Tanzania ni yetu na wanyama na wamasai ni wetu, na wanakopelekwa ni kwetu pia

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,288
12,579
Huwezi kuchanganya pamoja watu wanaoongeka idadi na wanyamapori wanaongezeka idadi kwenye eneo moja lisiloongezeka ukubwa milele. Kuendelea kufanya hivyo ni kuminya uhuru wa watu na wanyama hao.

Kama ilikuwa sahihi miaka mingi iliyopita haiwezi kuwa sawa Sasa na hata kesho na kesho kutwa, kwakuwa hata idadi na tabia za watu hao na wanyama hao zimebadilika sana, sio zile walizokuwa nazo wakati uwamuzi wa kuishi pamoja na wanyama kwenye eneo ulipofanywa.

Mmasai wa Leo anakula ubwabwa, anajenga nyumba za kudumu, anatibiwa Hospitali na anapeleka watoto shule.

Anaesema wamasai wasihame ngorongoro anawakosea heshima wamasai, wanyama na watanzania wote kwa wakati mmoja, atafakari.

Tanzania ni kubwa, sehemu tupu ya kuwapeleka tunapo bado, tuwapeleke TU ili wanyama na watu hao wawe huru kama wengine.
 
Kwahiyo miongoni mwa hoja zako za msingi ni umeona ajabu masai kula wali?

Hawa ndio vijana CCM inatamani waendelee kuwepo na ije iwatumie kama think -tanks.
 
Kwahiyo miongoni mwa hoja zako za msingi ni umeona ajabu masai kula wali?

Hawa ndio vijana CCM inatamani waendelee kuwepo na ije iwatumie kama think -tanks.
Wakati wamasai wanawekwa pale ngorongoro walikuwa wanakula nyama ya ng'ombe, mbuzi, kondoo, maziwa na damu TU, Leo hii wanakula samaki, wanyamapori, Kuku, ugali nk na kujenga nyumba za kudumu kama watanzania wengine. Siku hizi wanawinda wanyamapori, kuuza meno ya tembo.

Wamepoteza sifa ya kuishi na wanyama wetu kwenye eneo moja maana hawana ng'ombe na mbuzi tena wa kutosheleza kula nyama na maziwa kila siku, mpaka wengine wamehamia mikini kufanya kazi nyingine. Mbona watu hawahoji kuhusu mabadiliko haya ya wamasai?
 
kuna mtu alisema watanzania hazijatimia aisee naamini sasa
Yaani wewe unaona wale wakoloni waliowaweka wamasai kwenye kundi moja na wanyama ndio wenye akili. Akili huna kwakweli. Nilidhani unataka kusema wakoloni washitakiwe kwa kuwafanyia vile watanzania wenzetu. Shida yenu mlikuwa mnafaidika na ujangiri kwa kupitia mwanya ule.

Kwenye hili naiunga mkono serikali kuwaondoa wamasai kule kwakuwa

1. walijichomeka kule na wasiokuwa wamasai (wapiga dili kutoka Moshi)
2. Wamasai hawana ng'ombe tena za kuwatosheleza hivyo wanaohitaji maeneo ya kutosha kufanya na shughuli nyingine za kilimo, uvuvi, viwanda na biashara kama wengine.
3. Ujangili na majangili wanajificha humohumo
4. Idadi ya watu imezidi kuongezeka.
5. Kuwepo kwa wafugaji kule kunavutia wahamiaji wafugaji kutoka nchi nyingine.
 
Wakati wamasai wanawekwa pale ngorongoro walikuwa wanakula nyama ya ng'ombe, mbuzi, kondoo, maziwa na damu TU, Leo hii wanakula samaki, wanyamapori, Kuku...
Kwahiyo wamasai waliokuwepo hapo hata kabla ya nchi kuitwa Tanzania mmeona wanavuruga mazingira na wamebadilika?

Ila mkambiwa mbadili katiba mnashupaza shingo! Shame on you.

Waambieni wazi mmeuzia muarabu hapo sio kusema wanaharibu mazingira kwana JNHPP si ilionekana ni uharibifu wa mazingira mbona wameindeleza yaani kwa Ngorongoro kila mtu amekua environmentalist.
 
Kwahiyo wamasai waliokuwepo hapo hata kabla ya nchi kuitwa Tanzania mmeona wanavuruga mazingira na wamebadilika?

Ila mkambiwa mbadili katiba mnashupaza shingo! Shame on you...
Ngorongoro siku hizi imejaa wachagga bhana sio wamasai tena. Na hata hao wamasai siku hizi hawana ng'ombe tena bali wanawinda na kulima na kuongiza watalii na kutengeneza shanga TU za viunoni pale wauzie watalii
 
Huwezi kuchanganya pamoja watu wanaoongeka idadi na wanyamapori wanaongezeka idadi kwenye eneo moja lisiloongezeka ukubwa milele...
Kwa hoja hizo, nimekuelewa na kukuunga mkono kwa sehemu. Ila kwa mujibu wa hoja yako ambayo kwa kweli ni hoja iliyoshiba ni kuwa watu wanaongezeka, wanyama wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki.

Kwa hoja hiyo suluhisho siyo kuwaondoa wamasai wote bali ni kuwapunguza. kama kuna familia 1,500 leo kwa mfano, basi wangehamisha familia 1000 na kuacha familia 500. Hapo hoja yako ingekuwa na mantiki zaidi. Lakini kuhamisha wamasai wote hapo kuna walakini.
 
Kwa hoja hizo, nimekuelewa na kukuunga mkono kwa sehemu. Ila kwa mujibu wa hoja yako ambayo kwa kweli ni hoja iliyoshiba ni kuwa watu wanaongezeka, wanyama wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki. Kwa hoja hiyo suluhisho siyo kuwaondoa wamasai wote bali ni kuwapunguza. kama kuna familia 1,500 leo kwa mfano, basi wangehamisha familia 1000 na kuacha familia 500. Hapo hoja yako ingekuwa na mantiki zaidi. Lakini kuhamisha wamasai wote hapo kuna walakini.
Huko kutasababisha kuzitenga familia zao na watu wao muhimu. Lakini wamasai nao siku hizi hawana mifugo ya kuwatosheleza tena, wanaohitaji maeneo huru wafanye maendeleo Yao mengine.

Wakoloni waliwachukulia wamasai sawa na wanyamapori TU ndio maana wakawachanganya na wanyama sehemu moja.
 
Wakati watanzania wengine wakihamishwa kupisha upanuzi wa viwanja vya ndege, barabara, masoko, migodi ya madini wale wa Ngorongoro na Loliondo wawe ni untouchables kupisha hifadhi zetu za wanyama, hii haiwezi kuwa sawasawa. Tatizo ni wale wakoloni ambao hawakuwathamini wamasai sawa na binadamu wengine, bali waliwaona wamasai kama viumbe primitive, vya ajabu ambavyo ni nusu mtu na nusu wanyama kiasi cha kustahili treatment tofauti. Hii sio sawa kabisa maana wamasai ni binadamu kamili, ni watanzania na wana haki sawa na watanzania wengine.
 
Wamasai ni jamii ya wanyamapori.
kama Msukuma anaweza kuhamishwa kupisha wazungu wawekezaji kwenye madini, mzaramo anaweza kuhamishwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege na bandari, mdigo kuhamishwa kupisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda, basi hata mmasai anaweza kutakiwa kuhamishwa pia kupisha hifadhi za wanyama pori, ilimradi vigezo na masharti ya kuhamishwa vizingatiwe. Vinginevyo tutakuwa na double standard kwenye jambo lilelile moja. Vingine labda tukubaliane kuwa wamasai sio watu kamili (endangered specie), hivyo wanahitaji huruma maalumu na ya kipekee.
 
Huwezi kuchanganya pamoja watu wanaoongeka idadi na wanyamapori wanaongezeka idadi kwenye eneo moja lisiloongezeka ukubwa milele. Kuendelea kufanya hivyo ni kuminya uhuru wa watu na wanyama hao.

Kama ilikuwa sahihi miaka mingi iliyopita haiwezi kuwa sawa Sasa na hata kesho na kesho kutwa, kwakuwa hata idadi na tabia za watu hao na wanyama hao zimebadilika sana, sio zile walizokuwa nazo wakati uwamuzi wa kuishi pamoja na wanyama kwenye eneo ulipofanywa.

Mmasai wa Leo anakula ubwabwa, anajenga nyumba za kudumu, anatibiwa Hospitali na anapeleka watoto shule.

Anaesema wamasai wasihame ngorongoro anawakosea heshima wamasai, wanyama na watanzania wote kwa wakati mmoja, atafakari.

Tanzania ni kubwa, sehemu tupu ya kuwapeleka tunapo bado, tuwapeleke TU ili wanyama na watu hao wawe huru kama wengine.
Asante sana umeongea neno muhimu. kudos. Tusipotunza wanyama watapotea, mjue hata wanyama wana haki ya kuishi.
 
Asante sana umeongea neno muhimu. kudos. Tusipotunza wanyama watapotea, mjue hata wanyama wana haki ya kuishi.
Wale wamasai waliohamishwa kutoka serengeti kuja ngorongoro ni tofauti kabisa na hawa wamasai wanaotakiwa kuhama ngorongoro leo. Ni tofauti kuanzia vyakula, kuabudu, mavazi, matumizi, shelters, usafiri, malazi, shughuli, njia za mawasiliano na hata elimu. Wamepoteza kabisa sifa ya kuishi pamoja na wanyama pori wetu. Wamasai wa leo wanamiliki migodi ya madini, nyumba za kudumu, magari, pikipiki, tv, ng'ombe wa kisasa, shule, bunduki za kuua tembo, mavazi, vyakula na hata kuoa na kuolewa na makabila mengine.
 
Back
Top Bottom