Tanzania: Nini tatizo letu kama Taifa? Tunajikwamuaje?

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,414
Najua huu ni mjadala mpana sana ambao unaweza kugusa kila nyanja ya maisha yetu kama Taifa:

Je, tatizo ni Elimu? (kwamba wananchi wengi hawana, na vyombo vya habari pia vimo kwenye mkondo huohuo, vyeti feki, etc)

Uzalendo? (viongozi na sisi sote)

Rushwa/Ufisadi?

Uvivu wa Kufikiri? (Mkapa aliwahi kudai hivyo)

Wivu-kwa ujumla, au wa kijinga? (ref. Mzee wa Lupaso) au wa kike (ref. Msekwa ) au

Siasa mbovu?

Kutoheshimu Taaluma (ushauri wa kitaalam kutoka kwa wasomi na hasa wazalendo)?

Je, mkazo tuweke wapi ili tujikwamue?
 
Max,

Kwa mchango wangu kiduchu, nadhani tatizo kwetu leo ni ukosefu wa dira. Umesikia leo watu wanapendekeza eti umeme ubinafsishwe.

Hapa Marekani, huduma muhimu kama umeme na maji kamwe havitabinafsishwa. Hizo ni huduma za umma. Na hawa ni mabepari waliokubuhu.
 
KWA maoni yangu ujinga au ukosefu wa elimu ndiyo tatizo kubwa la taifa.

Katika utafiti wangu naonelea kuwa wasio na elimu tosha ni zaidi ya 95%. Hata wale wenye elimu baada ya elimu zao hushindwa kuendeleza ufikirio wao kwa kuwa baada ya kutoka kwenye instutions huingia kwenye societies/ communities ambazo zina makundi makubwa ya wasio na elimu.

Wasomi wetu wengi hushindwa kuwa-influence wale wasio na elimu, bali wao wasomi au wenye elimu ndiyo huwa influenced na kuwa kama wao. Kisa ni kuwa yale makundi yenye watu wasio na elimu ni makubwa kuliko yale yenye wenye elimu.

Solution ni kuimprove hali ya elimu, elimu za ngumbaru zirudishwe, watu wakubali ku-mix na mataifa mengine, education exchange programmes, teachers exchanges especially with the west, study tours etc etc.

Viongozi waache inferiority complex kwa mataifa yaliyoendelea wakubali makosa, siyo kumsingizia mkoloni au mzungu kwa kila kitu.

Katika elimu vile vile hasa ngumbaru wapewe elimu ya uraia, their rights na human rights
 
Kwa ufupi ni kuwa Tatizo siyo sera (kwani tunazo nzuri), siyo elimu (kwani tuna maprofesa hadi wenye shahada feki), siyo uvivu (kwani hilo ni tusi kwa Watanzania) na wala siyo dira (kwani dira tunazo hadi za mwaka 2020!). Tatizo tulilonalo sisi ni la kiongozi.

Tanzania tuna viongozi wababaishaji wasio na uwezo wa kutekeleza maamuzi ya kiserikali au chama. Viongozi wengi hawajui kuongoza, ingawa wengi wanajifanya wanajua kutawala! Ni viongozi ambao hawajui kuthubutu au kuchukua maamuzi ambayo yatawaharibia sifa au umaarufu wao! Ni viongozi ambao hawapendi kumuudhi mtu au kumkasirisha mtu. Ushahidi wa hili ni habari za hivi karibuni kuwa WM amekataa ripoti ya maendelea ya wilaya fulani huko Kigoma, kitu kilichosababisha viongozi wa wilaya za Iringa (atakakotembelea hivi karibuni kuanza kujihami. Kwa vile hawajui kuongoza, viongozi hawa uchwara wanajaribu kwa kila mbinu kujifanya wanajua kutawala!

Ni kwa sababu hiyo basi, utakuta viongozi wanaishia kukaa maofisini, kuweka majalada sahihi, kuangalia taarifa wazisoweza kuzielewa n.k! Ni viongozi hao ambao wanasubiri aliyejuu yao kuwaonesha njia (kama alivyofanya WM) na ambao hawatendi kwa kufuata maamuzi yanayoeleweka. Ni kwa sababu hiyo utakuta basi, jambo ambalo inabidi lifanywe na Mkuu wa Wilaya linapelekwa kwa mkuu wa Mkoa ambaye naye kwa ufinyu na udhaifu wa uwezo wake wa uongozi atapiga simu ofisi ya Tawala za Mikoa kuomba maelekezo!!

Ni viongozi hao ambao katika akili zao zilizodumaa kiuongozi wanaangalia suala fulani linamhusu mtu gani. Kwa viongozi hao, kuna haki ya watu mashuhuri na haki ya watu wa chini. Wanapokabiliana na tatizo wakiwa na mwenendo huo wa mawazo, utajikuta wanapinda sheria na wakati mwingine kuivunja kabisa! Migogoro ya ardhi kwa mfano, isingetokea kama haki ya watu wa chini ingekuwa inaonekana ni haki sawa na ile ya watu mashuhuri!! Viongozi wetu hawajui hilo.

Akitokea bwana Hamdani ambaye ni mfanyabiashara mashuhuri na akataka kujenga kwenye eneo fulani pale Igogo Mwanza, eneo ambalo linamilikiwa na mkulima Mzee Ngosha kwa uhalali wake, basi kiongozi wetu atatumia uwezo wake wa kiutawala kuhakikisha kuwa Bw. Hamdani anapata eneo hilo!!! Bw. Ngosha ataenda Polisi na Mahakamani kulalamikia jambo hilo. Akifika huko tatizo ni lile lile. Bi. Hakimu anaangalia hiyo kesi na kukuta kuwa inamhusu Bw. Hamdani ambaye ni mtu maarufu!! Kwa sababu anazozielewa yeye anatupilia mbali kesi ya Ngosha. Miaka inaenda na kurudi hadi anapotokea kiongozi ambaye hajali sura za watu au hadhi zao! Kiongozi huyo anasema kwa halali eneo ni la Ngosha!! Anamnyang'anya Hamdani kiwanja na kukirudisha kwa Ngosha. Watu wanamuona mtu huyo mkombozi!!! Mfano huo unaweza kutumiwa mahospitalini, mashuleni, kwenye mikopo ya mabenki n.k!

Kiongozi wa ngazi ya chini anayeonekana kufanya kazi vizuri haachwi huko. Kama ni hakimu mzuri, utasikia anapandishwa cheo na kuwa Jaji wa Mahakama ya juu, kama ni mwalimu atapelekwa Wizarani, kama ni Ofisa wa Polisi atapelekwa makao makuu n.k Halafu nafasi zao zinajazwa tena na manovisi!!! Gurudumu la maendeleo linaendelea kubiringishwa kinyumenyume!!

Hadi pale viongozi wetu watakapoelewa maana ya kuwa kiongozi, hapo ndipo tutakapoanza kuona mabadiliko! Semina ya Ngurdoto ilikuwa na lengo la kuwekana sawa miezi michache baadaye, WM analalamika kuwa semina haikuwaingia vichwani baadhi ya viongozi!! Uongozi ni kipaji na si elimu!! Uongozi mtu anazaliwa nao hafundishwi shuleni!! Aidha mtu ni kiongozi au siyo kiongozi! Sisi tunachanganya watawala, mameneja, mawaziri n.k na tunu ya uongozi!!!! Ni kwa sababu hiyo basi utakuta viongozi wa kweli bado wako nje ya mfumo!!!! Laiti wangepewa nafasi ya kuongoza! laiti Tanzania ingewatumia wana na mabinti wake ambao wamejaliwa vipaji vya uongozi bila ya kujali vyama vyao!!!
 
Mwanakijiji,
Nimekusikia, lakini napata hamu ya kuzidi kukuelewa...
Ina maana Tanzania tuna vipaji vichache (au hatuna) vya VIONGOZI? Nakumbuka hata JKN alisema ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa safi, na Uongozi Bora (si bora uongozi au viongozi).

Kama uongozi ni tunu, tufanyeje ili hizo tunu ziibuliwe, maana unasema hamna shule ya viongozi! Tutawapata wapi hio viongozi? Au ndiyo basi tena tusubiri majaliwa ya Mungu?!!
 
Bado ni yale yale ALIYOSEMA MWL IN SUMARY.

Ujinga, maradhi,umasikini na UKOSEFU WA VIONGOZI BORA AU VIONGOZI WENYE NIA YA KWELI YA KULIONGOZA GARI TANZANIA KATIKA MAISHA BORA.
KUTOKUWA NA SIASA BORA.


TATIZO NI KUWA WATU WENGI WANATAKA KUWA VIONGOZI KWA KUTUMIA UONGO NA MBINU ZA KILA AINA ILI TU WAKAJITARISHE NA SIYO KUSAIDIA KUONGOZA WATU WAONDOKANE NA TAABU ZINAZOWAKABILI.

TATIZO LA KUTOKUWA NA INFRASTRUCUTE NI BAYA SANA ANGALIA VYOO HAPO DAR(MANZESE) UATAMANIA KULIA!! VYOO VIMEJAAA UKITAKA KWENDA KUJISAIDIA INABIDI UFIRIE MARA 2!

LAKINI KIPINDUPINDU KIKITOKEA UTASIKIA MAMA NTILIE NK!!

TATIZO LA USAFIRI HASA WA TRENI NI KUBWA KWA NCHI YETU. TUNAHITAJI TRENI KAMA ZA ULAYA, ANAGALU RELI YA KATI IWE FAST!

LAKINI CHA AJBU TUNASIKIA WAMEPEWA WAHINDI KWA MIAKA 25??? KILA MTU AJUMLISHE UMRI WAKE ALIO NAO SASA HIVI UMRI+25= 55 .....

WAHINDI HAWATAFANYA LOLOTE TUTAKUFA NA KUACHA HALI YA USAFRI WA RELI MFANO YA KATI UKO HIVYO!


OMBI LANGU NI KUWA VIONGOZI WABADILIKE LABDA WAKUMBUKE KUWA WAO WANA KAZI YA KUTUKOMBOA NA SIYO KAZI YA KUJITAJIRISHA!!
PIA WAJUE KUWA KUWA KIONGOZI HAINA MAANA YOU KNOW EVERYTHING!

NA HILI LIKUWA TATIZO KUBWA LA SERIKALI YA AWAMU YA TATU.
 
Mwanakijiji,

Nasema tena: sera hatuna. Tunazo kwenye maandishi tu lakini katika utekelezaji hakuna kitu. Hatuna dira. Hivi leo CCM ukiwauliza wanaamini nini wanapatwa kigugumizi.

Sera anazojaribu kutekeleza sasa rais Kikwete kuhusu madini na rushwa ni malalamiko ya upinzani: Chadema na CUF.

Hakuna hata siku moja katika kampeni ulimsikia candidate Kikwete akisema ni sera ya CCM kupitia tena mikataba ya madini. Hiyo ndiyo point yangu. Hatuna sera, hatuna dira, hatuna maadili.

Mkapa alituambia sera zilizomwingiza mamlakani hazitekelezeki. Sijasahau. Angekuwa mtu mwenye maadili angejiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya. Lakini akang'ang'ania miaka kumi akitunisha mifuko yake na ya familia yake.

Huo ndio uongozi wetu.
 
Jasusi,
Inawezekana hawa jamaa walioko madarakani Hangari (Hungary) wamemwiga Mkapa nini? Maana Waziri Mkuu wao anasema chama chao kilidanganya lakini kagoma kujiuzulu! Duuh, madaraka matamu!!

Kwa hiyo kama nimekupata tatizo si sera wala dira, ila utekelezaji wake?? Ina maana hizo sera au hiyo dira ni nzuri?? Je, kwa nini wahusika wameshindwa kuzitekeleza? Je, ni kwa vile hawana Elimu? Au ni kukosa Uzalendo? Au ni kwa sababu ya Rushwa?
 
Kwenye Biblia sie Wakristo huwa tunakutana na fundisho moja miongoni mwa mengi yaliyomo humo.

Kwa kifupi (kwa vile huu sio mhadhara wa kidini) mfuasi mmoja wa Yesu alimuuliza ipi ni amri kuu. Yesu alimjibu kuwa amri kuu (mpya) ni upendo:mpende Bwana Mungu wako kwa nguvu zako zote...na mpende jirani yako kama unavojipenda mwenyewe.Hii inaweza kuwa applicable kwenye siasa zetu,ambapo mimi nadhani badala ya upendo kama unaozungumziwa kwenye Biblia,sisi tunahitaji kuipenda nchi yetu kwa nguvu zote na tuipende kama tunavyozipenda familia zetu.

Ntafafanua:

Nachokizungumzia hapa ni uzalendo na utaifa.Ukiipenda nchi yako huwezi kukubali rushwa ya shilingi 1000 au chupa ya bia ili umchague kiongozi mbovu (Mwanakijiji anasema tatizo ni uongozi/viongozi,nakubaliana nae...lakini nani anawaweka madarakani kama sio sisi wenyewe?)Ukiipenda nchi yako huwezi kukubali rushwa ili umpatie mkandarasi mbovu atakaejenga barabara mbovu itakayouwa watanzania wenzako.

Ukiipenda nchi yako huwezi kuvujisha mitihani baada ya kupewa kitu kidogo kwa vile unajua kwa kufanya hivyo unatengeneza wasomi vihiyo. Ukiipenda nchi yako huwezi kulegeza sheria kwa manufaa ya wauza madawa ya kulevya,wakwepa kodi,wala rushwa,makahaba,na "wadhambi" wengineo.Ukiipenda nchi yako huwezi kuingiza na hatimaye kuuza "unga" kwa vile kwa kufanya hivyo unaathiri nguvu-kazi ya Taifa,unatengeneza taifa la mataahira,na kuichosha sekta ya sekta ya afya.

Ukiwa mzalendo huwezi kutmia Kuran au Biblia kuisababishia nchi yako chuki, uadui na uhasama miongoni mwa wananchi wenzio.Ukiwa mzalendo huwezi ku-divert fedha za kupambana na malaria au ukimwi kwa vile kwa kufanya hivyo ni kuwauwa watanzania wenzio. Na ukiwa mzalendo, huwezi kutetea wala rushwa kama anavyofanya "tafiti then jadili". Pia ukiwa mzalendo, huwezi kuchagua viongozi kwa vile tu mnatoka dini moja au kwa vile mlikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Ni rahisi sana kuwalaumu viongozi wabovu,lakini la kujiuliza tena ni kwamba ni nani anaewaweka madarakani?Wapo watakaosema kwamba watu wanapokea rushwa kwa sababu ya umasikini.Lakini ni nani ambaye yuko tayari kumweka rehani mkewe kwa vile tu hana hela ya chakula nyumbani? Hawezi kufanya hivyo kwa vile ana upendo na mkewe/familia yake.

Hivi tumeshwahi kujiuliza tunaipenda nchi yetu kwa kiasi gani? Sisi ni wepesi sana wa kuwalaumu wanaotuongoza japo ni sisi wenyewe ndio tuliowaweka madarakani. Tukichagua viongozi wazuri, watatengeneza sera nzuri na kukumbuka kwamba wana deni kwetu,na watatuhudumia sisi badala ya kuwakumbatia wezi, majambazi, wala rushwa na wageni.

Kwa mtizamo wangu, tatizo kubwa zaidi ya yote ni kukosekana kwa uzalendo wa dhati. Simaanishi kwamba watanzania wote hawana uzalendo bali walionao ni wachache,uzalendo haupewi kipaumbele na wengi wetu tunategemea watu flani watufanyie mambo flani badala ya mambo hayo kufanywa na sisi wenyewe.

Naomba nitoe mifano miwili. Hapa UK idadi kubwa ya wanafunzi wa kigeni ni kutoka China.Nchi hiyo inafahamika zaidi kwa ukomunisti wake na ingetegemewa kwamba wanafunzi wengi wa Kichina wangeamua kubaki hapa baada ya masomo yao kukwepa sheria za mkono wa chuma huko kwao. Cha ajabu ni kwamba wanakuja kwa wingi,wanapata elimu,na ndio hao wanaoigeuza China kuwa taifa la kuogopewa duniani.

Hapa nilipo nimekutana na Wairani kibao, nao ni kama Wachina, wanakuja huku kwa mission maalum: Kupata ujuzi ambao kwao haupo kisha wakishaupata wanarudi kwao (licha ya ukweli kwamba kwa kufanya hivyo wanakwenda ku-miss anasa zinazoambatana na maisha ya huku Ulaya au Marekani) na wanatumia walichokipata huku kuendeleza nchi zao. Tena wangeamua kubaki huku wala isingekuwa shida kwa vile miongoni mwa sifa za kutoa makazi kwa wageni, kwa mfano hapa UK,ni track record ya human rights ya nchi anayotoka mwombaji. Hawataki kubaki hapa kwa vile wana uchungu (upendo/uzalendo) na nchi zao.

Jiulize ni watanzania wangapi wanaopotelea ughaibuni pindi wanapopata nafasi ya kuja huku...(Mwanakijiji hebu jaribu kutufanyai sensa ya Watanzania walioko huko ambao wamesomeshwa kwa Tanzanian taxpayers na hawana mpango wa kurejea Bongo)

Mfano wa pili:
Niliwahi kuongea na babu mmoja wa Kiskotishi na nikamwomba mawazo yake as to kwanini wenzetu wamepiga hatua zaidi ya sisi.Aliniambia kuwa tukiachana na sababu kama ukoloni (ambao alikiri kuwa una mchango flani) mabibi na mababu zao walikuwa na uchungu na nchi zao na hivyo kuenga misingi imara ambayo imedumu hadi leo. Alisema kuwa silaha kubwa enzi hizo ilikuwa dini,na ndio maana japokuwa dini kwa nchi kama Uingereza imebaki kuwa ya kinadharia zaidi ya kimatendo bado maadili ya uongozi na uwajibikaji kama raia uko juu sana.

Misingi ya kodi iliyoimarishwa na imani za kidini imekuwa ni muhimu sana kwa jamii za magharibi. Na nchi isiyokusanya kodi kama yetu ina nafasi gani ya maendeleo katika dunia ya sasa? Kwamba kutolipa kodi ni dhambi hapa duniani na kwenye afterlife, mwanasiasa au mfanyabiashara anayekwepa kodi anachukuliwa kama mwanaharamu flani. Na kwa vile viongozi ni waadilifu,kodi inayokusanywa inawezesha kudumisha maendeleo yaliyopo na kuyaendeleza na pia kuitumia kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.Wenzetu walijiwekea katiba zao karne kadhaa zilizopita na wameendelea kuziheshimu bila kuzifanyia mchezo kama tunavyofanya huko kwetu.

Uongozi si tatizo kwa vile hata hawa wenzetu pia hawajiongozi wenyewe bali wana viongozi,tofauti ni kwamba hawa wa wenzetu kwa kiasi kikubwa ni waadilifu na wanaingia kwenye uongozi kuhudumia jamii na sio matumbo yao.

Elimu si tatizo kwa vile tuna viongozi wenye elimu kama akina Prof Kapuya, Mwandosya, etc lakini matendo yao ni tofauti kabisa na elimu yao...why? Kwa sababu hawana uzalendo, period. Pia mfano mzuri kuwa elimu tunayo ni namna michango inavyoendeshwa kwenye forum hii.

Ardhi tunayo,na imekuwa kubwa zaidi hadi tunaikodisha na kuitoa zawadi kwa wageni,sera zetu ni nzuri hadi tunaweza kuwa-convince hawa wazungu kuendelea kumwaga misaada yao ambayo inaishia kuongeza mashangingi,mabangaluu na nyumba ndogo,sheria zetu ni nzuri japo hazitekelezwi,na nguvu-kazi (manpower) ipo ambayo ni mimi na wewe.

Nimalizie kwa kusema kwamba katika Biblie sie wakristo tunaambiwa kuwa kwenye upendo Mungu yupo.Na katika siasa,kwenye uzalendo maendeleo yapo.

Kwenye dini Mungu ndio kila kitu na kwenye nchi maendeleo ndio kila kitu.(nau-define UZALENDO kama UPENDO/MAPENZI/UCHUNGU KWA NCHI).
 
Jamani,

Great points zimetolewa, na great debate hii. Mimi nina mawazo tofauti.

TUNAKOSA ELIMU. PERIOD!

Tanzania kwa sasa hata CCM ikisimamisha kichaa kugombea urais anapata. WHY?. Sehemu zilizokuwa na shule toka zamani kama Kagera na Kilimanjaro, ndio tumeona wanapata angalau ubunge wapinzani. WHY?.

Elimu ni pana. Basic elimu ya secondary ni muhimu kwa kila Mtanzania, Lakini waelimishwe pia kuhusu Self awareness, Uraia, uzalendo etc.
Kungekuwa na somo shuleni (lipo uraia kwa sasa) linaloonyesha mabaya ya kutolipa kodi, mabaya ya kuchukua rushwa etc.

Wananchi waliopo sasa (asilimia 80% kwa mtazamo wangu) hawawezi kupembua lipi ni lipi. Ili tuendelee tunahitaji wananchi wenye mtazamo na uzalendo. Huwezi kuwa na mtazamo au uzalendo kama huna elimu angalau ya kati.

Leo unaenda kwa babu ambaye hata darasa la kwanza hakwenda, kisha unaanza kumuelezea sera ya majimbo, ataelewa nini?, au unamweleza kukua kwa uchumi, per capita income imekuwa blah blah!! what?!?, anachohitaji kumuambia utaijengea kijiji chake hospitali, shule, kuleta maji. Basi hapo umepata kura!!!, wanasiasa ni waongo, hivyo easily anadanganya anapata kura.

Kwahiyo hawa wananchi tukiwaelimisha basi ujue CCM tuna kazi ya ziada. Kwa maana wataweza kufanya Logical reasoning etc.

Bandugu nimeongelea Elimu katika narrow mind sasa naomba uelezee hiyo hiyo elimu kwa kusomesha nje vijana kwa ajili ya utaalaamu.
Elimu ya kusomesha nje itakuza uchumi haraka, elimu ya kati itasaidia wananchi kuamka na kuchagua viongozi bora.

Mi nalia na ELIMU.

FD
 
Mwanakijiji umesema:
"Kwa ufupi ni kuwa Tatizo siyo sera (kwani tunazo nzuri), siyo elimu (kwani tuna maprofesa hadi wenye shahada feki), siyo uvivu (kwani hilo ni tusi kwa Watanzania) na wala siyo dira (kwani dira tunazo hadi za mwaka 2020!). Tatizo tulilonalo sisi ni la kiongozi".

Believe me, Elimu ndiyo muhimu, na bila ya Elimu hata yule mtengenezewa sera kama hana Elimu hizo sera zitatekelezwa na nani? Jiulize swali moja kwa nini unabidi umsomeshe mwanao au ndugye kama ikiwezekana? Mtu akisoma hata mnavyojadiliana mnaelewana. Elimu inasaidia watu waelewane, elimu inakufanya uwe na access to information na inaongeza personal capacity of thinking. Mtu ambaye hana elimu huwezi kuelewana naye kwa sababu ni ujuaji tofauti kabisa. Kweli sera ni nying sana, unamtengenezea nani? Sawa sawa kabisa usemi wa kumpigia filimbi ng'ombe acheze.

Hata uwe na dira kiasi gani kama walengwa hawana elimu basi hakuna kitu. Hao maprofesa wa Tanzania wana-occupy percent ngapi ya population ya Tanzania? Ushauliza tuna-maengineer wangapi? Madoctor of medicine Wangapi? Uki-combine doctors, engineers, technicians, economists etc tunao wangapi? Or else ongelea ile quality education ni wangapi wameipata?

Hao watungaji wa sera wanachukua advantage ya wananchi kuwa hawana elimu na kuzembea kwa sababu population kubwa inawatetea na hiyo population kubwa ndiyo hawana elimu, na ndiyo wanashikilia majeshi, polisi etc

Wasomi wanaopinga mambo ambao kwa namba ni wachache sana kiasi kwamba sauti zao haziwezi kusikika. Wale wasio na elimu ni rahisi kurubuniwa kuwa hao wanaopinga ni traitors, nao huamini.

Sera huwasaidia tu wale wenye elimu, kwa mfano, sera za AGOA, import financing, investments imewasaidia sana wahindi kwa sababu ndiyo wengi wenye elimu ya biashara. Indigeneous anajua MISHENI TAUNI, hataki fedha inayo kuja baada ya miezi mitatu. Anataka pesa ya chap chap. Inasikitisha sana sana kuona kwamba sasa hivi hata opportunities ambazo ilibidi ziwe za indigeneous 90% zimeenda kwa aidha waasia au baadhi ya westerners. Mfano kama zile product representative. Hakuna mswahili anayewakilsha brand names, wote ni waasia au westerners. Sasa hii utaiitaje?

Obvious Elimu, ambayo ina mfanya mtu awe na access to information.
 
Mwanagenzi,

Naona Mlalahoi ameshakujibu swali uliloniuliza. Ingawa nachelea kukubaliana na FD juu ya elimu, nafikiria uzalendo ni nambari wani. Hivi leo watu hawagombei ubunge kuhudumia jumuiya zao. Wanagombea ubunge, ili wapate kuwa mawaziri, ili waukate, au waule, katika lugha iliyoibuka hivi karibuni.

Umemsikia waziri mmoja akilalamika kuwa wizarani mwake wamejaa watu wanaokula rushwa. Lakini kachukua hatua gani mpaka sasa kuishafisha hiyo rushwa? Na viongozi wengi ambao wametuangisha si ni wasomi?
 
Jasusi,

Soma maoni ya IO hapo juu. Sisi tunachosema na Interested Obs ni kuwa ukiwapa wananchi wotee elimu, viongozi watapata Uzalendo tu!, why simpo. Watu wote wanajua kupambanua sera ambazo zinatekelezeka na ambazo hazitekelezeki, ukidanganya next term nje!, wananchi wanafikra na wanaelewa kila kitu kama hapo kwenu.

Wanaoongozwa ni mambumbumbu mnooooooooooooo, unaweka kuwadanganya kila mwaka kwa miaka 30 ukawa unawaongoza. Fikiria hivi, kiongozi hana uzalendo, OK, wananchi wa nchi yake wana elimu ya kutosha, whats next?

Elimu jamani, elimu inaleta wataalamu, elimu inafanya uweze kupembenua mambo kiyakinifu, elimu inafanya viongozi waamke na kujua hatutawali wajinga, elimu inasaidia kupata info. Elimu..
Jasusi, Viongozi wanakosa uzalendo kwa sababu wanajua hatuna elimu ya kung'amua mambo. Laiti wangejua tuna elimu wasingethubutu.

Fikiria vizuri, utagundua Elimu ndo source. Jaribu kufikiria kuwa kama hawa viongozi wetu wa Tanzania wangekuwa ndio vingozi Marekani nini kingefanyika na mikataba yoote hii feki?

Naomba majibu

FD
 
Ni nchi gani inaongozwa na wafalme wanafalsafa?!! Ukisome Plato's Republic utaona kuwa nchi kinadharia inapaswa kuongozwa na wanafalsafa... Hata hivyo tangu enzi za enzi, viongozi mara nyingi sio wale wenye elimu zaidi katika jamii!!! Hivi Clinton, Bush, Blair, Mandela, n.k ni wasomi zaidi katika nchi zao? Ukiondoa India ambako Waziri Mkuu wake ni msomi aliyebobea.. nchi nyingi duniani haziongozwi na wasomi!!

Sasa usinielewe vibaya, sitaki kupuuza wasomi, au kuufanya usomi ni duni. La hasha, ninachojaribu kusema ni kuweka tofauti yakini kuwa tusichanganye mtu kuwa msomi na uwezo wa mtu kuongoza. Cha kwanza kinapatikana shuleni, cha pili ni cha kuzaliwa nacho!! Hivyo basi kinadharia, nchi na jamii zingeongozwa na wasomi-viongozi badala ya wasomi-watawala!

Tatizo la kutukuza wasomi ni kuwa wananchi wanaamini kila kinachosemwa na wasomi na hivyo ni rahisi kurubuniwa na kudanganywa kwani aliyesema ni "Profesa". Ni wasomi walioingiza Tanzania kubaya, ni hao walioandika mikataba mibovu, ni hao waliofujisha mashirika ya umma, na ni hao hao wanaoendelea kutumia nafasi zao kutunisha matumbo yao!! Kwa vile wao ni wasomi basi Watanzania wanakuwa rahisi kuwasikiliza!!!

Upande mwingine, hakuna nchi yoyote duniani ambayo watu wake wote wameelimika ndo zikaendelea!!! Unafikiri Marekani wote ni wasomi? au Uingereza wote wamesoma? Watu kutoa na kupokea rushwa si suala la usomi, ni suala la tumbo!! Mabilionea wanatoa rushwa kupata pesa zaidi, na masikini wanatoa rushwa kupata haki zaidi na haraka! Madaktari mabingwa wanapokea rushwa, na wenyewe wakienda kwenye maofisi fulani wanatoa rushwa!! So rushwa si suala la elimu hata chembe!

Taifa la watu walioelimika ni taifa bora zaidi. Watu walioelimika si rahisi kudanganywa, hilo nakubaliana nalo. Hata hivyo, kuwa na watu walioelimika wakiongozwa na viongozi wabovu walioelimika si suluhisho la tatizo letu. Elimu haimgeuzi mtu kuwa mzalendo!!!

Ni sawa na kile kisa cha Paka aliyepewa elimu ya haki na usawa wa wanyama wote. Paka huyo alifuzu mitihani yake yote na hatimaye kutunikiwa shahada ya juu ya uzalendo! Ilikuwa siku moja kwenye kikao cha wanyama wote, paka yule alipewa nafasi ya kuzungumza na wanachama na kuwaeleza kitaalamu juu ya usawa na haki za wanyama wote, wale wa nyumbani na wa porini. Kikao kiliendelea kwa muda mrefu hadi karibu jua lizame. Akiwa anaendelea na hotuba yake, huku tumbo linanguruma kwa njaa, alijikuta ameanza kumtamani yule panya aliyekuwa kwenye kona ambaye alikuwa anafurahi kuwa paka (ambaye ni adui wa kuzaliwa) ameelimika.

Kutokana na ubao uliokuwa umembana kwa muda mrefu, yule paka akaamua kuahirisha kikao ili watu waende kupata msosi. Kikao kilipoendelea, mjumbe mmoja alikosekana. Panya!

Hivyo anayedhania kuwa elimu itambadilisha mtu na kumfanya awe vile asivyo, anajidanganya! Uzalendo haufundishwi shuleni wala haupewi kwa heshima!! Tatizo letu bado nadai ni uongozi uchwara, usio na mwelekeo, usio na ushawishi wa uvutio. Ni uongozi duni ambao hauona uwezo wa kuongoza!!
 
Wazee kwa mtizamo wangu elimu ni sehemu tu ya tatizo. Uzalendo naamini ndio haswa tunaokosa, maana sisi wachahche tulienda shule tumekabishiwa dhamana na wananchi wote ya kuongoza na kufanya maamuzi kwa manufaa yao popote pale tunapofanya kazi.

Unajua kama elimu ndio ingekuwa ni mgogoro, mbona vyuo vyetu vikuu do not stand out of crowd katika utendaji? Actually it even gets to a point watu wanaita "vyoo vikuu" kwa jinsi mambo yao ya ndani kiutawala na kiutendaji yananyoweza kwenda kombo wakati mwingine. Na mara nyingi inakuwa kwenye misuse of funds.

Kwa hiyo japo elimu ni muhimu lakini uzalendo ndio ni muhimu zaidi.
 
Jamani,

Mi hata sielewi, HAKUNA ALIYESEMA VIONGOZI HAWANA ELIMU!!!!!!!!!!!!!

Kilichosemwa hapo juu ni Elimu kwa raia (wananchi) kwa ujumla. ambao umegawiwa kwenye pande mbili: Elimu ktk kufundisha/kutafuta wataalamu. Na nyingine elimu kwa Wananchi wa kawaida ili wawe na uelewa wa mambo waweze kung'amua viongozi wanapodanganya.

Au mimi ndo sijaelewa?

FD
 
Jamani,

Mi hata sielewi, HAKUNA ALIYESEMA VIONGOZI HAWANA ELIMU!!!!!!!!!!!!!

Kilichosemwa hapo juu ni Elimu kwa raia (wananchi) kwa ujumla. ambao umegawiwa kwenye pande mbili: Elimu ktk kufundisha/kutafuta wataalamu. Na nyingine elimu kwa Wananchi wa kawaida ili wawe na uelewa wa mambo waweze kung'amua viongozi wanapodanganya.

Au mimi ndo sijaelewa?

FD
 
Duuh! Nafurahia mjadala, hili ni darasa la hali ya juu...
Kimsingi hoja nyingi zinanikuna. Lakini imefika mahali labda tujiulize sasa, kwa nini hatuna UZALENDO? Tufanyeje ili watu wetu wengi zaidi (critical mass) wawe wazalendo?

Kuna wakati huwa nadhani tulikosea kuuacha Ujamaa (sijui kama CCM watakubaliana nami) kwa haraka bila tafakuri ya kina. Huenda tulipaswa kubadilisha siasa yetu taratibu. Mfano dhahiri ni kuacha Miiko ya Uongozi kama ilivyoainishwa na Azimio la Arusha, na badala yake kupitisha Azimio la Zanzibar. Matokeo yake ni mashindano ya viongozi wa leo kujilimbikizia mali, hususan kwa njia zinazotia shaka, au zenye "mazingira ya rushwa", kama si rushwa kabisa.

Sasa, tufanyeje tupate VIONGOZI WAZALENDO ambao watasimamia ujenzi wa taifa la kizalendo? Mambo ya Utandawazi na Mfumo wa Soko Huria (soma Ubepari) vimefanya baadhi ya watu kuuona uzalendo kama ujima, ukale, ushamba, uliopitwa na wakati. Inawezekana vitu kama magwaride na halaiki enzi hizo mashuleni na JKT vilisaidia kujenga taifa la wazalendo?

Lakini pia kwa nini mataifa mengi, kama si yote, ya Afrika yanafanana kwa hali na maisha yake (umaskini)? Yote hayana watu wazalendo, wasomi, viongozi? Tanzania iliwahi kulaumiwa kwa kuwa Wajamaa hapo nyuma. Je, kuna taifa gani la Afrika ambalo halikufuata Ujamaa na linaweza kutajwa kuwa limeendelea, au hata kuwa na dalili dhahiri kuwa litaendelea hivi karibuni? Najua baadhi ya wasomi hutaja Botswana kama mfano wa nchi pekee yenye maisha ya juu (vigezo vya UN, WB ). Lakini nchi hii haina wasomi wengi hata kidogo! Huenda ukweli huu unathibitisha kuwa ELIMU haioni ndani kwa UZALENDO? Uzalendo wa viongozi waanzilishi wa Botswana uliwasaidia kuingia mikataba ya uchimbaji madini yenye maslahi kwa taifa kiasi kwamba mpaka leo hii wananchi wanafaidika.
 
unaona, haijalishi kuwa na watu waliosoma, kama viongozi ni wabovu ni wabovu tu!!!! Kumbuka viongozi wana nguvu, waliosoma na ambao siyo viongozi hawana nguvu!!! Kiongozi mbovu aliyesoma, anatumia nguvu zake vibaya na anaweza kupinda sheria (kama ilivyotokea Hungary) ili kuwalaghai wananchi!!

FD, kama usomi unaosema wewe ni uwezo wa kufikiri unaotokana na uhuru wa kupata habari siyo digrii ya shuleni nakubaliana na wewe kwa upande fulani. Lakini kama uandhania kuwa watanzania wote wakipata digrii chuoni basi nchi itaendelea unajidanganya!! Unajua Wanigeria wangapi wamesoma!!? lakini wanahangaika kuishikilia nchi yao pamoja!
 
Back
Top Bottom