Tanzania on Twitter (TOT)

NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,077
2,245
Mimi ni mmoja wa mtumiaji wa mtandao wa Twitter karibu wiki nzima iliopita kuna uchaguzi uliokuwa unaendelea huko twitter kumchagua Rais wa Twitter Tanzania kama walivyotolea maelezo kwenye vituo vya redio na tv wahusika wa jambo ilo.

Ni jambo zuri sana na mimi nalipongeza ilo na pia napongeza maendeleo yanayofanyika na umoja huo mfano kuchangia madawati, kuchangia wagonjwa wanaoitaji msaada kwa ilo nawapongeza sana.

Lakini sasa kila jambo zuri alikosi kasoro je wanataka kutuaminisha kuwa mapendekezo ya waliokuwa wagombea waliyapata kutoka kwa watumiaji wa mtandao huo? Pili nimefatilia sana maojiano yao inaonekana ni kikundi cha watu wachache tu wanaofahamiana ama kwa kazi zao ama kwa utaalam wao na inaonekana baada ya majukumu ya hapa na pale basi hukutana sehemu ambazo wale watumiaji wa twitter tulio maeneo ya uswahilini atuwezi kukaa na hata ukitaka kupata ufafanuzi wa kitu flani juu ya hiyo Tot kama ujulikani huwezi kupata ni kikundi cha watu maarufu na marafiki zao inavyoonekana.

Sasa ombi langu uchaguzi ujao muweke uwazi mpana watumiaji wa twitter Tanzania waamue kama ilivyokuwa kenya na Msibague mtu hata kama sio maarufu ana haki kwa kuwa tu ni mmoja wa watumiaji wa mtandao huo.
 
Yap nimemuona mkuu nipo kitambo kule zaidi ya miaka 3 nahisi japo nasoma zaidi ya kutweets
Mkuu wale ni watu ambao ukijiunga twitter tu lazima ukutane nao. Miaka mitatu mingi pia labda sababu hau tweets inapelekea watu wasi ku follow na inategemea TL yako imejaa mambo gani.
 
Mkuu wale ni watu ambao ukijiunga twitter tu lazima ukutane nao. Miaka mitatu mingi pia labda sababu hau tweets inapelekea watu wasi ku follow na inategemea TL yako imejaa mambo gani.
Mkuu TL yangu ipo alone sana haina mambo mengi pia nimefollow account nyingi za motivation,lyrics na comedy

Hua sichangiagi kabisa naretweet mara chache natweets na watu wachache pia ambao ni marafiki nami sina base kubwa kabisa
 
Basi ndio maana mkuu. Ila hauitaji base kikubwa unachotaka unakipata basi
 
Ngoja wasake sifa eti rais wa twitter, itakusaidia nn maishani mwako?
#Je, unalipwa?
 
Back
Top Bottom