Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
TANZANIA ni nchi ya 10 barani Afrika kati ya nchi 16 kwa uzalishaji wa gesi asilia, huku ikishika nafasi ya 66 duniani, FikraPevu inaripoti.
Hatua hiyo imetokana na ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi asilia unaoendelea kufanyika, hali inayoleta matumaini kwamba taifa hilo linaweza kujikwamua kiuchumi ikiwa rasilimali hizo zitasimamiwa ipasavyo.
Kwa mujibu wa Wakala wa Nishati wa Kimataifa (International Energy Agancy – IEA), nafasi ya Tanzania katika uzalishaji wa gesi asilia inatokana na rekodi za mwaka 2011, ambapo taifa hilo lilizalisha meta za ujazo milioni 860 kwa mwaka.
ZAIDI...