Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Demokrasia inayolenga kubadilisha vyama au watu eti ili tu sura na majina yaonekane yamebadilika hapa na pale, ndio tunayoizungumzia hapa. Demokrasia ya namna hii haijawahi kuwa na faida ya maana sana kokote duniani.
Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba kwa mfano, wanafiki wakiwa chama A wanaweza kuwa bora kuliko wanafiki wakiwa chama B? au wanaweza kuwa na faida zaidi wakiwa wana madaraka au hawana au ‘Vise versa?’?
Hivi ni kwa nini tufikiri kwamba mtu ambaye hana wazo jipya akiwa nje ya madaraka anaweza kuwa na wazo jipya akiwa madarakani na likawa wazo la maana?eti tu kwa kuwa yuko madarakani!
Mtu ambaye huwa hatoi sadaka au kusaidia mtu kwenye maisha yake akidai atafanya hivyo akiwa tajiri, kwa nini tuamini kwamba kweli atafanya na hali tunajua kuwa kutoa au kutotoa ni tabia na si utajiri?
Kwa nini tudhani kwamba viongozi wa chama ‘A’ kwa mfano ambao hawajawahi kujengewa uwezo wa kufikiri katika mfumo flani ‘positive’ ;wanaweza kuwa bora kuliko wa chama ‘B’ ambao nao hawajawahi kujengewa uwezo vile vile?
Unadhani mtu ambaye ni mhuni kwa mfano, au dhulumati au mafia, akihama kutoka chama ‘A’ akaenda ‘B’, atakuwa mtu mwema sasa kwa kuwa tu kahama na ‘vice versa’?
Unadhani kama cha ‘A’ kwa mfano kina wahuni kibao, na chama ‘B’wahuni kibao, ukibadilisha vyama A kwenda B na B kwenda A, output itabadilika, na mabadiliko yatakuwa positive? na kama jibu ni ndio kwa nini?
Ukisema chama ‘A’ wana matatizo kuliko chama ‘B’ na wakati kwenye vyama vyote watu wanaingia ‘randomly’ kutokea kwenye chanzo kimoja kwa msukumo wa kusaka madaraka, na hakuna ‘intervention’ yoyote inayofanyika katika level ya vyama kuwafanya wanachama na viongozi wafikiri ‘positively’, huoni utakuwa unajidanganya na hata kama kweli kuna matatizo yanaonekana zaidi upande mmoja kuliko mwingine, huoni itakuwa ni kulingana na ‘Angle’ ambayo kila chama kipo kwa wakati husika?na kama tufe likizungushwa na wahusika wakawa kinyume chake tunategemea ‘A’ iwe ‘B’ na ‘B’ iwe A?
Wakuu, Demokrasia ni kitu kizuri na muhimu lakini demokrasia inayoweza kuwa na manufaa kwa taifa ni lazima iwe ‘Scientific’. Isiwe ya kufikiria tu kubadilisha sura za watu na vyama bali iwe ya kubadilisha na kubadilishana mawazo ‘chanya’ . Kinachotakiwa kuanza kwanza ni mawazo chanya kisha matendo katika level za chini, kisha ndio kufikiria mambo mengine. Hata hivyo mawazo hayo ni lazima yawe yanapandikizwa kwa watu bila kujali vyama vyao kwa imani kwamba watakapokuwa wengi, maana yake tayari kutakuwa kuna ‘over spread of positive input’ na hivyo ‘positive output’ pia itakuwa inatarajiwa bila kujali chama gani kiko kwenye ‘angle’ gani.
Kama kweli kuna watu wanapenda mabadiliko ya kweli, eneo la kujitoa ni kwenye kupanda mbegu. kujenga mawazo chanya kwenye kila level bila kujali mipaka ya vyama. Mbegu nyingi zikipandwa itafika wakati mavuno yatakuwa mengi kiasi kwamba haitajalisha nani kaenda kuvuna kwa niaba ya wengine kwa sababu kila mtu atanufaika.
Lakini kujitoa kupigania siasa na demokrasia za madaraka pekee ni sawa na kugombania kuvuna mazao kidogo yaliyopo huku hakuna anayepanda na kila mvunaji anataka watu wamuunge mkono akavune yeye halafu akishavuna anajifanya kwamba wale wale waliojitoa kumuunga mkono hawajui n.k
Mwisho, nidhamu kwenye mambo makubwa hutokana na nidhamu tunayojijengea kwenye mambo madogomadogo. Usitarajie kwamba mtu ana au ataweza kuwa na nidhamu kwenye mambo makubwa bila kuwa na nidhamu kwenye mambo madogo madogo kwanza.
Kwa lugha nyingine kujijengea na kujenga nidhamu na fikra positive kwanza. Vinginevyo ni sawa na kila mtu kukimbilia kuvuna bila kupanda na hiyo haitakuwa na manufaa.Nchi zote zilizofaikiwa kuwa na demokrasia ya maana na maendeleo, kwanza zilijenga jamii yenye nidhamu, hivyo kuwa na wanachama wenye nidham na kupelekea viongozi wenye nidhamu na hatimaye nchi yenye nidhamu. Sisi tuna watu na vyama visivyoamini juu ya falsafa au misingi yoyote bali mashindano ya kimadaraka na kila mmoja/kimoja kinataka kiungwe mkono kwa hilo.