Tanzania ni yetu sote! Tukikupa uongozi ukumbuke ni neema tu za Mungu

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,217
Tanzania ni yetu sote na tusifike mahali vyeo vyetu na nafasi kuwafanya watu wajisikie wakimbizi ama wasio na haki na taifa lao.

Mimi ni mtanzania kitovu changu kipo tanzania na nitafia tanzania hiyo ndio silaha pekee kwa kila mwenye pumzi ndani ya taifa hili.

Wapo viongozi wanataka kufanya watu eti wajione wao sio watanzania, hawana haki hawana chakusema isipokuwa wao tu jambo ambalo sii kweli.

Wanasahau jambo moja kubwa kuwa kiongozi ni processes ambayo mwanadam hawezi ikamilisha bila Neema za Mungu. Wanasahau kuna watu katikati yao wanaakili kuliko hata yeye anajiita kiongozi lakini hawakuwa viongozi. Wanasahau ata shuleni kulikuwa na vipanga zaidi yao ila uwenda kutokana na hali ya maisha wao walishindwa kwenda mbele au hawakubaatika kufika pale wamefika but wapo vizuri kuliko wao.

Usingiz huu wa madaraka kwa viongozi wa kitaifa huwafanya kuwanyanyasa watu wao nakufikia hatuwa kuwafanya wajione wao sio wenye kitu mbele ya taifa lao pendwa na hili hufanya wao kuwa juu wakati walio wachaguwa wakiwa chini.

Wapo ambao hujiona wanahaki yakula cake yataifa peke yao na familia zao na hawa ujeuka kuwa mabeberu mabinafsi

Wapo wanao ona akuna mwenye akili isipokuwa yeye na hawa ujeuka kuwa makatili na wasio furahia lolote lakujenga toka kwa wengine isipokuwa kwao hawa uwa mabeberu wa fikra za watu wake na mara nyingi nihatari kwa ustawi wa watu wa taifa lake kwakuwa ana amini kile ana amini.

Wapo wano ona maliyote ya taifa ni yake na mara nyingi hawa kile kipo kizuri wanataka kwanza wao na wengine watafuwata na hapa ndipo mafisadi utokea.

Kitu ambacho viongozi hawa hawana na utashi wakujuwa nafasi aliopo inaitaji mtu mmoja tu ktktaifa na ili uyo mtu apayikane basi watu walikaa na kuchambuwa mengi wakampa nafasi sii kwamba ndio bora peke yake hapana ila kwakuwa anaitajika mtu mmoja tu naa kwa neema yeye wamempa kwa mapatano na watu wengine uwenda wazuri kuliko yeye hata hawakupata...

Shida inakuja akisha pata anasahu yote nakuwa peke yake nakuanza kupiga mziki ambao kwakuwa yeye ndoe mpiga ngoma,jitaa,dramss,piano,muimbaji yeye hushuudia aina ya mziki atawadikilizaji wanashindwa kuelewa amepata wapi melods zake kwakweli anasikitisha. Na mbaya hurudi kwa mashabiki nakujisifia ngoma anayopiga mwenyewe na kama hayupo smart mashabiki wanaweza kuwa wakipiga chereko zaakutosha pasipo sikia sauti toka toka toka ujiwi kuimba..

Ukiwa kiongozi na ukitaka kuwa kiongoz wa watu uishi ktk maisha yao kumbuka watu wako yani amini wao ndio watu wako wanakufanya uwe hapo jisikie uchungu wao na uwe mwenye kusikia maumivu yao...
Msikilize hata mtoto uwenda akawa na jambo kubwa kuliko wewe.

Kiongozi wa watu anawezakuwa yule mwenye kujali sio kwa vipande vipande ilabkwa ujumla wao.

Ukiwa kiongozi lazima uwe natabia yakuondoa hisia mbaya kwa wale unawaongoz anaukumbuke pale walipo ni nguvu na jasho lao na wewe wape shavu wazidi kuwa namaisha mazuri...

Usisome sheria nakushindwa itafasiri ita watu wakusaidie maana zipo sheria mbadala kuliko kile unakiwaza.

Kama wewe ni last say aisee chunga sana kauli zako maana watu watatekeleza mwanzo mwisho na kwa kuws wewe ni last say basi hakuna kurudi nyuma na hapo ndipo panaya
.
Kama wew upo kiongoz wa kati basi heshimu wengine wala usipende sana watu wajuwe una mtu juu maana ukifanya hivyo unajichimbia kaburi lakujizika mwenyewe ktk uongozi.

Taifa hili ni letu na kiukweli hatuwezi kuwa viongozi ila wale viongozi tuna waheshim sana na tunawapend hata kama wao hawatupendi hiyo ni sheria ya Mungu na marabnyingi ulilpa.

Nawashangaa wanao pambana na viongozi na ona wamesahau kutii bika shuruti na mwisho watapata taji.

Sisi tutaheshim mamlaka zilizopo hata kama watatuona jatufai. Kumbukumbu zinasema walikuwepo viongozi walio itikisa dunia na wengine wakawa Mungu ila leo hawapo tena wala sehem yao aijulikani. Kwanini uwe mpweke kwa taifa lako na ni kwanin umdharau mwingine

Tujifunze kwa kukumbuka hapo tena na sisi ni nani....
Taifa langu Tanzania
 
[h=5]Hakika ukiona mahali ndani ya nchi wananchi wake wanamaisha magumu ya dhiki isiyosemeka na serikali haiwajali na bado watu hao wako kimya usijidanganye kuwa sehemu hiyo ina amani kwani yawezekana ukimya wao ni matokeo ya: Ujinga uliowatawala ama hawajui pa kuanzia hivyo wanasubiri tu nani amfunge paka kengele.

Kwa viongozi tulionao kuliona hili kwa ukweli wake ni vigumu mno kwa sababu akilini mwao bado wanaamini wananchi wanaowaongoza hawajajitambua hivyo hakuna haja ya kuwafikiria kwani hata hivyo ujinga wao ndio mtaji wao kisiasa kwa sababu wakikumbukwa kipindi cha "come Pain" kwa kupewa Tsht,kofia,kanga na Tsh 5000 kwa wale walioshinda juani siku nzima basi hayo ni maisha kwao na kila afanyaye hivyo ni mtu mwema sana kwao na fadhila pekee ya kumlipa ni kumpigia kura.

Watanzania wenzangu tumetumiwa vya kutosha na tumelipwa mabaya vya kutosha na kwa maumivu haya ya maisha magumu,mfumuko wa bei,anguko la elimu ya vijana wetu,viongozi kushutumiwa kushiriki kuhujumu nchi kwa kuuza nyara za serikali kama wanyama na pembe za ndovu nje ya nchi bila kusikia kauli thabiti ya kukea zaidi ya kuteteana na kupeana nyadhifa kubwa ndani ya chama,manyanyaso yanayofanywa na wanaoitwa wawekezaji chini ya msaada wa vyombo vya dola kama kule nyamongo,Geita na Loliondo na mambo mengine chungu nzima basi tujitathmini na kupima mambo hayo.

Maamuzi yetu sharti yawe bayana kama tumeumizwa vya kutosha na huu mfumo wa kulindana na kulinda maovu basi tuamue na kama bado hatujaumizwa vya kutosha basi tuendelee kuwaacha wajanja wachache chini ya mfumo wao waendelee kuitafuna nchi huku tukisubiri fadhila zao pindi watakapojisikia kufanya hivyo na kamwe asitokee wa kulalamika hata mambo yakiwa magumu zaidi ya hapo.

Mwisho kabisa niwaombe sote tujiandae kushiriki katika njia za kidemokrasia zitakazowekwa ili kuwapata wale tunaodhani watasimama kwa niaba yetu na kwa ajili yetu kwani kwa kushiriki huko tutakuwa tumeamua kwa maamuzi ya pamoja kujiweka rehani au kubaki na hatamu.

Asanteni sana kwa wote mtakaonielewa kwa nia njema,aidha niwashukuru pia wale watakaoona nimegusa maslahi yao na kuyahatarisha. Niseme tu nipo tayari kwa changamoto za pande zote mbili.

By: Tanzania Nchi Yetu Sote[/h]
 
Habari ya mda huu wakuu?

Naomba tuwe makini na mienendo ya namna serikali yetu inavyoendesha mambo yake kuna mambo kadhaa nabaini mdogo mdogo

Tangu vita ya madawa ya kulevya kutangazwa mvurugano ndani ya chama na serikali umekuwa mkubwa sana. Kulikoni?

Juzi nape kaonyeshewa bomba wameshtuka mbona kwa akina Lema wanaenda na SMG akina mwigulu hakuongea? je wapinzani sio watanzania? Nchi hii sio ya ccm ni yetu wote wenye vyama na wasio na vyama ubaguzi gani huu?

Sisi wengine baada ya kuona nape anaonyeshwa bastola tulijua kuna mambo mengi maovu yaliyopelekea hali ile anazuiwa kuongea kuzuia nini?

Kingine ni kwamba sasa ukweli utakuwa hadharani mda si mrefu je madawa ya kulevya tanzania makonda, Rais na watu ndani ya chama na serikali na wabunge wote hawa tutajua nani anasema ukweli mana mvurugano huu ni mkali sana.

Mwisho Rais anasema nikisema ukweli mtalia tunamtaka aseme tulie ili uchungu huu utoke au kuna siri anayo makonda ambayo hatujui?

Karibuni kwa mjadala
 
Alisema "msema kweli ni mpenzi wa Mungu", wengine wakatubeza kuwa watanzania hatupendi kusikia ukweli!Mbona alituchana makavu live tena tukiwa na msiba kagera,tukalia tukapiga moyo konde!Leo yeye huyo huyo anasema watz tukiujua ukweli tutalia,huu unafiki gani?Atueleze huo ukweli!
 
he he! yamebaki maneno tu kwamba tanzania ni ya watanzania..wengine wanajitukuza nakuwa kama wafalme tufanyenini wasiwe kama wafalme..?
 
Alisema "msema kweli ni mpenzi wa Mungu", wengine wakatubeza kuwa watanzania hatupendi kusikia ukweli!Mbona alituchana makavu live tena tukiwa na msiba kagera,tukalia tukapiga moyo konde!Leo yeye huyo huyo anasema watz tukiujua ukweli tutalia,huu unafiki gani?Atueleze huo ukweli!
kuna uchungu zaidi ya ule wa bukoba na njaa au rafiki zake ndo anawaogopa aseme ndo namsubir asituhadae kama kuna jambo kubwa huyu dogo anafanya kusaidia tanzania atuambie kuliko kumpiga mawe usoni mwake tutamsameh matatizo yake
 
Si kweli Tanzania ni ya Magufuli na Makonda acha kutupotosha.
download.jpg

 
Alisema "msema kweli ni mpenzi wa Mungu", wengine wakatubeza kuwa watanzania hatupendi kusikia ukweli!Mbona alituchana makavu live tena tukiwa na msiba kagera,tukalia tukapiga moyo konde!Leo yeye huyo huyo anasema watz tukiujua ukweli tutalia,huu unafiki gani?Atueleze huo ukweli!
tapatalk_1488873578481.jpeg

Labda anamaanisha huyu ndie atalia....
 
Hili sakata litawatoa nyoka, panya, kunguni na buibui pamgoni kuna nini nyuma ya bashite what is so special?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom