TANZANIA ni nini machoni pa CAF ? Uwakilishi vilabu na timu ya taifa. Suala la Zanzibar.

Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,896
4,495
Habari zenu wanajumuiya ya michezo JF....

Kwa muda sasa nimekua nikipata mkanganyiko juu ya 'nchi ya Tanzania' machoni pa CAF (Shirikisho la soka barani Afrika).

NINA MASWALI MANNE:

1. Kama kweli Zanzibar si mwanachama wa CAF, bali Tanzania ndiye mwanachama, Je, ni kwanini Zanzibar ina nafasi mbili za uwakilishi katika mashindano ya CAF ngazi ya vilabu....?

2. Kama hauhitaji kuwa mwanachama ili uweze kushiriki mashindano ya CAF kama ambavyo vilabu vya Zanzibar vinashiriki (rejea namba 1 hapo juu), ni kwanini timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar heroes' haishiriki mashindano ya AFCON (Kuanzia hatua za awali za kufuzu na kuendelea)...?

3. Kama vilabu vya Zanzibar vinashiriki ligi ya mabingwa na shirikisho kwa mgongo wa 'Tanzania', inakuwaje katika ranking za idadi ya ushiriki wa vilabu, Tanzania ilikua na timu mbili tu (moja shirikisho, moja ligi ya mabingwa) badala ya timu nne (ukijumlisha mbili za kule Zanzibar) ?

NB: Kumbuka baada ya Simba kufanya vizuri mwaka huu kwenye klabu bingwa, ukijumlisha na pointi alizopata yanga kwenye shirikisho miaka kadhaa iliyopita, sasa 'TANZANIA' itapelek
a timu NNE kwenye mashindano ya CAF...
Kwa muktadha huu (Zanzibar kwa mgongo wa Tanzania), Je, Tanzania itakua na timu SITA ?

4. Swali la msingi, 'TANZANIA' ni nini machoni pa CAF ?

Wajuzi naombeni msaada katika hili, lengo ni kurefusha uelewa wangu na wa wadau wengine....

Karibuni kwa mjadala huru tafadhali
 
Sidhani kama mwakani tutapeleka timu 4 hizi ni habari za mitandaonitu hazijathibitishwa na TFF. Nadhani bado poit hazitatosha kutuwezesha kuongezewa idadi ya timu 4 kama tutapata nafasi tena mwakani ya kucheza group stage hapo point zitatosha kabisa kuongeza uwakilishi 2021
 
👏👏👏👏
 
Points zimetosha ila uwakilishi utaanza msimu wa mwaka 2020/2021
 
Back
Top Bottom