Tanzania ni nchi ya 88 kwa Uvumbuzi (Innovation) Duniani na ya pili kwa Afrika Mashariki

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Jarida la Global Innovation Index limeionyesha Tanzania kuwa nchi ya 88 katika ugunduzi kwa mwaka 2020. Jarida hilo linatolewa na World Intellectual Property Organization, WIPO.

Tanzania imekuwa ni nchi ya pili kwa Afrika Mashariki, ya kwanza ikiwa ni Kenya ambayo imeshika nafasi ya 86. Rwanda ni ya 91 na Uganda imekuwa ni nchi ya 114

Jarida hilo limeiweka Switzerland (Uswizi) kuwa Nchi ya kwanza kwa ugunduzi ikifuatiwa na Sweden na Marekani.

Aidha nchi tatu za mwisho kwa Ugunduzi ni Yemen, Guinea na Myanmar.

Release of the Global Innovation Index 2020: Who Will Finance Innovation?
 
Attachments

  • wipo_pub_gii_2020.pdf
    22.5 MB · Views: 19
Tanzania ingeweza kuwa nafasi ya juu kama mambo ya ugunduzi yangepewa nafasi.

Kuna watu waligundua helicopter badala ya kusaidiwa wakaanza kuulizwa vibali.

Kuna watu walizalisha umeme wakaanza kuulizwa vyeti kama sio rai kuingilia kati sijui ingekuwaje.

Kuna watu wanatengeneza generator za umeme tena zinatumia solar wengine wanatengeneza incubator lakini hawapoti sapoti inayostahili juzijuzi mwingine katengeneza bajaj hiyo ni mifano michache.
 
"Wagunduzi wapo, ila usaidizi ndio hakuna"
Nadhani hiyo ripoti ingeandika hivyo ingekua poa sana
 
Jarida la Global Innovation Index limeionyesha Tanzania kuwa nchi ya 88 katika ugunduzi kwa mwaka 2020. Jarida hilo linatolewa na World Intellectual Property Organization, WIPO.

Tanzania imekuwa ni nchi ya pili kwa Afrika Mashariki, ya kwanza ikiwa ni Kenya ambayo imeshika nafasi ya 86. Rwanda ni ya 91 na Uganda imekuwa ni nchi ya 114

Jarida hilo limeiweka Switzerland (Uswizi) kuwa nchi ya kwanza kwa ugunduzi ikifuatiwa na Sweden na Marekani.

Aidha nchi tatu za mwisho kwa Ugunduzi ni Yemen, Guinea na Myanmar.

Release of the Global Innovation Index 2020: Who Will Finance Innovation?
Ugunduzi wa nn mbona cjaelewa
 
Gunduzi zipo ila hazifiki popote sababu elimu ni ndogo juu ya ufanyaji gunduzi ili zihalalishwe na serikali haitoi elimu hiyo ili kusaidia kuboresha gunduzi hizo.
 
Tanzania ingeweza kuwa nafasi ya juu kama mambo ya ugunduzi yangepewa nafasi.

Kuna watu waligundua helicopter badala ya kusaidiwa wakaanza kuulizwa vibali.

Kuna watu walizalisha umeme wakaanza kuulizwa vyeti kama sio rai kuingilia kati sijui ingekuwaje.

Kuna watu wanatengeneza generator za umeme tena zinatumia solar wengine wanatengeneza incubator lakini hawapoti sapoti inayostahili juzijuzi mwingine katengeneza bajaj hiyo ni mifano michache.
helkopter gani mpya unaigundua leo mkuu.

maana zipo za kizungu ambazo tayari zimewekeza utaratibu namna ya kufanya kazi, hiyo yako sio mpya na haiko salama, lazima tukukabe usijeangukia nyumba za watu,au ukaanguka nayo porini huko.

wewe gundua dawa ya ukimwi leo, uone kama kuna kima atakugusa.
 
Ila hawajawahi kutamani nchi zao ziwe kama Afrika
serious!!! au kwavile hujawahi sikia wakisema mkuu??

hawatamani kuwa kama waafrica, leo hii wale jamaa ingetokea tubadirishane maeneo wangekubali.
 
helkopter gani mpya unaigundua leo mkuu.

maana zipo za kizungu ambazo tayari zimewekeza utaratibu namna ya kufanya kazi, hiyo yako sio mpya na haiko salama, lazima tukukabe usijeangukia nyumba za watu,au ukaanguka nayo porini huko.

wewe gundua dawa ya ukimwi leo, uone kama kuna kima atakugusa.
Basi tumegundua dawa ya corona umeridhika
 
Tanzania ingeweza kuwa nafasi ya juu kama mambo ya ugunduzi yangepewa nafasi.

Kuna watu waligundua helicopter badala ya kusaidiwa wakaanza kuulizwa vibali.

Kuna watu walizalisha umeme wakaanza kuulizwa vyeti kama sio rai kuingilia kati sijui ingekuwaje.

Kuna watu wanatengeneza generator za umeme tena zinatumia solar wengine wanatengeneza incubator lakini hawapoti sapoti inayostahili juzijuzi mwingine katengeneza bajaj hiyo ni mifano michache.

huo si ugunduzi, elewa maaana ni innovation na kufanya assembly
 
Asante kutaarifu., najua 'NYUNGU' imetupaisha, ila sijui Nyayo wametuzidi kwa kipi.
 
Back
Top Bottom