Elections 2010 Tanzania ni kinara wa misamaha ya kodi-utafiti

ehamaro

Member
May 11, 2009
10
0
Tanzania inaongoza kwa kutoa misamaha mikubwa zaidi ya kodi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki pamoja na bajeti yake kuwa tegemezi kwa misaada ya nje kwa zaidi ya asilimia 30.
Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rose Aiko, mchambuzi wa utafiti toka Uwazi (Pata picha kamili) alipokuwa akiwasilisha muhtasari wa utafiti uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Uwazi-Twaweza kuhusiana na misamaha ya kodi Tanzania.
Aiko alisema kiwango cha misamaha ya kodi inayotolewa Tanzania ni kikubwa ukilinganisha na misamaha inayotolewa na nchi za Uganda na Kenya.
“Hapa kwetu, kati ya miaka ya 2005/06 na 2007/08, misamaha ya kodi ilikadiriwa kuwa wastani wa asilimia 3.9 ya pato la taifa. Mwaka 2008/09, ilikuwa asilimia 2.8 na mwaka 2009/10 asilimia 2.3,” alisema.
chanzo :: IPPMEDIA
 
Sio kweli labda tumuulize kwanza kikwete,kinana,makamba na mafisadi wanosamehewa kodi.........
 
Back
Top Bottom