Tanzania niliyoifahamu na kuielewa imepotea tunahitaji malaika kuirejesha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania niliyoifahamu na kuielewa imepotea tunahitaji malaika kuirejesha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jul 18, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tanzania ambayo mtu alihukumiwa na umma kwa udhaifu wake leo haiko. Bali imezaliwa Tanzania ambayo dini kwanza hoja baadaye. Ukimshambulia mkosefu wa umma leo hakikisha uko karibu na shimo la kukimbilia kama yule unaemshambulia mnatofauti ya kiimani kwani watu hawataangalia ubora wa hoja yako bali watakuuliza wewe ni wa dini gani, kama hawakuulizi watasemezana mpaka wakujue ndipo waanze kukupinga. . Dini na kabila vimekuwa ni vigezo vya kutetea uovu. Mungu wa wapi anatusikiliza kwa hilo. Udhaifu wa kiongozi ni wake si wa dini wala dhehebu lake. Udhaifu wa Lowasa hauwezi kuwa kashifa kwa walutheri, udhaifu wa Kikwete si kashifa kwa waislamu, udhaifu wa Pinda si fedheha kwa wakatoliki. Kitu gani kimetufikisha hapa tulipo, mwenyekiti wa Chadema akishambuliwa na watanzania atetewe na chama chake vivyo hivyo kwa Mwenyekiti wa CCM akishambuliwa na watanzania atetewe na wenye dhamana hiyo ambao ni wanachama na viongozi wa chama chake. Kikwete, Lowasa , maalimu Seif, Karume na wengineo wengi ni watumishi wa kisiasa, na siasa ni uzandiki, unafiki, fitina na uzuri kidogo. Viongozi hawa ni waumini wetu lakini si alama ya imani zetu. Wakishindwa wapokee mashambulizi kwa waliowachagua. Viongozi wadini wakae mbali eneo hilo sio lao watapakwa matope. Wao wanapoingilia ugovi wa viongozi na wananchi walio wachagua viongozi hao ndio hasa udini unapoanzia. Haijarishi ameshambuliwa na watu wangapi yeye amekubali kuwa kiongozi, uchache si alama ya kubeza dawa ni kuwajibu.


  Viongozi wa kisiasa kauli za kidini zinazowapendelea zikataeni wazi ili mzibe mianya na nyufa za kujenga udini
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tabia ya udini na ukabila inaletwa na ccm wakiona chama kina sera nzuri na kinaungwa mkono na wananch weng wanazusha kuwa ni cha kidini/kikabila, miaka ya nyuma cuf kilikuwa chama chenye nguvu sana na kiliungwa mkono na watanzania wengi ikiwemo mimi lakini ghafla ccm ikawapiga vita waziwazi kuwa ni chama cha kidini na maskini watanzania wakaamini na kuichukia cuf ikiwemo mimi, sasa chama chenye nguvu ni chadema ccm wanakipiga vita na kupotosha wananch kw ni cha kidini [wakristo] na kikabila [wachagga] jambo ambalo si kweli, chadema wanafanya kazi kwa maslai ya watanzania woote, ccm ndio wabaya tena wanatenda maovu na wanamkosea sn mwenyez mungu sana kwa kuchanganya siasa chafu na dini.
   
Loading...