Tanzania politics beyond emotions, Extraction of truth from facts

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
1575358046030.png
Binafsi naamini demokrasia ni mfumo bora ukilinganisha na mifumo mingine. Hata hivyo ukweli ni kwamba ‘Utopian democracy’ au unaweza kusema demokrasia uchwara; haiwezi kuwa na manufaa kwa Taifa lolote na tayari tuna uzoefu kutoka nchi mbalimbali duniani.Kwa hiyo unaweza usiwe uamuzi sahihi kwa mtu yoyote ku ‘take risk’ kupigania demokrasia uchara ijapokuwa hiyo haimaanishi kwamba demokrasia sio muhimu.

Demokrasia inayolenga kubadilisha vyama au watu eti ili tu sura na majina yaonekane yamebadilika hapa na pale, ndio tunayoizungumzia hapa. Demokrasia ya namna hii haijawahi kuwa na faida ya maana sana kokote duniani.

Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba kwa mfano, wanafiki wakiwa chama A wanaweza kuwa bora kuliko wanafiki wakiwa chama B? au wanaweza kuwa na faida zaidi wakiwa wana madaraka au hawana au ‘Vise versa?’?

Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba mtu ambaye hana wazo jipya akiwa nje ya madaraka anaweza kuwa na wazo jipya akiwa madarakani na likawa wazo la maana?eti tu kwa kuwa yuko madarakani!

Mtu ambaye huwa hatoi sadaka au kusaidia mtu kwenye maisha yake akidai atafanya hivyo akiwa tajiri, kwa nini tuamini kwamba kweli atafanya na hali tunajua kuwa kutoa au kutotoa ni tabia na si utajiri?

Kwa nini tudhani kwamba viongozi wa chama ‘A’ kwa mfano ambao hawajawahi kujengewa uwezo wa kufikiri katika mfumo flani ‘positive’ ;wanaweza kuwa bora kuliko wa chama ‘B’ ambao nao hawajawahi kujengewa uwezo vile vile?

Unadhani mtu ambaye ni mhuni kwa mfano, au dhulumati au mafia, akihama kutoka chama ‘A’ akaenda ‘B’, atakuwa mtu mwema sasa kwa kuwa tu kahama na ‘vice versa’?

Unadhani kama cha ‘A’ kwa mfano kina wahuni kibao, na chama ‘B’wahuni kibao, ukibadilisha vyama A kwenda B na B kwenda A, output itabadilika, na mabadiliko yatakuwa positive? na kama jibu ni ndio kwa nini?

Ukisema chama ‘A’ wana matatizo kuliko chama ‘B’ na wakati kwenye vyama vyote watu wanaingia ‘randomly’ kutokea kwenye chanzo kimoja kwa msukumo wa kusaka madaraka, na hakuna ‘intervention’ yoyote inayofanyika katika level ya vyama kuwafanya wanachama na viongozi wafikiri ‘positively’, huoni utakuwa unajidanganya na hata kama kweli kuna matatizo yanaonekana zaidi upande mmoja kuliko mwingine, huoni itakuwa ni kulingana na ‘Angle’ ambayo kila chama kipo kwa wakati husika?na kama tufe likizungushwa na wahusika wakawa kinyume chake tunategemea ‘A’ iwe ‘B’ na ‘B’ iwe A?

Wakuu, Demokrasia ni kitu kizuri na muhimu lakini demokrasia inayoweza kuwa na manufaa kwa taifa ni lazima iwe ‘Scientific’. Isiwe ya kufikiria tu kubadilisha sura za watu na vyama bali iwe ya kubadilisha na kubadilishana mawazo ‘chanya’ . Kinachotakiwa kuanza kwanza ni mawazo chanya kisha matendo katika level za chini, kisha ndio kufikiria mambo mengine. Hata hivyo mawazo hayo ni lazima yawe yanapandikizwa kwa watu bila kujali vyama vyao kwa imani kwamba watakapokuwa wengi, maana yake tayari kutakuwa kuna ‘over spread of positive input’ na hivyo ‘positive output’ pia itakuwa inatarajiwa bila kujali chama gani kiko kwenye ‘angle’ gani.

Kama kweli kuna watu wanapenda mabadiliko ya kweli, eneo la kujitoa ni kwenye kupanda mbegu. kujenga mawazo chanya kwenye kila level bila kujali mipaka ya vyama. Mbegu nyingi zikipandwa itafika wakati mavuno yatakuwa mengi kiasi kwamba haitajalisha nani kaenda kuvuna kwa niaba ya wengine kwa sababu kila mtu atanufaika.

Lakini kujitoa kupigania siasa na demokrasia za madaraka pekee ni sawa na kugombania kuvuna mazao kidogo yaliyopo huku hakuna anayepanda na kila mvunaji anataka watu wamuunge mkono akavune yeye halafu akishavuna anajifanya kwamba wale wale waliojitoa kumuunga mkono hawajui n.k

Mwisho, nidhamu kwenye mambo makubwa hutokana na nidhamu tunayojijengea kwenye mambo madogomadogo. Usitarajie kwamba mtu ana au ataweza kuwa na nidhamu kwenye mambo makubwa bila kuwa na nidhamu kwenye mambo madogo madogo kwanza.

Kwa lugha nyingine kujijengea na kujenga nidhamu na fikra positive kwanza. Vinginevyo ni sawa na kila mtu kukimbilia kuvuna bila kupanda na hiyo haitakuwa na manufaa.Nchi zote zilizofaikiwa kuwa na demokrasia ya maana na maendeleo, kwanza zilijenga jamii yenye nidhamu, hivyo kuwa na wanachama wenye nidham na kupelekea viongozi wenye nidhamu na hatimaye nchi yenye nidhamu. Sisi tuna watu na vyama visivyoamini juu ya falsafa au misingi yoyote bali mashindano ya kimadaraka na kila mmoja/kimoja kinataka kiungwe mkono kwa hilo.
 
Kwa mfano unakuta mtu hana madaraka makubwa ila hashauriki, kwa nini udhani akiwa na madaraka makubwa atashaurika?
 
Au unadhani kwa mfano kama mimi ni mtu mwenye mawazo mabaya (negative) nikiwa chama 'A' naweza kuwa mzuri na nikiwa chama 'B' nikawa mbaya au Vise versa? Kweli? sio kwamba mimi ni mimi tu na nilivyo ndivyo nilivyo?

Kwa sababu isipofika hatua tukaelewa mzizi wa tatizo hasa ni nini ni balaa tupu, na ili hilo liwezekana ni lazima tuamue kuachana emotions na kuchuja ukweli kutoka kwenye uhalisia
 
Binafsi naamini demokrasia ni mfumo bora ukilinganisha na mifumo mingine. Hata hivyo ukweli ni kwamba ‘Utopian democracy’ au unaweza kusema demokrasia uchwara; haiwezi kuwa na manufaa kwa Taifa lolote na tayari tuna uzoefu kutoka nchi mbalimbali duniani.Kwa hiyo unaweza usiwe uamuzi sahihi kwa mtu yoyote ku ‘take risk’ kupigania demokrasia uchara ijapokuwa hiyo haimaanishi kwamba demokrasia sio muhimu.

Demokrasia inayolenga kubadilisha vyama au watu eti ili tu sura na majina yaonekane yamebadilika hapa na pale, ndio tunayoizungumzia hapa. Demokrasia ya namna hii haijawahi kuwa na faida ya maana sana kokote duniani.

Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba kwa mfano, wanafiki wakiwa chama A wanaweza kuwa bora kuliko wanafiki wakiwa chama B? au wanaweza kuwa na faida zaidi wakiwa wana madaraka au hawana au ‘Vise versa?’?

Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba mtu ambaye hana wazo jipya akiwa nje ya madaraka anaweza kuwa na wazo jipya akiwa madarakani na likawa wazo la maana?eti tu kwa kuwa yuko madarakani!

Mtu ambaye huwa hatoi sadaka au kusaidia mtu kwenye maisha yake akidai atafanya hivyo akiwa tajiri, kwa nini tuamini kwamba kweli atafanya na hali tunajua kuwa kutoa au kutotoa ni tabia na si utajiri?

Kwa nini tudhani kwamba viongozi wa chama ‘A’ kwa mfano ambao hawajawahi kujengewa uwezo wa kufikiri katika mfumo flani ‘positive’ ;wanaweza kuwa bora kuliko wa chama ‘B’ ambao nao hawajawahi kujengewa uwezo vile vile?

Unadhani mtu ambaye ni mhuni kwa mfano, au dhulumati au mafia, akihama kutoka chama ‘A’ akaenda ‘B’, atakuwa mtu mwema sasa kwa kuwa tu kahama na ‘vice versa’?

Unadhani kama cha ‘A’ kwa mfano kina wahuni kibao, na chama ‘B’wahuni kibao, ukibadilisha vyama A kwenda B na B kwenda A, output itabadilika, na mabadiliko yatakuwa positive? na kama jibu ni ndio kwa nini?

Ukisema chama ‘A’ wana matatizo kuliko chama ‘B’ na wakati kwenye vyama vyote watu wanaingia ‘randomly’ kutokea kwenye chanzo kimoja kwa msukumo wa kusaka madaraka, na hakuna ‘intervention’ yoyote inayofanyika katika level ya vyama kuwafanya wanachama na viongozi wafikiri ‘positively’, huoni utakuwa unajidanganya na hata kama kweli kuna matatizo yanaonekana zaidi upande mmoja kuliko mwingine, huoni itakuwa ni kulingana na ‘Angle’ ambayo kila chama kipo kwa wakati husika?na kama tufe likizungushwa na wahusika wakawa kinyume chake tunategemea ‘A’ iwe ‘B’ na ‘B’ iwe A?

Wakuu, Demokrasia ni kitu kizuri na muhimu lakini demokrasia inayoweza kuwa na manufaa kwa taifa ni lazima iwe ‘Scientific’. Isiwe ya kufikiria tu kubadilisha sura za watu na vyama bali iwe ya kubadilisha na kubadilishana mawazo ‘chanya’ . Kinachotakiwa kuanza kwanza ni mawazo chanya kisha matendo katika level za chini, kisha ndio kufikiria mambo mengine. Hata hivyo mawazo hayo ni lazima yawe yanapandikizwa kwa watu bila kujali vyama vyao kwa imani kwamba watakapokuwa wengi, maana yake tayari kutakuwa kuna ‘over spread of positive input’ na hivyo ‘positive output’ pia itakuwa inatarajiwa bila kujali chama gani kiko kwenye ‘angle’ gani.

Kama kweli kuna watu wanapenda mabadiliko ya kweli, eneo la kujitoa ni kwenye kupanda mbegu. kujenga mawazo chanya kwenye kila level bila kujali mipaka ya vyama. Mbegu nyingi zikipandwa itafika wakati mavuno yatakuwa mengi kiasi kwamba haitajalisha nani kaenda kuvuna kwa niaba ya wengine kwa sababu kila mtu atanufaika.

Lakini kujitoa kupigania siasa na demokrasia za madaraka pekee ni sawa na kugombania kuvuna mazao kidogo yaliyopo huku hakuna anayepanda na kila mvunaji anataka watu wamuunge mkono akavune yeye halafu akishavuna anajifanya kwamba wale wale waliojitoa kumuunga mkono hawajui n.k

Mwisho, nidhamu kwenye mambo makubwa hutokana na nidhamu tunayojijengea kwenye mambo madogomadogo. Usitarajie kwamba mtu ana au ataweza kuwa na nidhamu kwenye mambo makubwa bila kuwa na nidhamu kwenye mambo madogo madogo kwanza.

Kwa lugha nyingine kujijengea na kujenga nidhamu na fikra positive kwanza. Vinginevyo ni sawa na kila mtu kukimbilia kuvuna bila kupanda na hiyo haitakuwa na manufaa.Nchi zote zilizofaikiwa kuwa na demokrasia ya maana na maendeleo, kwanza zilijenga jamii yenye nidhamu, hivyo kuwa na wanachama wenye nidham na kupelekea viongozi wenye nidhamu na hatimaye nchi yenye nidhamu. Sisi tuna watu na vyama visivyoamini juu ya falsafa au misingi yoyote bali mashindano ya kimadaraka na kila mmoja/kimoja kinataka kiungwe mkono kwa hilo.
Our society is too younger for real democracy.....kama viongozi wa kuu kama Raisi haelewi msigi ya democrasi na utawala bora unategemea raia wakawaida do wajue nakuifanya hapana....
 
Mkuu, inabidi kwanza kuelewa kipi kinaanza kabla ya kipi, viongozi ni zao la jamii na hivyo tabia ya jamii inaakisi tabia ya viongozi, au jamii ni ni zao la viongozi?

ukishaelewa hii, itakuwa ni rahisi kupata picha ya mambo mengine na mtitririko wake.
Pia kila unapoona kitu jiulize mbadala wake ni nini, na huo mbadala upo au haupo, na una uhakika na conclusion zako?
 
Hoja yako inafikirisha sana.
Nikiangalia katika bara la Afrika wakati wa vuguvugu la siasa ya Vyama vingi na demokrasia.
Waafrika wengi wakapata matumaini mapya kwa siasa wakiamini sasa wanaweza kupata maendeleo katika nchi zao. Miaka ya katikati ya Tisini vyama vingi vikongwe vilimudu kubaki madarakani, lakini mwanzoni mwa miaka ya 2000 tulishuhudia wimbi kubwa la vyama vya ukombozi vikipoteza nafasi.
Nchi za Malawi na Zambia ni mfano hai wa nchi ambazo vyama tawala vilianguka lakini wananchi wakajikuta kuwa wamechangua wanasiasa walewale lakini sasa wakiwa katika vyama tofauti.
Hakuna maendeleo ya kisiasa yaliyopatikana katika kuchagua vyama tofauti na vile vya awali kwa sababu
1. Watu wale wale waliokuwa kwenye siasa ndio wakaendelea kuwa kwenye mamlaka
2. Mawazo yaleyale ya tangu ukoloni pia yakaendelea
3. Maslahi binafsi yakawekwa mbele na viongozi kushindana kwa wingi wa mali badala ya mipango ya maendeleo.

Zambia ya Kenneth Kaunda ndio Zambia ya leo, Malawi ya Kamuzu Banda ndio Malawi ya leo. Utendaji ule ule wa kisiasa na watu walewale kimawazo na kifikra.

Huku kwetu siasa ni kazi na fursa binafsi.
 
Zambia ya Kenneth Kaunda ndio Zambia ya leo, Malawi ya Kamuzu Banda ndio Malawi ya leo. Utendaji ule ule wa kisiasa na watu walewale kimawazo na kifikra.
Angalau mkuu nimefurahi umeelewa mada. Kuna wakati huwa naandika naona watu wanasoma tu bila kuchangia, najiuliza usije ukakuta ninachoaandika nakiona tu peke yangu.

Najiuliza hivi mfano jalia CCM ikaibuka ikasema baada ya masaa 24 tutaachia madaraka chama kimojawapo mbadala kichukue (ni mfano tu tu ili kuelewa hoja), ni nini kinatarajiwa kutokea tukiweka pembeni ushabiki? kitakachotokea kitakuwa ni positive? kwa nini tufikiri hivyo? hiyo positivity kwa sasa iko wapi?

Hatupingi kwamba kusiwe na vyama vingi, kisiwe na chaguzi huru na haki, pasiwe na kubadilishana madaraka lakini hilo pekee halitoshi kama ulivyoeleza. Kubadilisha sura na majina kuna faida gani ya maana katika upana wake? ni sawa na mimi nibadilishe jina hapa JF nianze kujiita YYX, hiyo haifanyi mimi nisiwe mimi na ninavyofikiria au kuamini yakawa sivyo.
 
Mbona nyuzi zako huwa unazijaza mwenyewe?! Hawakuelewi au hueleweki?!
Naona unachangia uzi hadi unaishia hii ni jamii forums wape nafasi wanajamii.
 
Hawakuelewi au hueleweki?!
Naona unachangia uzi hadi unaishia hii ni jamii forums wape nafasi wanajamii.
Wewe umeelewa au hujaelewa?
Haya umepata nafasi mchango wako ni upi sasa? au ni nafasi gani ya ziada unataka upewe?kinachokukabili ni sehemu ya tatizo linaloelezwa kwenye uzi wa msingi.
 
Angalau mkuu nimefurahi umeelewa mada. Kuna wakati huwa naandika naona watu wanasoma tu bila kuchangia, najiuliza usije ukakuta ninachoaandika nakiona tu peke yangu.

Najiuliza hivi mfano jalia CCM ikaibuka ikasema baada ya masaa 24 tutaachia madaraka chama kimojawapo mbadala kichukue (ni mfano tu tu ili kuelewa hoja), ni nini kinatarajiwa kutokea tukiweka pembeni ushabiki? kitakachotokea kitakuwa ni positive? kwa nini tufikiri hivyo? hiyo positivity kwa sasa iko wapi?

Hatupingi kwamba kusiwe na vyama vingi, kisiwe na chaguzi huru na haki, pasiwe na kubadilishana madaraka lakini hilo pekee halitoshi kama ulivyoeleza. Kubadilisha sura na majina kuna faida gani ya maana katika upana wake? ni sawa na mimi nibadilishe jina hapa JF nianze kujiita YYX, hiyo haifanyi mimi nisiwe mimi na ninavyofikiria au kuamini yakawa sivyo.

Nimefanya Politcs Studies kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara- kuna siku nita-share hapa ''Thesis'' yangu.
Kuhusu kueleweka mkuu mada kama hizi zinahitaji mtu anayesoma na kufuatilia mambo aweze kuelewa na kuchangia. Bahati mbaya wengi wetu ni watu wa ushabiki na hatuangalii mambo kwa upana wake.
Nchi zetu zina shida moja kubwa sana, vyama vilivyoko madarakani vina itikadi na sera zisizotekelezwa na vyama vya upinzani vina lengo moja tu - kuondoa chama tawala na kushika dola.
Ukiuliza leo chama X kikishiki madaraka kitafanya nini, utakachojibiwa unaweza kustaajabu kwa maana watarudi kwenye kujenga barabara na hospitali, sasa unajiuliza hivi tukimaliza kujenga barabara na hospitali hatuhitaji tena kuwa na vyama vingi?
Nimefurahi kukutana na mada hii hapa japokuwa nimeshamaliza ''Thesis'' yangu.

Shukrani.
 
jerrytz,
Mkuu ngoja nikucheki PM, kuna kitu unaweza kunisaidia kama una utafiti rasmi kuhusu siasa za Kusini mwa janga la sahara. Shukuran sana.

By the way unayozungumza hapa ndio ukweli wenyewe lakini kwa bahati mbaya ni watu wachache sana wako tayari kuuona ukweli achiilia mbali kuukubali
 
Watanzania wengi sana wana fikra chanya, lakini hakuna room ya wapi wazifikishe na wapi wakaziwakilishe ili ziweze kusikulizwa in a formal way.. kifupi hakuna mfumo rasmi unaotambuika kisheria ambao unaweza kuwasilisha mawazo yako ili yafanyiwe kazi kitaifa... room pekee iliyopo ni kupitia chama cha siasa na mbali zaidi chama hicho ni lazima kiwe kinatawala nchi ili walau wazo lako liwe na ka uzito.

Nje ya mfumo wa siasa hakuna room inayotambulika ya kufikisha fikra zako; wenzetu wa nchi zilizostarabika kwa mfano mataifa makubwa wao wana mifumo pekee ya kupokea mawazo mbadala ambayo baadaye hutambulika kisheria kama dira ya taifa husika.
Sasa hata hawa wanasiasa wakipata political positions kama Urais ama uwaziri nk hawawezi kubadilli mambo watakavyo, nina maana kuna mambo ambayo wana siasa hanana uwezo wa kuyagusa watakavyo.

Kwa mfano miaka michache tuliteketeza mabillioni ili kutengeneza katiba - je ipo wapi? leo tunajenga reli ya kisasa je tukipata Rais mwingine akasema hataki kuendelea na mradi huo tutafanyaje? leo tunahamia Dodoma je hilo ni hitaji la kitaifa na la muhimu kwa sasa? nk

Kwa hiyo ndugu zangu mzizi wa haya mambo unaanzia kwenye katiba ambayo ni kama ya kifalme; mtawala anapewa mamlalka yote na milki zote za nchi, nyie wengine mnasubiri leo atasema nini ili mfuate.
 
Binafsi naamini demokrasia ni mfumo bora ukilinganisha na mifumo mingine. Hata hivyo ukweli ni kwamba ‘Utopian democracy’ au unaweza kusema demokrasia uchwara; haiwezi kuwa na manufaa kwa Taifa lolote na tayari tuna uzoefu kutoka nchi mbalimbali duniani.Kwa hiyo unaweza usiwe uamuzi sahihi kwa mtu yoyote ku ‘take risk’ kupigania demokrasia uchara ijapokuwa hiyo haimaanishi kwamba demokrasia sio muhimu.

Demokrasia inayolenga kubadilisha vyama au watu eti ili tu sura na majina yaonekane yamebadilika hapa na pale, ndio tunayoizungumzia hapa. Demokrasia ya namna hii haijawahi kuwa na faida ya maana sana kokote duniani.

Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba kwa mfano, wanafiki wakiwa chama A wanaweza kuwa bora kuliko wanafiki wakiwa chama B? au wanaweza kuwa na faida zaidi wakiwa wana madaraka au hawana au ‘Vise versa?’?

Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba mtu ambaye hana wazo jipya akiwa nje ya madaraka anaweza kuwa na wazo jipya akiwa madarakani na likawa wazo la maana?eti tu kwa kuwa yuko madarakani!

Mtu ambaye huwa hatoi sadaka au kusaidia mtu kwenye maisha yake akidai atafanya hivyo akiwa tajiri, kwa nini tuamini kwamba kweli atafanya na hali tunajua kuwa kutoa au kutotoa ni tabia na si utajiri?

Kwa nini tudhani kwamba viongozi wa chama ‘A’ kwa mfano ambao hawajawahi kujengewa uwezo wa kufikiri katika mfumo flani ‘positive’ ;wanaweza kuwa bora kuliko wa chama ‘B’ ambao nao hawajawahi kujengewa uwezo vile vile?

Unadhani mtu ambaye ni mhuni kwa mfano, au dhulumati au mafia, akihama kutoka chama ‘A’ akaenda ‘B’, atakuwa mtu mwema sasa kwa kuwa tu kahama na ‘vice versa’?

Unadhani kama cha ‘A’ kwa mfano kina wahuni kibao, na chama ‘B’wahuni kibao, ukibadilisha vyama A kwenda B na B kwenda A, output itabadilika, na mabadiliko yatakuwa positive? na kama jibu ni ndio kwa nini?

Ukisema chama ‘A’ wana matatizo kuliko chama ‘B’ na wakati kwenye vyama vyote watu wanaingia ‘randomly’ kutokea kwenye chanzo kimoja kwa msukumo wa kusaka madaraka, na hakuna ‘intervention’ yoyote inayofanyika katika level ya vyama kuwafanya wanachama na viongozi wafikiri ‘positively’, huoni utakuwa unajidanganya na hata kama kweli kuna matatizo yanaonekana zaidi upande mmoja kuliko mwingine, huoni itakuwa ni kulingana na ‘Angle’ ambayo kila chama kipo kwa wakati husika?na kama tufe likizungushwa na wahusika wakawa kinyume chake tunategemea ‘A’ iwe ‘B’ na ‘B’ iwe A?

Wakuu, Demokrasia ni kitu kizuri na muhimu lakini demokrasia inayoweza kuwa na manufaa kwa taifa ni lazima iwe ‘Scientific’. Isiwe ya kufikiria tu kubadilisha sura za watu na vyama bali iwe ya kubadilisha na kubadilishana mawazo ‘chanya’ . Kinachotakiwa kuanza kwanza ni mawazo chanya kisha matendo katika level za chini, kisha ndio kufikiria mambo mengine. Hata hivyo mawazo hayo ni lazima yawe yanapandikizwa kwa watu bila kujali vyama vyao kwa imani kwamba watakapokuwa wengi, maana yake tayari kutakuwa kuna ‘over spread of positive input’ na hivyo ‘positive output’ pia itakuwa inatarajiwa bila kujali chama gani kiko kwenye ‘angle’ gani.

Kama kweli kuna watu wanapenda mabadiliko ya kweli, eneo la kujitoa ni kwenye kupanda mbegu. kujenga mawazo chanya kwenye kila level bila kujali mipaka ya vyama. Mbegu nyingi zikipandwa itafika wakati mavuno yatakuwa mengi kiasi kwamba haitajalisha nani kaenda kuvuna kwa niaba ya wengine kwa sababu kila mtu atanufaika.

Lakini kujitoa kupigania siasa na demokrasia za madaraka pekee ni sawa na kugombania kuvuna mazao kidogo yaliyopo huku hakuna anayepanda na kila mvunaji anataka watu wamuunge mkono akavune yeye halafu akishavuna anajifanya kwamba wale wale waliojitoa kumuunga mkono hawajui n.k

Mwisho, nidhamu kwenye mambo makubwa hutokana na nidhamu tunayojijengea kwenye mambo madogomadogo. Usitarajie kwamba mtu ana au ataweza kuwa na nidhamu kwenye mambo makubwa bila kuwa na nidhamu kwenye mambo madogo madogo kwanza.

Kwa lugha nyingine kujijengea na kujenga nidhamu na fikra positive kwanza. Vinginevyo ni sawa na kila mtu kukimbilia kuvuna bila kupanda na hiyo haitakuwa na manufaa.Nchi zote zilizofaikiwa kuwa na demokrasia ya maana na maendeleo, kwanza zilijenga jamii yenye nidhamu, hivyo kuwa na wanachama wenye nidham na kupelekea viongozi wenye nidhamu na hatimaye nchi yenye nidhamu. Sisi tuna watu na vyama visivyoamini juu ya falsafa au misingi yoyote bali mashindano ya kimadaraka na kila mmoja/kimoja kinataka kiungwe mkono kwa hilo.
Another great piece of work from Azizi Mussa ! Just genius! Nakubaliana na wewe mia kwa mia.
 
Thread kama hizi zimepotea miaka mingi hapa JF. Ni vizuri kuona zinaanza kurudi na pia kupata wachangiaji wenye weledi
Pamoja mkuu, tuendelee kushirikiana kufanya kila tunaloweza kuhakikisha kuwa Tanzania ya kesho inakuwa bora kuliko ya leo.
 
hata magonjwa ya kuambukiza inashauriwa kuangalia Zaidi namna ya kuzuia yasitokee ikiwemo kutumia chanjo kuliko kuacha yatokee halafu yakishatokea unajadili yanavyotokea na kushughulika na wagonjwa waliopo halafu pia hufikiri namna ya kutoa chanjo sasa ili wangonjwa waliopo wakishapita wasitokee wagonjwa wapya, hapo vipi? huoni unaweza ukawa unajadili wa gojwa wa leo (halafu pengine tiba huna) halafu kesho maambukizi mapya mara2, kesho kutwa x3, baadae mara 100...…..

Hatuoni ni busara zaidi kuzalisha chanjo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom