[Tanzania]Potential to produce 735 million barrels of oil

Fundi wacha utani Bwana. Wewe ni msomi na unajua siku zote Unapotaja Tanzania Unamaana Tanzania Bara. Kwa hiyo ndiyo maana na sisi tunashadidia Zanzibar kumaanaisha Visiwa vyetu viwili pale tunapotaka kujieleza bila ya kuwamo Bara. Fanya reference si kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( ambayo ndio Bara au Tanganyika -ukitaka) na kuna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Two entities- hakuna ya tatu hapo. Fundi -analysis isikupige chenga Ndugu yangu- tena wakati huu.

Pakacha wewe umetengenezewa kwa mnazi wa kitamli nini? naona huvujishi. Give it to.......!
 
735 million barrels ni ndogo sana kama watazalisha 500,000 barrels per day basi kazi itakuwa imekwisha kwa miezi 49. Mambo ya mafuta kwa nchi nyingi hawasemi ukweli, hata Saud Arabia hawajaweza kueleza waziwazi wana akiba gani ya mafuta ghafi ardhini.
 
735 million barrels ni ndogo sana kama watazalisha 500,000 barrels per day basi kazi itakuwa imekwisha kwa miezi 49. Mambo ya mafuta kwa nchi nyingi hawasemi ukweli, hata Saud Arabia hawajaweza kueleza waziwazi wana akiba gani ya mafuta ghafi ardhini.

Mkuu, hawasemi wazi wazi kwa vile hawajui yapo kiasi gani, kutokana na Earth complicated filtration system, mafuta yanaendelea tengenezwa kila siku huko ardhini.."GarageRules Theory 2009"
Mafuta kama maji vile hayakauki ila yanaweza pungua au yakahamisha mkondo!!!
Na mitambo hii hapa www.nation.co.ke/business/news/-/1006/525058/-/j2e0nlz/-/index.html
 
Last edited:
Inatia moyo, lakini bado ni Kiasi kidogo .... could dry up in no time.
 
Wananchi,

Tunahangaika bure. Mafuta yanaweza kuwapo Tanzania, lakini je, yatakuwa yetu? Au yetu ni ile ile 3% (nchi) na mtiaji saini mkataba (pangu pakavu)10% na na mwenye mali (mchimba mafuta) 87% ????????????
 
735 million barrels ni ndogo sana kama watazalisha 500,000 barrels per day basi kazi itakuwa imekwisha kwa miezi 49. Mambo ya mafuta kwa nchi nyingi hawasemi ukweli, hata Saud Arabia hawajaweza kueleza waziwazi wana akiba gani ya mafuta ghafi ardhini.

Mkuu usipotoshe watu, ukajikuta unamwaga wino kwa 3%. Huwezi ukawa na field ya 735ml bbl halafu ukamue 500K bbls kwa siku. It doesnt work like that. Angalia nchi yeyote yenye akiba ya billions of barrels, wanatoa kwa siku kama 1ml hadi 2ml.
Kuna makampuni mengine makubwa kwa siku wanatoa kati ya 200K hadi 700K bbls, hiyo ni katika visima vyao vyote duniani. Assuming hapo ipo hiyo 735m bbls, unahitaji investiment kwanza ya atleast a few hundred million dollars hadi around a billion, ikitegemea kuna nini hapo. Kutengeneza tu mabomba ni 3 years. Sasa mtu hawezi kuwekeza pesa nyingi hivyo halafu apotee within 5years. You can not create and kill an industry within 5 years. Not worth it!! Atakayepigwa bao hapo ni Tanzania. Pia field inavyo-operate inabidi ufuate conditions fulani fulani ili u-maximise field production yako. Makampuni yanayochimba chap chap hivyo yanakimbia sehemu za vita, and in the long run it hurts the country and the company's investment itself (so you need 15 to 20 years plan). Ndio maana makampuni yaliyo katika nchi za vita, yanacheza na pande zote mbili waprotect interest zao.

Chukua mfano kuna kampuni Uganda wanauhakika na mafuta na wana estimate 400m bbls field yao. Inabidi wasuke mabomba hadi Mombasa, cost em around $1 billion. Hizi kampuni hazina hizi pesa, inabidi wachukue kwa investors au sana sana mikopo benki. Na mwekezaji hatoi hiyo pesa mpaka awe na uhakika hayo mafuta kweli yapo (na incase ya gas, lazima soko liwepo). Ndio maana nasema hiyo press release yao iko tata, maana oil OR gas makes a difference on how you can attract investors.

Pia, sijaona sehemu yoyote wanasema Zanzibar kuna mafuta kiasi fulani na fulani. Ukijua hicho, ndio unasema ni economical au?

Saudi Arabia majority ya reserves iko mikononi mwao. Kwahiyo kuficha ukweli wana kiasi gani ni kama silaha. Ndio maana nchi zote zinazoweza kushikiria reserves zao wanashikilia na wanatingisha kiberiti ala Hugo Chavez.
 
Kwani waungwana mnaweza kunitajia nchi SSA yenye mafuta iliyosonga mbele kimaendeleo?

Ktk Development Index..Mauritius ndo wanaongoza SSA wakifuatiwa na South Afrika...Nigeria na Equatolial Guinea wanatoa mafuta mengi ila ni choka mbaya tu!

Nasema we invest massively in human resources kwanza!
 
kuna kitu lazima tuwe sensitive, haya mambo ya mikataba sio mambo ya siasa ni mambo ya kitaalamu kwanza na siasa inafata baadaye, naomba nizungumzie kama ifuatavyo
tunavyozungumzia natural resources formation yake si mara zote iko hivyohivyo kwa maana hiyo hata dhahabu iliyopo ardhini haifanani kwa jinsi ilivyoform na pia haiwezi kufanana jinsi ya kuichukua (Mining)
sasa katika mikataba lazima uwashirikishe wataalamu waangalie ile dhahabu ni ya aina gani na kuna tonnage( reserve) kiasi gani, na njia gani ya ku-mine (underground/open cast)
baada ya kupata gharama iliyopo plus gharama ya utafiti (Exploration) ndio watu wanakaa mezani na kuangalia serikali ipate ngapi kwani kwa sababu kama madini yapo Tanzania automatically serikali inakuwa na 50%, sasa hii 50% ya serikali inapungua taratibu kutokana na gharama za utafiti na uendeshaji wa mgodi, lakini pamoja na hayo yote serikali aiwezi kuwa chini ya 35%
mfano ni huu
kuna mgodi mmoja wa barrick unaitwa Tulawaka Gold mine Upo Biharamulo/Chato Disrtict, kilichotokea hapo ni kwamba kulikuwa na kampuni (MDN) inahodhi hayo maeneo lakini fungu lao lilikuwa dogo, barrick walivyokuja na kuona potential ya area wakaingia ubiya na na hao Jamaa(MDN) , MDN 30% na Barrick 70%, sasa angalia jamaa kuhodhi maeneo tu wanapata 30% na walikuwa wanalipa serikalini 2500$ kwa kuhodhi hivyo viwanja kwa mwaka,
swali inakuaje mtu aliyehodhi viwanja aweze kupata 30% na serikali mwenye maeneo hayupo kaibsa kwenye share,
mfano wa pili angalia hii kampuni ya almasi De Beers, hii kampuni ipo kusini mwa afrika, Bot,Nab,Swazi. Leth, RSA, lakini kote huko wanafanya mining na hizo nchi zote zinapata more than30% na kweli inalipwa lakini kampuni hiyohiyo hapa Tanzania hawezi kufanya kama hivyo pale Williamson Diamond, habari za pale NI WIZI MTUPU
hapa point inakuja palepale kwamba huwezi kuweka mikataba bila kuwashirikisha wataalamu
 
ibrah, tukitaka tufaid hayo mafuta kama watz tusimwamin mtu yeyote. kuanzia president mpaka mtu wa chini kabisa. huko nyuma tulishawaamin sana lakin wametufanya na wanatufanya ndivyo sivyo. wengine kwa kutojua (wanaingia mikataba kama mongungo wa msovero - chifu) au kwa tamaa zao (kwa kuchukua au kutegemea rushwa).
tusiwaamin kwa vip?
tusimwamin mtu yeyote kwa kulikabidhi suala lote kwa mtu mmoja au mamlaka moja. kwamfano tukisema rais awe ndo mwamuz wa mwisho katka suala hili, anaweza kutuuza. leo tuna kikwete ambaye tunaamin sio fisad (japo mafisad labda wanamdrive), kesho itakuwaje? tuna uhakika wa kuwa na presidaa kama yeye? vip akitokea kuwa fisad?
mambo kama haya ni ya kuyaweka katka mikono ya watu wengi. kitu kama bunge. na kila kitu kiwe waz.
kumhonga kikwete au rais si vigumu kwa multinational companies. kuhonga kundi la watu wengi ambao wanaweza kubadilishwa na wanaoongozwa na taratibu imara zilizowekwa ni vigumu

Sija kuelewa; JK si fisadi?
Rais hawezi kupewa rushwa? Mmmmm, sasa hapo kabla hata hayo mawazo yako hujamaliza kuandika ushaibiwa tayari!
 
Back
Top Bottom