Tanzania ni muhanga mkubwa wa biashara haramu ya meno ya ndovu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni muhanga mkubwa wa biashara haramu ya meno ya ndovu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dark City, Jul 22, 2009.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pamoja na kuwa watuhumiwa sita waliohusika na dili la kusafirisha meno ya tembo kwenda Phillipines na Vietnamu walifikishwa mahakani jana, habari nilizozipata ni kuwa Tz ni mhanga mkubwa wa hiyo biashara. Huu ni mzigo wa watatu mkubwa kukamatwa katika nchi za Asia ya mbali na taarifa zilizopo zinaonesha kuwa hali ni mbaya sana. Hiyo document hapo Forensic Tools Battle Ivory Poachers: Scientific American inatoa picha zaidi.
   
  Last edited: Jul 22, 2009
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii ni sawa na biashara ya dawa za kulevya. Au inafanana kiasi na issue ya ufisadi. Watakaokamatwa sio wahusika ila ni punda wanaosafirisha au wanaofanya kazi ya uchuuzi. Wenyewe wanaoipitisha Airport na bandarini kiulaini wanaendelea kupeta. Hakuna anayejali, This is Tanzania. Inabidi tuizoee.
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Wakuu nilishangaa sana kuona waliopandishwa kizimbani si wahusika!!! Aliyepeleka mzigo kuupakia ni nani?? Na alishirikiana na nani katika Wizara?? Hawa ndiyo tunawataka!!! A tuseme hayo makampuni ya clearing and forwarding waliingizwa mkenge na kuandika kuwa mzigo ni wao?? Kama walifanya hivyo, ni kwamba kesi inawaangukiwa wao kama ambavyo vinara wa EPA wengi walitumia watu au makapuni mengine kujichotea pesa na wenye makampuni halisi wanakoma ubishi sasa hivi. Tusubiri tuone?? Watakuambia hakuna ushahidi wa kutosha kumpata mwenye mali na pia maafisa wa mali asili na utalii. Au tuseme ndiyo plan B ya finances of 2010?? baada ya ile ya EPA kuwaka moto!!!!???

  Halafu pia kule TRA si wanakagua mzigo in and out?? Au huwa wanaamini kinachoandikwa na mteja wao tu?? Tuambiwe na kitengo cha Inspection hakifanyi kazi yake sawa sawa!!! Kama ni kesi basi vinara bado hawajafikishwa kwa pilato. Kama serikali haihusiki na iko serious tunataka tuone haki ikitendeka na si kutafuta dogs wa kufa nao!!!!
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu TRA kwenye kunalalamikiwa ufisadi sasa unategemea nini kama dili za kifisadi linaptia huko. Si ndio njia ile ile? Chammuhimu ni kuwa kesi hiyo imeonesha kuwa TRA, bandari zetu (port of entry and exit) nako ufisadi ni kama kazi. Hii inaonesha uozo wetu mkuu.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wakuu mkisoma vizuri hiyo taarifa ya watafiti nguli wa kimataifa, mtaona kuwa kazi ya biashara ya pembe za ndovu kama ilivyo unga haifanywi na watu viazi (i.e watu wa hovyo hovyo); kwa pesa na akili. Ni biashara ya magenge yenye pesa za kutisha. Mizigo 3 yote iliyokamatwa 2006 ilitokea Tz na huu wa mwaka hivi karibu pia umetoka hapa nchini. Kwa uzoefu wangu watu wa pembe za ndovu hawawezi kukamatika katika mazingira ya sasa ambapo serikali yetu ni kibogoyo kwa kila kitu na imelala usingizi wa pono linapokuja suala la kuthubutu! Nadhani sasa kama wapiga debe hawataibuka kupiga kelele, tembo wetu wanaisha. Vyombo vya habari inabidi sasa vilichukue suala hili juu kwa juu pamoja na ufisadi ili tuokoe hicho kidogo kilichobaki! Tukithubutu kufanya hivyo tunaweza kuhakikisha kuwa watoto wetu na wajukuu zetu wataowaona tembo wetu na meno yao badala ya picha!
   
Loading...