Tanzania ni nchi yenye democracy ndani ya chama kimoja, ( ina chama kimoja tu cha siasa)

DR.RWEYENDERA

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
404
386
Democrasia na kuwa na vyama vingi ni vitu viwili tofauti

Tanzania ni nchi ambayo kila dalili inaonesha ni ya chama kimoja tu,
Chama tawala CCM , ndo chama pekee ambacho
1.mkutano wake mkuu unakuwa umeshehen afisa usalama wa taifa na ulinzi mkali sana,
2. Chama pekee kinachotawala mihimili yote mitatu ya dola, mahakama, na bunge, siku za karibuni kuna majaji walikuwa wanastaafu na unamkuta na kadi ya Ccm, pia SAA nyingine ni vigum kutenganisha nguvu ya Ccm na mahakama zetu, hii ni kwakuwa Ccm inasimama katika haki na usawa ambao vile vile unapitiwa na mahakama, jaji mkuu ana majaji wengine wanateuliwa na mwenyekiti wa Ccm au anayepaswa kuwa mwenyekiti wa Ccm, suala la bunge spika wa bunge niliowahi kuwashuhudia wanatoka Ccm , ambavyo inafanya niamini spika wa bunge lazima hawe Ccm,
Miswada na mijadala ya bungeni haijawahi kupita ya chama pinzani , ni ya Ccm tu, sasa utasemaje kuwa kuna vyama vya siasa vingine
3. Ccm ndo chama pekee ambacho SAA nyingine kinaratibu vyama vya muda viendeshwe vipi, ndo inewapa viongozi kama maalimu seif, lipumba, mbowe na wengine ni wana Ccm hai ila wapo kutimiza malengo ya nchi kuonekana nchi INA democrasia ya vyama vingi,
4. Ccm ndo chama ambacho mgombea wa urais akipitishwa mnajua automatically ni raid,
5. Ccm ndo chama ambacho kina hazina ya wazee wenye busara wanaokaa chimwaga kutatua mambo, vyama vingine wazee wake huibuka wakati wa matukio na matamko tu,

Nataka kuwaeleza watanzania mjue kuwa sisi hatuna vyama vingi vya viasa, tuna chama kimoja cha siasa vingine ni vikundi vya wanahatakati tena wasiojua wanaharakatia nn,

Vikundi hivyo vilisajiliwa tu kutimiza malengo ya IMF,WB, IrDS na wengine,
 
Umezunguka mno bila sababu, kwa kifupi CCM ni chamaDOLA na uwepo wake ni KUBARIKIWA KISHERIA siyo kwa kusajaliwa soma sheria multparty uone.Thatswhy wanaohama ccm huwa hawarudishi KADI maana uanachama wa ccm kwa waliokuwepo kabla ya multiparty ni wa MILELE labda wakufukuze tena kwa vikao.So kuiondoa ccm ni mpaka kizazi kile kipite na muomuombee mwenyekiti wa sasa afute huu utaratibu wa KIZAZA KILE kurithisha watoto wao uongozi
 
Back
Top Bottom