Tanzania ni nchi ya masihara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni nchi ya masihara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngambo Ngali, Jul 7, 2011.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kupitia Tangazo la serikali GN NO 185, 186 na 189, serikali imefanya mabadiliko kwenye ada inayolipwa na watu wanaotaka huduma ya vibali vya Makazi ( residence permits),visa, ada ya maombi ya uraia na vibali vya kuishi.

  Kinachonishangaza kwenye upande wa huduma za makazi kuna category nne:

  Class A: Wawekezaji wakubwa kwenye makampuni ya madini, kilimo, uvuvi na viwanda
  Class A: Peasants (wakulima wadogo)
  Class B: Wafanyakazi kwenye viwanda, makampuni Binafsi,Mashirika ya umma,Uvuvi, Madini, usafirishaji na fani ya muziki
  Class C: Wamisionari,Watafiti na wanafunzi

  Masihara yanakuja pale unapoambiwa kuwa peasant anatoka kwao kuja kufanya kazi Tanzania na sisi tunatoa kibali cha makazi kwa mtu kama huyo.

  Ni sawa kuleta peasants toka nje kuja kufanya kazi hapa kwetu?
   
 2. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kuna siku viongozi weengi saa wa hii nchi watafungwa baada ya kufilisiwa.labda hata kunyongwa.
  kama yametokea tunisia na egypt tanzania ni suala la mdatu.yatakuaja.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hata mimi ilibidi nisome mara mbilimbili maana sikuamini macho yangu!

  Niliiweka kiporo nije kuuliza wahusika wanipe undani zaidi wa hekma iliyoongoza uamuzi huo.
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  WOS, hakuna atakayepuja jibu na ukipewa hutamuelewa,

  Nilisoma kwa kiswahili nikaona wakulima wadogo nikadhani wamekosea, gazeti la kiingereza wameandika peasant nikapata goose pimples.

  Tujiulize seriously, hivi huku juu viongozi wanafikiria kweli au wamechoka. Usikute mtu kapewa mamilioni kutengeneza hii GN akafanya Copy and Paste toka South Africa.
   
Loading...