Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,299
- 3,055
Kwa hiyo uliamini takwimu za kupika na taarifa za magumashi kuwa Tanzania imeingia uchumi wa kati? Kwa nini usijishughulishe kidogo kutafuta ukweli wa takwimu, taarifa na maarifa?Wewe ndio unaropoka mkuu,
Tanzania iliweka mpango, ifikapo 2025, ifikie Uchumi wa kati wa Chini, mwaka 2020 Tanzania ikafikia uchumi wa kati wa chini.
Mipango ni kitu kimoja, kutekeleza mipango ni kitu kingine.
Kupanga ni rahisi sana ila kutekeleza ni kazi inayohitaji kujitoa sadaka.
Nadhani utaacha uropokaji baada ya hapa.
Hivi unajua kuwa dikteta Adolf Hitler alifanya "maendeleo" makubwa sana Ujerumani miaka ya 1930 kuliko haya ya dikteta uchwara mnayoyaimbia? Sasa kama kupeleka huduma rahisi kama maji (ambao ni ushahidi mwingine wa ubovu na ufisadi wa CCM kwa miaka yote), angefanya maendeleo ya kweli si mngemwabudu? Lakini kwa nini Hitler anatajwa kuwa miongoni mwa watawala na watu waovu katika historia ya ulimwengu huu.....kama vile Nimrod, Antioch, Nero, Julius Cesar na wenzao? Katika nchi inayojitambua, yenye utawala wa Sheria, kupeleka maji ni kazi ya Diwani au Mbunge, na haitopigiwa mwingi.
Tambua: Juhudi au harakati zozote za kujaribu kumsafisha au kumsifia hayati Magufuli tayari zimeshindwa na zitaendelea kushindwa maradufu kila uchao, maana uongo hauwezi kuushinda ukweli, na dhuluma haiwezi kuishinda haki, NEVER!
Mapambio yenu yataendelea kumfifisha na kumfedhesha hayati Magu, yaani hata mje na gia gani au hadithi za namna gani; ukweli unabaki kuwa hayati Magufuli alikuwa rais na mtu alikuwa mwovu, katili na mbovu katika historia ya Tanganyika na Tanzania.