Tanzania Premier League 'TPL' Simba SC Vs Mtibwa Sugar, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
18,749
Points
2,000
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
18,749 2,000
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea leo Mei 16, 2019 kwa Bingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, Lunyasi kwa kuwakaribisha Mtibwa Sugar, WakataMiwa kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salam.

Mchezo huu wa leo miongoni mwa michezo ya ukingoni kuelekea kumalizika kwa msimu wa 2018/2019, TPL, unategemewa kuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote wa dakika tisini, hasa ukizingatia matokeo yaliyopita kutoridhisha kwa pande zote zinazokutana, ambapo Simba SC imetoka kugawana alama kwa kwenda sare ya bila kufungana na Azam FC huku Mtibwa Sugar wakiambulia kipigo cha 1-0 na Coastal Union.

Je Simba SC watarekebisha makosa na kuondoka na ushindi na kurudi kileleni ama watapokea Surprise kutoka kwa Mtibwa Sugar? tusubiri mwisho wa mchezo..! Usikose Ukaambiwa na kumbuka kabumbu hili murua litakuwa Mubashara Azam Sports 2 kuanzia saa 10: 00 jioni.
fb_img_1558001401082-jpeg.1099296
img_20190516_133632_338-jpeg.1099299


Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Uhuru.

Naaaaaaam mpira umeanza TPL

Simba SC 0-0 Mtibwa Sugar

10' Simba wanafanya shambulizi kuelekea Mtibwa, lakini Kado golikipa anaokoa.

15' Mtibwa Sugar wanajaribu kwenda mbele kutafuta bao nguvu yao ni chache mbele.

20' Simba wanakosa nafasi ya wazi kabisa kwa washambuliaji Okwi na Kagere.

25' Uwanja unachezwa upande wa Mtibwa Sugar, lakíni Simba hawajafanikiwa kupata bao..!

Hatari lango la Simba...Dickson Daudi anapiga nje na kuwa goal kick

30' Simba wanapata kona, ambayo haijaza matunda

Simba SC 0-0 Mtibwa Sugar

32' Gooooooaaaal Simba wanaandika bao kwanza kupitia kwa John Bocco baada ya kupokea krosi ya Maddie Kagere

Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar


35' Mtibwa wagong pasi ndefu ambazo zinaokolewa na walinzi wa Simba

La la la la kwa mara nyingine tena Simba wanakosa bao la wazi...kupitia kwa Kagere ilikuwa gonga safi kwa washambuliaji wa Simba

Mpambano ni wa upande mmoja hakika kutokana mpira kuchezwa Sana eneo la Mtibwa

40' Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar

Ni faulo kuelekea Simba, inapigwa na Kibaya lakini unatoka nje..! Na kuwa goal kick..!

45+3' kuelekea kuwa mapumziko TPL

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wanatoka wakiwa mbele kwa bao la kutangulia kupitia kwaJohn Bocco kunako dakika ya 32


Kipindi cha pili cha lala salama kimeanza uwanja wa Uhuru jijini Dar es, Salaam

47' Goooooooaal gooooaaal Chama anaandika la pili baada ya kuwahi mpira uliopotezwa na mabeki wa Mtibwa Sugar

Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar

50' Simba wameanza kwa mashambuliza ya nguvu sana, ambapo Mtibwa

56' Okwiiiiiiiiii gooooooooooooaal
Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la tatu.

Simba SC 3-0 Mtibwa Sugar

60' Anatoka John Bocco anaingia Mzamir Yasin upande wa Simba SC..!

Wakati huohuo Mtibwa wanamuingiza Ismail kuongeza nguvu

65' Ni piga nikupige upande wa Mtibwa Sugar ambapo Simba wapo mbele.

68' Kihimbwa anapiga shuti lakini golikipa Manula anatokea na kuruka juu na kudaka bila wasiwasi

70' Simba SC wako mbele kwa bao 3 na dhahir Mtibwa Sugar wana wakati mgumu kusawazisha

73' Adam Salamba anaingia kuchukua nafasi ya Maddie Kagere

74' Saleh anakwenda mbele na kupiga shuti ambalo halikuzaa matunda upande wa Mtibwa

80' Salamba anapiga Krosi lakini mabeki wa Mtibwa Sugar wanaokoa

83' Anatoka Niyonzima anaingia Dilunga..! Upande wa Simba na Anatoka Kihimbwa anaingia Juma Luzio kwa Mtibwa Sugar

85' Chama chamaaaa anampigia Salamba lakini Salamba anapiga shuti golikipa Kado anatokea na kudaka.

88' Simba SC 3-0 Mtibwa Sugar

Makarani anafanyiwa madhambi, ni free kick kuelekea Simba...

Dhahir kabisa hakuna mipango ya kuweza kupata bao kwa Mtibwa Sugar

90+3' kuelekea kumalizika kwa mpambano huu wa TPL

Naaaaaaaaam mpira umekwisha Uwanja wa Uhuru ambapo Simba wanaibuka na ushindi wa mabao matatu bila majibu kwa mabao ya John Bocco 32' na Chama 47' Okwi 56.

Simba SC 3 -0 Mtibwa Sugar
 
Twamo

Twamo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2017
Messages
1,144
Points
2,000
Twamo

Twamo

JF-Expert Member
Joined May 27, 2017
1,144 2,000
Kila la kheri Mtibwa! Si mnajua wenzenu Kagera vile huwafanyaga mikia!
 
B

belak

Senior Member
Joined
Jul 23, 2016
Messages
183
Points
500
B

belak

Senior Member
Joined Jul 23, 2016
183 500
Simba nawapenda ila wana kampira fulani hivi kakijingajinga sana kwenye mechi muhimu kama hii
 
Prince Kunta

Prince Kunta

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2014
Messages
13,514
Points
2,000
Prince Kunta

Prince Kunta

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2014
13,514 2,000
Come on Mtibwa sugar wenzenu Kagera sugar wameweza kwanini nyie

Mpigeni mikia goli moja tu cha mkwezi
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
18,749
Points
2,000
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
18,749 2,000
Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Uhuru

00' Naaaaaam mpira umeanza TPL

Simba SC 0-0 Mtibwa Sugar
 
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
3,364
Points
2,000
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
3,364 2,000
Tuko pamoja pnt 3 lazima
 
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Messages
12,288
Points
2,000
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2014
12,288 2,000
Simba asiposhinda hii basi tena ubingwa
 

Forum statistics

Threads 1,295,406
Members 498,303
Posts 31,210,959
Top