Tanzania Presidents: Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete

kwa hiyo unamaanisha makosa ya mwinyi na mkapa sio yao bali ni ya nyerere?
Kwa hiyo wizi wa mwinyi na mkapa sio wao ni wa nyerere?

Kama waliiba ni wao wenyewe lakini nina wasiwasi na huyo wa kwanza kama aliwahi kuiba nasikia huyu Mzee ni Alhaji.
 
Mwinyi alijitahidi kwa kuruhusu mitumba bongo watu wakapata nguo za kuvaa,but ndiye aliyetoa mianya mikubwa ya rushwa. Ndiye aliyeanzisha biashara ikulu ambapo mkapa naye akaiga na mengine mengi. Tusimtupia kila lawama nyerere (rip) kilakitu!!


Shukurani za Punda! hivyo alileta mitumba tu? Hata alifanya jitihadaya kuhakikisha kuwa huna utapia mlo.
 
Lakini mwinyi si ndio aliofungua dirisha ili hewa safi iingie katika chumba baada ya kuwa na joto kali kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya vijidudu kama mbu na nzi ndo wakajiingiza (rushwa) au mshasahau Tanzania ilivyokuwa (kiuchumi) kipindi cha nyerere, kwamba hata kama ulikuwa unapesa, chakula utauziwa kijamaa jamaa, eg. 2kg kwa kila mtu regardless una hela kiasi gani, nguo wote wanavaa sare, kumiliki TV ni mhujumu uchumi. Hata hivyo kama utafanya cost benefit analysis basi benefit ni kubwa zaidi kuliko maafa, hivyo ni kiongozi bora.

1979 - 1980 tz ilipigana vita na ikatumia hela nyingi
1983 kula kuna njaa kali east africa and central...
tv - haziusina na mwinyi hata kidogo bali kushuka kwa gharama ya technologia duniani, TV kubwa zinatupwa watu wanaleta africa. mimi nimekuja UK 2000 na hali ya TV naijua ilivyokuwa sasa wewe tafuta watu waliokuja ulaya 1994/95 watakuambia hali ya technologia ilikuaje ulaya

yanayotakiwa kujadiliwa ni ya mwinyi na mkapa na sio ya nyerere, nyerere kuna thread nyingi mno.
 
Sasa Mwinyi utamjadili nini zaidi ya kumuombea maaisha marefu.Labda kama kuna vijana wasiokumbuka wakati wa utawala wa Nyerere lakini sisi tulioonja joto ya jiwe ya Nyenyere we will always thank Mzee ruksa labda kwa wale wasio na haya na wenye agenda zao binafsi.Hili halihitaji dini ama kabila ni common sense tu huna haja ya Phd.watakaomlaumu mzee huyu aidha wana maradhi ya akili au wana yale maradhi yanayoitwa Nyerereism.

SAHIBA.
 
Wakuu heshima zenu,
Hapa JF pamekuwa mahali penye uchambuzi yakinifu wa masuala yote.

LEO naleta hoja hii wakuu:-

Tuwachambue na kuwatathmini Marais wa awamu zote nne za uongozi hapa Tanzania.


Uchambuzi na tathmini hiyo ifanywe kulingana na mtu apendavyo au aonavyo, kijumla au jambo specific ila kwa heshima na nidhamu kubwa kwa wakuu wetu.

NYERERE,
MWINYI,
MKAPA,
KIKWETE.
 
Nyerere alituletea baraka ya njaa, miungano isio kuwa na maana na ujamaa mwingiiiii....hicho ndio ninachokijua mimi.

Hapo rais mwema labda ni huyo Mwinyi, maana nakumbuka alipewa nchi ikiwa imekufa kabisa na akabadilisha mambo mengi kuwakwamua watanzania wenzake.

Mkapa mie nakumbuka mauji ya Pemba tuu!!!Huyu Mkapa lazima wazanzibari tumpandishe mahakamani kwa uvunjaji haki za binadaamu!!!!

JK ni ufisadi tuu na holiday zisizokwisha huko Jamaica kwenye mabembea!!!!

Tathmini safi hiyo....
 
Nyerere alituletea baraka ya njaa, miungano isio kuwa na maana na ujamaa mwingiiiii....hicho ndio ninachokijua mimi.

Hapo rais mwema labda ni huyo Mwinyi, maana nakumbuka alipewa nchi ikiwa imekufa kabisa na akabadilisha mambo mengi kuwakwamua watanzania wenzake.

Mkapa mie nakumbuka mauji ya Pemba tuu!!!Huyu Mkapa lazima wazanzibari tumpandishe mahakamani kwa uvunjaji haki za binadaamu!!!!

JK ni ufisadi tuu na holiday zisizokwisha huko Jamaica kwenye mabembea!!!!

Tathmini safi hiyo....

mhhhh,
mtazamo kweli kweli.
 
KIFIMBO alijaribu kuweka usawa kwa wananchi wake
MWINYI aligawa fedha ka muuza karanga
MKAPA aliuza nchi kwa wageni
JK hana cha kufanya anakula starehe anawaogopa "mafisadi wenye nguvu kuishinda serikali"
 
Nyerere: aliendesha nchi kama duka la kijijini(anavyo penda yeye na haambiliki)
Mwinyi: Katajirisha wadosi na 1st lady ndo alikua mtoa uamuzi wote.
Mkapa: Jambazi namba moja
Kikwete: Ni picha ya rais tu(rostam ndo rais), hakustaili kupewa urais kabisa..
 
Nyerere:hakuvumilia upinzani toka enzi,angalia history ya miaka ya 60s akina
Fundikira,Mapalala,Kasanga Tumbo,Makwaia etc.Alileta udikteta,kuabudu mtu
Mmoja.Ndio aliileta CCM ambayo tunasota nayo sasa.Kulikuwa hakuna TV,
magazeti ya serikali tu,hakuna kumkosoa,RTD ilikuwa propaganda(Ujumbe wa
Leo)
Mwinyi:Mzee Rukhsa na waarabu wake(morality illianza kushuka,mama Sitti na
Biashara zake?Lowassa mambo yake yaliianza akiwa Ardhi na Wahindi wake.
Ndio Mtikila akawa na chuki na Wahindi maana Ikulu ilikuwa kama kwao.
Credit to him alifungulia mbwa,TV,magazeti,radio etc ambazo ni basic human
right for any free society.lakini Rich wakawa Rich and poor more to poverty
Mkapa:Alijifanya mzuri kumbe ni chui.Hilo ni chaguo la Nyerere.Atakumbukwa alikalia
Corruption za hali ya juu!EPA,BOT,ANBEN,Meremeta etc.
Kama ningekutana naye ana kwa ana:nitamwuliza why you started business
wakati uko rais?registered in your premises?Kujiiuzia bei poa Kiwira,then
Kuiuzia TANESCO?mama Ana Mkapa ni corrupt First Lady ever come from
Ikulu.
Kikwete:Binafsi namuona kama Playboy tu.ameshindwa kabisa kuelewa wa TZ
wakawaida tunaonanje nchi inavyokwenda.Big fishes wanapeta tu,Lowassa,
Rostam na wahindi wake.Anasafiri kama kipanga.Oh my God



Mungu Ibariki Tanzania
 
kifimbo ni kweli alisaidiana na wenzake kuleta uhuru,tatizo ni kwamba alishindwa kutengeneza wanafunzi wa uongozi wa style yake,matokeo yake,tukampata mwinyi kibahatibahati tu.
mwinyi nae akakosa washauri wa maana kwahiyo mambo yakawa yanaenda kama hatuna katiba vile,leo huyu kaibuka na hili mara kuna cheo cha naibu waziri mkuu ambaye nusura azidi cheo cha waziri mkuu kwa ufuatiliaji wa watendaji wa serikali.
baada ya hayo wananchi wakawa na hasira na kifimbo tena akaja na product nyingine aliyodhani itafuata itikadi zake baada ya kukasirishwa na utendaji wa serikali iliyokuwa inamaliza muda wake,product hiyo ya mchonga nayo ikaja na mikakati mizuri kweli ya kuinua uchumi,mfumuko wa bei ukashuka,ukausanyaji wa mapato ukaongezeka,lakini mwishoni mwa utawala huo kila mmoja huko serikalini akawa na kamuhogo kake,ikawa kila mtu anachukua chake mapema,zikafunguliwa kampuni zenye anuani ya magogoni na ngo zilizo kwenye maofisi ya umma,ikaja kugundulika kuwa kumbe biashara nyingi zilizofanywa kipindi hicho haswa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 zilikuwa ni kwa ajili ya makundi[wenyewe wanasema hayapo kwa sasa]yaliyokuwa yanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi kushika dola,basi ikawa mwenye kisu kikali ndiye anakula nyama,
si ndio tukaipata hii awamu ya nne ya wafanyabiasiasa bwana,ile biashara waliyofanya katika kutafuta ushindi wa chama chao kumbe bwana kuna njuruku walidhulumiana,wengine waliahidiwa vyeo hawakuvipata,wengine[mf.waandishi wa habari]wakalalamika wakavipata,ule mvutano wa kuzulumiana pesa na vyeo si wakalipuana bwana,tukaaza kushuhudia ndani ya chama kimoja hiki kauli zikawa zinatolewa tofauti wenyewe wakasema ndio demokrasia hiyo wanapingana kwa hoja,lakini tumeona pia wakifunguliana na kesi za kutuzuga tujue kwamba wako serious kupiga vita rushwa na ufisadi ambao hata wao ni washiriki wakubwa tu tokea enzi wakiwa mabosi kwenye awmu zilizopita,waliaza na mkwara wa kuwakamata majambazi sugu,tulipowaona wakitabasamu wawapo mahakamani tukajua iko namna sio bure bwana,mtuhumiwa mahakamani akunje nne,na tabasamu nene kama la presidaa wetu,sasa zoezi hilo la majambazi ni kahistoria kalikopita,na hata ule usanii wa kupeleka watuhumiwa wa wizi mkubwa nao unakaribia kuwa historia,hii ndio awamu ambayo inaongoza kwa kuogopa kufanya maamuzi magumu,machungu,unajua kwa nini?ni awamu ya wapwa na maswaiba kula kuku.

alaaaaaa kumbe naota ndoto,
 
[1] J K Nyerere alijaribu kuleta usawa kwa wananchi wote ingawa alikuwa na udikteta wa kisiriri.Alitumia rasilimali za Tanzania kupigania ukombozi kusini mwa Afrika,nchi za Zambia,Msumbiji,Zimbabwe na South Africa ni mfano hai jinsi rasilimali za taifa zilivyotumika kukomboa nchi zingine.Alijenga mfumo ambao uliifanya Tanzania kusifika kimataifa wakati nyumbani wananchi walikuwa wanakosa chakula na mavazi.Wakati wa utawala wake mafisadi hawakuwa na nguvu tunayoishuhudia leo.

[2] Alhaj Ali Hassan Mwinyi alijitahidi mwanzo mwa utawala wake kusimamia vizuri mabadiliko ya uchumi.Kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele ndivyo alivyozidi kuharibu,wakati wa utawala wake serekali ilishindwa kukusanya kodi wananchi walikuwa na fedha nyingi kuliko serekali.Serekali kushindwa kukusanya kodi maana yake ni kushindwa kutoa huduma muhimu kwa wanachi wake kama huduma za afya,huduma ya maji,ulinzi na usalama nao pia ulihathirika sana.Kuna wakati nilikuwa nikikutana na wanajeshi wakiwa wamevalia sare zilizochakaa sana,viatu vilivyopasuka na hata makambi ya jeshi la polisi hali ilikuwa mbaya sana.

[3] Benjamin William Mkapa mwanzoni alianza vizuri hasa katika eneo la kukusanya kodi.serekali ya Bwana Mkapa ilikusanya kodi kweli kweli lakini matumizi ya kodi yalikuwa ya hovyo haswa.Kipindi cha pili cha utawala wake tulishuhudia aina ya ufisadi ambao ulikuwa haujawahi kutokea tangu kuzaliwa kwa taifa hili kuanza kuitwa Tanganyika na hatimae Tanzania.Sijui sheria zetu zikoje lakini Bwana Mkapa anastahili kufikishwa mahakani kujibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili.Chini ya uongozi wake taifa liliingizwa kwenye mikataba mibovu ya madini ambayo mpaka sasa taifa linapoteza mabilioni ya fedha.Ufisadi wa EPA,Meremeta,ununuzi wa ndege ya Rais na mambo mengine kibao yalifanyika kwa baraka zake.

[4] J M Kikwete ni kiongozi aliyeingia madarakani kwa kuwaamisha wananchi atafanya kile ambacho marais wengine waliomtangulia walishindwa kukifanya.Bahati mbaya wapiga kura wengi hawakujua nguvu iliyokuwa nyuma yake.J Kikwete alipokuwa waziri enzi za Mzee Mwinyi na baadae Bwana Mkapa hakuwa amefanya kazi za kumfanya awe maarufu ukimlinganisha na Bwana J Magufu au A L Mrema na wengineo lakini alipochukua form ya kugombea urais mafisadi waliokuwa nyuma yake waliwaaminisha wapiga kura kwamba J Kikwete ni jibu la matatizo [muarobaini] yote kumbe haikuwa hivyo.Rais J kikwete ni kiongozi anayefikiri urais wa JMT ni lelemama.amekuwa ni kiongozi anayependa kusafiri sana,anapenda kuzua safari za nje kwa kutumia visingizio dhaifu.Alipoingia madarakani alibuni safari za kujitambulisha,siku za karibuni za kwenda kuchekiwa ubongo na akili na pengine kubembea.Rais J Kikwete ameshindwa kutoa maamuzi magumu kwa faida ya wananchi na taifa kwa ujumla.Chini ya utawala wake amejaribu kuwatetea na kuwalinda maswahiba wake waliohusika katika kashfa ya Richmond,merereta,ununuzi wa rada na nk.
 
Wa kwanza: Alitutoa matongotongo na akaweka misingi utawala bora, alikuwa mkali
kwa mambo ya kijinga kijinga, aliwatimua wote waliokuwa na akili wakati
huo ( Babu, Kambona etc) alitaka kufanya kazi na watu wenye itikadi
moja. alitaka watanzania tuendelee as a group kwamba hakuna
mabwana na watwana. Aliongoza kwa mifano na matendo,hakuiba
hata ndururu moja ya mtanganyika. Mali asili aliziacha ili kizazi kijacho kifaidi
wakati watanganyika wana upeo wa kuona mbali. Aliipenda tanzania kwa
moyo wote kuliko hata kina makongoro, Si sura tu aliyokuwa nayo nzuri
bari pia moyo wake mweupe usiyo na kinyongo kwa wale
wanaomwamini - wasiomwamini hakuwaamini pia. Alikuwa mcheshi na
alikuwa na uwezo wa KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU. Malecela na
Lowassa wanamkumbuka kwa uongozi wake uliotukuka.




Wa pili: Jamaa alipoingia tu, akafungua milango yote, serikali yake ikakosa pesa,
ikawa inakopa kwa mafisadi, kipindi hiki ndo wahindi walianza kufanya
dili chafu na serikali. alikuwa weak sana na first lady ndo alikuwa
kiongozi wa nchi - wahindi walikuwa wakienda IKULU ka vile Jamatini.
Watu walimpenda sababu aliruhusu kila kitu - Vijana wa Chuo
wakamchora kwa Punch - ila hakukasirika mzee wa watu - Hakuwa na
IQ kubwa na hakuwa na uwezo wa kuchukua MAAMUZI MAGUMU. Watu bado wanampenda sana - Huyu ni MZEE RUKSA...
Nakumbuka sentensi zake mbili
Moja: Jamaniii ngonjwaa hili mimekalia pahala pabayaaaa
Pili: Jamanii tushakuwa kichwa cha wendawazimu ........



Wa Tatu: Awamu ya kwanza aliingia kwa mbwebwe, kakusanya kodi, karudisha
hadhi ya Ikulu, imani ya wananchi wa serikali yao ikarudi, akapendwa na
watu, kajenga barabara kupitia kijana wake magufuli - Akapata Nuksi za
ajali Lukuki kama MV bukoba, ajali za mabasi Nk - Tathimini awamu ya kwanza ilikuwa
nzuri.

Awamu ya pili balaa, jamaa si akaamua kubadilika bila sababu maalum,
pamoja na jamaa zake wacha waanze kubinafsisha kila kitu, kila kona
mpaka kujipatia mali za umma - First lady naye hakuwa nyuma ya mzee kulamba alichoona kimekaa ki hasara hasara. Tathimini awamu ya Pili ya huyu bwana
hakufanya kazi ila aliamua kuuza na kugawana raslimali za watanganyika.

Namkumbuka wa sentensi mbili
Moja: Watanzania ni wavivu....
Pili: Na huo ndio UKWELIIIII


Awamu ya Nne: Hapa ndo usiseme, bwembwe kibao na Maisha bora kila mtanganyika,
maneno ya matumaini kila kona - Semina elekezi na mbwembwe
nyingi tu, miezi kadhaa Jamaa wakalamba Richard Moduli - Serikali
chali. hakuna kinachoendelea miaka mitano ndo hiyoooo - ahadi hata
15% hazijafanyikwa kazi. wengine wanahoji uthubutu wa jamaa
(guts) kutolea maamuzi mambo muhimu kuwa ni weak. Yawezekana serikali
inaongozwa na watu wengine mzee yupo tu pale Jengo Jeupeee.

Hapa bwana kila mtu kawa msemaji, kila mtu hakimu kila mtu police, kila mtu usalama
wa taifa, ngojera, mipasho, maigizo ndo hapa - mafisadi ndo wana kiburi ka nini. hali ya maisha inazidi kuwa chini bora hata wakati wa mchonga, sasa tumebaki tunatazamana tu hatuna matumaini.

Sentensi Moja: Tena kwa sauti na sura ya upole "Ndugu watanzania wenzangu......"
 
Mwalimu Nyerere; alifundisha sana baadhi ya masomo yalieleweka mangine hayakueleweka.
Mwalimu Mwinyi; alijaribu kuliongoza darasa kufanya masahihisho katika masomo ya uchumi na siasa
Mwandishi Mkapa; alituletea habari za zama za utandawazi na ujasiriamali
Afande Kikwete.; aah, waungwana kama nchi haiko katika vita kwanini tusibembee?
Wakuu, ni kama vile kuna uhusiano kati ya taaluma ya mtu na aina yake ya uongozi.
 
Enzi za Mwalimu watoto wa maskini waliokuwa hawana mbele wala nyuma na elimu kwao ilikuwa kama ndoto waliweza kwenda shule wakasoma bure/kwa kulipiwa gharama zote na serikali tangu darasa la kwanza hadi Chuo kikuu.

Mwalimu Nyerere na viongozi wenziwe walishika sururu na majembe kuchimba barabara, kusaidiana na wananchi kujenga shule na zahanati na si kwa staili ya kutaka kupigwa picha.

Enzi za Mwalimu vilijengwa viwanda vya kila aina - vya nguo, zana za kilimo, magurudumu, vya kusindika nyama; vikaanzishwa viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya watu wasiokuwa na mtaji mkubwa n.k. n.k.

Mwalimu alianzisha Benki ya Biashara ya Wananchi NBC ambayo matawi yake yalitanda nchi nzima kwa manufaa ya wananchi wote.

Utawala wa Mwalimu lilianzishwa Jeshi la Kujenga Taifa ambalo kwalo vijana wasomi na wasiosoma sana waliweza kuishi na kufanya kazi za ujenzi wa taifa pamoja na hatimaye kujenga UMOJA wa kitaifa.

Mwalimu alileta AZIMIO LA ARUSHA lililokuwa na miiko ya uongozi ili kuwadhibiti viongozi walafi wasipate nafasi ya kujinufaisha wao binafsi na kuwasahau wananchi.......
 
Nyerere alituletea baraka ya njaa, miungano isio kuwa na maana na ujamaa mwingiiiii....hicho ndio ninachokijua mimi.

Hapo rais mwema labda ni huyo Mwinyi, maana nakumbuka alipewa nchi ikiwa imekufa kabisa na akabadilisha mambo mengi kuwakwamua watanzania wenzake.

Mkapa mie nakumbuka mauji ya Pemba tuu!!!Huyu Mkapa lazima wazanzibari tumpandishe mahakamani kwa uvunjaji haki za binadaamu!!!!

JK ni ufisadi tuu na holiday zisizokwisha huko Jamaica kwenye mabembea!!!!

Tathmini safi hiyo....

Kaka, Mwinyi aliuza nchi. Loliondo unaifahamu? Aliuza nchi kwa waarab. Watu wetu wakisogelea, wapigwa risasi na hamna kesi. Wanawinda mwanyama wetu bila restriction yoyote. Subiri miaka 10 kama tutakua na wanya tena huko Loliondo
 
Jamani hata kama kweli tunamshambulia Kikwete, hii sasa inakuwa too much.

Hivi kubembea Jamaica si alibembea siku moja tu? Sasa imekuwa ni shida sana? Labda alienda kuangalia jinsi bembea lilivyo ili na yeye ajenge Lushoto?

Si kuwa namtetea kwa yote. Ila hii ya BEMBEA naona sasa tunaanza ule wivu Mkapa alisema. Kuna mengi tu ya kumshambulia Kikwete kama unataka ila hili la BEMBEA liko low sana. Labda tukisikia kuwa kwa mwaka anaenda mara mbili, tatu nk hapo kuna kuwa na haki ya kurusha scud. Tuendelee...
 
Mwalimu Nyerere; alifundisha sana baadhi ya masomo yalieleweka mangine hayakueleweka.
Mwalimu Mwinyi; alijaribu kuliongoza darasa kufanya masahihisho katika masomo ya uchumi na siasa
Mwandishi Mkapa; alituletea habari za zama za utandawazi na ujasiriamali
Afande Kikwete.; aah, waungwana kama nchi haiko katika vita kwanini tusibembee?
Wakuu, ni kama vile kuna uhusiano kati ya taaluma ya mtu na aina yake ya uongozi.

Wakuu,
Hapa naona Waridi katoa Falsafa inayotoa changamoto ya utafiti kuhusu uhusiano uliopo kati ya taaluma ya mtu na aina yake ya uongozi.
 
Nyerere: Uhuru wa kujadiliana (freedom of speech) ulikuwa mdogo, wananch walikuwa wanasikiliza one man show, aliweza kuwaunganisha watanzania kwa hofu na nguvu, vijiji vya ujamaa vilileta umaskini (sera ya wote tuwe maskini), utajiri wa halali ulionekana kama dhambi, elimu ya sekondari ilikuwa "kuchaguliwa na siyo kufaulu" ubaguzi katika nafasi mbalimbali za uongozi..dhambi hii inakula nchi mpaka leo

Mwinyi: Uhuru mpana zaidi, fursa nyingi za kusoma na kufanya biashara, wezi na watu wasiowaaminifu walishindwa kuthibitiwa, serikali ilikosa pesa, mpole kupita kiasi kushughulikia wahalifu...

Mkapa: yuko focused, aliweza kusimamia jambo lolote hata kama siyo popular, mjeuri shule nyingi zilijengwa, sekondari ilikuwa kufaulu siyo kuchaguliwa, kuabudu wazungu na kuingiza nchi kwenye mikataba mibovu

JK: msafiri, chaguo la mungu, matumaini mengi, too much expectation. ametoa freedom of speech, uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo sana, weak politician. amewashughulikia mafisadi kwasababu ya donors pressure! anaabudu wazungu

My take: Mwinyi and Mkapa were better than JKN and JK
 
Back
Top Bottom