Tanzania: Nini tatizo letu kama Taifa? Tunajikwamuaje?

Bonnie1974,

Mkuu kama ulikuwepo vile....

Unajua mwaka 2000 niliwahi kuyasema haya ktk mjadala mwingine na sidhani kama wengi walinielewa wakati ule kwani ndio kwanza uwekezaji ulivuma sana nchini..

Kila tunachokiona leo hii ni mpango uliopangwa na CCM toka mwalimu Nyerere alipotuondoka..Hii ni baada ya wazee waasisi wa chama na Uhuru wetu kujikuta wanazeeka pasipo kuwa na mali, utajiri na kwamba nguvu zao zote zimefikia kikomo wakibakia maskini kama walivyoachwa na mkoloni..As to say all those years wamefanya kazi for NOTHING!..yaani wanakufa maskini?..

Hapana haiwezekani ndipo walipotunga mwelekeo mpya!

Hizo strategies zote walizopanga toka Mwinyi, Mkapa na hadi leo hii zilikuwa ktk kujinufaisha wao na sii taifa. Tusidanganywe na mtu yeyote kuhusu sijui sera na mipango ya IMF.. Ni wizi mtupu ulitumika wakielewa wazi wanafanya nini..

Hakuna kitu kimefanyika bila mpangilio topka Azimio la Zanzibar wapate kufanya biashara, Kuuzwa kwa nyumba za serikali na mashirika ya Umma na mikataba yote inayohusu sehemu nyeti kama vile Umeme, Mawasiliano na kugawana sehemu majumba ya msajili..Wakati wote wa Mwinyi na Mkapa mambo mengi yalifanyika kwa hatua na uangalifu mkubwa sana kutowashtua wananchi lakini kama tujuavyo siku za mwizi ni Arobaini.. Wakati wa Kikwete wamefikia kukiuka miiko ya Utapeli nayo ni kujisahau. wamekuwa wakiiba waziwazi na ndicho kilichowaponza..

Hadi leo hii bado yapo mashirika ya nje yanayouzwa baada ya miaka mitano kukwepa kodi na wanafanikiwa...Yapo mashirika baada ya wizi hata rais wa nchi anashindwa kuwaambia wananchi ni kina nani wamiliki wa shirika lilihujumu uchumi wa nchi..kama vile wanatutaka tusahau. na kibaya zaidi mashirka haya yanapata baraka za wabunge na viongozi wetu kwamba hakuna utapeli wowote laa sivyo sisi wananchi tulete Ushahidi!..

I mean ni lini serikali ya nchi ikawaomba wananchi wake walete ushahidi wala sii wa maneno against kiongozi ili uchunguzi ufanyike.. Navyoelewa mimi mashtaka ndiyo yanahitaji ushahidi lakini uchunguzi kweli nao unahitaji ushahidi. Leo hii mimi hapa nikiinua simu na kuwaita Polisi niasema kuna mtu anazunguka zunguka karibu na nyumba yangu simfahamu.. watakuja, watachunguza na pengine hata kumhoji mhusika kabla haijafikia maamuzi yoyote yale. leo tanzania uchunguzi unafanyika, kunaonekana kuna Ubadhilifu wa fedha na mali ya nchi lakini kwa sababu mhusika ni ktk team ya CCM.. Utawala unaogopa matokeo ya mashatka hayo ati yatakuja sambaratisha nchi..

tawala zote duniani hupata sifa kwa kuwakamata wahalifu, hupata sifa ya Uobngozi bora sio kwa kuwalinda viongozi wabaya bali kuwaweka hadharani, kuwaadhibu na hata kuhakikisha viongozi hao hawapati tena nafasi ya kuongoza vyombo vya uzalishaji.. Ni adhabu kali sana, sawa na kifungo cha maisha uraiani lakini inaweka funzo zito kwa kila anayetaka kugombea Uongozi kwamba Uongozi sii lelemama..Sii kazi ambayo kila mtu anaweza kuikimbilia na kuacha profession yake kwa sababu kuna Ulaji..

Lakini yote haya sii hoja.. Nini Tatizo letu kama Taifa?..

Ni sisi wananchi wenyewe! wananchi wameshindwa kugundua kwamba kinachowa kii nguoni mwao...wameshindwa kusimama against Utawala mbaya kwa kuogopa nguvu ya dola ambayo bado inatumia milki ya Kidikteta..na kibaya zaidi ni kwamba wachache wanaofikiria kufanya mageuzi wanaopoga kwani wananchi ni wepesi wa kuwaacha nje, wakawakimbia, kuwacheka na kuwabeza kwa sifa zote mbaya ambazo zinawafanya wao kuonekana wabaya kuliko hata Mafisadi wenyewe..

Kwa maskini siku zote, tajiri ndiye mtume wao hata kama ni Jambazi..wao husema mkono mtupu haulambwi!..
 
umasikini ni matokeo ya uvivu wa kufikiri.

Umasikini wetu unatokana na uvivu wa kufikiri, kuanzia mwananchi wa kawaida mpaka kiongozi aliye madarakani.

kutokana na uvivu huo wa kufikiri, kujituma, na kielimu, watanzania huchagua bora kiongozi badala ya kiongozi bora, ...na matokeo yake ndio haya... Tunakaribia Golden jubilee (50 yrs) tangu tujipatie uhuru ilhali 40% ya bajeti yetu inategemea msaada wa wafadhili! ...tunahitaji 'mental stimulation' ili kujikwamua na kilema hiki.

Tanzania is so rich, so stable, but so poor

...No wonder 'wanatushangaa!'
 
TATIZO LETU KAMA TAIFA NI UBINAFSI=UCHOYO

UBINAFSI unazaa UFISADI
UBINAFSI unazaa UKABILA/UDINI
UBINAFSI unazaa KUKOSA NIDHAMU/UJEURI

ili tuondokane na MDUDU UBINAFSI inabidi wananchi tubadilike..........tusiogope kuwawajibisha viongozi walio WABINAFSI.......tukiendelea kuwachagua viongozi Wabinafsi........they will always undermine us (wananchi).........

Sisi Wananchi bado hatujajua nguvu tulizo nazo kubadilisha uongozi.....tukisha jua na tukawaonyesha WABINAFSI kuwa tunaweza kuwafukuza.......hakuna watakaotu-undermine tena...........

Hivyo basi na tuongeze nguvu kuwaelimisha wananchi juu ya uwezo tulio nao ambao hatuutumii.........
 
kubadilisha viongozi kwa TZ ni kama kuota ndoto maana system ilishajengwa siku nyingi kuwezesha watu wachache wateule ku run the show no matter what.Ukijaribu kuingilia huo mfumo utapambana na mkono wa dola na hutajua nini kimekupata.Ofcourse forces of nature (old age, natural death etc)soon zitawafagia walioko kwa muda wote toka tupate uhuru.Tatizo ni kuwa even with that hakuna mabadiliko makubwa yatakuja maana walioko madarakani sasa wanajizalisha through watoto wao, ndugu zao na marafiki.Kama hauko kwenye system mpaka sasa just forget it.Wapya wanaoingia madarakani nao wanajikuta wamerithi mfumo wanaoukuta na hivyo kutokuleta mabadiliko yanayotarajiwa.
Having said this, I am at a loss as to what to do!Wananchi mbona wanapewa elimu through civic education and mbinu nyingine lakini mambo yanabaki yaleyale
 
...naam, naam, naaam! kuukubali ukweli ni hatua ya kwanza kuondokana na tatizo linalotukabili. Kama mnakumbuka, wale wagombea watatu waliosimama mpaka mwisho kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM walisema haya;

BTW, jamani msione uvivu kusoma, kuyatafakari na kuyaelewa maneno haya na kisha kujiuliza, tulipatia/tulikosea wapi? na huko tunakoelekea itakuwaje?

; Mimi ndiye Mrisho Jakaye Kikwete, hii ni mara yangu ya pili kusimama katika jukwaa hili kuomba uteuzi wa kugombea nafasi ya Urais.
Batm mbaya mwaka 1995 nilipojitokeza kwa mara ya kwanza kura hazikutosha. Nimesimama tena mwaka huu kuomba kura zitoshe.

Naomba kupewa kazi ya kusimamia Ilani ya CCM. Ninaomba katika miaka hii mitano kazi hii ya kuisimamia na kuitekeleza Ilani ya CCM nipewe mimi. Mwenyekiti, uongozi unaweza kufananishwa na mbio za kupokezana vijiti. Kiongozi wetu, Baba yetu marehemu Mwalimu Nyerere, alimkabidhi Mzee wetu Alhaji Mwinyi, na yeye alimkabidhi Rais wetu Mkapa na yeye anatazamia kukabdhi kijiti hicho.

Ndugu wajumbe naomba kijiti hicho nikabidhiwe mimi.
Mambo ninayoyaona makubwa na muhimu ni kudumisha na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya tatu ili kutoka hapa tuende mbele zaidi.

Kulinda na kudumisha umoja wa taifa letu. Tanzania ni nchi inayotokana na Tanganyika na Zanzibar. Kwangu mimi kudumisha Muungano wa Tanzania ni jambo la msingi. Tanzania ni nchi yenye watu wanaotofautiana kwa kabila, dini na rangi. Kuimarisha hali hiyo kwangu mimi ni jambo la msingi.

Nikijaaliwa kuwa Rais, jambo hilo nitalidumisha kama mboni ya jicho langu. Nikijaaliwa nitaendeleza jitihada za kuondoa umaskini kwa nguvu mpya na ari mpya. Nitaunda serikali inayotekeleza wajibu wake kwa utawala wa sheria na haki za binadamu na wanyonge.

Ninapambana na rushwa, nitaimarisha uhai wa chama, kiuongozi na kiutendaji.
Naomba mniteue kuwa mgombea, ninaamini ninayo maarifa na uzoefu wa kutosha na umri wangu sasa ni muafaka. Mimi ni waziri kwa miaka 17 sasa, tangu mwaka 1988.

Katika miaka kumi hii nimekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na kujifunza maarifa mengi ya wenzetu. Umri wangu wa miaka 30 katika uongozi baada ya kumaliza Chuo Kikuu, nilikubali kuwa mtumishi wa chama. Ninakijua vizuri chama. Naamini nikijaliwa chama kitakuwa katika mikono salama. Ndugu wajumbe naomba kura zenu.

Profesa Mwandosya: Hakika kuna wajibu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kutufikisha hapa leo hii kwa kupata kiongozi atakayetuongoza. Bendera yetu inapendeza kwa rangi yake ya kijani yenye nyundo na jembe.
Urais ni kazi ya juu na yenye upeo. Tunaamini kwamba mamlaka Ouani yanatokana na Mwenyezji Mungu.
Nasimama mbele yenu nikiwa kama mgombea wa chama chetu, kuwania nafasi ya kugombea Urais.

Nia ya kuwania nafasi hii ni kutaka kuendeleza uchumi wa nchi katika uongozi. Uongozi wa awamu ya nne utaongeza ajira bila kujali dini wala ukabila.
Utadumisha amani, utulivu na mshikamano na kulindwa kwa pande zote mbili za muungano. Aidha kulinda mapinduzi na viongozi wetu. CCM itajitahidi kwa kutumia Ilani ya Chama.

Naomba kura zenu na dua zenu mgombea niwe mimi. Umaarufu usiwe wa mtu bali uwe wa chama.
Mimi nilisomeshwa bure, nimekuwa mwanachama tangu enzi za TANU na sasa CCM tangu mwaka 1977.

Sina ahadi kwa wajumbe na wanachama, ila nitawatumikia wananchi wangu kwa moyo wangu, nguvu na utukufu. Eeh Mungu nisaidie.
Walatini walisema Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu . Mheshimwa Kikwete, Mheshimiwa Salim, naomba kura zenu.

Dk. Salim: Nimesimama hapa kuomba kwenu, mniteue ili niweze kuwa mgombea wa CCM ili niweze kuwa Rais wa nchi yetu.
Naona uzito wa uamuzi ninaoomba muufanye. Uamuzi ulionifikisha hapa ulikuwa mgumu kuliko wowote niliowahi kufanya katika maisha yangu.
Urais ni madaraka na mamlaka makubwa ya nchi.
Kwa muda wa zaidi ya miaka 40 tumekuwa katika safari ndefu ya kujiletea maendeleo. Chini ya viongozi wetu waliopita, tumeweza kudumisha Muungano na kuulinda.

Katika mambo yaliyonivutia wakati nikitembelea mikoa niliyotembelea ni jinsi maendeleo niliyoyaona hasa katika barabara na ujenzi wa shule na mambo mengine ya kimaendeleo ya wananchi.
Naelewa matatizo ya nchi yetu pamoja na kuwa nje kwa miaka 12, ilikuwa muhimu kujionea hali halisi ya nchi yetu.

Katika nchi yetu tunahitaji nahodha mwenye uzoefu na ujuzi, pia awe na upeo wa kuona Mbale ili kulinda hazina yetu na vizazi vyetu.
Nawashukuru viongozi wetu waliopita kwa kunikabidhi madaraka nikiwa bado mdogo.

Naamini naweza kumudu unahodha katika bahari inayoachwa na Rais wetu Mheshimwa Mkapa.
Uzoefu katika nchi na kimataifa unaniweka katika hali nzuri ya uongozi.
Exima tuliyojijengea hatupaswi kuipoteza, pamoja na uzito wa dhamana nilioyoomba kwenu naamini uongozi ni wa pamoja unaoongozwa na Ilani ya chama chetu.

Nitajitahidi kuepusha misingi ya kibaguzi, kikaburu nitaimarisha haki za binadamu, haki za wanawaake, vijana na watoto na kuzingatia matatizo ya wazee wetu.
Wajumbe wa Mkutano huu wanadhamana kubwa wanapaswa kufanya uamuzi huu kwa kufikiri sana.

Nitazingatia utumishi wangu katika nchi na chama changu. Nimekuwa mwanachama wa ASP. CCM kwa miaka 38.
Naomba kura zenu, Mapinduzi daima.

...yalopita si ndwele, lakini.." watanzania, where did we go wrong?" iwapo Katika watatu hao, mh.JK ndiye aliyeibuka mbora ilhali naye anatutenda namna hii basi kazi ipo huko 2015!
 
Kwa hesima na taadhima,
Wakuu, huko nyuma nilishawahi kuanzisha thread Inside Africa(Tanzania)My perspective na nilinena haya yafuatayo.....

Inside Africa (Tanzania): My Perspective

--------------------------------------------------------------------------------

As CNN newsmagazine Inside Africa was airing, I just happened to be thinking of my motherland and its political, social, and cultural issues, which are the segments that aired, but with prompt and without formality I put the segment with Tanzania which country I hail from into My-Perspective

Politically- I do not understand if it is Ideology that steers our political and policy processes or Individualism but in the same context, I also understand that we are neither radical nor a one party state, hence, my conviction that, it is neither or Individualism but going through a process of defining so.

Economically- Africa and Tanzania in particular are moving towards better economy stability. With the global, economic indexes showing better GDP's And GNP's in spite of gross 'Manfraudovandalism' Man-Fraud-O-Vandalism. Where man (from our leaders to ordinary citizen) has entered onto Individual realm with this Fraud has become an escape from collectivism hence Vandalism of our national natural resources! Is there much assay?

Culturally- We are shocked! (Thank god to 75%+ literacy rate), bruised but not ruined.

Socially- We are awakening from the hypnotic state. A state which is directly or indirectly attributed by the cultural shock, and we are entering Realism state, with a fact that we are not poor or poverty stricken, thank god!

Lastly according to Webster’s dictionary poverty is a condition or quality of being poor; need 2.deficiency; inadequacy 3. Scarcity

Poor is having little or no means of support 2. Lacking some quality, this has to be specific; inferior or worthless

However, when it comes to Tanzania and Africa as a whole I find I have the strongest objection to being poor, on the other hand, Africa as a whole has made a major leap than otherwise thought, contrary to the so called ‘Developed Nations’ notion that this might take a long time! Deficiency? No African people are not deficient rather efficient. Inadequacy? No, Does Africa have a big Affluence in the Global trade? Yes!

Therefore, we are not poor in the context.

Poverty-stricken or Poor Africans does not rhyme in my vocabulary- I call upon my brothers and sisters to declare poverty, poor Africans and any other use unfit for Africa’s public media consumption

Aluta Contunia

Aluta Contunia -Mungu Ibariki Afrika! Mungu Ibariki Tanzania!

My hope hii itachangia kwa namna moja au nyingine kwenye huu mjadala.
 
Bonnie1974,

Mkuu kama ulikuwepo vile....

Unajua mwaka 2000 niliwahi kuyasema haya ktk mjadala mwingine na sidhani kama wengi walinielewa wakati ule kwani ndio kwanza uwekezaji ulivuma sana nchini..

Kila tunachokiona leo hii ni mpango uliopangwa na CCM toka mwalimu Nyerere alipotuondoka..Hii ni baada ya wazee waasisi wa chama na Uhuru wetu kujikuta wanazeeka pasipo kuwa na mali, utajiri na kwamba nguvu zao zote zimefikia kikomo wakibakia maskini kama walivyoachwa na mkoloni..As to say all those years wamefanya kazi for NOTHING!..yaani wanakufa maskini?..

Hapana haiwezekani ndipo walipotunga mwelekeo mpya!

Hizo strategies zote walizopanga toka Mwinyi, Mkapa na hadi leo hii zilikuwa ktk kujinufaisha wao na sii taifa. Tusidanganywe na mtu yeyote kuhusu sijui sera na mipango ya IMF.. Ni wizi mtupu ulitumika wakielewa wazi wanafanya nini..

Hakuna kitu kimefanyika bila mpangilio topka Azimio la Zanzibar wapate kufanya biashara, Kuuzwa kwa nyumba za serikali na mashirika ya Umma na mikataba yote inayohusu sehemu nyeti kama vile Umeme, Mawasiliano na kugawana sehemu majumba ya msajili..Wakati wote wa Mwinyi na Mkapa mambo mengi yalifanyika kwa hatua na uangalifu mkubwa sana kutowashtua wananchi lakini kama tujuavyo siku za mwizi ni Arobaini.. Wakati wa Kikwete wamefikia kukiuka miiko ya Utapeli nayo ni kujisahau. wamekuwa wakiiba waziwazi na ndicho kilichowaponza..

Hadi leo hii bado yapo mashirika ya nje yanayouzwa baada ya miaka mitano kukwepa kodi na wanafanikiwa...Yapo mashirika baada ya wizi hata rais wa nchi anashindwa kuwaambia wananchi ni kina nani wamiliki wa shirika lilihujumu uchumi wa nchi..kama vile wanatutaka tusahau. na kibaya zaidi mashirka haya yanapata baraka za wabunge na viongozi wetu kwamba hakuna utapeli wowote laa sivyo sisi wananchi tulete Ushahidi!..

I mean ni lini serikali ya nchi ikawaomba wananchi wake walete ushahidi wala sii wa maneno against kiongozi ili uchunguzi ufanyike.. Navyoelewa mimi mashtaka ndiyo yanahitaji ushahidi lakini uchunguzi kweli nao unahitaji ushahidi. Leo hii mimi hapa nikiinua simu na kuwaita Polisi niasema kuna mtu anazunguka zunguka karibu na nyumba yangu simfahamu.. watakuja, watachunguza na pengine hata kumhoji mhusika kabla haijafikia maamuzi yoyote yale. leo tanzania uchunguzi unafanyika, kunaonekana kuna Ubadhilifu wa fedha na mali ya nchi lakini kwa sababu mhusika ni ktk team ya CCM.. Utawala unaogopa matokeo ya mashatka hayo ati yatakuja sambaratisha nchi..

tawala zote duniani hupata sifa kwa kuwakamata wahalifu, hupata sifa ya Uobngozi bora sio kwa kuwalinda viongozi wabaya bali kuwaweka hadharani, kuwaadhibu na hata kuhakikisha viongozi hao hawapati tena nafasi ya kuongoza vyombo vya uzalishaji.. Ni adhabu kali sana, sawa na kifungo cha maisha uraiani lakini inaweka funzo zito kwa kila anayetaka kugombea Uongozi kwamba Uongozi sii lelemama..Sii kazi ambayo kila mtu anaweza kuikimbilia na kuacha profession yake kwa sababu kuna Ulaji..

Lakini yote haya sii hoja.. Nini Tatizo letu kama Taifa?..

Ni sisi wananchi wenyewe! wananchi wameshindwa kugundua kwamba kinachowa kii nguoni mwao...wameshindwa kusimama against Utawala mbaya kwa kuogopa nguvu ya dola ambayo bado inatumia milki ya Kidikteta..na kibaya zaidi ni kwamba wachache wanaofikiria kufanya mageuzi wanaopoga kwani wananchi ni wepesi wa kuwaacha nje, wakawakimbia, kuwacheka na kuwabeza kwa sifa zote mbaya ambazo zinawafanya wao kuonekana wabaya kuliko hata Mafisadi wenyewe..

Kwa maskini siku zote, tajiri ndiye mtume wao hata kama ni Jambazi..wao husema mkono mtupu haulambwi!..

Nakubaliana nawe Bwana Mkandara kwa 100%. Kwa kifupi tatizo letu lipo kwenye DHAMIRA, na kama ulivyosema walidhamiria haya tunayoyaona kwa muda mrefu na tunachokiona ni utekelezaji tu. Ingawa ni kweli elimu yetu bado iko chini kwa ujumla lakini isingekuwa sababu kutokuendelea kabisa. Wenzetu wameamua mpaka wao kwanza washibe, na sijui watashiba lini!. Kibaya zaidi inaonekana kuwa kama wamekula kiapo, kwani katika hali kama hii tungetegemea wazee waliopo (Mzee Kawawa, Kingunge, Malecela, n.k) ndio wasaidie kuwakemea. Cha kushangaza ni kuwa wanadiriki hata kutetea, kumbuka Kingunge alivyoitetea serikali juu ya taarifa juu ya EPA wakati zilipotoka hapa JF, na kukanusha kabisa kuwa ni uongo. TATIZO LETU NI DHAMIRA, DHAMIRA ZA VIONGOZI WETU SI SAFI!
 
Tatizo kubwa ni ubinafsi ndani ya chama na serekali yake ,unapokuta serekali inaongozwa kwa kurithiana uongozi ndani ya taifa kama hilo lina hatma mbaya.

Leo tuangalie chama cha mapinduzi na serekali yake wanapokezana uongozi akiondoka baba anapewa mtoto au mtoto anapewa ukubwa fulani kwa sabau baba yake au mama yake alikuwa kiongozi au bado kiongozi huku marafiki nao wanapewa nyadhifa ili mtu uongozi wake usiwe na upinzani wakati wa mamuzi na ndio tulishuhudia serikali ya sadam wa Iraq iliongozwa na ndugu jamaa na watoto wate na hatma yake ndio mtu unalewa kwa madara na kutowa uamuzi anaopenda au wanopenda
 
Let me take rather a different path of throwing everything to our leaders. Let us be honest to ourselves, do we really care? are we kind to ourselves that we want the country to sail in the note! guys each one of us has a part to play in this misery. had we smart enough to tell our leaders enough is enough then we shouldnt be the situation we all are today! Does it a rocket science to know that our leaders are liars and dont live up to their promises! Does require a first degree to understand that the top leadership is messing around? Look at the people who believe in change and have revolutionary ideas, most came or represented the oppressed population! it our duty and call to take the higher authority to task and be responsible. each one of us has a tool to do at least the right thing...if you cant fight them in the street then deploy your arsenals during election. your card can and means alot to all the changes we need and may be, who know, it will discipline those who perceive that they were born to rule and they are there by default! Guys for how long can sit by the mkondo wa jangwani with sad faces, hopeless while they go around preaching the wrong gospel to our pipo. it is a wake up call for the forthcoming election. Make it a point to use it wisely
 
Ndugu yangu sio rahisi hivyo!
Hebu fikiria baada ya yote haya yaliotokea, tayari mikoa imeanza kampeni. Wameanza Dodoma, Tanga tayari, same tayari na inaendelea, watu wanaunga mkono kauli ya Kikwete kutokuwa na mpinzani. Na kama atatokea mpinzani basi ashughulikiwe! CAN U IMAGINE!
 
Orkesumet,
Does it take a rocket science to know that our leaders are liars and dont live up to their promises! Does require a first degree to understand that the top leadership is messing around?
U better believe my brother..It's gotta be...If it ain't green/yellow (CCM) - it ain't in! - Only in Tanzania, and They know that.
 
Ile filosofia ya MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO inajibu swali. Waafrika tumejaa CHUKI, FITNA, TAMAA, UBINAFSI NA UMASIKINI. And all these factors are internal; within somebody, huwezi gundua nani ni safi na nani ni mchafu. We all look clean from outside. Ndio maana swala la uzalendo na utaifa kwetu litakuwa ndoto. Leo hii viongozi wetu wamebase kuombaomba na badala at least ya kuomba misaada ya kutuwezesha kupiga hatua kama science and technology, experts in different fields and education scholorships wao wanalilia misaada ambayo haina manufaa in a long run. Na misaada hii inaishia matumboni mwao. We need to change; Internally and Externally; without that nothing will be possible in Tanzania and Africa in general. Let's check out these countries; Namibia; South Africa and Zimbabwe before Mugabe's crazyness, they were much more developed and that's because they left people who can administrate to do their work and those are the civil migrant investors na maana Mwl. Julias Kambarage Ujamaa ulimshinda maana swala la kujisimamia hatukuliweza. Kweli hizi genes zetu zinahitaji kusafishwa.
 
kubadilisha viongozi kwa TZ ni kama kuota ndoto maana system ilishajengwa siku nyingi kuwezesha watu wachache wateule ku run the show no matter what.Ukijaribu kuingilia huo mfumo utapambana na mkono wa dola na hutajua nini kimekupata.Ofcourse forces of nature (old age, natural death etc)soon zitawafagia walioko kwa muda wote toka tupate uhuru.Tatizo ni kuwa even with that hakuna mabadiliko makubwa yatakuja maana walioko madarakani sasa wanajizalisha through watoto wao, ndugu zao na marafiki.Kama hauko kwenye system mpaka sasa just forget it.Wapya wanaoingia madarakani nao wanajikuta wamerithi mfumo wanaoukuta na hivyo kutokuleta mabadiliko yanayotarajiwa.
Having said this, I am at a loss as to what to do!Wananchi mbona wanapewa elimu through civic education and mbinu nyingine lakini mambo yanabaki yaleyale

WoS,

Ni kweli kabisa uyasemayo....lakini hizo education kwa society zetu baaaado saaana.........trust me sehemu kubwa ya jamii yetu haijaelimika ipasavyo kuhusu...demokrasia.........watu bado wanaamini bila kuichagua CCM pekee basi mambo ni magumu kwao..................na CCM wanahakikisha hilo linaonekana wazi kwa wananchi...........

Dawa nyingine ninayoifikiria ni kuwa.......tupiganie ili vipindi vya ubunge viwe na limit, maximum 2 terms.......trust me hii itaondoa ukiritimba wa watu fulani kujiona Miungu watu.........inaudhi sana
 
Nikumnukuu Waizri mstaafu wa Marekani Donald Rumsfeld,

Donald Rumsfeld said:
There are known knowns. These are things we know that we know. There are known unknowns. That is to say, there are things that we know we don't know. But there are also unknown unknowns. There are things we don't know we don't know.

Kwa tafsiri nyepesi ni hivi:-

- Kuna tunayojua tunayajua - haya ni mambo tulio na hakika nayo kuwa tunayajua.
- Kuna tunayojua hatuyajui - haya ni yale mambo tunayokubali hatuyajui.
- Lakini kuna tusiojua hatuyajui - haya ni yale ambayo hatujui kama hatuyajui.

My take - Ukiwa na uhakika wa jambo, ni halali kulitekeleza na hapo sidhani kama kutakuwapo na tatizo. Ukiwa una hakika kuwa jambo hulijui, ni heri kufanya jitihada za kulifahamu kwanza - ni ujinga kujaribu kulitekeleza kabla ya hapo. Lakini ikitokea jambo hujui kuwa hulijui basi unakuwa sawa na asiyeona wala kusikia - hapo ndipo viongozi wetu walipo. Hawaoni wanatupeleka wapi wala hawasikii vilio vyetu na sisi kama makondoo tunafuata hata kama ni machinjoni.

Tatizo la kwanza ni katiba inayowawezesha hawa kutwaa madaraka kwa hila na kutumia kutumia mapungufu kwenye katiba kuhalalisha matendo yao maovu. Tatizo la pili ni wananchi wanaokubali kuwaachia kuendelea kujikita kwenye uongozi kwa kutumia katiba hiyo hiyo. Historia inatuambia kuwa watawala wa aina hii kamwe hawajui hata lini waachie madaraka kwa hiari yao. Tutabaki kuwafuata kama kondoo hadi machinjoni ? - kwangu hili ndilo swali la msingi.
 
- Finally unaongea reality, yaani hii ndio siasa ya bongo zile zingine hwua ni za kusadikika, heshima mbele kwamba finally umeshuka kwenye ukweli, hapa tupo pamoja mkuu wangu.

FMES!
 
Taifa limefika pabaya

• Ufisadi, rushwa, chuki malumbano vyazidisha uhasama

na Mwandishi Wetu

Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KUNA kila dalili kuwa taifa halielekei pazuri hasa baada ya siku za hivi karibuni kuibuka matukio kadhaa ambayo kwa kiasi kikubwa yameishtua jamii kiasi cha kuhoji taifa linakoelekea.

Matukio ya kiongozi wa nchi kudhalilishwa kwenye mtandao wa kompyuta, malumbano ya wabunge juu ya kuvuja kwa siri za serikali na kuanikwa kwa mishahara yao pamoja na hatua ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kutaja majina ya watu anaowatuhumu kuwa mafisadi ‘papa’ hadharani.

Kutokea kwa matukio hayo katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani kumeelezwa ni mambo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kuliyumbisha taifa.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii wanayaona matukio hayo kama ni mapambano ya hatari yanayowahusisha baadhi ya wafanyabiashara na vigogo wa siasa ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuhakikisha wanafanikisha mikakati ya kuongoza.

Tukio la Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kuwataja baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa maarufu hapa nchini kuhusika na kashfa za ufisadi limezua mtafaruku miongoni mwa jamii ambapo baadhi ya watu wanaiona hatua hiyo ni mapambano ya hadharani baina ya pande hizo mbili.

Mapambano hayo ambayo katika siku za hivi karibuni yamefikia hatua mbaya kiasi cha kuanza kuhusisha uandishi wa habari usiozingatia maadili ya fani ya habari umeonekana kutumika kwa ajili ya kukashfu na kudhalilisha utu wa baadhi ya walengwa.

Vita ya pande hizo mbili vinaonekana kuanza kushika kasi na kuna habari kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliotajwa na Mengi wamejipanga kujibu mashambulizi hayo kwa gharama zozote zile.

Wakati mapambano hayo yakionekana ni ya pande mbili wanasiasa, wafanyabiashara na wananchi mbalimbali wamejikuta ama wanaunga mkono upande mmoja au mwingine hali inayozidisha utete wa vita hivyo.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii wamebainisha kuwa hali hii ya sasa imekuja hasa baada ya ufisadi wa EPA, Meremeta, Richmond na kadhalika ambao ulisababisha baadhi ya viongozi akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa kujiuzulu.

Kujiuzulu kwa viongozi hao na kufikishwa mahakamani kwa baadhi ya watuhumiwa walioshiriki katika kashfa hizo na za matumizi mabaya ya madaraka kumechochea vita dhidi ya ufisadi huku baadhi ya wananchi wakitaka pia Rais wa mstaafu, Benjamini Mkapa, naye aondolewe kinga ili aweze kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Hatua ya Mengi kujitokeza hadharani na kutaka majina ya watu anaowatuhumu kwa kashfa za ufisadi na baadhi ya wabunge kuwachachamalia watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi nako kumezidisha joto na hofu ya mapambano hayo.

Wakati mawazo ya watu yakiwa bado katika mzozo huo, limetokea tukio jingine la kusikitisha katika mtandao ambapo kiongozi wa nchi amejikuta akidhalilishwa kwa picha zisizofaa mbele ya jamii.

Tukio hilo kwa kiasi kikubwa linaonyesha ukosefu wa ustaarabu na maadili kwa baadhi ya watu ambao wameamua kutumia vibaya teknolojia ya kisasa hususan upashanaji habari kwa kutumia mtandao.

Jambo hilo kwa kiasi kikubwa limekuwa likihusishwa na mbinu za kuchafuliana majina hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na kubainishwa kuwa kama hatua za haraka za kuwakamata wanaohusika na mitandao hiyo zisipochukuliwa kuna hatari ya viongozi wengi zaidi kudhalilishwa kupitia mambo mbalimbali.

Moja kati ya tukio la udhalilishaji wa viongozi ni hatua ya kijana mmoja kuamua kumpiga kofi Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, katika sherehe za Maulid zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Daimond Jubilee, Dar es salaam.

Sakata jingine ambalo limeonekana kuwagawa zaidi Watanzania na wanasiasa ni kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma, kuwa kuanzia sasa wabunge na watendaji wote watakaovujisha siri za serikali watashughulikiwa ipasavyo.

Kauli hiyo ambayo ilionekana kumlenga Mbunge wa Karatu Dk. Wilbrod Slaa (CHADEMA) na baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakitumia nyaraka mbalimbali zinazodaiwa kuwa za siri kuiumbua serikali sasa watakumbana na mikono ya sheria endapo watakutwa na nyaraka hizo.

Kauli hiyo imeonekana kupingwa na wananchi wengi kwa madai kuwa sasa serikali inataka kuwa ya kidikteta hasa kwa kuficha nyaraka za ufisadi uliofanywa au unaofanywa na viongozi waliopo na waliomaliza muda wao madarakani.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakiihusisha kauli hiyo kama ni njama za kuficha uovu ambao umekuwa ukipoteza fedha nyingi za Watanzania kupitia rasilimali mbalimbali.

Mshangao huo wa wananchi uliongezeka zaidi pale baadhi ya wabunge walimshutumu hadharani Dk. Slaa kwa kubainisha vipato wanavyovipata wabunge na kutaka fedha hizo zipunguzwe ili zitumike kwa maendeleo ya wananchi.

Baadhi ya wabunge walimtuhumu Dk. Slaa kwa kutaka kujitafutia umaarufu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao jambo ambalo limepingwa vikali na wananchi wanaoonekana kukubaliana na ushauri wa Dk. Slaa.

Matukio haya kwa kiasi kikubwa kwa namna moja au nyingine yanaonyesha kuliweka taifa katika sehemu mbaya na iwapo kama hatua za kurekebisha baadhi ya mambo hazitachukuliwa kuna kila dalili za kutokea mpasuko mkubwa miongoni mwa jamii.

Naye Rahel Chizoza anaripoti kutoka Dodoma kuwa sakata la wizi wa nyaraka za serikali na kuwekwa hadharani kwa mishahara minono na marupurupu wanayopata wabunge kulikoibuliwa na Mbunge wa Karatu Dk. Wilbrod Slaa (CHADEMA), hivi karibuni limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wabunge kuonyesha kumchukia mbunge huyo.

Hali hiyo imejitokeza jana kwenye semina ya maboresho ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma iliyoendeshwa kwa wabunge ambao baadhi yao walionyesha hali ya kumbeza mbunge huyo aliposimama kwa ajili ya kuchangia hoja.

Hali hiyo ilisababisha mwenyekiti wa semina hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje, kuingilia kati na kuwasihi wabunge kupunguza minong’ono.

“Hivi hizi nyaraka zinazodaiwa kuwa ni za siri, kwa nini zinawekwa kwenye makabati ya serikali, naomba Katibu Mkuu aniambie kama ni halali kwa nyaraka za wizi kuwepo katika kabati za serikali,” alihoji Dk. Slaa.
 
Jamani, nathani tumeanza kupoteza Mwelekeo wa Vita ya Mafisadi. Hii Drama ya Mzee Mengi na Rostam it sound very political to me. Hata kama kuna ukweli katika madai yao but they are distructing us kutoka kwenye Vita yetu ya Mafisadi.

Tunaomba Tuendelee kuwashugulikia wote independetly. Naona sasa wanatuibia attention kwa wao kupigana madongo.

What Next, Tunamhitaji Rostam mahakamani, atueleze mambo yote ambayo tunamtuhumu, Kama Mahakam inashindwa kumhukumu, tunaweza kumhukumu wenyewe next year.

Pili Mzee Mengi nae anatakiwa ajibu tuhuma zote tulizo nazo, Mahakamani.

They all need to be answerable to us na si wao kwa wao.
 
Sawa, nakubaliana na wachangia mada waliotangulia kuwa, "Tatizo la Tanzania kama Taifa au nchi ni ukosefu wa Elimu." Sawa, lakini swali msingi tunalopaswa kujiuliza ni elimu ya namna gani tunayohitaji?

Ukweli ni kwamba elimu inayotolewa Tanzania na Dunia ambayo tunayoishi ni vitu viwili tofauti, haviendani. Elimu inayotolewa au mfumo tulionao ni sawa na mfumo wa elimu waliokuwa nao nchi za ugaibuni hasa nchi zile zinazoiendesha dunia kwa mafanikio ya kiuchumi na kiteknolojia karne saba zilizopita. Nachukulia mfano, somo la Historia. Haina maana kwa Mtanzania leo kumkaririsha aelewe kuwa tulitawaliwa na wakoloni kadha wa kadha miaka fulani iliyopita! Haina maana yoyote! Ndio, ni vyema kulijua hili lakini, mtu akishaelewa, ...then, what next?

For what end do we teach our children all these! Our education system and curicula have failed to provide a link forward!I even wonder of the Tanzanian's who were educated abroad and especially when one compares the motives of the nation sending these individuals abroad and what they are doing in return, to this very country! They are still asleep, or may be the systems in which Tanzania as a country is operating is outerly outdated, and thus, needs a complete overhaule! The few elites, and the country they serve, is asleep; and I wonder who will awaken them?

Supposedly, the intellectuals should? Unfortunately they are not because, their education has caused them or rather indused them to an 'idubitable slumber.!Who then will awaken our Tanzanian intellectuals? The answer into this question is the very essence of what is missing in our education because the kind of education needed in this country is not just education but rather the education for improved and sustained development. In simple words, a radical education, and a radical education does not simply happen in a county without having in place Principles of Philosophy as a driving force or engine to the very system of Education.Specifically, Tanzania's System of Education and its Education per se lacks PHILOSOPHY AND ETHICS. The kind of Philosophy being taught in our insitutions is too frigile to create an impact into the nation. To my suprise further, ETHICS as a subject of study is left to some discipline, again it is barely touched. No wonder, moral decadence in the Tanzanian society is a serious issue of concern let alone escalerting incidences of corruption.

Mtoto wa chui ni chui - so, you don't expect a 'naive mother and father' taken lightly to mean our education system in place, to give birth to a 'radical' meaning, extremely logical and smart/shrewed thinkers -or in the Platonic sense, Philosophers who according to Plato, a leader should be the Philosopher, who in the strict sense should be a METAPHYSICIAN.

Therefore, the on goind shortfalls in Tanzanian Education can only be iron-out where PHILOSOPHY WILL BE INTRODUSED AS A MANDATORY SUBJECT OF STUDY ESPECIALL FOR THOSE PUSUING PUBLIC ADMINISTRATION AND POLITICAL SCIENCE. BESIDES, ETHICS, OUGHT TO BE MADE MANDATORY TO ALL DISCIPLINES OF STUDY IN THIS COUNTRY, TANZANIA, BECAUSE ANY COURSE OF STUDY ONE PURSUES, PEOPLE ARE THE ULTIMATE END, AND THUS, ONE OUGHT TO LEARN HOW TO RELATE TO PEOPLE WHO ARE THE ULTIMATE END OF HIS/HER SERVICE.

IT'S TIME TO BRING ETHICS INTO THE LIMELIGHT OF OUR EDUCATION PROGRAMME; AND IN THIS REGARD, WE OUGHT TO HIRE EXPERTS TO TEACH THIS ONOUROUS SUBJECT TO THE TANZANIA PEOPLE STARTING FROM ALL INSTITUTIONS OF LEARNING.

Lack of Ethics and Philosophy in the Tanzanian Society has resulted into what I wish to painfully say, "A FAITHLESS SOCIETY." I can write a book explain this, but in short, all the shortfalls happening in whatever endeavour of our country, Tanzania, wouldn't have happened or be what it is today, misfigured, if individuals concerned were "GOD FEARING" and thus, BELIEVING IN HIM." Because, GOD FEARING IS THE BEGINING OF WISDOM! What then can impart wisdom in the mind of our Intellectuals? None, except ETHICS! It does not matter how repected or educated the person is, if he/she is devoid of Ethical principles. Because, "AN INDIVIDUAL WITHOUT ETHICS IS NO BODY BUT A THING (from Principles of Ethics and Metaphysics)."
 
Last edited:
Tatizo letu kama taifa ni kwamba hatutengenezi vitu. Na hata vile kidogo tunavyotengeneza vina ubora hafifu na haviwezi kushindana kwenye soko la dunia.

Matokeo yake sisi (watawala na watu wa kawaida) ni watu wa kutegemea misaada na hongo (beggars and rent seekers). Pia ni watu wa kutegemea miujiza kutoka kwa miungu yetu. Ndo maana tunarubuniwa kirahisi. Mfano ni ishu ya maalbino. Mwingine ni DECI. Watu wanajenga imani potofu za kupata pesa na mali bila kufanya kazi yoyote ya maana. Hatujiamini.

Mataifa yote makubwa yalianza kwa kutengeneza vitu. Mpaka leo hii mataifa yote yaliyokwisha kuendelea na yanayoendelea yanatengeneza vitu na kuuza nchi nyingine. Yanaongeza thamani kwa rasilimali zao.

Tanzania, kama nchi zingine masikini, zinategemea rasilimali ilizopewa na Mungu. Mfano kilimo, ufugaji asilia, uvuvi, utalii na madini. Thamani tunayoongeza kwenye hizi rasilimali ni kidogo sana hivyo kipato chetu pia ni kidogo sana.

Wasomi wetu hawavumbui technologia yoyote mpya. Hata kuiga za zamani kutoka nchi nyingine hawawezi. Wao kazi kutegemea ajira na siasa tu. Watawala wetu nao kazi kutembeza bakuli. Hawana mkakati wowote zaidi ya kubakia madarakani na kutapanya kile kidogo kinachopatikana. Namna hii kamwe hatuwezi kufika.

Watanzania kama tunataka kuendelea inabidi tuache kupumbazana na tuanze kutengeneza vitu. Malumbano ya kisiasa hayatatufikisha popote. Matatizo yetu ni ya kawaida. Ufisadi, rushwa na matatizo mengine yapo kila nchi. Haya matatizo hayajazuia nchi zingine kutengeneza vitu na kujiendeleza kiuchumi.

Tatizo letu kubwa hatutengenezi vitu. Tutengeneze vitu na maendeleo yatakuja 'automatically'.
 
Kwa mara ya kwanza nakubaliana na yote aliyoyasema PM Pinda hapa chini. Nchi haina viongozi wanaochukia umaskini na ambao wanajua namna ya kuwaondoa wananchi kutoka huko kwenye maisha duni.
Pinda maadili ya viongozi mikoa sita

Na Mwandishi Maalum

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kati ya mambo manne ambayo hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius K. Nyerere aliwafundisha Watanzania, uongozi bora ni jambo linalohitaji kutazamwa kwa umakini zaidi.

Akizungumza na wakuu wa mikoa sita ya Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Kigoma na Rukwa pamoja na wakuu wa wilaya za mikoa hiyo kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara zake mjini Sumbawanga, Rukwa, Waziri Pinda alisema kutokana na mjadala wa kikao hicho hana hakika kama uongozi bora bado upo.

"Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji mambo manne muhimu ambayo ni ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Katika mikoa hii sita mambo matatu ya mwanzo nina uhakika yapo, je uongozi bora tunao? Sina hakika lakini mjadala umeonyesha ni lazima turekebishe hali iliyopo," alisema.

Alisema ardhi ipo na watu wapo na hata siasa safi kuhusu kilimo imewekwa bayana na kwa kina katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2005, sura ya tatu kuanzia ukurasa wa 22 hadi wa 46 na kwa sentensi moja ilani inasema "Kilimo cha Kisasa ndio Msingi wa Uchumi wa Kisasa."

Alisema ilani hiyo imebainisha matatizo ya kilimo cha Tanzania ambayo mengi amekutana nayo katika ziara hiyo.

Alitaja baadhi ya matatizo hayo kuwa ni wakulima wengi kutojua na kutotekeleza kanuni za kilimo bora cha mazao wanayoyalima kukosa tija na mavuno yao kuwa kidogo; wakulima wengi kulima vishamba vidogo vidogo na kutegemea zana duni za jadi, na hasa jembe la mkono.

Aliyataja matatizo mengine kuwa ni upatikanaji wa mbegu bora na mbolea; kutokuwa na mfumo wa uhakika na matumizi yake kutoenezwa kwa wakulima; kazi nyingi za kilimo kutegemea nguvukazi ya binadamu hasa ya wanawake na kuacha maji ya mvua yaendelee kwenda baharini au kwenye maziwa badala ya kuyakinga kwenye visima, malambo na mabwawa kwa matumizi ya watu, mifugo na kilimo cha umwagiliaji.

Waziri Pinda, ambaye amepania kuongoza Mapinduzi ya Kijani, alisema matatizo yote haya yanahitaji kiongozi bora ili yapatiwe ufumbuzi.

"Hapa tunahitaji viongozi wanaojituma kuwasaidia wananchi ili waondokane na umaskini. Wawe ni watu wanaochukia hali ya umaskini walionao wananchi wengi; wanaojinyima kutumia bajeti ya serikali kwa kujinufaisha bali kwa kununua zana za kilimo na kuongeza huduma kwa wakulima," alisema huku akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo.

"Wanapaswa waongoze kwa mfano, kwa maana ya kuwa na mashamba yanayohudumiwa kitaalam na yenye kuwa na uzalishaji wenye tija... Ili kuleta mapinduzi ya kilimo, ni vizuri viongozi wawe na mashamba yao ya mfano ili wananchi waige kutoka kwao.

"Hizi ni sifa muhimu anazotakiwa kuwa nazo kiongozi katika ngazi zote ili kuweza kutekeleza kikamilifu maazimio ya mkutano wa Morogoro."

Waziri mkuu aliitisha kikao hicho cha majumuisho akitaka wakuu wa wilaya wamweleze jinsi walivyotekeleza maazimio 21 yaliyofikiwa katika mkutano aliouitisha mjini Morogoro Oktoba 16 -18, 2008 kuweka malengo ya kuinua kilimo katika mikoa hiyo sita.

Pia alitaka wakuu wa mikoa hiyo waelezee changamoto za jumla katika mikoa yao kwenye sekta ya kilimo na jinsi walivyojipanga kukabiliana nazo.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Celina Kombani; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. Mathayo David; Naibu Waziri wa Fedha, Jeremiah Sumari; na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji; Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Makundi mengine yaliyohudhuria mkutano huo ni wabunge wanne wa mkoa wa Rukwa, baadhi ya makatibu tawala wa mikoa, baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri, washauri wa kilimo wa kila mkoa na makatibu wa CCM kutoka kila mkoa.
 
Back
Top Bottom