Tanzania ni Simba mwenye kujihisi ana nguvu kama za Sungura

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Kila nikiiwaza Tanzania kwanini tupo kama tulivyo mpaka sasa nakosa majibu.

Tanzania imashika namba tano kwa idadi kubwa ya watu nyuma ya Nigeria, Ethiopia, Misri na DR Congo. Idadi kubwa ya watu huwa ni mtaji muhimu sana katika maendelea ya nchi.

Mbali na idadi kubwa ya watu wake lakini pia Tanzania ni nchi yenye raslamali nyingi sana za kuweza kuwa tishio kwa mataifa mengine kiuchumi, kisiasa, kiulinzi na mambo kama hayo.

Ardhi ya Tanzania ni yenye rutuba ya kutosha achana na rasilimali maji katika bahari, maziwa na mito yetu. Chakushangaza ni kwamba ni mara chache sana kuiona Tanzania ikichomoza kwenye mambo yenye sifa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa.

Mara nyingi sana Tanzania hu trend sana kwenye mambo ya ajabu sana kama kuua albinos na mambo mabaya kama hayo. Hata uchaguzi wetu huwa hauvutii sana vyombo vya kimataifa kama zilivyo nchi nyingine kama Kenya, Ghana, Uganda, South Africa na hata Somalia na DRC ambazo ni nchi zenye vurugu.

Tanzania haivumi sana kwa kuwa nchi pekee duniani yenye madini ya Tanzanite. Tanzania haivumi kwa kuwa na mlima mrefu kuliko yote Afrika lakini pia mlima wenye barafu kileleni huku ukiwa ukanda wa Kitropiki kitu ambacho si cha kawaida.

Ni rahisi sana nchi kama Senegal, Burkina Faso, Morroco, Zimbabwe habari zao kuvuma kwenye vyombo vya kimataifa huku Tanzania na ukubwa wetu tukiwa hatuandikowi kabisaaaa kwenye vyombo hivyo. Kidogo hayati JPM aliweza kuiweka Tanzania kwenye ramani za dunia kwa misimamo yake kwenye baadhi ya mambo ikiwemo MAKINIKIA na Corona.

Ni wakati sana wa kui brand upya Tanzania kama ilivuokuwa zamani wakati wa vita ya UKOMBOZI ambapo mataifa mengi rejea yao katika siasa na diplomasia ilikuwa ni Tanzania. Cha kufanya ni kutumia ukubwa wetu kwa maana ya idadi kubwa ya watu na ukubwa wa mipaka yetu kijitangaza kwa mema.
 
Hatuhitaji kuibrand Tanzania kama walivyofanya Kigwangala na wasanii wa bongo movie.

Tunachohitaji ni katiba mpya na taasisi imara
 
Back
Top Bottom