Tanzania ni haki ya wote, hakuna mwenye haki miliki

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Muda huu niko job mwenye matokeo zaidi kutoka MUVI TV atujuze ila hiyo ni salamu kwa CCM kutoka Zambia mnamo mwaka 2015,
Watu wa Zambia wanasemaone Zambia one nation, no one can own Zambia Forever si maneno yangu bali ni maneno ya wapiga kura waliokuwa wakiimba ndani ya MUVI TV leo huko zambia.

Ndugu Watanzania Kauli hii ya Wazambia imenikuna kichwa sana "One Zambie one nation, no one can own Zambia forever." Habari hii nimeinukuru kutoka kwa mdau aliyeleta mada ya humu jamii forums kuhusu uchaguzi wa Zambia unaoendelea hivi sasa. Kauli mbio hii ya Wazambia imekaa vizuri mno na ni falsafa yenye kuleta matumaini na haki za kitaifa bila kujali majina ya watu.

Moja ya malalamiko nchini mwetu ni kurithishana madaraka kifamilia, lakini mapinduzi ya masanduku ya kura yangefanyika kwa uhalali na hakika historia itabadilika na wenye majina itabaki histora kurithishana vyeo na kukirimiana nafasi za uongozi kwa maana ya kufuata miongozo sahihi ya demikrasia.
 
Jitihada za serikali ya CCM na CCM yenyewe ni kuhakikisha wanaendelea kushika dola kwa gharama yo yote, kwamba maendeleo nchi hii inapata au la, lakini hauli hii ya kwamba "Tanzania mmoja na ni taifa moja, na hakuna mmoja kuihodhi forever" ina mshiko, na hili ndilo linalotutesa na hakika mwamko kama wa Wazambia unazidi kukolea hadi vijijini.
 
hii kauli mbiu inatufaa saana watanzania kwa safari yakuelekea 2015 ili kila mtu aielewe! inaeleweka na rahisi kutamkika!
 
Kuna mwanasiasa mmoja maarufu nchini aliwahi kusema kwamba ccm ndio watakao haribu amani ya nchi.

Ni silka za mtu mjinga kujiamini zaidi kunakoendana na uwezo mdogo wa kufikiri ndicho kinachowafanya ccm kuto jiandaa kisaikolojia kwamba katika siasa lolote linaweza kutokea muda na saa yoyote.

Nani alijua kama malawi , zambia ,kenya, etc mambo yangekuwa vile. Nani alijua kama watawala walio tawala muda mrefu itafika kipindi tawala zao zitaangushwa tena kwa aibu kubwa.

Hakuna chama chenye hati miliki ya kututawala watanzania milele , kwa sababu hata vitabu vitakatifu na misaafu yote vinatamka wazi kwamba hakuna utawala wa milele katika dunia hii ,utawala wa milele ni wa mwenyezi Mungu tu.

Hata kama si leo, wala mwakani na kuendelea ccm inapaswa kujiandaa kwamba uko muda watanzania watakiondoa madarakani kwani mtanzania wa leo si yule wa miaka ya 1995, 2000. Watanzania wa leo kula watakula lakini kwa kupeleka kura inakuwa ni siri yao.

Nani alijua kama ccm wataporomoka kura toka 82% hadi 58% mwaka 2010.
 
Sema alishindwa ule uchaguzi, walichakachua hadi aibu
 
Kuna wimbi la mabadiliko litakuja kupiga watu watakimbiana, dalili zipo wazi kabisa, kama hili la katiba wameingia kwenye mtego mbaya sana..
 
Na ukioma watu wanalazimisha kupata ushindi na kubaki madarakani ujue ni watu hatari sn hao.Na wataanguka tu kwani umma huamua kuchukua hatua hata wakilazimisha kwa nguvu lakini majeshi huwa yanasoma alama za nyakati
 
Back
Top Bottom