Tanzania nzima inaweza msahau Hayati Magufuli ila sio Tabora

Uchumi wa dunia unahusiana nini na Nzega, Isikizya, Tabora, Urambo, Kaliua, Igunga, Sikonge na vijiji vinavyozunguka miji hii kukosa maji ya uhakika toka tupate uhuru? Au miaka sitini baada ya uhuru tunajengewa vyoo na USAID katika shule zetu? Au tunazungumzia matundu ya vyoo miaka sitini baada ya uhuru badala ya shule ( utajengaje shule isio na vyoo vya kuaminika au utatumiaje majengo kama shule yasio na vyoo vyakuaminika) ?

Tatizo ni kubwa sana kama miaka 60 baada ya uhuru kuna watu kama wewe ambao wanadhani ni wajibu wa mabeberu kutupatia maji.

Amandla....
Ni aibu huku kukiwa matumizi ni makubwa hasa
 
Singida Maji yalikuwepo kabla ya Tabora...usikariri mkuu
Maji Singida yameanza kupatikana miaka ya hivi karibuni baada ya well field mpya kuanza kutoa maji. Kabla ya hapo Singida walitegemea visima vichache vilivyopo katikati ya mji ambavyo maji yake hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuwa na nitrates na nitrites nyingi. Nitrites ni hatari sana kwa watoto wachanga kwa sababu huwasababishia kupata matatizo ya kupumua na kubadilika rangi na kuwa na ubluu katika ngozi. Kubadilika rangi na kuwa na ubluu kunasababishwa na upungufu wa oxygen ambayo huliwa na nitrites iliyo ndani ya maji na hatimaye kuingia katika damu.

Hivyo mpango wa muda mrefu wa serikali ni kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria ili kuongezea katika maji ya visima kutoka well field mpya. Hii itawezesha mji wa Singida kuwa na maji ya kutosha kikabiliana na ongezeko la watu na ukuaji wa mji.
 
Acha kuropoka, mpango wa kupeleka maji Tabora, Singida hadi Dodoma kutoka Ziwa Victoria uliandaliwa tangu enzi za Rais Mkapa wakati Lowassa akiwa waziri wa maji. Na mpango huo bado unatekelezwa!
Mwache aendelee kujiliza
 
Acha kuropoka, mpango wa kupeleka maji Tabora, Singida hadi Dodoma kutoka Ziwa Victoria uliandaliwa tangu enzi za Rais Mkapa wakati Lowassa akiwa waziri wa maji. Na mpango huo bado unatekelezwa!
kuandaa mpango si kuidhinisha fedha itoke.

Hili taifa lina mipango lukuki toka uhuru

Hata kuhamia dodoma ni mpango pia toka zamani

Kwan usingetekeleza huo mpango wewe ukienda kushtak wapi.
 
Nimefika Tabora ndugu zangu, nimelia sana baada ya kukumbuka kuwa JPM hayupo tena duniani.

Magufuli, Magufuli, Magufuli, nimekuita mara tatu, najua hunisikii, ila Mungu atakulipa siku ya ufufuo. Ni miaka 60 tangu tupate uhuru, mkoa wa Tabora ulisahaulika sana...hasahasa kwenye huduma muhimu za kijamii.

Awamu zote kabla ya JPM zilipita,bila kuwaletea wana Tabora maji safi na salama. JPM aliwahi kusema, ukiomba mkopo ili upeleke huduma ya maji Tabora, wahisani wanakataa.... JPM aliamua kutumia hela anayokusanya (Kodi) kupeleka maji katika mkoa mkubwa wenye historia iliyotukuka.

Kilichoniliza sio JPM kufa, wala kuleta maji Tabora. Kilichoniliza, kuna bibi mmoja, aliniomba hela 2,000...nikasita kumpatia maana anaonekana ni mlevi. Mimi msabato, ni makosa kumpatia mtu hela akanunue kitu kitakachomuangamiza.

Nikamuuliza ya nini 2000, akanambia "Mjukuu wangu, hii naenda kulipia mkopo wa bomba la maji" Nilishituka, ikabidi nimuite dogo mmoja, alikuwa anapita, nikamuuliza kama kuna mikopo ya hivyo.

Dogo akanambia baada ya maji kufika wilaya ya nzega kipindi cha JPM, changamoto ilikuwa wananchi wengi hawakuwa na uwezo wa kuvuta mabomba ya maji kutoka ziwa Viktoria. Serikali ya wanyonge, kupitia rais Magufuli akatoa order, kila asiyenauwezo wa kuvuta bomba la maji, atakopeshwa, atakuwa analipa 2000 kila wiki mpaka itakapo timia 40,000.

Bibi yule nilimpa 2000. Sasa leo Napita zangu mitaa ile yule bibi ananiletea risti inayodhibitisha kalipia maji. Nilishangaa sana. Nilimpa 20,000 ili akalipe deni lote. Baada ya kufika, napolalaga, nilianza kulia baada ya kukumbuka kuwa JPM hayupo tena duniani.

Tabora nayoifahamu mimi, leo ndoo mbili shilingi 50? Miaka 60 bila maji, Magufuli akaleta maji.

AsanteMagufuli- Kweli vizuri havidumu
Sisi huku Mtwara tumeshasahau kabisa kama kulikuwa na katili mwenye jina kama hilo amewahi kuishi duniani
 
Watakubeza
 
Magufuli anachukiwa na watu wachache sana hapa duniani, niamini mimi bro. Fanya research mkuu. Wanaomchukia ni kikundi cha watu wachache sana ambao wako JF, twitter na Ufipa basi.
Na hapa JF wanajulikana. Idadi yao hapa haifiki hata 300. Hawawezi kujenga hoja na wakaeleweka au kushawishi uma bila ya kudhihaki wengine. Tushawazoea sas, hakuna hata haya ya kujibizana nao. Tuwaache tu maana roho zao zinapata amani kwa kuanzisha threads za kukashifu wengine na ku comment wao wenyewe kwa kukashifu zaidi.
 
Acha kuropoka, mpango wa kupeleka maji Tabora, Singida hadi Dodoma kutoka Ziwa Victoria uliandaliwa tangu enzi za Rais Mkapa wakati Lowassa akiwa waziri wa maji. Na mpango huo bado unatekelezwa!
Hata mpango wa kuhamia dodoma, kujengwa kwa bwawa la kuzalisha umeme uliandaliwa wakati raisi ni Nyerere. Take note kupanga ni tofauti na kutekeleza

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Acha kuropoka, mpango wa kupeleka maji Tabora, Singida hadi Dodoma kutoka Ziwa Victoria uliandaliwa tangu enzi za Rais Mkapa wakati Lowassa akiwa waziri wa maji. Na mpango huo bado unatekelezwa!
Mipango ipo mingi tu tatizo utekelezaji.Ngosha aliwapiga BAO la kisigino kwa kuwa yeye alikuwa man of action.Mtamchukia lakini pengo hamtaliziba.Jamaa atabaki juu kama timu ya Italy.Mtasubiri sana
 
Acha kuropoka, mpango wa kupeleka maji Tabora, Singida hadi Dodoma kutoka Ziwa Victoria uliandaliwa tangu enzi za Rais Mkapa wakati Lowassa akiwa waziri wa maji. Na mpango huo bado unatekelezwa!
Kumbuka hizo enzi zilikua za kuweka miradi kwenye makaratasi lakini utekelezaji ulikua ni zero.
 
Back
Top Bottom