Tanzania overtaking Kenya to become the leading economy in the region

erfan

Member
Nov 20, 2011
70
17
Kenya's economy will grow at a slower pace in the next two years than that of most of her East African neighbours, the World Bank has forecasted.

This vindicates research results released by Standard Chartered bank in November last year that indicated a possibility of Tanzania overtaking Kenya to become the leading economy in the region by the year 2030 if the country maintained consistency in the current growth rate.


Source: http://www.nation.co.ke/business/ne...+years+/-/1006/1312766/-/k9jff1z/-/index.html
 
As long as tutaendelea kuwa wanunuzi na hatuna cha kuuza nje Kenya watakuwa hatua moja mbele yetu daima. Wenzetu wana viwanda, tayari wako kwa wingi katika soko jipya la South Sudan. Sisi ni kutembeza bakuli tu na kufikiria kuwa wawekezaji watatukwamua.
 
This is a joke!!! Isiwe kuwa tunaletewa habari tunazotaka kuzisikia!!!
 
95% ya uchumi umeshikwa na wageni. Uchumi Unakuwa ndiyo, lakini mgeni amepewa ruhusa kuhamisha faida yote huko anakojua yeye, kwa mtindo huu tutabaki kuwa wachuuzi 'petty traders' for a long time.
 
Sio kweli, kama kenya wamenunua package ya kurusha afcon euro 150000 nyinyi mshindwa. Uchumi ovyooooooo. Poor marketing in tanzania do a research guy. Tusikurupuke< ichukue pesa ya kenya compare na yetu then useme
 
kumbe bado unawategemea IMF and WB kukupa forecast za nchi yako!
Watakwambia uchumi unakua kwa sababu TZ inaongoza kwa uzalishaji dhahabu duniani!
 
given massive resources we are having, we were suppose to be Africa largest economies
 
WB wakuletee habari unayotaka wewe kusikia ili iweje.
Watanzania mnaendekeza siasa na kutokupenda nchi yenu.
OTIS

Mkuu ni kweli aanyosema Nyunyu hata post namba 10 ya Lukindo vigezo vya uchumi kukua havi-reflect maisha ya Mtanzania wa chini!
 
95% ya uchumi umeshikwa na wageni. Uchumi Unakuwa ndiyo, lakini mgeni amepewa ruhusa kuhamisha faida yote huko anakojua yeye, kwa mtindo huu tutabaki kuwa wachuuzi 'petty traders' for a long time.


Mkuu mimi sio mbishi lakini hapo kwa 95% naomba kubisha. Samahani. Ukiangalia mchango wa kisekta kwenye uchumi, kilimo, ambacho kinategemewa na zaidi ya asilimia 80 ya watanzania kinachangia takriban asilimia 25 ya pato la taifa( uchumi). Kumbuka pia shughuli za serikali ( public adimin) nazo zina mchango wake katika uchumi. Kwa talkwimu za mwaka 2010 shughuli za serikali zilichanigia takriban 20% ya pato la taifa. Kwa kuangalia hizi sekta mbili sioini jinsi ya kusema kwamba asimia 95 ya uchumi wa TZ uko mikononi mwa wageni. Ni kweli zipo sekta amabazo zinamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wageni, lakini mchango wa sekta hizo kwenye uchumi ni mdogo. Mfano sekta ya madini pamoja na kukua kwa kasi sana inachangia asilimia 2.5 tu ya pato la taifa( 2010). Hoteli na migawa inachangia asilimia 2 tu ya pato lataifa. Mawasiliano( akina voda, airtel tigo, zantel n.k) yanachangia 3% ya pato la taifa, kwa mujibu wa takwimu za 2010. Yote katika yote, nafikiri si sahihi kusema kwamba 95% ya uchumi wa Tanzania uko mikononi mwa wageni.
 
Hii wala haihitaji utafiti. Kwa resources tulizo nazo; madini ya kila aina hadi uranium, vivutio kibao vya utalii, billions of metric tons of natural gas, maziwa na bahari, geographical location, ardhi nzuri kwa kilimo, hali ya hewa nzuri, mifugo, watu wakarimu, nk. Tanzania (or Tanganyika if you like) ina uwezo sio wa kuipita tu Kenya bali kuwa the leading economy in Africa.

Tunachohitaji, ni viongozi wenye vision na sera bora na sahihi za kiuchumi. Wenye nidhamu na uwezo mzuri wa kusimamia sera na sheria za nchi kwa ukamilifu. Huu wala sio muujiza, inawezekana.
 
Wana Tz tusibishane sana hapa. Tuichukue taarifa hii kama changamoto. Tuifanyie kazi na utashangaa matokeo yake. Tz ina ardhi nzuri, Ina madini, Ina maji, Ina bahari, Ina misitu nk. Ukilinganisha na Kenya. Kwa nini tusipete? Tujisahihishe, Tujiamini tufanye kweli na tutafika kabisa hapo panaposemwa.
 
Ufike wakati Watanzania tuache kulalamika, Tukiacha visingizio vya kisiasa, Mimi naamini ndio inawezekana Uchumi wetu kuwa bora zaidi ya Kenya, Mfano mdogo tu, Mmarekani ametupatia fursa za soko la AGOA, takwimu zinaonyesha walionufaika zaidi na Soko hilo ni Wakenya, kwanini Watanzania tushindwe, kipi ambacho Wakenya wana uwezo wa kutengeneza na kupeleka Marekani sie tumeshindwa?!!.
Watanzania wenzangu Inawezekana tufanye kazi
 
As long as tutaendelea kuwa wanunuzi na hatuna cha kuuza nje Kenya watakuwa hatua moja mbele yetu daima. Wenzetu wana viwanda, tayari wako kwa wingi katika soko jipya la South Sudan. Sisi ni kutembeza bakuli tu na kufikiria kuwa wawekezaji watatukwamua.
Prof. Karim Hirji ameandika article nzuri sana kwa watu wenye fikra kama zako 'Tanzania has become a nation of complainers'

Inapatikana hapa:

Tanzania has become a nation of complainers  - Magazine |theeastafrican.co.ke
 
Back
Top Bottom