Tanzania ni Taifa la sasa lililokosa viongozi na wasomi wa kuliendeleza kiuchumi

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Kuna wakati unawaza na kujiuliza mambo mengi tu bila hata kupata chembe ya jibu , sasa unajiuliza hawa watu wanaojiita Maprofesa , Madaktari wa kisomi, Engineers wanafanya nini katika hili taifa ukiacha hao mprofesa kuna taasisi zinazojigamba kila siku kuwa ni best katika uchumi mfano REPOA, ESRF, COSTECH, UDSM, TIC, BOT, SUA na takataka zingine kwanini kila mwaka zinashindwa kubuni vyanzo vya mapato kiuchumi bila kuathiri uchumi wa mwananchi, hivi vichwa vinavyojifanya ni technical thinking mbona sio creative wala sio innovative in economical parameter katika kukuza vyonzo vya mapato? au ni vichwa vinavyofikiri kupitia matumbo yao?

Utasikia tumeongeza kodi katika Bia, Sigara, sijui vinywaji vikali, mawigi, yani hakuna ubunifu kabisa na tafsiri ya uchumi ni kuwa unapoongeza kitu hiki ndani ya kitu kinachoambatana lazima kitaathiri kitu kingine kinachoambatana nacho kwasababu hivi vitu vinategemeana, kwa mwaka mzima watu waliopewa dhamana ya kiongozi wamekaa chini kitako na kupokea kodi kama sehemu ya posho yao kutoka kwa mwananchi kwa kutunga sheria ya kumuumiza huyohuyo mwananchi aliyekupa nafsi ya kukaa hapo ulipo , huu ni uwendawazimu kabisa na uzwazwa wa kufikiri watu wanavimba matumbo mpaka wanapoteza uwezo wa kufikiri huu ni ugonjwa kabisa.

Mwalimu Nyerere miaka ya 1960 alikuwa na vyanzo vichache tu lakini aliweza kuliendeleza taifa kwa hali ya juu nakumbuka kipindi kile tulisoma bure ikiwa pamoja na kupewa baadhi vitu kama vile madaftari na tukumbuke kipindi hicho rasilimali madini ilikuwa bado kuchimbwa.

Yani waziri mzima aliyejaa tumbo kubwa anasema kuwa hizo kodi zitajenga sijui Hospital, mashule, Mabarabara, vituo vya afya kitu ambacho sio reliable kwa mfano mtu akaacha kutumia e- money maana yake hizo shule, hospital n.k hazitajengwa si ndio? Yani unajenga matumaini ya kimaendeleo ya kibajeti kwa kitu ambacho sio sustainable kiuchumi what if wananchi wakaacha kutuma hela kupitia mitandao au matumizi ya e- money yakashuka mpaka asilimia 20 utafanyaje?

Mimi nafikiri hawa viongozi ni bure kabisa katika akili zao, ushauri wangu ni kuwa kwasababu hawa matumbo kujaa wa Bungeni wameshindwa kuwa wabunifu katika kutengeneza vyanzo vya mapato ndani ya taifa ni bora taifa likodi kampuni maalum itakayoweza kufanya utafiti juu ya rasilimali za taifa na kufanya ubunifu wa kupata mapato ya kuliongoza taifa hili lakini sio jamii ya Mwigulu kuchamba na matumbo mengine ya bungeni.
 
Back
Top Bottom