Tanzania ni Taifa imara na tuna Kiongozi imara. Hoja za Bunge la EU zinajibika kwa Hoja

Oct 1, 2019
74
125
Salaam wana JF,

Nianze andiko hili fupi kwa kusema Tanzania ni taifa imara kwa misingi ya siasa, uchumi, utamaduni na utawala bora, Tanzania kama yalivyo mataifa mengine ulimwengu tunayo misingi na taratibu za ndani za kuendesha shughuli zetu za kiutawala kulingana serikali iliyopo madarakani, Aidha Tanzania tunayo aina ya demokrasia yetu tunayoiishi katika kuendesha mambo yetu ya ndani.

Pia Tanzania kwa sasa tunaye kiongozi mwenye misimamo isiyoyumbishwa na mamluki kutoka aidha nje au ndani ya taifa letu, ni wazi kuwa Chuki kutoka mataifa makubwa zinaanzia hapa "kwenye dhana ya misimamo ya Mkuu wa nchi"

Viongozi wengi wa Afrika, Asia na Amerika ya mwambao wa Kaskazini Kusini wamechukiwa na kuwa maadui wa mataifa ya Ulaya na Marekani kwa sababu ya misimamo yao ya uzalendo kwa mataifa wanayoyaongoza, Kwa bahati mbaya mataifa haya yamekuwa na wasaliti wa ndani wanaoshiriki kuhujumu mataifa yao kwa maslahi yao binafsi, hata hiyo historia inaonyesha wasaliti ndani ya bara la Afrika wamekuwepo tangu karne ya kumi, Kwahiyo usaliti si jambo geni kwa Afrika.

Watanzania Juzi walipokea taarifa ya kamati ya Bunge la Ulaya wakihoji baadhi ya mambo, wapo waliofurahi na kushangilia mitandaoni kana kwamba wao si wananufaika na misaada ya walipa kodi wa Ulaya, Ukweli ni kwamba Mimi na wewe kwa kujua au kwa kutokujua tumekuwa wananufaika wa kodi ya wazungu kwa muda mrefu, Swali ni je wote wanaofurahia hoja iliyotolewa bungeni Juzi wanajitambua au hawajitambui kwamba na wao ni sehemu ya wanufaika ya kile kinachohojiwa?

Pengine nitajibiwa kwa mapana yake, Hata hivyo hoja ya Bunge ya EU inajibiwa kwa hoja, kwa sababu ni hoja ambayo imeibuliwa na upande wa pili una nafasi ya kujibu kwa mapana yake, Watanzania Kilichoongelewa juzi ni hoja na wala sio maazimio ya bunge aidha ni Hoja za kamati mojawapo kati ya kamati nyingi zinazounda bunge hilo, Rai yangu nikutanguliza uzalendo mbele na si Upotoshaji usio kuwa na Tija kwa taifa letu na vizazi vyetu vya sasa na hapo badae, Tuache ushabiki wenye kubomoa badala yake tuwe na ushabiki wenye kujenga taifa letu.​
 

Iblis Bin Shetan

JF-Expert Member
Sep 24, 2018
545
500
Hakuna cha uzalendo wala shangazi yake uzalendo yaan muibe halafu msingizie uzalendo.

Kwanza mtuambie hizo hela mmetumiaje yaan zimefanya kazi gani.

La sivyo wekeni Euro milioni 27 za watu mmeshazoe kuiba halafu mnakimbilia uzalendo mtazitapika hizo.
 

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
3,748
2,000
Yaani mimi mzazi nikupe hela ukanunue mfuko, badala ya kununulia mfuko wewe ukaenda kununulia kondomu afu unarudi home unataka mimi mzazi nipige kimya ili nidumishe uzalendo wa nyumbani? Acha uboya man. Utakuja kugongewa wife kwa uzalendo wako huo.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,447
2,000
Tulioshangilia tunajitambua sana na ndo WAZALENDO wa kweli sio nyie wachumia tumbo. Hamuwezi kuua watu, kuwafungulia makesi ya uongo, kuwapora ushindi kwenye uchaguzi alafu mnasema eti tuwe Wazalendo.

Kwa hiyo unamaanisha huo ufedhuli ndo uzalendo??? Na bado, lazima muite Maji mmaaaa Safari hii.
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,031
2,000
Mwalimu, utajuwa umejichanganya sana, maana jamaa alishasema hateui tena! Wewe mwalimu na wewe si ulishiriki wizi wa kura pale kituoni kwako? Mna laana nyie walimu!!
 

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,440
2,000
Umemaliza vyema kaka kuwa tuache ushabiki wenye kubomoa badala yake tuwe na ushabiki wenye kujenga taifa letu. Kwa maswali haya machache upi ni ushabiki wa kubomoa na upi wa kujenga:-

1. Kushabikaa wadau woote wanaolaani vitendo vya uvunjifu wa demokrasia ikiwa ni pamoja kulaani unyanyasaji kwa wadau wa siasa?
2. Kushabikia wadau woote wanaounga mkono hatua za uvunjifu wa Demokrasia na unyanasaji kwa wadau wa saisasa.?

Hakuna cha uzalendo wala shangazi yake uzalendo yaan muibe halafu msingizie uzalendo
Kwanza mtuambie hizo hela mmetumiaje yaan zimefanya kazi gani
La sivyo wekeni Euro milioni 27 za watu mmeshazoe kuiba halafu mnakimbilia uzalendo mtazitapika hizo
 

Mjamaa86

JF-Expert Member
Jul 10, 2018
472
500
Mtu mwongo siku zote, ukimshtukiza na swali ghafla au hoja ambayo hakuitarajia kutokana na kile alichofanya/kusema/au anachojaribu kuaminisha kuwa ni kweli basi atatapatapa sana kukupa jibu ili asijichanganye, nachoamini sasa Lumumba wamejichimbia wakipika jibu la kutoa. Ila mzungu huwezi mdanganya kirahisi kama watz kwa hiyo wajipange sana.
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,275
2,000
Ni misimamo gani ya mkuu wa nchi inayoleta chuki toka kwa mataifa makubwa? Tuanzie hapo.
 

if cap fits

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
1,046
2,000
Serikali ina matumizi mengi inayo kuhudumia, tuvute subira wenye mamlaka watajibu, nina imani hizo Euro hazijaibiwa.
Dawa yenu ipo jikoni inatokota, wewe kama huna mamlaka ya kuelezea zilitumikaje hizo pesa sasa haya mamlaka ya kutuamisha na serikalii hii iliyo jaa ukilitimba umetoa wapi, serikali ya kipuuzi sana haijawahi kutokea.
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,275
2,000
Munataka wananchi wote wafurahie misaada ya walipa kodi wa ulaya. Lakini unasema misimamo ya rais inawachukiza hao walipa kodi wa Ulaya.

Halafu utalazimisha ueleweke? Na ukiitwa kilaza utaanza kutukana.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,553
2,000
Serikali ina matumizi mengi inayo kuhudumia, tuvute subira wenye mamlaka watajibu, nina imani hizo Euro hazijaibiwa.

1. Ndugu, katika hili huwezi kujitetea kwa kusema "serikali ina matumizi mengi" kwa fedha ambazo umepewa matumizi yakiwa tayari specified na mtoa fedha.

2. Kwenye hili la fedha za package ya Covid19 toka EU, serikali ilishajichanganya yenyewe toka awali kwa matendo yake yenyewe hususani kwenye swala zima la "transparency" ama uwazi ishu nzima hii.

Hili ni tatizo linalozikabili serikali nyingi za dunia ya tatu kwa kukosa UWAZI na UAMINIFU ambavyo hivi ndiyo viashiria halisi vya UFISADI.
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,785
2,000
Mbona wanachota kujua Bunge la EU ni jambo dogo sana, "Matumizi ya Euro zao mlizochukua kwa kisingizio cha corona huku mkiwa mnautangazia ulimwengu kuwa mmeishinda corona kwa maombi"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom