Tanzania ni ya mwisho duniani kujitosheleza kwa madaktari

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,886
Inaonekana kwa Tanzania madaktari (MD na kuendelea) watatu wanahudumia watu 100,000. hii ni ripoti ya mwaka 2014 ya CIA. inaiweka Tanzania kuwa nchi ya mwisho duniani kwa uwiano wa daktari:watu. Ripoti zingine zinasema kuna daktari 2 kwa watu 100,000. Cuba ni nchi inayojitosheleza sana. Ina madaktari 670 kwa watu 100,000.
hili ni janga na ndiyo sababu vituo vya maombezi, wakina Ndodi na waganga-wachawi wameshamiri sana. Tufanye nini?

upload_2016-12-3_1-16-49.png
upload_2016-12-3_1-19-20.png
upload_2016-12-3_1-22-46.png
 
Attachments

  • upload_2016-12-3_1-20-41.png
    upload_2016-12-3_1-20-41.png
    11.8 KB · Views: 66
Inaonekana kwa Tanzania madaktari (MD na kuendelea) watatu wanahudumia watu 100,000. hii ni ripoti ya mwaka 2014 ya CIA. inaiweka Tanzania kuwa nchi ya mwisho duniani kwa uwiano wa daktari:watu. Ripoti zingine zinasema kuna daktari 2 kwa watu 100,000. Cuba ni nchi inayojitosheleza sana. Ina madaktari 670 kwa watu 100,000.
hili ni janga na ndiyo sababu vituo vya maombezi, wakina Ndodi na waganga-wachawi wameshamiri sana. Tufanye nini?

View attachment 442213View attachment 442214View attachment 442216
Mbona hizo report zina mashaka na data zake kwa Tanzania sio za kweli kabisa. hiyo report ya mwaka 2007 ya human development report inasema Tanzania ina physician 2/100000 kwa hivyo kwa wakati huo hata population ya Tz siikumbuki vizuri lakini idadi yako inakuwa kwenye 800 physician. na ya CIA inasema 0.01/1000 kwa hivyo na hiyo report ya mwama 2013 na inaifanya TZ kuwa na physician less than 500. Kwa hivyo hizo data sio za kweli.Nakubaliana na wewe idadi ya physician haikidhi haja lakini siyo kwa uhaba kama ulivyotuletea hapo
 
Utawala haupo kusaidia wananchi wake kinachofanyika ni ubabaishaji tu.
Sasa utawala unamsaidia nani? Siasa za kishamba hizo. Bodi ya mkopo inakusanya pesa ilizokopesha ili wanafunzi wa sayansi wengi zaidi wapate mikopo ya elimu ya juu. Huoni kama hio ni plan nzuri? Au ulitaka usaidiwaje
 
Inaonekana kwa Tanzania madaktari (MD na kuendelea) watatu wanahudumia watu 100,000. hii ni ripoti ya mwaka 2014 ya CIA. inaiweka Tanzania kuwa nchi ya mwisho duniani kwa uwiano wa daktari:watu. Ripoti zingine zinasema kuna daktari 2 kwa watu 100,000. Cuba ni nchi inayojitosheleza sana. Ina madaktari 670 kwa watu 100,000.
hili ni janga na ndiyo sababu vituo vya maombezi, wakina Ndodi na waganga-wachawi wameshamiri sana. Tufanye nini?

View attachment 442213View attachment 442214View attachment 442216
Mbona nchi zingine hazipo. mfano USA na Uingereza. huenda hizo ndo za mwisho kuliko TZ
 
Sasa utawala unamsaidia nani? Siasa za kishamba hizo. Bodi ya mkopo inakusanya pesa ilizokopesha ili wanafunzi wa sayansi wengi zaidi wapate mikopo ya elimu ya juu. Huoni kama hio ni plan nzuri? Au ulitaka usaidiwaje
"Kipofu haambiwi tazama"
 
Sasa utawala unamsaidia nani? Siasa za kishamba hizo. Bodi ya mkopo inakusanya pesa ilizokopesha ili wanafunzi wa sayansi wengi zaidi wapate mikopo ya elimu ya juu. Huoni kama hio ni plan nzuri? Au ulitaka usaidiwaje
Mkuu unauhakika na unacho kizungumza?
 
Mbona hizo report zina mashaka na data zake kwa Tanzania sio za kweli kabisa. hiyo report ya mwaka 2007 ya human development report inasema Tanzania ina physician 2/100000 kwa hivyo kwa wakati huo hata population ya Tz siikumbuki vizuri lakini idadi yako inakuwa kwenye 800 physician. na ya CIA inasema 0.01/1000 kwa hivyo na hiyo report ya mwama 2013 na inaifanya TZ kuwa na physician less than 500. Kwa hivyo hizo data sio za kweli.Nakubaliana na wewe idadi ya physician haikidhi haja lakini siyo kwa uhaba kama ulivyotuletea hapo
Tanzania imejaa madaktari wa cheti, diploma na advanced diploma. wenye digrii ni wachache sana. hiyo ripoti inaweza kuwa na mapungufu lakini ukiwaza kuwa yote inamapungufu bado tunabaki wa mwisho.
 
Na bado hatutoi mikopo kwa wanafunzi wenye sifa waliosoma shule binafsi, hii ndiyo awamu ya tano inayobagua watanzania
 
Mbona hizo report zina mashaka na data zake kwa Tanzania sio za kweli kabisa. hiyo report ya mwaka 2007 ya human development report inasema Tanzania ina physician 2/100000 kwa hivyo kwa wakati huo hata population ya Tz siikumbuki vizuri lakini idadi yako inakuwa kwenye 800 physician. na ya CIA inasema 0.01/1000 kwa hivyo na hiyo report ya mwama 2013 na inaifanya TZ kuwa na physician less than 500. Kwa hivyo hizo data sio za kweli.Nakubaliana na wewe idadi ya physician haikidhi haja lakini siyo kwa uhaba kama ulivyotuletea hapo
Unapoongelea physician kwa TZ unamaanisha kitu kingine kabisa.. tumia neno daktari, physician ni mtu mwenye masters ya Internal medicine
 
Inaonekana kwa Tanzania madaktari (MD na kuendelea) watatu wanahudumia watu 100,000. hii ni ripoti ya mwaka 2014 ya CIA. inaiweka Tanzania kuwa nchi ya mwisho duniani kwa uwiano wa daktari:watu. Ripoti zingine zinasema kuna daktari 2 kwa watu 100,000. Cuba ni nchi inayojitosheleza sana. Ina madaktari 670 kwa watu 100,000.
hili ni janga na ndiyo sababu vituo vya maombezi, wakina Ndodi na waganga-wachawi wameshamiri sana. Tufanye nini?

View attachment 442213View attachment 442214View attachment 442216
Hua napatwa na mshangao, hawa ambao hutokea kwenye vyombo vya habari na kutueleza kuwa hawaajiri madaktari kwa sababu wana madaktari wakutosha, na kutuzungusha kwa lugha zisizoeleweka huwa WANATUONA MAMBUMBU? Mara nyingi huhitaji hata kuwa na utalaam wowote, ukitembea kidogo kwenye nchi hii pamoja na kwenye huduma za afya unajua kuwa kuna uhaba wa madaktari pamoja na huduma duni za afya.
 
Mbona hizo report zina mashaka na data zake kwa Tanzania sio za kweli kabisa. hiyo report ya mwaka 2007 ya human development report inasema Tanzania ina physician 2/100000 kwa hivyo kwa wakati huo hata population ya Tz siikumbuki vizuri lakini idadi yako inakuwa kwenye 800 physician. na ya CIA inasema 0.01/1000 kwa hivyo na hiyo report ya mwama 2013 na inaifanya TZ kuwa na physician less than 500. Kwa hivyo hizo data sio za kweli.Nakubaliana na wewe idadi ya physician haikidhi haja lakini siyo kwa uhaba kama ulivyotuletea hapo
Kwahiyo unataka kusema sisi tumevuka malengo? Kwa taarifa yako mimi nimechaguliwa mwaka huu MD nimefaulu form six ila nimekosa mkopo. Ndo ujue kuwa viongozi hawapo siriaz. Nimeenda bodi ya mikopo wanasema nijisomeshe kwani serikali inatoa mkopo kwa yatima na vilema. You cant imagine ntawezaje kujigharamia kwa miaka mitano kila kitu.

Kwahiyo wewe mchangiaji usishangilie ujinga huu wa CCM, mimi binafsi inaniuma sana
 
Mhhh tz Hii hii inayoshindwa kuajiri madaktar zaidi ya 500 na inatangaza kabsa et.....
 
Kwahiyo unataka kusema sisi tumevuka malengo? Kwa taarifa yako mimi nimechaguliwa mwaka huu MD nimefaulu form six ila nimekosa mkopo. Ndo ujue kuwa viongozi hawapo siriaz. Nimeenda bodi ya mikopo wanasema nijisomeshe kwani serikali inatoa mkopo kwa yatima na vilema. You cant imagine ntawezaje kujigharamia kwa miaka mitano kila kitu.

Kwahiyo wewe mchangiaji usishangilie ujinga huu wa CCM, mimi binafsi inaniuma sana
Nimesemema idadi ya madaktari haikidhi haja lakini siyo kwa idadi hiyo waliyosema. Sasa wapi nime endorse serikali ya CCM hapo?
 
Tanzania imejaa madaktari wa cheti, diploma na advanced diploma. wenye digrii ni wachache sana. hiyo ripoti inaweza kuwa na mapungufu lakini ukiwaza kuwa yote inamapungufu bado tunabaki wa mwisho.
Mimi hiyo situation naijua vizuri na ndiyo maana nikasema idadi haikidhi haja. lakini hizo data zao walozitoa sizo
 
Unapoongelea physician kwa TZ unamaanisha kitu kingine kabisa.. tumia neno daktari, physician ni mtu mwenye masters ya Internal medicine
Hiyo report haijasema hivyo isome vizuri mimi najua fika nani ni physician kwa sababu mimi mwenyewe ni physician lakini kwa maelezo ya hapo juu hawaongelea physician as internist bali ni MD au MBBS kwa hivyo soma hiyo report ya physician density ya CIA halafu chini wakatoa definition ya nani physician kwa wa;ivyotumia wao.. Au inaonyesha hukuisoma hiyo na umekurupuka kujibu tu
 
Mimi hiyo situation naijua vizuri na ndiyo maana nikasema idadi haikidhi haja. lakini hizo data zao walozitoa sizo
ndiyo nikasema pengine methodology waliyotumia inamapungufu na kuleta idadi ndogo. kama walitumia hiyohiyo dunia nzima basi kote idadi inapungua na bado tunabaki wa mwisho. lakini data ya idadi ya madaktari si rahisi kukosea na ni rahisi kupata. madaktari wote wamesajiliwa wizarani.
 
Back
Top Bottom