Tanzania ni nchi ya Ajabu sana. Tuna kiwango kikubwa sana cha ustaarabu

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,124
2,000
Habari za wakati ndugu zangu wapendwa;

Andiko langu hili ninaliandika katika hali ya furaha na huzuni kwani najua kwamba kila atakaeseoma atatoa na tafakari yake.

Mimi ni Mtanzania ambaye kwa kiasi fulani huwa ninafuatilia siasa na uchumi wa nchi yetu.Kwa kipindi cha zaidi ya Miaka 30 nimefuatilia serikali na siasa za nchi yetu katika kiwango ambacho kinaofautiana kwa sababu ufahamu, uelewa na mtazamo wangu juu ya Mambo fulani umebdailika sana katika kipindi hiki kutokana na mazingira na mazingara.

Hata hivyo kuna jambo moja ambalo lazima niliseme. Tanzania kama taifa tunayo jamii ambayo iko katika kiwango kikubwa sana cha ustaarbu na werevu. Hii ni katika siasa na uongozi na katika mitaa na vijiwe. Ukitaka kuelewa hili jaribu kufuatilia historia ya siasa za tanzania na watu ambao wamewahi kuibuka na kuanguka katika siasa. Fuatilia pia eneo la uchumi na hata kijamii utagundua kwamba taifa letu limestaarabika sana.

Kwa nini nasema tumestaarabika?

Kwanza ni katika eneo la TOLERANCE kuvumiliana bila kujali tofauti zetu.Watanzania tunavumiliana sana,wachache wenye muhemuko wanaishia kuonekana vituko na ndio maana tunaona hata sasa kuna ambao wanamuunga mkono Mama Samia huku wakimkosoa JPM as if Mama Samia hakuwa makamu wa JPM. Kwa ufupi Watanzania wamempa mama Samia Nafasi ya kujenga legacy yake mwenyewe bila kutegemea kivuli cha JPM jambo ambalo utaliona katika jamii iliostaarabika tu.

Pili ni uwezo wa kubadilika kutokana na mazingira.

Watanzania wan uwezo mkubwa sana wa kubadillika kutokana na mazingira na kukubliana na hali halisi.Utaona katika chaguzi na harakati mbalimbali ambazo zilifanyika watu walikuwa wepesi sana kuhama katika jambo moja na kuendelea na maisha as if hakuna kilichotokea. Uwezo huu wa kubalance na kuaadapt ni wa kipekee ambao unapatikana katika jamii zilizostaarabika tu.

Tatu ni uwezo wa kubalance mambo;
Ukiwaangalia watanzania unaweza kufikiri kwamba huwa wanaburuzwa na kuendeshwa lakini asilimia kuwa ya watanzania wanatabia ya kubalance mambo kwa kadiri ya upeo na uwezo wao wa kuelewa. Ni wazito wa kukurupuka kama hawajaelewa jambo na hata wakimfuata mtu na kumuunga mkono wanakuwa na machale na mashake mpaka wathibitishe kwamba wako na mtu sahihi.

Nne ni uwezo wa kupambania maslahi yao binafsi;
Hili ni eneo ambalo watanzania wako vizuri, Kila mtanzania huanza kwa kuangalia maslahi yake kwanza, kisha maslahi ya jamii yake na mwsho maslahi ya jamii kwa ujumla. Ndio maana katika kila eneo utakuta watu wanaangalia namna ya kuneemeka wao na wale wa karibu yao kisha ndo mengine yafuate, hawaidhulumu nchi bali wanahakikisha kwamba katika kulitumikia taifa hawaishii kutumika tu bila kupata na wao kidogo, ambayo inaitwa win win.

Kuna maeneo mengi ambayo watanzania wameonesha upekee na ukomavu wao ambao unapatikana katika jamii ambayo imestaarabika tu na sio jamii za watu wajima (Primitive) ambao hawajua thamani ya utu, uhai, amani etc. Kwa andiko hili sisemi kwamba hakuna element watu ambao wameonesha kutokustaarabika na ambao tupo na kama wana jamiii au viongozi.Tuendelee kuoneshana njia na kukemeana pale tunapoona wenzetu wanaenda njia ambayo sio

Nawatakieni maisha mema.

Tutaona nakatika Mawingu.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,270
2,000
Siyo kwamba kiwango chetu cha kutokujua mambo yanayotuzunguka ndiyo kikubwa!! (Primitive ratio).

Mifano ipo mingi sana ku justify point yangu kama ikihitajika!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom