Tanzania: Nini tatizo letu kama Taifa? Tunajikwamuaje?

Ndugu zanguni, uzalendo, nafikiri hiyo ndiyo charisma, kila mtu anao kama mimi na wewe sasa hivi tunapotoa mawazo yetu. Sisi hapa is true tunaweza tukawa wazalendo kwa sasa kwa hali tuliyonayo. Binadamu is guilty, naturally, halafu kuna kitu kinaitwa temptation. Uzalendo unakwishaje; ni pale mtu anaona kuna loophole kuwa anaweza kufaidika hata kwa haramu bila madhara yoyote. Kama watu ni wajinga basi wenye akili ndiyo hufaidika. Waulize waasia wote au westerner wote (I mean wote) wanakuja Africa kuchuma kwetu, moja ya sababu kubwa ni kuwa sisi tumelala. Yaani hatuna elimu, hata wale wenye elimu ni rahisi kununuliwa kwa sababu wana uelewo mkubwa kuliko watu wao, lakini wnauelewo mdogo kuliko hao foreigners.

Waasia au Westerners wanaokuja huku wanataka kuonana na waziri au director au Rais, kwa nini? Unajua jibu. Sasa kama sisi tungekuwa tumelimika wengi na ile quality education ingekuwa vigumu sana viongozi wetu kupuuza sheria. Sheria zinapuuzwa kwa sababu sheria hizo wanazijua viongozi wengi, wengi wao wana elimu, na wale wananchi weng hawajui sheria. Hivi tunajua kuwa gari likipinduka watu wakifariki inabidi walipwe insurance, hivi kuna wangapi wa hawa wanachi ambao huwa wanadai insurance!! mfano mdogo sana huu, ambao unaonyesha watu wanasukumwa tu bila ya elimu na wanakubali kila kitu.

Unaongelea kuwa wasomi ndiyo walifanya mikataba, je, hivi wewe unajua nchi za Africa, kama Tanzania kuna gap kiasi gani kiongozi na mwananchi wa kawaida. Hivi jamani Tanzania ya sasa ina middle class? Mimi naona tu kuna walalahoi na viongozi wao. Walalahoi ndiyo wamechanganyana humo humo wenye elimu ambao ni wachache na wale wasio na elimu wengi. Hiyo mikataba husainiwa tu na sisi aidha kuarifiwa magazetini au la baada ya kutokea scandal. Semeni jamani ile ya IPTL, ya Mkapa kupewa million tatu dollar, nani alijua? NSSF, nk nk Hata ile ya IPTL ingekuwa siyo yule mzungu kuandika ule ushahidi hatungejua.

Elimu kuzungumziwa ni neno pana sana, ubora na hata dicipline, je elimu yetu inatufaa, tunahitaji exchange na wenzetu? Hata wachina baada kujifungia miaka zaidi ya 50 ilibidi wafungue ili wafanye exchange, akili zao zinafumbuka. Elimu yetu haitoshi.

Clinton ni msomi sana alikuwa professa, blair kasoma, na wanaeleweka. Watu wao wamesoma na wako informed. Hata kama sisi watu wa nchi hii wangekuwa informed basi tungekuwa mbali.

Tuache ubishi, hasa nyie mlie majuu mnajua wazi kuwa huko mliko mtiririko wa information upo babu kubwa, na mtu ambaye anazembea hana nafasi.

Solution is massive investment in education, including adult education. Access to information.
Education is liberation of mind, information is power!
 
IO, hivi unataka kuniambia tukimpa nchi Profesa Lipumba, nchi itaendelea? Je tukimpa nchi Masumbuko Lamwai nchi itaendelea? Vipi kuhusu Dr. Malyamkono? IO unachanganya mambo access to information is not the same as education! The way I understand what ur talking about ni formal education. Kwa maoni yako, formal education itatatua matatizo yetu yote.. hilo nalikataa! Kama mtu hajui kuongoza na hana kipaji cha kuongoza basi hata kama ana PHD na ni professa wa Chuo Kikuu zaidi duniani, hataleta tofauti yoyote!!!
 
Mwanakijiji tafadhali mie bahati mbaya sio mwalimu, halafu lugha yangu nayo siyo nzuri; lakini nathani wastani naweza nikaeleweka. Sijasema tunahitaji substitute ya viongozi wenye elimu. La hapana, mie nasemaje watanzania wengi wangekuwa na elimu halafu wawe na access to information wangekuwa mbali. I mean viongozi wanatumia loophole ya wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuwa yes people, no access to information na kufanya maovu yao. You make me sick if a learned man can say education and access to education are separable. As I pointed out we need massive investment in both formal and informal education. I mention also adult education. Kipaji cha kuongoza? Sasa hapo ndiyo unaleta superstition na metaphysics, kwenye democratic system hakuna kipaji; kama ni kipaji basi ni pale mtu anapomwaga sera zake na watu wanamuelewa na kumpa kura. Wapiga kura wanakuwa wanaweza kureason. Siyo hawa wapiga kura wabongo majority ambao hawana quality education and access to information. Gazeti la Kasheshe lianasomwa na 90% ya watanzania, nalo ndiyo money maker. I never bought kasheshe or Komesha. Sasa wasomaji wa kasheshe au komesha wanapata information ipi. Gazeti la Daily news linanunuliwa sana tu wakati simba na yanga wanamenyana.

I believe in one thing "lack of education denies us access to information" na uelewe kuwa Umaskini is an enemy of environment" Again massive investment needed in education.

Education na Information vinaenda pamoja. Hata labda kwa kiswahili kizuri tuseme kisomo kinakupa mwanga, halafu information inakuodoa ushamba.
 
Mzee Mwanakijiji said:
Kama viongozi hawana uzalendo, je watu wa chini watakuwa nao!! Tatizo ni viongozi!!!!

Mwanakijiji,viongozi nao ni wananchi ila sie wananchi wa kawaida ndio tumewakabidhi dhamana ya kutuongoza.Tukisema viongozi ndio tatizo basi labda tunataka kusema kuwa process nzima ya maendeleo ni top to down,wakati mimi nadhani ni down to top.Tunaanza na wananchi wa kawaida ambao ndani yao watatoka viongozi badala ya kuanza na viongozi ambao ndani yao watatoka wananchi wa kawaida (viongozi wanakuwa wananchi wa kawaida only kwa kustaafu,kunyimwa kura au kufukuzwa madarakani).Sasa kama uzalendo hauko katika level ya mwananchi wa kawaida,how can kiongozi-ambaye essentially ametoka ktk kundi hilo la wananchi wa kawaida- ataweza kuwa mzalendo?Hivi mtu anajifunza kuipenda nchi yake akiwa kiongozi au akiwa mwananchi wa kawaida?

Pengine mfano huu utasaidia.Ili kuwa na national team nzuri nadhani tunahitaji timu bora za kawaida eg Simba na Yanga bcoz from them ndio kocha anapick timu ya Taifa.Kulaumu timu za kawaida kwa vile tu timu ya Taifa ni mbovu itakuwa kichekesho.Mfano huu ulinganishwe namna hii (timu za kawaida ndio wananchi,timu ya Taifa ndio viongozi).

Simple logic,isnt it?
 
Elimu bila uzalendo ni kazi bure kwa sababu watu wasio na machungu na nchi yao hata wakielimishwa watapeleka nguvu zao zaidi kwenye kujineemesha wao na si nchi yao.Nilitoa challenge kwa Mzee Mwanakijiji atusaidie kupata takwimu za watanzania ambao wanapatiwa nafasi za kwenda nje kujiendeleza kielimu na matokeo yake wanapotelea hukohuko.Why wachina au wairani hawafanyi the same?Bcoz wana uzalendo.Kwao,ni bora kurudi makwao na kukosa MTV lakini waendeleze nchi yao hoping that siku moja watatengeneza kitu bora zaidi ya MTV (plz note:MTV imetumika hapa ku-symbolize luxurious western lifestyle)
 
Nimeona hoja za wengi, nakubaliana na Mwanakiji. Elimu si hoja hapa.

kuna mtu anasema Tony Blair kasoma elimu yake ni degree moja tu ya sheria. kwa nchi iliyoendelea kama UK degree moja ni kitu cha kawaida sana.

kabla ya Tony BLAIR kulikuwa na John Major tena ametoka eneo la masikini sana na wahuni Brixton huyu bwana alikuwa konda kwenye basi hana shule kabisa lakini hadi 1997 ndio alikuwa Waziri mkuu je UK wanaupungufu wa wasomi?

ukienda kwa watu waliofanikiwa mfano Richard Brandson tajiri mkubwa UK na anamiliki makampuni mengi pamoja na virgin Airline hana elimu kabisa.

hata kiongozi anayekumbukwa na Waingereza wengi na kusema wanadeni kwake ni Waziri mkuu Churchhill ambaye amefanya makubwa kwa waingereza na hakuwa na elimu.

tizama wasomi wengi tuliona nao nyumbani wamefanya mabadiliko yapi? je wamekuwa part ya kusolve problem au ni creater wa problems zaidi? hao wasomi tizama familia zao tu wanashindwa kuzifundisha tabia ya kuishi na watu. kifupi hawana impact kwa jamii yao. na mfano mzuri tizama taratibu za siku za nyuma aidha mjini au kijijini wazee wetu walikuwa na utaratibu mzuri kwa kusaidiana kwenye shida na kuleta suluhu kwenye kila jambo lao waliishi kama community- lakini wasomi wetu leo hata jirani yake hamjui anaishi vipi?

kuna mchangiaji anadai KILIMANJARO wameelimika ndio maana kuna upinzani hilo sio kweli upinzani wa kweli uko Zanzibar mfano pemba toka Diwani hadi wabunge wote wapinzani jee sababu ya elimu au uzalendo kwa nchi yao?

pia nenda Mbagala huko siku zote CCM inapata taabu kuwaelimisha wananchi kuchukua kura na kuna mitaa ambapo wenyekiti wa serikali za mitaa wote kutoka upinzani je watu wa mbagala wamefanya haya kwa kuwa na elimu zaidi?

Zanzibar wako tayari kutoa hata roho zao kwa maslahi ya nchi yao jee wapinzani waliopo moshi wanaweza kujiumiza sababu ya haki zao?

Kama mlifuatilia vizuri Kampeni ya Rais Kikwete sehemu alizopata taabu na hata kuzomewa ni maeneo ya Lindi hasa Kilwa, Pwani na Mtwara. tena pwani ndio anakotoka na Lindi ni ukwenu lakini vijana walisahau yote haya. jee maeneo haya wameelimika zaidi?

Kwanini hao wanaoitwa WASOMI wamepelekwa kwenye semina -Arusha?hawajui kuishi na watu.

Wasomi hawa wametupeleka na kuua mashirika kama Gapex, NDL n.k. Je, nani anamjua mwenyekiti wa wenyekiti wa CCM aliyekuwa na nguvu sana na aliyekuwa karibu na Mwalimu Nyerere? Alikuwa marehemu mzee Masudi Mtandika na hakusoma hata darasa moja lakini hawa walikuwa kwenye chama chenye maadili (uzalendo) mchango wa Bibi Titi Mohammed je akina Nchimbi na PHD zao wanaweza kufanya yaliyofanywa na hawa miamba?

Utakuta mtu anasoma Accounting halafu anakwambia kozi hii ukimaliza baada ya mwaka tu umejenga! yaani hata nia ya kusoma kwetu ni kufikiria jinsi ya kuiibia jamii.

Tizama leo wanaoendesha nchi ndio hao wasomi wao walisoma bure leo wanaweka ada za shule hadi milion 2 kwa sekondari wala hawana woga kuwa vipi kizazi kijacho kitaopata elimu kama walivyopata wao? hakuna anayeshtuka.

Wazee wetu walikuwa wakiufikiria UMMA wote ndio maana maisha baada ya kushikwa na hawa mnaowaita wasomi yamekuwa mabaya zaidi. ni bora tungesipata uhuru atleast tungepiga hatua.

Je, Rwanda wanakouana na Burundi ni sababu ya kusoma? Maana tumeambiwa ukisoma huburuzwi.

Kifupi UZALENDO ndio dira ya maendeleo. hata ukipeleka watu wote Harvard lakini kama hakuna uzalendo hamna kitu.

UK wamepiga hatua na watazidi sikia (Mlalahoi) ni sababu ya uzalendo. Kwani kila mtu nafikiria kuleta maximum Impact kwa jamii yake- mzungu haoni raha bila kusaidia mtu aliye na taabu
ndio utaona Gap year mtu nakwenda kusaidia hadi Namibia- kwetu sisi roho mbaya na chuki.
mfano Magufuli ni msomi lakini amesema ukiwa na kiwanja ujenge baada ya miaka mitatu. jee sera hii inafikiria WTZ walalahoi? Fikiria mwl wa primary school amepewa zawadi ya kiwanja anaweza kujenga ndani ya miezi 36?

JEE huko UK uliko. umeona viongozi wakijiuzia nyumba? jee umeona viongozi wana msururu wa mashangingi? Mfano mzuri meya wao Livingstone anatumia public Transport-train kwenda kazini kwake.

Je, wabunge wana mashangingi?

Umeona mabosi ofisini wana msururu wa masecretary? Je, kuna wapika chai? Na vipi speed ya kazi?

Je, waziri wa mambo ya ndani aliyejiuzulu.David Blanket alijiuzulu kwa kiasi gani cha harufu ya rushwa? alikuwa ameweka hisa kwenye kampuni chini ya pound elfu kumi. Je, hayo yanafanywa na wanasiasa wetu?

Maofisa wa idara nyingi nchi za Ulaya hasa UK DEGREE kwao si sababu ya mtu kupewa kazi. na hata watumishi wengi hawana degree lakini tizama ufanisi wao.

Katika CV kama mtu hakuwahi kuvolunteer anaona taabu. Binasfi ninae jirani yangu ana PhD lakini majirani wote haongei nao na hata mabaraza mawili tofauti ya wazee ktk eneo letu yamemfukuza. Je, mtu ana PhD kumbe hata adabu ya kuishi na watu haijui?

Ndugu zangu uzalendo ndio msingi.
 
Kimsingi nakubaliana na mawazo ya watu wengi hapa,matatizo tuliyonayo ni mengi na complex,matatizo ya kimsingi yamezaa matatizo mengine ambayo yametusababishia tukwame katika "poverty circle" na kujenga utamaduni ujulikanao kitaalamu kama "culture of poverty".

Tatizo la kimsingi kabisa ni ELIMU,elimu tunayoizungumzia hapa si ile ya kusoma ili upate cheti ili ujulikane kama msomi. Tunahitaji kuwa na mfumo mzuri wa elimu ya UWEZESHAJI, kuanzia elimu ya msingi ambayo inawezesha watu kuondoa ujinga kwa kuwazesha kujua kusoma na kuandika na kwa kujiandaa kwa elimu ya juu zaidi, tunahitaji pia elimu nzuri za sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu ambayo inawezesha watu kufikiri na kufanya analysis na kuweza kutumuia ule ujuzi na maarifa waliyonayo katika kutatua matatizo yanayoikabili jamii yetu.

Ukiangalia katika mfumo wa elimu ya tanzania utakuta kuna mapungufu mengi saana, tuna wasomi wengi sasa hivi, mfano wahandisi, wachumi, wataalam wa kilimo nk, lakini wengi wao hawana uwezo wa kutumia elimu yao katika kutatua matatizo yanayotukabili,si jambo lakushangaza ukakuta mhandisi wa umeme kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akashindwa kubadilisha "tubelight" na wakati huohuo is "proud to be an engineer", haya ni matokeo ya mfumo tulionao ambao wanafunzi wanastruggle kumaliza shule na kupata vyeti au titles instead of knowledge.

Na mbaya zaidi hii trend mpya iliyoingia kienyeji ya watu kujinunulia title mbalimbali mfano "DK" ili aweze kujipatia "ULAJI" na si ajabu nasikia hata baadhi ya mawaziri na wahadhiri wa vyuo vikuu na wamo katika mfumo huu.

PILI, nakubalia na mwanakijiji kuwa tatizo la UONGOZI. Tusipoweza kupata viongozi wazuri, waadilifu na wazalendo hatutaweza kubadilisha mfumo huu tulionao, mfano rahisi ni jinsi gani tulivyo bahatika kumpata mwalimu Nyerere (rip) ambaye alikuwa na sifa zote za kiongozi,mwalimu alijua umuhimu wa elimu kwa jamii ya watanzania ndio maana mara alipochukua madaraka aliweza kutaifisha shule zote na kuruhusu watanzania wote bila ubaguzi kupata elimu bure kuanzia msingi mpaka chuo kikuu, na kulikuwa kuna idadi ya watu wengi walikuwa wanapelekwa kusoma nje na alihakikisha wote wanarudi kulitumikia taifa.

Kwahiyo tunahitaji viongozi wazuri katika taifa hili, na viiongozi wenye sifa kama za mwalimu wapo isipokuwa hawapewi nafasi sikuhizi na wengi wamekuwa waoga na wamekosa ujasiri kwa kuwa na hofu ya utawala uliopo.

TATU nakubaliana na mchangiaji hapo juu kuwa kuna makosa mkubwa yalitokea wakati tunabadirisha kutoka mfumo wa ujamaa kwenda mfumo wa ubepari. Viongozi wa CCM wakati huo walikuwa "reckless" na walipeleka mambo mengi kwa pupa. Nakumbuka mwalimu alilizungumzia hili aliposema kuwa viongozi wetu baada ya kwenda zanzibar na kuja na AZIMIO LA ZANZIBAR, mambo mengi yalianza kwenda kihorela, walifungua mianya ya rushwa na kila mtu hasa viongozi ndio kilikuwa kipindi cha chukua chako mapema kiasi kwamba sasa tulipofikia ni pagumu, kwasababu sasa hivi mambo mengi yameshakuwa ni mazoea, rushwa imekuwa ni sehemu ya maisha,utapeli,udanganyifu na kutojali yamekuwa ni mambo ya kawaida katika jamii hili, kwasababu misingi mingi ambayo ilikuwa inajengataifa hili ilivunjwa,
mfano kuvunjwa kwa JESHI LA KUJENGA TAIFA, hiki chombo kilikuwa kinasaidia sana katika kujenga raia wazalendo, wenye ujasasili, wachapa kazi na watiifu.

Lakini toka chombo hiki kivujwe unaweza kuona tofauti kati ya kizazi kile kilichopitia JKT na hiki ambacho hakikupitia huko.

Nakubaliana na hoja ya kuwa tulihitaji mabadiliko ya kwenda sambamba na uchumi huria lakini tulihitaji kuwa makini zaidi.

NNE mfumo wasiwasi wa demokrasia tulionao,watanzania bado hatuko "serious" na bado hatupo makini hatuji nini tunataka, tuliamua wenyewe kutoka kwenye mfumo wa chama kimoja kwenda mfumo kwa vyama vingi karibu miaka 15 iliyopita, lakini unaweza kuoana katika kipindi hicho hakuna hatua yeyote tuliyopiga mpaka sasa.vyama vingi mpaka leo havina tofauti wakati vilipoanza miaka 15 iliyopita na wala hakuna dalili kama vitabadirika katika miaka 15 ijayo.sisi watanzania wote kwa ujumla tunawajibu wa kuviimairisha vya hivi kwa kuwasupport kwa kila hari.

Tusifikiri kuwa vyama hivi ni mali binasfi ya kina freeman mbowe,hivi vyama ni kwa faida yetu sisi watanzania na sisi wote tunawajibu wakuviimarisha vyama hivi, wapo vijana waliotoa mfano thabiti kama John Mnyika na wengine, tunahitaji sisi wengine tuwaige wao kwa kujiunga na kuwa wanachama thabiti wa vyama hivi, na kutoa michango ya kila hali pamoja na kipesa.

Chama Cha Mapinduzi kina ajenda tofauti kabisa na mfumo huu tulionao, ajenda yao ni kujiimarisha zaidi na kusambaza propaganda kuwa hakuna chama mbadala zaidi yake, na sababu za hili ni wasiwasi wa viongozi wa ccm kupoteza ulaji, maana wanajua kupitia ccm ndio wanaweza kujichukulia pesa kirahisi na kufanya yale wanayotaka bila kuhojiwa na bila bugha mpaka wanapokufa.

Tatizo la vyama hivi ni pesa, hata hawa viongozi tunaosikia wanahama kutoka chadema kurudi ccm, hamna cha zaidi wanatafuta chakula.

Kama CHADEMA ingekuwa inatoa mishahara minono watu wengi wangekimblia kuongoza vyama hivi. Kwahiyo ni muhimu kwa viongozi wa vyama vyetu vya upinzani wajifunze kutoka vyama vingine ni jinsi gani ya kuongoza mapato ya vyama. Wasitegemee ruzuku kutoka serikali ya CCM, instead waangalie ni jinsi gani wanaweza kucreate source of income na kuwa na property za kueleweka,then automatically vitaanza kuvutia watu.

NA kwa kumalizia kwakweli sisi watanzania tunahitaji UZALENDO na nchi yetu, katika sekta mbalimbali mambo yanaendeshwa kibinafsi na ki-mimi mno. Yaani mtu yuko tayari kuliibia taifa mabilioni ya pesa ili ale yeye na watoto wake huku mamilioni ya watanzania wakifa na njaa,
hata hawa wanafunzi wa vyuo vikuu ambao leo wanaomba mikopo yao lakini wakishamaliza shule hawafikirii kurudisha ile mikopo ili na wadogo zao nao waje wakope,we need to be responsible.

Namalizia kwa msemo wa nyerere

WE CAN DO, PLAY YOUR PART.
 
Tafadhali natanguliza kusema kuwa post hii hapo juu nimeiandika bila kusoma hoja za wachangiaji wachache waliotangulia.

Kwahiyo huenda ingekuwa na mtiririko tofauti kidogo ili kukwepa kurudiarudia, ahsante.
 
Jasusi,

Elimu tunayosema jamani si ya viongozi tu!!, elimu kwa umma, wananchi waweze kufunguka matongotongo, waweze kuwa tambua viongozi wazuri kwa wabaya, waondoke ndani ya asilimia 80%, nchi yenye wananchi wenye elimu na demokrasia rais hawezi kupata 80%!!!

Jamani wananchi ndio wa kulaumiwa, wamelala hawana shule!, tayari viongozi hawana uzalendo sasa? ELIMISHA WANANCHI MUONE.

FD
 
Hakika huu ni mjadala mzito sana. Ni kweli elimu ni tatizo,watu ni tatizo na viongozi na siasa yenyewe ndio ovyo kabisa! Tumeachia watu wasio na uwezo kutuongoza.

Kwanini mjadala huu usihamie kwenye utatuzi pia? je matatizo yetu hayatatuliki? hatuwezi kutoa mchango wowote kubadili mambo? tumekata tamaa? Ni jukumu la nani kubalusha hali hii?

Si imesemwa kwamba ouvu hushamiri pale ambapo watu wazuri(makini) huamua kukaa kimya. Ni kweli nchi yetu haina dira ni kweli hatuna viongozi makini.

Masuala haya yote,utatuzi wake unarejea kwenye siasa? ni wakina nani wapo kwenye siasa? siasa ta Tz zina sura gani? tunasukumaje mabadiliko katika hali hii? hakuna njia nyingine mbadala,ili tuwe na dira, ili tuwe na elimu kuna ulazima watu makini kuingia kwenye siasa.Suala ni kivipi? itawezekanaje? Tutafakarini basi ili tuwe na siasa zitakazo sababisha mruko,ili tuwe wanasiasa wenye upeo na uzalendo. Kuna haja ya kuingilia.

"kila kizazi lazima kitambue utume wake,na ni ama kiutekeleze au kiutelekeze"
 
Eric,

Inabidi tuwe na mipango ya muda mrefu, Serikali iongeze budget ya elimu angalau 35% ya budget yote. Hela hizo zifuatilie quality ya elimu na iongeze idadi. Elimu. Wananchi wakiwa na elimu rais kuwaelimisha mambo mengi kama kulipa kodi, sera etc etc.

FD
 
Wazee,
Inawezekana ni kweli tunahitaji "ELIMU" kama suluhisho la matatizo yetu. Lakini Elimu hii ni lazima iwe "defined": yaani iwe ni elimu itakayotujengea UZALENDO; watu KUJIAMINI na hivyo kutokuwa na UOGA (rejea kwa mfano hoja za mjadala kuhusu maswali kwa JK New York), watu kujua HAKI ZAO; itakayowafanya watu wawe na UBUNIFU (matatizo mengi ya wananchi wilayani na vijijini hayahitaji kusubiri ziara za WM au Rais ndo yapatiwe ufumbuzi); elimu itakayowapatia watu wetu UPEO wa mambo na UWEZO wa KUFIKIRI kwa kina (kila mara husikia tukiambiwa Watanzania tu "wavivu wa kufikiri") na kuchambua mambo (Independent and Critical Thinking); elimu itakayoibua vipaji mbalimbali iwe ni katika siasa na uongozi, au sayansi na utamaduni; elimu itakayotupatia VIONGOZI wa umma na si WATAWALA; elimu itakayojenga MAADILI kwa WANANCHI na VIONGOZI; elimu itakayotupa UMOJA kama Watanzania kwanza badala ya Ubinafsi, Ukabila, Udini, Ukanda, Umajimbo na vitu vingine ambavyo vinaweza kutugawa; na elimu ambayo itafanya siasa iwe ni kitu cha kujivunia badala ya sasa ambako imekuwa kimbilio na kichaka cha walafi na wabinafsi (kuanzia wasomi, wafanyabiashara, majambazi) na kuishushia hadhi na kuwa na msemo kuwa "Siasa ni Si Hasa", kitu cha ujanja ujanja.

Iwe elimu itakayotuwezesha kuyatawala MAZINGIRA yetu kwa manufaa yetu. Nadhani wengi wetu, kama taifa, elimu tuliyonayo haijaweza kulisaidia sana taifa letu na ndiyo maana kila kukicha ni matatizo tu, kila kitu mpaka aje Mfadhili!

Tukikiri upungufu tulionao, tukatambua kuwa kweli tuna matatizo, na tukakubaliana kuwa tunahitaji kuangalia upya "elimu yetu ya darasani", kisha tukakubaliana kuhusu elimu tunayoitaka, tunaweza kukubaliana jinsi ya kuipata elimu hiyo.
 
Mzee Mwanakijiji said:
Je Kikwete ni msomi au ni kiongozi?

Nadhani kwa upande mmoja ni kiongozi (he's the President,and that's uongozi).As to usomi,nadhani hili linahitaji mjadala mpana zaidi.Je usomi ni idadi ya shahada alizonazo mtu,jinsi anavyotumia elimu aliyonayo regardless of its level,au ujuzi wa mambo bila kujali kama mtu amekwenda shule or not.Pengine JK ni msomi pia kwa vile ana BA,if holding a BA ni usomi.Pengine ni "kilaza" kwa vile hatujui kama BA hiyo ilikuwa first class or not.Au pengine si msomi kwa vile makamu wake ni PhD holder,na mawaziri zake kadhaa ni maprofesa.Hey,who is "msomi" and what is "usomi"?
 
JAMII NZIMA YA WATANZANIA TUNAHITAJI ELIMU YA AINA HII. LAKINI KWA BAHATI MBAYA VIJANA WENGI WANAOSOMA KOZI NYINGINE HAWAMBIWI HUU UKWELI BALI HUU UKWELI WANAAMBIWA WALE WANAOSOMEA UALIMU!


(1) Elimu ni lazima kwanza IWAFANYE WALIOSOMA WAJUE KUWA WAO NI SEHEMU YA JAMII NA SIYO WATU TOFAUTI NA KWAMBA WAO WANAPASWA KUISAIDIA JAMII KUJIKWAMUA KATIKA SHIDA ZAO KIJAMII HASA.

(2)ELIMU NI LAZIMA IWE EDUCATION FOR LIBERATION(UKOMBOZI) WA KIAKILI.

WENGI WETU TUMESOMA LAKINI NOT MENTALLY LIBERATED BADO NI WAFUNGWA WA MAWAZO. Therefore our minds should be liberated first.


(3) TUNAHITAJI ELIMU FOR EMPOWERMENT. HII NI LAZIMA IKUPATIE POWER TO DECISION MAKING. HII NI VERY CRUCIAL WENGI HAWANA NA WALA HAWAJUI KUWA KAZI YA ELIMU NI KUWAFANYA WAME NA NGUVU ZA KUFANYA MAAMUZI YA MAANA KWA MASLAHI YA TAIFA NA KULINDA UHURU WAO BILA KUTISHWA NA VIKARAGOSI AU VIONGOZI WEZI.


(4) TUNAHITAJI EDUCATION FOR CONSCIETISATION. HII ITAKUSAIDIA KUWA CONSCIOUS OF YOUR PROBLEM AS AN INDIVIDUAL AND OUR PROBLEMS AS A SOCIETY. ELIMU IKISHA KUFANYA KUWA NA UTAMBUZI WA MATATIZO YAKO THAT WILL BE SUPERB. LAZIMA IKUWEZESHE KUJUA KUWA UNAHITAJI KUKOSOA NA KUKOSOLEWA NA LAZIMA UKUBALI. UKIONA HUTAKI KUKOSELEWA UJUE UNA TATIZO LA UKOSEFU WA HII SILAHA.

BAADA YA HAPO HUWA TUNASEMA ELIMU IKISHA KUWEZESHA KUJUA MATATIZO YAKO NA YA JAMII UNACHOTAKIWA KUFANYA NI NINI??

NI KUCHUKUA UAMZI/MAAMUZI(TAKE ACTION(S))

WHY??

TAKE ACTION(S) TO TRANSFORM THE SITUATIONS/PROBLEM(S)

IN ORDER TO BE FREE OF THOSE PROBLEMS AN INDIVIDUAL IN PARTICULAR OR SOCIETY IN GENERAL!!

KWA HIYO WATANZANIA WENGI HAWANA NA HAWAJUI HAYA BALI WACHACHE SANA LABDA 0.001% TENA WENGI WALIOBAHATIKA KUPTA ELIMU I'M AFRAID TO SAY YA UALIMU. NA PIA KATI AYAO NI WACHACHE WANAOLEWA AU KUKUBALI KUWA ELIMU INAWEZEA KUFANYA YOTE HAPO JUU.


TANZANIA TUNA MATATIZO KAMA YA RUSHWA HILI LINASABABISHWA MATATIZO MENGI SANA.

MFANO WATU KUKOSWA HUDUMA MUHIMU MAHOSPITALINI, KAZINI NK, KUINGIA MIKATABA ISIYO NA MASLAHI KITAIFA KUNAADHHOFISHA UWEZO WA SERIKALI KUPTA FEDHA/AU PATO LA KUTOSHA NA MATOKEO YAKE NI WANAFUNZI KUKOSWA NAFASI ZA KUSOMA ELIMU YA JUU.

THEREFORE WHAT SHOULD BE DONE TO TRANSFORM THE SYSTEM??
 
Mzee JK, ni kiongozi naturally I mean hiyo lazima tumpe credit yake wheree it is due, anao uwezo wa kuongoza yaani yeye kuwa mbele na wengine wakafuata nyuma,

ila swali ni kwamba anao uwezo wakuongoza katika haya mazingara ya leo ambayo ni very complicated?

One thing for sure ni kuwa sio msomi, yaani JK sio intellectual,

Halafu viongozi wakuu wa nchi yetu wanasisitiza kuwa eti Tanzania bado ni nchi ya ujmaaa na kujitegemea mpaka kesho, wanasema kama anayetaka kutafsiri tofauti ni RUKHSA, lakini as far as CCM is concerned bado ni siasa ile ile ya ujamaa!
 
Back
Top Bottom