahindi walikuwa wakienda IKULU ka vile Jamatini.
Watu walimpenda sababu aliruhusu kila kitu - Vijana wa Chuo
wakamchora kwa Punch - ila hakukasirika mzee wa watu - Hakuwa na
IQ kubwa na hakuwa na uwezo wa kuchukua MAAMUZI MAGUMU. Watu bado wanampenda sana - Huyu ni MZEE RUKSA...
Nakumbuka sentensi zake mbili
Moja: Jamaniii ngonjwaa hili mimekalia pahala pabayaaaa
Pili: Jamanii tushakuwa kichwa cha wendawazimu ........

Wa Tatu: Awamu ya kwanza aliingia kwa mbwebwe, kakusanya kodi, karudisha
hadhi ya Ikulu, imani ya wananchi wa serikali yao ikarudi, akapendwa na
watu, kajenga barabara kupitia kijana wake magufuli - Akapata Nuksi za
ajali Lukuki kama MV bukoba, ajali za mabasi Nk - Tathimini awamu ya kwanza ilikuwa
nzuri.

Awamu ya pili balaa, jamaa si akaamua kubadilika bila sababu maalum,
pamoja na jamaa zake wacha waanze kubinafsisha kila kitu, kila kona
mpaka kujipatia mali za umma - First lady naye hakuwa nyuma ya mzee kulamba alichoona kimekaa ki hasara hasara. Tathimini awamu ya Pili ya huyu bwana
hakufanya kazi ila aliamua kuuza na kugawana raslimali za watanganyika.

Namkumbuka wa sentensi mbili
Moja: Watanzania ni wavivu....
Pili: Na huo ndio UKWELIIIII

Awamu ya Nne: Hapa ndo usiseme, bwembwe kibao na Maisha bora kila mtanganyika,
maneno ya matumaini kila kona - Semina elekezi na mbwembwe
nyingi tu, miezi kadhaa Jamaa wakalamba Richard Moduli - Serikali
chali. hakuna kinachoendelea miaka mitano ndo hiyoooo - ahadi hata
15% hazijafanyikwa kazi. wengine wanahoji uthubutu wa jamaa
(guts) kutolea maamuzi mambo muhimu kuwa ni weak. Yawezekana serikali
inaongozwa na watu wengine mzee yupo tu pale Jengo Jeupeee.

Hapa bwana kila mtu kawa msemaji, kila mtu hakimu kila mtu police, kila mtu usalama
wa taifa, ngojera, mipasho, maigizo ndo hapa - mafisadi ndo wana kiburi ka nini. hali ya maisha inazidi kuwa chini bora hata wakati wa mchonga, sasa tumebaki tunatazamana tu hatuna matumaini.

Sentensi Moja: Tena kwa sauti na sura ya upole "Ndugu watanzania wenzangu......"

Nimecheka siyo kwa furaha bali kwa uchungu.
Ina maana watanzania ni wadanganyika au wajinga kiasi hiki?
Ina maana wakati wa kuchagua watanzania wanakuwa wamefunga macho na kushindwa kupata mtu wa kuwafaa?
Ina maana hawa wote hawajatufaa kwa lolote?
 
Wakuu,
Hapa naona Waridi katoa Falsafa inayotoa changamoto ya utafiti kuhusu uhusiano uliopo kati ya taaluma ya mtu na aina yake ya uongozi.

Jamani hivi raisi wa TZ anatakiwa kuwa na taaluma ya aina gani? Au kama nchi ni chombo gani kinaangalia kuwa mgombea uraisi toka chama cha mafisadi(CCM) au chama kingine chochote anastahili kuwa raisi wa nchi. sina hakika kama Twendwa au tume ya uchaguzi tu ndo inatosha kuamua hili suala?
 
....Kuhusu baba wa Taifa Nyerere mimi sijui sana, maana kipindi chake wakati anatawala mie sikuwepo. Zaidi nimesoma tu history yake ya kujitahidi kutukomboa sisi watanzania kutoka mikononi mwa wakoloni.Hivyo baba wa taifa Nyerere atakumbukwa daima katika harakati zake za kudai uhuru hadi ukapatikana.
Japo naye anamapungufu yake kama binadamu, kuna baadhi ya watu wanamlaumu eti Nyerere ndio alisababisha Taifa kuwa na umasikini hadi leo.

.......Kipindi cha Mhe; Mwinyi hapa nilikuwepo na kushuhudia utawala wake, hapa mambo yalikuwa poa, watu watu walikuwa huru kufanya kila kitu, huyu aliitwa mzee wa Ruksa. Pesa zilikuwa nje nje, ukizitafuta utapata kwa urahisi tu. Maisha yalikuwa poa tu kipindi cha mzee ruksa.watu waliruhusiwa kumiliki mali zao bila masharti magumu.
Naye kama binadamu alikuwa na mapungufu yake, eti nilisikia aliuza baadhi ya wanyama wa porini kama twiga, tembo na simba nje ya nchi.

.........Mhe:Mkapahapa ndio kila kitu kilikuwa mteremko, alijitahidi kupunguza madeni ya nchi na mengine tukapata msamaha kabisa wa kulipa. Hivyo Mkapa alijitahidi sana. Uchumi wa nchi uliongezeka, na maisha ya mtanzania hayakuwa magumu kama leo hii.
Naye kama binadamu alikuwa na mapungufu yake, eti nasikia alijihusisha ufisadi wa mradi wa makaa ya mawe huko kiwira na issue za EPA na mengineyo.

........Mhe:Kikwete watu walikuwa na matumaini na huyu rais, alishinda kwa kishindo. Nakumbuka kipindi cha uchaguzi nilikuwa bado dent, basi wanafunzi tulikuwa tunamshabikia rais kijana.
Kikwete alikuja na usemi wa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, lakini imekuwa tofauti ni BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA. Kitu cha maana alichofanya huyu president labda ni kufichua mafisadi hata hivyo hajafanikiwa bado, maana mafisadi wanajulikana lakini bado sheria haichukui mkondo wake.
Hata hivyo Kikwete ana kipindi chake kingine cha miaka 5, hivyo labda utendaji wake bado haujakamilika, hivyo tusubiri tuone.
 
Kwa jinsi nchi hii ilivyonichosha ki uongozi kwangu mimi naona kama kufuru vile kumlinganisha Nyerere na hawa jamaa waliomfuatia, na sababu ni kama ifuatavyo: Sisi kama binadamu mara nyingi tunahukumiwa kwa nia na sio kwa matokeo ya maamuzi. Kwa maelezo hayo utaona kwamba Nyerere aka mwalimu kwa kweli alikuwa na nia nzuri sana na hii nchi, hakuwahi kusema maisha bora kwa kila mtanzania na badala yake yeye alisema uhuru na kazi ! Namuepusha na hukumu ya ubinafsi kwa sababu Tanzania ya wakati ule tulivyokuwa tumelala na jinsi alivyokuwa na nguvu angeshindwa nini kuwa kama Mobutu kama angekuwa na nia mbaya na nchi hii?

Nia yake njema kwa future ya taifa hili ndio imefanya hawa wezi kukuta rasilimali na kuchanganyikiwa wakaanza kwenda ulaya kuzinadi mahotelini, we ulina wapi baba mkwe anamfuata mchumba wa binti yake kwenda kupokelea posa hotelini na ugenini? Jibu ni moja tu (uhayawani) wa baba mkwe lakini kwa suala la migodi ni wizi mtupu. Naupenda muda wangu siwezi kuwajadili hao wengine, wenzangu wameshasemea hili.

Tanzania bila viongozi wezi inawezekana.
 
lol! Good for a laugh but body build and attractiveness do not run the country. Uraisi siyo umodel au mashindano ya umiss. Kinacho takiwa ni performance, performance & performance!

Akhaa sikumaanisha kuwa sura ndiyo inaoongoza....nimechoshwa na mambo yanayoendelea tz toka uhuru nikaona bora niwachambue kwa sura na vimo ili nipunguze jazba...maaana ningewachambua kwa mambo ya performance ningeharibu siku yangu bure
 
"uongozi wangu ulkikuwa na mazuri na mabaya yake lakini kwa vile ninyi ni majitu ya ajabu na wavivu wa fikra basi mnayachukua yale mabaya na kuayaacha yale mazuri na kaitika uongozi wenu mnaongezea na maya, kwahiyo kila anayekuja anarithi bayana na kuongezea mabaya yakle ndio maana kama taifa tunarudi nyuma rasilimali zinakwisha.
"ruksahaa"
"majitu ya ajabu kabisa wavivu wa kufikiri"
awamu ya nne inatia kinyaa kabisa kwakila kitu yaani miaka mne hakuana hata moja la kujivunia ndio.

TANZANIA BILA RAISI INAWEZEKA KABISA NDIO MAANA ANAJIRUSHA TU NJE YA NCHI NA MAMBO YANAKWENDA HUKU NCHI KWAKE AKIRUDI HAPA YAANI KAJA TU KUPIGA PICHA ZA SHEREHE FLANI HUYO ANAONDOKA ZAKE MAANA BILA YEYE PICHA HAZITOKI VIZURI KWANI NYIE MNAJUA KUBATASABU?

HATA NYUMBANI INAONEKA NI MAMA NDIO ANAYEENDESHA FAMILI BABA YUKO YUKO TU KAMA ZEZETA
 
I beg to differ,
Mkapa na baraza lake la mawaziri walitaka perfomance kwenye taasisi za kibenki wakataka ushauri kutoka wataalamu WB wakamsahuri hicho alichofanya. note nimesema ana weakness ya kuabudu wazungu akaingizwa mkenge

Mkapa akipelekwa segerea tutaandamana kwasababu makosa mengine ni kibinadamu na tunastahili kwenda mbele siyo kuangalia nyuma...jamaa kwa hulka yake ni mjeuri lakini siyo sababu tosha kumpeleka huko

Watu wangepafahamu unapokaa ungeipata fresh
 
Nyerere: Uhuru wa kujadiliana (freedom of speech) ulikuwa mdogo, wananch walikuwa wanasikiliza one man show, aliweza kuwaunganisha watanzania kwa hofu na nguvu, vijiji vya ujamaa vilileta umaskini (sera ya wote tuwe maskini), utajiri wa halali ulionekana kama dhambi, elimu ya sekondari ilikuwa "kuchaguliwa na siyo kufaulu" ubaguzi katika nafasi mbalimbali za uongozi..dhambi hii inakula nchi mpaka leo

Mwinyi: Uhuru mpana zaidi, fursa nyingi za kusoma na kufanya biashara, wezi na watu wasiowaaminifu walishindwa kuthibitiwa, serikali ilikosa pesa, mpole kupita kiasi kushughulikia wahalifu...

Mkapa: yuko focused, aliweza kusimamia jambo lolote hata kama siyo popular, mjeuri shule nyingi zilijengwa, sekondari ilikuwa kufaulu siyo kuchaguliwa, kuabudu wazungu na kuingiza nchi kwenye mikataba mibovu

JK: msafiri, chaguo la mungu, matumaini mengi, too much expectation. ametoa freedom of speech, uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo sana, weak politician. amewashughulikia mafisadi kwasababu ya donors pressure! anaabudu wazungu

My take: Mwinyi and Mkapa were better than JKN and JK

I beg to differ on your take about Mwalimu. Juhudi za JKN na wapigania Uhuru wenzake walileta Uhuru wa taifa hili ka njia za amani bila kumwaga damu kwa hiyo kamwe hawezi kulinganishwa na Rais yeyote aliyekuja baada yake.

JKN alilijengea Taifa hili misingi imara na madhubuti ya Umoja, Amani na Mshikamano hadi tukaweza kutembea vifua mbele ndani ya Afrika na nchi za nje kwa ajili yake.

Kwa taarifa yako enzi za Mwalimu wananchi walikuwa wanashikiri vizuri katika kujiamulia mambo yao kuliko wakati mwingine wowote. Ndani ya mfumo wa Chama Kimoja wananchi walikuwa wamoja - kulikuwa na vikao vya wananchi tangu ngazi ya juu kitaifa hadi chini kwenye nyumba kumi-kumi kujadili mustakabali na maendeleo ya mitaa na kaya. Hata kesi ndogo ndogo ambazo leo zinapelekwa mahakamani na watu kutozwa rushwa ziliweza kumalizwa kwenye vikao vya nyumba kumi vilivyoendeshwa kwa haki na usawa chini ya Mjumbe wa Nyumba kumi na wazee wa mtaa bila rushwa wala hongo!

Kitaifa, mambo muhimu yalikuwa yakijadiliwa kwa uwazi na ukweli bila fitna majungu ama makundi. Ofukozi kiongozi bora na mahiri ni yule ambaye anaweza kujenga hoja zenye mantiki na kuzitetea zikakubalika. Uwezo huo Mwalimu alikuwa nao. Akijenga hoja, wakishakubaliana kwenye vikao ndipo huyo Nyerere aliweza kupata nguvu na kujitokeza kwa kujiamini kabisa akatamba majukwaani kuwaeleze wananchi kwa lugha nyepesi inayoeleweka juu ya yaliyoamuliwa iwe kwenye Baraza la Mawaziri ama Vikao vya juu vya Chama hususan Halmashauri Kuu na hatimaye wananchi waliridhika na kudai Nyerere ni kiboko!

Kuhusu vijiji vya ujamaa havikuongeza umaskini. On the contrary, viliwawezesha wananchi waliokuwa wakiishi mbali mbali kwa kikaya (moja pale na nyingine kulee umbali wa maili tatu hadi tano) wasogezwe na kuishi pamoja katika vijiji vikubwa ili Serikali iweze kuwafikishia kwa urahisi huduma za jamii - shule, zahanati, barabara n.k. ili kupata maendeleo ya haraka.

Sera nzuri za 'wote tuwe matajiri' zimetufikisha wapi? Matajiri wachache na maskini wengi?!!

Utajiri enzi za Mwalimu haukuwa dhambi. Dhambi ilikuwa ni namna utajiri huo ulivyopatikana. Walikuwepo watu waliokuja nchini wakiwa maskini (wajenga reli ya kati) baadaye wakawa wafanyabiashara. Baada ya muda si mrefu waliibuka kuwa matajiri wakajenga magorofa kutokana na kuwaibia wananchi kijanja katika biashara. Waliwanyonya wananchi Kitu kwa bei mara nne au hata mara kumi ya bei halali! Hao ndio matajiri aliowakataa Mwalimu - matajiri waliokuwa wakijitajirisha kwa kuwanyonya wananchi wengine bila huruma! Wengine ndio hao babu zao walikuja kufanya biashara za utumwa wakikamata na kuwapeleka ndugu zetu kuwauza ughaibuni. Utajiri uliopatikana kwa njia hizo Mwalimu aliupiga vita kali.

'Utajiri' mwingine alioukataa Mwalimu hadi ikawekwa miiko ya uongozi ndani ya Azimio la Arusha ni ule wa Wamatumbi wenzetu waliopewa dhamana ya uongozi na vyeo mbalimbali lakini wakaanza kutumia nafasi walizopewa kujitajirisha. Kwa mfano mtu anateuliwa kuwa waziri/Meneja wa Shirika n.k. akiwa hana hata kibanda kwao au mjini. Baada ya kipindi kifupi anakuwa na majumba mawili, matatu ya kupangisha magari ya bei mbaya n.k.! Mshahara wa wake unajulikana, kapata wapi fedha za kuwa na mali yote hiyo kama sio kwa kutumia madaraka aliyopewa?

Elimu: Enzi za Mwalimu nia na madhumuni ilikuwa ni kuondoa ujinga miongoni mwa wananchi wote (si wachache wenye uwezo) ili wajue kuandika, kusoma na kuhesabu. Kwa maana hiyo watoto wote waliofikia umri wa kuanza shule walitakiwa wapate fursa hiyo. Shule zilikuwa chache kwa hiyo isingeliwezekana kwa wafaulu wote kuendelea na masomo ya Sekondari. Wale waliochaguliwa na kuzidi kuonyesha uwezo wao waliweza kwenda hadi Chuo Kikuu na hata kupelekwa kusoma nje ya nchi kwa kulipiwa na Serikali bila upendeleo wowote.

Hoja kwamba Mwalimu alikuwa na ubaguzi katika nafasi za uongozi hutolewa na watu wenye chuki binafsi. Orodha ya viongozi waandamizi wote wa enzi za Mwalimu ikitolewa itadhihirisha wazi kwamba Mwalimu alikuwa anateua viongozi kwa uwezo wao kulingana na mazingira ya wakati huo na si kwa upendeleo wa aina yoyote ile.

Mkapa hakuabudu Wazungu bali alitaka afanane nao! Wizi na kuvuja kwa mitihani kutokana na uongozi mbovu wa Baraza la Mitihani vilishamiri wakati wa uongozi wa Mkapa kwa hiyo kusema kwamba wanafunzi walifaulu ni kutoa sifa hewa.
 
Back
Top Bottom