Tanzania: Pato la Taifa lakua kwa asilimia 6.9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Pato la Taifa lakua kwa asilimia 6.9

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Informer, Oct 4, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  Pato la Taifa kwa robo mwaka ya pili ya mwaka huu limekua kwa kwa asilimia 6.9, ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka jana, ambapo thamani halisi ya pato hilo ni Sh. 4,730709, ikilinganishwa na Sh. 4,426,905 mwaka jana.

  Ripoti hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Maurice Oyuke, jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwezi Aprili na Juni, 2012.

  Oyuke alisema kuwa pato katika kilimo limekua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.9 kwa robo pili ya mwaka jana na kwamba ongezeko hilo limetokana na mvua za kutosha pia na juhudi za serikali katika uboreshaji wa masuala ya kilimo.

  Aliongeza shughuli za madini limekua kwa asilimia 1.0 ikilinganishwa kwa asilimia 5.6 mwaka jana kutokana na kupungua kwa kasi ya ukuaji baada ya ikufungwa kwa muda mgodi wa dhahabu wa Geita ili kupisha ukarabati wa mitambo.

  Kwa upande wa uvuvi, alisema pato limekua kwa asilimia 4.0 kutoka asilimia 0.3 ya mwaka jana kutokana na ongezeko la uvunmaji wa samaki kwa ajili ya soko la ndani na nje.

  Kwa upande wa viwanda, alisema pato limekua kwa asilimia 8.2 ikilindanishwa kwa asilimia 8.5 mwaka jana. Alisema kiwango hicho kimefikiwa kutokana na upatikanaji wa umeme.

  Kuhusu umeme, gesi na maji, Oyuke alisema pato limekua kwa asilimia 5.6 ikilinganishwa kwa asilimia 10.3 ya mwaka jana kutokana na kupungua uzalishaji wa umeme katika kipindi hicho.

  Katika sekta za chukuzi na mawasiliano, alisema patolimekua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 16.6 mwaka jana na kwamba hali hiyo imetokana na matumizi ya simu, usafilishaji wa abaria na mazigo. Pato la huduma ya fedha limekua kwa asilimia 14.1 ikilinganishwa kwa asilimia 10.0 mwaka jana kutokana na kuongezeka kwa amana na mikopo.

  CHANZO: NIPASHE | Oktoba 04, 2012
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii ni taarifa njema kwa MAFISADI na siyo sisi walala hoi. Kwamba bado watakuwa na mahala pa kulikamua Taifa na Maziwa yakapatikana.
   
 3. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Inflation 18%, income growth 6.7%, Kwani nani ni kichaa kuamini kwamba pato la taifa limekua. Hebu convert hizo sh kwenye pound. Uongo mtupu.
   
 4. r

  robbins emmy Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakadanganye wapumbav sie cku hiz ni wasomi,waerevu na waelewa sn!
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hizo shillingi zilikuwa pounds bado Pato litakuwa limeongezeka hapa kipimo ni mwaka jana na mwaka huu. Unless uniambie kwamba thamani ya Pounds imeongezeka sana kipindi cha mwaka mmoja.
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hizo namba huwa zina misslead sana zinaposomwa mbele yetu sisi wananchi.

  Kukuwa kwa pato la taifa haimaanishi kama sisi mmoja mmoja tunanufaika.

  Pengine kiasi kikubwa income za kina Bakhresa ndio zimeongezeka halafu sisi tutashangilia.
   
 7. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hizi ni takwimu za kisiasa kiasi cha kutotuelekeza kwenye uhalisia wa maisha. Hivi ni taarifa nzuri kwa wenye meno wanaokula kwa niaba yetu wanyonge, hizi ni takwim mfu. Its not alwalys easy , beacause povelty is preveiling in TZ and people don't their fate as today is worse than yesterday.
   
 8. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  LIAR !!!

  Kuna difference gani kati ya 6.9% na 7.0%. Masaibu yote haya ya uchumi pato lisishuke? Don't anybody believe this liar!

   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Faida kwa mabeberu wa Nchi yetu!


  Mwisho wao waja hakika!
   
 10. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Hizo ndizo takwimu za mchumi wetu Maurice Oyuke.

  1. Kwenye kilimo, hajasema ni mazao gani yameuzwa kwa wingi na ni zao lipi linatuletea fedha nyingi za kigeni.

  2. Kwenye shughuli za madini, hajasema ni kiasi gani cha madini kimechimbwa kimeuzwa kwa muda huo aliotoa.

  3. Kwenye eneo la uvuvi hajasema ni kiasi gani cha samaki wamevunwa yaani tani ngapi, na wale wanaosafirishwa nje kama malighafi ni kiasi gani walipatikana. meli za uvuvi za nje zinailipa Tanzania kiasi gani kwa kuvuna samaki katika eneo letu kwenye bahari ya Hindi. Kwa ujuma ni pesa kiasi gani ukilinganisha na mwaka jana.

  4. Kwenye eneo la viwanda ni bidhaa za aina gani zinazalishwa nchini mwetu na kutupatia fedha nje ya nchi au kuongeza pato la ndani. Maana mpaka sasa hata kiwanda cha Mtibwa Sugar kinazalisha tani chache za sukari.

  5. Kwenye umeme ni kiasi cha megawati ngapi zinazalishwa kwa sasa na kama kuna migao inafuata baabda ya hii ya sasa, Gesi pia ni kiasi gani inazalishwa na maji je vyanzo vyote vya maji vina ujazo unaotosheleza mahitaji?. Je takwimu za eneo hili zinatayarishwaje na ni vigezo vipi vinatumika?

  6. Uchukuzi na mawasiliano je ni abiria wangapi wanatumia usafiri wa garimoshi, ndege na (ukiondoa daladala) na huduma hizi zinaiingizia serikali fedha kiasi gani kwa mwaka? Halikadhalika ni wateja kiasi gani sasa wanatumia simu za mikononi kwa na kuna ongezeko la wateja wangapi tokea mwaka jana.

  7. Huduma ya fedha je ni kiasi gani Tanzania inapata kwa mwaka kutokana na huduma ya fedha za kigeni na je watalii wametuingizia kiasi gani tokea mwaka jana.

  Sasa yote haya yanahitaji uangalifu katika ukusanyaji taarifa na kama kuna viunganisho kati ya idara ya takwimu na sekta husika.

  Tumechoka kulishwa taarifa zilizojaa neno pato limekua, pato limekua....pato, pato bila vigezo vinavyoeleweka, hii mpaka lini?
   
 11. u

  umulitho JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 18, 2012
  Messages: 419
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Kwa kweli mie nashindwa kuelewa mchumi anapo sema pato la Taifa limekuwa na wakati huo mfumuko wa bei unapanda kwa kasi kama graph ya maisha ya wadudu wa malaria katika mwili wa mwanadamu!!!!.Mie ninafikri wale wafanya biashara wakubwa na mabeberu ndiyo mambo yao yamekuw na sio mtu wa kawaida mnyonge wa kijijini.Here the National statistics shows the Gross Domestic Product t0 increase by 6.9% while inflation is 18%?This describe the so called "Economy without Development".Tafadhalini nyinyi mnaojiita wachumi mwache unafiki na mtoe takwimu za uhakika kwani nyinyi ndio adui wa maendeleo namba moja kwa kufanya watu wabweteke na takwimu za uongo.
   
 12. u

  umulitho JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 18, 2012
  Messages: 419
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Wachumi tufanyeni kazi kama wanajeshi kwani Wanajeshi wao wana kanuni iayosema kuwa"usiamini yeyote na tegemea chochote kutokea" na siyo kufanya kazi kwa msemo:Bussiness as usual
   
Loading...