Tanzania ni uwanja wa vita vya kiuchumi,je kuna muwekezaji atawekeza eneo la VITA?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,943
20,496
Mbiu ya mgambo imekuwa ikilia kila mara, wito imekuwa ukitolewa majukwaani

"NCHI IKO KATIKA VITA,VITA YA KIUCHUMI"

Na juzi tu,Amiri Jeshi Mkuu amelithibitishia Taifa kwamba huwa anapeleka askari kwa ajili ya kupambana katika vita hii

Kawaida ya vita,huacha majeruhi na vifo kwa pande zote(casualties) zinazopigana

Vita haina macho,kombora toka upande wowote,linaweza kumuua yeyote

Je,kuna mwekezaji ambaye atathubutu kuleta mabilioni yake eneo la vita halafu yapigwe kombora na kuharibika kabisa au haya yeye kuwa muhanga na kuteseka?

Je kuna kampuni itaongeza uwekezaji eneo la vita?

Je eneo la vita ajira huwa zinaongezeka?

Natarajia wawekezaji pamoja na consulting firms zao watazuia mamia ya matrilioni ya mitaji isiingie eneo la vita
 
Theory za uchumi za mtakatifu Pogba/Sizonje zinamuelekeza kuwa kadiri serikali inavyopambana na wawekezaji, ndivyo jinsi wawekezaji wapya wanavyovutika kuwekeza katika eneo hilo la uchumi. Pia Theory nyingine inamuelekeza kuwa kufilisika kwa mabenki na mabenki kusitisha kutoa mikopo ni moja ya vichocheo vya kukua kwa uchumi!
 
Ajabu kabisa

Kagame na umwamba wake kwa wawekezaji huwa anatumia busara
 
So point yako bora tuendelee kuibiwa?? Though wezi ni watanzania na wawekezaji...

Point nzuri ni ile mwishoni iwe na suggestions au advice kwa maendeleo ya taifa, sio kukosoa na kulalamika haviwezi saidia.

Au wewe sio mtanzania??
 
Kama unaibiwa,kumkamata mwizi ndio unatangaza dunia nzima kwamba nchi yako iko vitani dhidi ya wawekezaji?

Kuna mtu kamzuia kukamata hao wezi bila kuleta athari kwa kauli zinazotishia imani ya wawekezaji kwa nchi?

Unajua imetumika miaka mingapi kufanya nchi hii ianze kuaminika kwa wawekezaji? Na makovu ya utaifishaji hayajapona tunayaibua,makovu ya kuchukia matajiri wenye mitaji hayajapoa tunayaibua,

Imani ya wawekezaji kwa Tanzania iko chini sana na inaendelea kushuka,hii INA madhara ya moja kwa moja kwenye uchumi wa nchi

Serikali haiwezi kuajiri,lakini hata wale wawekezaji binafsi ambao wangeajiri,wanaondoka,hawa vijana unadhani watavumilia mpaka lini kukaa bila ajira?

Mahitaji ya taifa kuhudumia wananchi yanaongezeka,ni wazi serikali inahitaji kupata wawekezaji ili iongeze kodi iweze kuhudumia taifa,badala yake tunaitangazia dunia kwamba tuko kwenye vita dhidi ya wawekezaji

Wawekezaji watarajiwa watasubiri mjimalize na vita zenu kwanza
 
Back
Top Bottom