Tanzania ni kubwa = Ngumu kutawalika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni kubwa = Ngumu kutawalika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, May 8, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli nimekuwa pembeni kuangalia muelekeo wa Tanzania ,nilichokiona ni kule tunakoelekea hakuna faida nasi na nikionacho ni giza tupu ,kwa maana ya machafuko yatakayoisambaratisha Tanzania haswa upande wa Tanganyika na kuiwacha kama Somalia.

  Inawezekana kabisa mmoja wetu akalipinga hili na kuona ni kama ndoto, huyo atakuwa ni mtu asiekuwa na uelewa wa utitiri wa matatizo yaliomo hivi sasa ndani ya Tanzania.

  Kama kulinganisha labda itasemwa mbona wakati wa Nyerere ilitawalika ,huyo atakuwa hajui maana ya demokrasia ,wakati wa mwalimu hakuna aliethubutu kusema kitu seuze kuropoka katika mikutano ya bunge, ni mtu mmoja tu aliewahi kulumbana na Mwalimu ndani ya Bunge nae si mwengine ila ni Seif Sharifu ,ikawa patashika.

  Sasa tupo katika utawala wa kibabe ,kila mmoja mmbabe Raisi mbabe ,Mawaziri wababe, yaani mpaka yule balozi wa nyumba kumi nae huwa ni mbabe.
  Nchi yetu Tanzania kusema kweli ni kubwa ,kiasi ya kukosa uongozi unaoweza kusimamia kila kipembe cha nchi hii na kuona haki inatendeka na kutendwa katika misingi ya usawa kwa kila mzalendo.

  Sudani ni kubwa na hivi sasa wapo katika mchakato wa kuigawanya katika mapande ili kuepuka ukosefu wa kiutawala ambao imeonekana kuna wengine wanadharauliwa na hawatendewi haki. Nakumbuka Kigoma iliwahi kusema ikiwa haitatendewa haki itajitenga aidha kuwa upande mwengine na kuachana na Tanzania.

  Utaona kama haiwezekani lakini kwa jinsi ya hapa tulipo ,matukio ya kujitenga hayapo mbali na yanachochewa na serikali zilizopo madarakani kwa kutokutenda haki na pia ongezeko la kulindana na kuhifadhiana kwa wezi waliomo ndani ya madaraka ,inakuwa sheria haziwagusi ,wakati wananchi walio wengi wapo katika shida ,na shida zikizidi kila upande utaamua kujikata kivyakevyake,kama utaangalia chokochoko za Zanzibar na Pemba za kutaka aidha kuwa na mamlaka yake au kuwa mtazamo wake kiutawala na hata kule Pemba kufika kusema waachiwe wajitawale ,kusema kweli hawatakuwa na tofauti na wale wa Kigoma.

  Yote hayo hutokana na shida zinapozidi na wananchi kushindwa kuzivumilia ,kama ikitokea Tanzania kugawika katika mapande manne unafikiri ,ni mikoa gani ingeweza kukaa pamoja.
  Naota kuiona East Tanzania as South Yemen or North Korea au United States of Tanzania.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  May 8, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ni lini Kigoma ilitaka kujitoa Tanzania? Acha mawazo ya kibaguzi ya ki-CUF ambao hawapendi Tanzania kuendelea kuwa nchi moja!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,164
  Trophy Points: 280
  Muda wa utawala wa kimajimbo ndio huu.
  Tunahitaji mfumo mpya.
  Tusiogope kukabiliana na changamoto mpya
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  May 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Tanzania ni ngumu kwa kiongozi mwenye simple mind, mwepesi wa kufikiri, kiongozi anaejizungushia vilaza wenzake katika madaraka, kiongozi anaewazia mapenzi, kiongozi anaetumia muda wake katika kuhudhulia sherehe za jando na unyago kijijini kwao kila mwezi, ni ngumu Kuitawala.
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wewe ndo unachekesha kabisa! Ungesema kinyume chake ningekuelewa. Mtu akishindwa kuitawala tanzania atatawala nchi gani tena hapa duniani? Ni nchi pekee duniani yenye kutawalika tena kirahisi. Wapi pengine?
   
 6. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Umenifanya nicheke sana! Kwako wewe kutawala ni sawa na kuchunga mbuzi sio ukimwona anatoka kundini inapiga kirungu sio kama ni hivyo Obama au HU JING TAO anayokazi! Kinachotawala sio usimamizi wa kila pembe ni sheria inayotekelezwa kikamilifu, uadilifu wa kiutedaji, kujituma na kutenda kwa ajili ya wengine. Kiongozi anayejali watenda kazi wake bila shaka hawatamwangusha!
  Kama ni kutawalika tumetawalika sana na tunaendelea kutawalika ila tunapelekwa pelekwa tu na hawa watawala wanafiki, wasio jali wanaowatawala! nahama kidogo"Hivi niulize swali kama huu mgomo ungekuwa ni wa wakulima amabo ni 80% angethubutu kusema hataki kura yao? Kwa maana nyingine concern yake kubwa ni kurudi madarakani wa/kazi mtajua wenyewe mimi naenda kumwona Linda na Gathe! au Billy Zane, Pia nitapitia Hollywood kuona tuzo za grammy"

  Kwa kigezo chako Rwanda na Burundi zingekuwa ni nchi zinazotawaliwa kiu rahisi kama kusukuma mlevi! Endelea kuota lakini hautaiona Tanzania iliyogawanyika hata siku moja
   
Loading...