Tanzania president urged to quit | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania president urged to quit

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chapakazi, May 12, 2009.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Imetoka BBC

  Tanzania president urged to quit


  [​IMG]
  Shockwaves from the blasts were felt throughout the city

  A Tanzanian opposition party is calling for the resignation of the president and defence minister, over a recent deadly blast at an ammunition depot.

  The National Convention for Construction and Reform (NCCR) says the government was negligent to allow the weapons so near a residential area.
  Twenty-six people died and hundreds were injured by the blasts on the outskirts of the capital Dar es Salaam.

  The government said it cannot comment until an official inquiry is completed.

  The BBC's Vicky Ntetema in Dar es Salaam says this is the first time a political party has come out with such a direct attack on the government, nearly a fortnight since the explosions near Mbagala army base.

  Accountability
  Speaking to the BBC's Network Africa, Samuel Ruhuza, secretary general of the NCCR, said: "These missiles, they have to be kept not in Dar es Salam, because the city is expanding. Who invited them there? It was the government.

  "After his resignation [Defence Minister Hussein Mwinyi], in a really democratic government, this was supposed to be the president [Jakaya Kikwete] who would resign.

  "It would be absolutely right [if he did]. As soon as possible. They have been very late. This involves people's lives."

  Responding, the defence minister told Network Africa he could not comment until an inquiry into the explosions was concluded. The investigation was commissioned last week.

  The armoury next to the army camp, which lies 14km (nine miles) outside the city centre, contains arms used in military operations for the African Union.


  Kikwete naye afuate nyayo za Lowassa? Si ndo kuwajibika huko? Tufuate demokrasia ya nchi zilizoendelea au na sisi tuangalie mfumo wetu wenyewe?

  Nadhani kwa muundo wa katiba yetu, Rais hawezi kuwajibika kwa ishu kama hii. Maana ukumbuke kwa nchi kama Uingereza, wao hawamchagui waziri mkuu, na hivyo yeye akitoka, mwingine kupokea ni rahisi, kwetu sisi hadi uchaguzi!
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  NCCR need to come out with analytical findings before they can stand firm and say that "KMJ should go"!
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  NCCR ni wazee wa ntoke vipi, hapa wameshapata style ya kutokea. Baada ya issue hii watasubiri issue nyingine watoke nayo.

  Hauchi hauchi unakucha, kipindi cha miaka 5 kinakwisha, kampeni za uchaguzi zinaanza nao wanasimamisha mgombea wao kugombea urais.
   
  Last edited by a moderator: May 12, 2009
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ama kweli! Wenzao wanafanya kazi ya siasa wao wamejifungia vyumbani na kutoa matamko ya Kikwete ajiuzulu, yaani tutegemee kuiondoa CCM kwa kuwaomba wajiuzulu! Safari bado ndefu.
   
 5. s

  skasuku Senior Member

  #5
  May 12, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kweli upinzani (NCCR) umechoka. Sasa kama kwa ishu kama hii jamaa wanataka Rais ajiuzulu, mbona tutakua na ma-Rais wengi sana kwa kipindi kifupi.

  Hebu waje na hoja zinazoonyesha madhumuni.. sio makelele...
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  May 12, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Ruzuku si ipo? waongee, wakae kimya, mwisho wa mwezi mifuko imenona!

  ruzuku ni bomu fulani hili!
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hawa hawana ruzuku mkuu, wanalamba mkono mtupu
   
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hawa bora liende nao..
   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  NCCR wao kazi yao ni kelele, they have never accomplished anything. Rais wa nchi hawezi kuwajibika na ishu kama hii. Kwanza hata kwa mkuu wa majesh kuwajibika ni vigumu sana. Kuna watu ambao huwezi kuwaondoa hivi hivi. Labda defence minister. Lakini sina uhakika na portfolio yake inamuhusisha na nini hasa. Labda kwenye ishu ya radar!
   
 10. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hao Jamaa wa NCCR, wanatumia kifungu kipi cha katiba kumtaka Rais ajiuzulu?
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  sina uhakika, nadhani wanataka kuiga mifumo ya wengine. Ndo maana nasema kwa tanzania, hatuwezi kutumia mifumo hiyo mingine. Kila nchi ina demokrasia tofauti. Ya Uingereza na Marekani ni tofauti. Ni rahisi zaidi kwa PM wa Uingereza kuwajibika kutokana na mfumo wao.
   
 12. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri nawaelewa NCCR wanachosema. Wako sahihi kabisa kwamba raisi na waziri wake wa ulinzi waachie ngazi. Hata mkuu wa majeshi, kwani anafanya nini pale?

  Mnataka kuniambia hakuna mkubwa hata mmoja anayehusika na hii disaster? Nyie mnaiona hii ni kasheshe ndogo sana au? Watu zaidi ya 26 wamekufa na mamia majeruhi, maelfu bila makazi? Bila hata ya kufanya uchunguzi raisi anatakiwa amng'oe mzito mmoja chap chap, kisha huo uzembe utafutiwe chanzo. Vinginevyo tutaishia tu kupewa ripoti ya tume iliyojaa sisa nyiiiingi, wakati huo mambo yalishasahaulika na hakuna atayewajibishwa. Waliolala wataendelea na usingizi wao huku wakiitwa waheshimiwa na kesho tutasikia makubwa zaidi ya hilo yametokea. Kama raisi hawezi kuwawajibisha watu wake basi awajibike yeye kwisha.
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kuna kitu kinaitwa natural justice. Huwezi kumfukuza mtu kazi bila kusikia pande zote mbili. Wote watakaowajibishwa wana haki ya kujua makosa yao, wanavyo husika na pia kutoa maelezo yao. It's part of public law. Kama sivyo, watu wasingekuwa na uhakika wa ajira zao. Labda mkuu mwenye aamue kuteremka.
  Mkuu wa majeshi ni ngumu kumtuo maana hapo unadili na jeshi. Ukitoa kipenzi chao na wewe ujue utatoka. Serikali zote zinajua jinsi ya kulipooza jeshi, na sio kuwatibua. Unataka kuanza kuwawajibisha wao bila hata kuwapa maelezo. Unadhani rais ni mjinga hivyo?...hehehe...itaishiakula kwake
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Japo ni tokea la kusikitisha this does not require the resignation of the president. Do people here remember Hurricane Katrina and president Bush? If the president was to resign for ever mishap in a country then none would last over a year. Hawa NCCR mageuzi wawape pole waathirika na watoe misaada kama wengine.I didn't even know this party still exist.

  If the NCCR party was following what it was preaching then it's chairman would have resigned in 2005 after the parties poor showing in the elections.
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  NCCR hawana kosa lolote lile .kama wao ni chama cha upinzani basi dongo lolote lile linafaa kuichucha serikali na hili walilolifanya ndio pahala pake kabisa ,yaani vyovyote vile ni lazima waiweke serikali katika utendaji mbovu na unaposema Waziri hafai na waziri anaonekana kuendelea inamaana hata Raisi hafai kwa sababu ndani ya serikali yake kuna watendaji vihio.
  Hivyo katika kupopoa unaweza kugonga sehemu yeyote ile ,iwe mkuu wa majeshi,iwe waziri wa ulinzi ,iwe Raisi wote hao unaweza kuwapa mtihani ,yaani hata mkuu wa mkoa ambae nae anaingia moja kwa moja kwa maana ni lazima awe na uelewa wa mkoa wake ,wapi ni hatari na wapi ni salama kwa mwananchi sio wawavunjie majumba wale wanaojenga kwenye miporomoko au mabonde ,hata hawa wanaojenga na kuinyemelea kambi kwa kumega viwanja ,vilevile kwa waliogawa viwanja eneo hilo ,yaani NCCR wamefanya ndivyo kabisa ,ila naona udhaifu wa baadhi yetu hapa ni kama waoga na wanaogopa ,watamchafua Raisi wakati kuna watendaji chini yake ,jamani upinzani sio lelemama ni jambo ambalo linataka ujasiri wa kurusha dongo sehemu yeyote ile kwenye serikali iliyopo madarakani ,ikiondoka CCM na kukaa CUF au Chadema au chama kingine chochote haina maana kuwa upinzani ndio utakuwa umeshinda na ndio basi ,CCM imeondoka madarakani na kuanza kufurahi na kucheza mdundiko na Kanyoe ,hapana wandugu ,Chama chochote kitakachoshika madaraka basi waliobakia pamoja na wananchi huwa wanakuwa katika kambi ya upinzani ili kuwakodolea macho na kuwahoji hao walioko madarakani.

  Haina maana mimi nipo CUF au Chadema ndio chama changu kikishika madaraka ndo itakuwa zamu yangu kutesa ,upinzani unamaana kubwa sana ,na hii ni faida aliyonayo mwananchi ili aone wale walio madarakani wanawajibika kikamilifu kasoro ndogo tu itabidi ianikwe na kusemwa kuwa ni ujinga na kutokujua namna ya kuendesha nchi.

  Mimi nitajiunga na CCM siku nikisikia imepoteza madaraka na kuiandama hicho chama mbadala kwa madongo tena hizi hotuba za akina Zitto na Seifu huwa naziifazi ,siku nikisikia Vyama vyao vimeukwaa Uraisi basi nawapa siku mia za mwanzo tu. Ei ndio maana yake na haswa kama hawakuwakamata mafisadi wote kwa mpigo ,JF patakuwa hapatoshi.
   
 16. ngoshombasa

  ngoshombasa JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 431
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Bongo hii bwana, hata kama mabomu hayo yangeteketeza Dar nzima...hamna kujiuzuru mtu kwani bongo tambarare bwana. Labda mabomu hayo yangevunja vunja miguu ya kina Ridhiwani ndo labda angejiuzuru mtu.
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  wana piga mbwembwe tu ili wajulikane wapo lakini ukweli ni kwamba njaa tupu wale hata siasa siku hizi wameacha. Kilicho baki wanadandia hoja juu kwa juu kama lipumba.
   
 18. U

  Utatu JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2009
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Si kwamba NCCR hawajui waliongealo. Ni sawa kabisa, Uwajibikiaji kwa Waziri na Raisi wake kwa uzembe wa hali ya juu. Mimi binafsi siwataki.
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuwaona NCCR ni wakosa huko ni kuwa na kaugonjwa cha kuzoea kutawaliwa na kuburuzwa tu kama ng'ombe alietiwa shemere.
   
 20. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Jema ni jema hata kama limesemwa na kichaa. Mbona CCM wamepeleka vijana wao Mbagala, eti kusaidia kazi ndogo ndogo. Zipi? Kwa CCM umekuwa mtaji wa kisiasa.

  Wiki jana pale USA afisa wa jeshi kajiuzulu kwa kutozuia ndege ya Rais kuruka chini ya anga isiyoruhusiwa na kusababisha hofu (siyo kifo) kwa wanannchi, wakihofia shambulio la ndege kama lile la 9/11.

  Tunapoendelea kulea uzembe kama huu ndo maana hutuna muelekeo wowote. Lazima watu wawajibike hata kwa matamushi mabaya, inatosha kuondoka. Kuna mbunge mmoja aliwahi kusema Bungeni kwamba walipigwa risasi Pemba wakati wa machafuko, walijitakia. na wenzake wakashangilia. SAME!


  Jeshi lipo kuleta usalama kwa raia na siyo kuhatarisha usalama wao. Hapo hakika naona kuna uzembe kama siyo wa Rais, ni Waziri. Kama siyo hao wote ni Mkuu wa majeshi.

  Wale munaodhani ni ajali kama zingine, nawalaani kwamba mu-wazembe wa kutupwa.
   
Loading...