Tanzania ni kinara wa misamaha ya kodi-utafiti

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,378
2,000
Tanzania inaongoza kwa kutoa misamaha mikubwa zaidi ya kodi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki pamoja na bajeti yake kuwa tegemezi kwa misaada ya nje kwa zaidi ya asilimia 30.
Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rose Aiko, mchambuzi wa utafiti toka Uwazi (Pata

picha kamili) alipokuwa akiwasilisha muhtasari wa utafiti uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Uwazi-Twaweza kuhusiana na misamaha ya kodi
Tanzania.
Aiko alisema kiwango cha misamaha ya kodi inayotolewa Tanzania ni kikubwa ukilinganisha na misamaha inayotolewa na nchi za Uganda na Kenya.

“Hapa kwetu, kati ya miaka ya 2005/06 na 2007/08, misamaha ya kodi ilikadiriwa kuwa wastani wa asilimia 3.9 ya pato la taifa. Mwaka 2008/09, ilikuwa asilimia 2.8 na mwaka 2009/10 asilimia 2.3,” alisema.


Aiko alieleza wakati hali iko hivyo nchini, misamaha ya kodi katika kipindi chote hicho kwa
Kenya ilikuwa ni asilimia moja ya pato la Taifa na kwa Uganda ilikuwa ni asilimia 0.4.
Alisema ukiachilia mbali Uganda ambayo inatoa misamaha kwa kiwango cha chini kabisa, kama

Tanzania ingerekebisha viwango vya misamaha ya kodi ili kulingana na kiwango kilichofikiwa na Kenya, zaidi ya Sh. bilioni 600 zingeokolewa kwa mwaka 2007/08 peke yake.

Aidha, Aiko alisema ukubwa wa kiwango cha misamaha inayotolewa unaweza kuelezwa kwa

kulinganisha na malengo ya ukusanyaji wa mapato ya kodi ambayo
Tanzania inashindwa kuyafikia.
“Mwaka 2008/09 na 2009/10, Serikali haikutimiza lengo lake la kukusanya mapato kwa wastani wa Sh. bilioni 453 kila mwaka. Katika kipindi hicho hicho, misamaha ya kodi iliyotolewa ilifikia wastani wa Sh. bilioni 724 kwa mwaka,” alisema. Alisema kama misamaha ya kodi ingetolewa katika kiwango

kinachofanana na kiwango cha misamaha ya kodi inayotolewa
Kenya, Sh. bilioni 484 zingeokolewa mwaka 2008/9 na Sh. bilioni 302 mwaka 2009/10.
Kwa maneno mengine, upungufu katika ukusanyaji wa mapato ungepunguzwa kwa kiasi kikubwa, alifafanua.

Kadhalika, Aiko alieleza kuwa wawekezaji wakubwa wa kimataifa nchini wananufaika zaidi na misamaha ya kodi kuliko makundi mengine yanayopata misamaha hiyo.

Alisema makampuni hayo ni yale yenye vyeti vya kupatiwa motisha vinavyotolewa chini ya sheria ya uwekezaji Tanzania na sheria ya kuendeleza na kulinda uwekezaji Zanzibar, ambayo yanapata misamaha inayofikia asilimia 45.12.

“Kundi linalofuata ni la walipaji kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) chini ya vifungu namba 220,223 na 224 ambalo linapata misamaha ya asilimia 24.22 na kundi la tatu ni la makampuni ya madini, chini ya Sheria ya Madini,” alisema Aiko.


Akijibu swali la NIPASHE lililohusu sababu za kufanya utafiti kama huu na kuutoa siku chache kabla ya uchaguzi, Mkurugenzi Mkuu wa Twaweza, Rakesh Rajani, alisema wao
kama taasisi hawafungwi na muda wa kueleza walichonacho.

“Sisi kama taasisi tunafanya tafiti nyingi. Tuliona umuhimu wa kufanya tafiti za misamaha ya kodi ili wananchi waone
kama kutolewa kwa misamaha hiyo kuna ulazima kwa nchi inayokabiliwa na changamoto ya kukusanya fedha za kutosha kugharimia bajeti yake,” alisema.
Alisema utafiti wao umetumia takwimu za ripoti ya mapato kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wameyatoa matokeo ya utafiti huo sasa ili Watanzania waelewe kuhusiana na rasilimali zao na wakapige kura wakiwa na ufahamu huo.CHANZO: NIPASHE
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,378
2,000
Si inaongoza tu bali ni Maarufu kwa msemo rahisi
wakati huku nje Ughaibuni Serikali inategemea kodi toka kwa wananchi na wageni ukinunuwa kitu chochote Dukani basi ujuwe utalipa kodi ya Serikali ndio maana Nchi za wenzetu

zinaendelea kwa kila kitu zina mabarabara kwa juu na chini,zina Town Train bus zinazotombea katikati ya mji hakuna huku shida ya Usafiri kwa mfano mimi ninapoishi mji

ninaoishi takriban una watu karibu wanapata 20 millioni na kila siku watu wanakwenda makazini na hakun ahata siku moja kuna shida ya usafiri itakuwa kaji mji chetu cha Dares-salaam hakizidi zaidi ya watu 4 millioni shida ya usafiri ipo kwetu hapo Dar. Kasheshe kweli

Nchi yetu imeoza hatuna viongozi wazuri wanaoipenda nchi yao kila unayemuona Kiongozi kazi yake kubwa ni ufisadi tutakwenda kweli kule tunakotaka kwenda? Safari yetu naona inaishia shimoni tu. Huku ni kuchakachuwa
 

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,508
0
Uzalendo Tanzania Kwishny. Hatuna wazalendo tena ni Mafisadi tu. Na wateule wachache ambao kutokana na uchache wao wanadhulumiwa.
Nchi yetu imeoza hatuna viongozi wazuri wanaoipenda nchi yao kila unayemuona Kiongozi kazi yake kubwa ni ufisadi tutakwenda kweli kule tunakotaka kwenda? Safari yetu naona inaishia shimoni tu. Huku ni kuchakachuwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom