Tanzania ni moja ya nchi chache zenye hali ya hewa nzuri duniani

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
488
f617dddd0c6c11af7fb657858e2b81cd.jpg


“Dar es Salaam: Annual Weather Averages. January is the hottest month in Dar es Salaam with an average temperature of 27°C (81°F) and the coldest is July at 23°C (73°F) with the most daily sunshine hours at 10 in September.

January ndio mwezi wa joto zaidi. Wastani wa joto la mwezi huo ni nyuzi 27 (81F). Wape watu wa Marekani na Ulaya joto hilo kwa mwaka mzima watafanya sikukuu mwaka mzima.

Mwezi wa baridi sana ni July wenye joto la nyuzi 23 (73F). Kaka tafadhali. Hapo ndio utakuta wazungu wa nchi kama Ujerumani wanachanganyikiwa. Ni vibukta tu barabarani na kwenye mapaki wakiota jua.

Lakini watanzania hatuachi kulalamika jua kali. Jua kali nendeni Libya ambako joto linafikia nyuzi 56 (173F). Miji ya joto ya Marekani kama Las Vegas na Phoenix joto la zaidi ya nyuzi 37.8 (100 F) Ukienda kimasihara unapigwa homa ya joto kali (heat stroke)

Tanzania hakuna joto. Kuna watu wasiojua kudhibiti joto. Utakuta mtaa mzima nyumba zimesongamana, madirisha yamezibana na hakuna hata mwenye feni la mezani.

Wanaojimudu kidogo wana mafeni ya darini. Matajiri na maofisini ndio kuna viyoyozi vya ndani au vya kuning’ing’inia nje. Viyoyozi hivi havina raha kwa sababu ni baridi sana na vinaleta magonjwa ya baridi bila ya watumiaji kujishtukia.

Joto la Tanzania linadhibitika kwa madirisha makubwa bila hata ya kuhitaji kiyoyozi. Lala kwenye chumba kisicho kwenye msongamano, kuwa na madirsha mawili yanayoingiza hewa kwa mbele na ubavuni uone kama utahitaji kiyoyozi.

Njia nyingine ya kulimudu joto la Tanzania ni kuishi nyumba za gorofani na kuwa na madirisha yanayopitisha hewa. Gorofani upepo wake umepoa kuliko nyumba ya chini.

Najua watapiga kelele pesa, pesa, pesa. Sio pesa ni mipango au wanasema miundo mbinu. Wakazi wote wa Magomeni wanaweza kuishi kwenye magorofa mawili au matatu yenye nafasi na kuacha eneo la wazi kubwa kwa kupanda miti na kuleta hewa safi.

Vilevile tubadilishe mfumo wetu wa viyoyozi. Viyoyozi vyetu ni vya kufunga katika kila chumba. Wenzetu wanatumia Central Cooling System. Mashine ya kiyoyozi ni moja inakaa nje ya nyumba. Halafu inasambazwa kama mabomba ya maji kufikisha hewa katika kila chumba ndani ya nyumba. Haina mzizimo wa friji kama viyoyozi vyetu vya Tanzania. Na kwenye vyoo kuna njja za kutolea hewa chafu. Jikoni kuna njia ya kutoa moshi nje.
689b9fad026c60b89c4dbcaba95ae469.jpg


8c26ec877478d0e974c135e5e046ac8c.jpg


f15a2f0da176164715ab6113d922b42c.jpg


Watu wote wa Magomeni wanaweza kukaa kwenye huu mjengo mmoja na ardhi inayobaki tukaweka gadeni, shule, hospitali na huduma nyingine muhimu.

eeec49801831c5d10e18cfaa7266c163.jpg


Watu wakielimishwa ndio mwanzo wa utekelezaji na uthubutu. Mwanzo wa ngoma ni lele mama!


Watanzania tungekuwa na usiku wa namna hii jee?

1163f4d5a5a7eb1e3b0b0229b71731fa.jpg
 
7d031f1a9feb79c6502a9d9e8c3c8d26.jpg


Watasema moto. Mjengo huu ukiwepo Magomeni Mapipa moto ukiwaka dakika sifuri magari ya faya yatakuwa yameshafika. Haya niambie gari la faya linafikaje bondeni Magomeni mzimuni?
 
Niliwahi kumsikia rais mmoja wa zamani akisema tungekuwa na mabarafu watanzania tungekufa wote.
 
69ac1780e4019841e02d12f5192cefca.jpg


Kiyoyozi nioze mapafu?

Hapo ni kufungua madirisha tu. Na ukifinga madirisha hivyo vidirisha viwili vidogo kwenye sakafu ndivyo vinavyotumika kuingiza hewa ya kupoza chumba kizima.

Uzuri wake madirisha hayo hayazuii kuweka nondo za kuzuia vibaka.
 
Vyumba vya aina hii vinalipiwa bei mbaya kwenye mabichi yenye hali ya hewa nzuri. Sisi hata madirisha vioo tunahakikisha hayafunguki
88f51dc19afe85979e75234fdc5d619b.jpg
 
Back
Top Bottom