Tanzania ni kama mtu anayejipiga risasi huku akijitapa kushinda marathon

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Amani iwe kwenu wadau.

Nisiwachoshe sana. Nimeamka na kuanza kuangalia taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Hai akiwa anamgalagaza mwekezaji wa kilimo huko wilayani Hai ambaye kwa haraka anaonekana alitapeliwa na watu wa Bakwata na kuuziwa Ardhi ya Bakwata kinyume na utaratibu.

Ingawa hii taarifa inaonekana ni ya Mwaka 2018, ila kwenye mitandao bado inapatikana. Kibaya sijawai kama Serikali iliwai kulitolea ufafanuzi hili suala.

Kilichonishangaza kwenye taarifa ile ni yule Mkuu wa Wilaya kuwa Waziri wa Ardhi, Kamishna wa Ardhi, Mwendesha Mashtaka, Polisi na Mahakama kwenye lile tukio.

Yeye ndiye aliyetoa shutuma, akashtaki, akakamata na kutoa hukumu palepale. Yeye pia ndo aliyetoa maamuzi ya kugawa ardhi kama yeye ndo kamishna wa Ardhi au Waziri.

Kibaya zaidi hakuangalia investment aliyofanya yule mwekezaji, aliamuru mara moja ndani ya saa 48 vitu vyote alivyoinvest yule mwekezaji vitolewe.

Katika kipindi kirefu sasa Tanzania tumekuwa tunafanya vibaya sana hasa kwenye urahisi wa kufanya biashara.

Tumejenga picha kimataifa kuwa wawekezaji wanaonewa, hawapewi nafasi ya kusikilizwa. Na pia wanafanyiwa maamuzi ya hovyo yasiyozingatia uwekezaji wao wa pesa.

Hili tukio la huyu Mkuu wa Wilaya limethibitisha Madai haya na nina uhakika video hii ikisambaa huko nje tutakuwa tunazidi kujipiga risasi wakati tukitegemea kushiriki Marathon.

Aliwai kuongea sana Ndugu Mwambe wa TIC kuwa hawa wawekezaji lazima wapewe treatment ya kipekee kwa kuzingatia reputation ya taifa kimataifa na hasa kiuchumi na mitaji waliyowekeza hapa nchini. Ndiyo, huu ni mwaka wa uchaguzi na CCM inataka kura za Waislamu ila kwa kitengo hichi napenda kusema tumezidi kujiweka vibaya hasa kiuchumi kwenye suala la uwekezaji.

Mh. Magufuli kaa vizuri na watendaji wako hasa wa chini. Nchi haiko vizuri kimataifa ikiwemo kwenye suala la uwekezaji. Naomba umtume Waziri wako mwenye akili kidogo Hussein Bashe akaliweke sawa lile jambo kabla wabaya wako kina Kigogo, Karume na Maria Sarungi na Zitto kuanza kuisambaza ile video jambo ambalo litaiharibu nchi kiuwekezaji na kimataifa.

Mwisho, Mh. Waziri Mkuu - Wizara ya uwekezaji ipo chini yako sasa. Toa maagizo jambo lolote linalohusu uwekezaji lisitolewe maamuzi bila ridhaa yako.

Hakuna shida Bakwata kurudishiwa eneo lao ila kuna tatizo gani kama mwekezaji angeruhusiwa kulima na kuvuna yale mazao yake aliyolima?

Tanzania bila umaskini inawezekana!

Tunaitaji akili kubwa na hekima ya kutosha.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom