Tanzania Pekupeku na 'kichwa cha mwendawazimu': ni laana au ujinga wetu!!??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Pekupeku na 'kichwa cha mwendawazimu': ni laana au ujinga wetu!!???

Discussion in 'Sports' started by omujubi, Sep 10, 2012.

 1. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wasalaamu wanajamvi,

  Nimefuatilia mashindano ya riadha yaliyoisha mwishoni mwa juma Uwanja wa Taifa hapo Dar es Salaam, japo sikuweza kwenda lakini kupitia vyombo vya habari niliweza kujua kilichokuwa kikiendelea.

  Moja ya vilivyonivutia ilikuwa ni Waziri wa Michezo kushindwa kufungua mashindano hayo huku akiwa ametaarifiwa.
  Nikiwa nimedhani kuwa hiyo ilikuwa uzembe, nilishtushwa zaidi na picha za wanariadha wakikimbia pekupeku. Na hata wale waliohojiwa kila mmoja alikuwa na story yake, kwa mfano washiriki wa Tabora walisema wanadaiwa pesa za mkopo wa nauli na kampuni ya mabasi ya NBS, wa Kigoma anasema alisikia kwa 'washikaji' juu ya mashindano hayo na alivyokwenda kwenye mamlaka husika wakamwambia kama anaweza aende!, mwingine alikuwa nashangaa kuwa "Tanzania ina wadhamini wa 'kanga party' lakini riadha wanakimbia peku", nilimuona Suleimani Nyambui pia kama kawaidia analalamika na kutia huruma, nk, nk, nk

  Lakini hoja yangu kubwa ni matokeo ya mashindano!!!
  Mshindi aliyepata dhahabu Mita 100 kutoka Tabora, Tumaini Elisha alitumia muda wa Sekunde 13.42
  Mshindi wa dunia anayeshikilia rekodi Usain Bolt (Rekodi ya dunia) amekimbia kwa Sekunde 9.63

  Tofauti ya hizi ni kama sekunde 4 hivi ambayo ni karibia nusu ya muda wa rekodi ya dunia.
  Sasa kama mshindi wa dhahabu kutoka Tanzania yuko nyuma ya viwango kwa nusu ya muda wa dunia, si ndio maajabu mengine haya!? ...japo wote ni 'gold medal holders'!!!?

  My take:
  Matumaini yangu yalikuwa ni kuwa tungeliweza kufanya mazoezi na kupata wawakilishi huko Rio de Jeneiro 2016 pamoja na kupunguza tofauti ya sekunde nne lakini kama kweli mashindano ya taifa yanafanyika huku washiriki wakiwa pekupeku, wanaume wamevaa suruali badala ya trucksuits na hata wadada wengine wamevaa magauni badala ya nguo maalumu za michezo, unaweza kusema nini zaidi ya "TUSAHAU"????

  Je, ni kweli kuwa haya yanatokea sababu ya umasikini wetu , laana au ni ujinga tu wa kutokujua ni nini tufanye na hiki 'kidogo' tulichonacho ili kituletee mafanikio!?

  Nawasilisha

  Pekupeku.jpg Pekupeku2.jpg
   
 2. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
 3. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  hii ndo tz bwana.....bado tunasonga na tuna jiandaa na olympic ijayo!!!
   
 4. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  maana binafsi nashindwa kuamini kama ofisi ya michezo/utamaduni ya wilaya/mkoa kushindwa hata kujiondolea aibu ya wanamkoa wake kukimbia pekupeku. Dunia haiwezi kutuelewa na tunazidi kujishushia hadhi mbele ya binadamu wenzetu
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hawakimbii pekupeku kwa kushindwa kununuwa viatu vya kukimbilia. Fungukeni. Hao ukiwapa viatu hawawezi kukimbia, wameshazowea kukimbia pekupeku.
   
 6. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hili ni wazo jipya na la msingi mkuu ...je, inaruhusiwa Olympic au mashindano ya kimataifa kukimbia pekupeku!?
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Inaruhusiwa na wengi tu wameshafanya hivyo, alikuwepo Zola Budd maarufu san Afrika Kusini na medali kisha chukuwa akiwa peku, wala si ajabu:

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
Loading...