Tanzania:nchi yenye raia na mambo ya ajabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania:nchi yenye raia na mambo ya ajabu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Mar 21, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  Nimefikia hitimisho hili baada ya kutafakari yafuatayo:

  • Hii ni nchi pekee ambapo raia wake wamefikia hatua ya kuishi kwa kufuata upepo wa matukio(yawe ya kisiasa au kijamii)ili mradi lililojadiliwa jana hata kama halijapatiwa ufumbuzi basi litafutwa kwa lililojitokeza leo(mfano jamii sasa imejikita kujadili swala la babu wa loliondo na kusahau kuwa nchi iko gizani)
  • Hii ni nchi pekee ambapo raia wake wanaishi kwa woga wa ajabu na kushindwa kujikita kutatua matatizo yao kwa kuwa tu wanaishi kwa fikra ya kuendeleza amani wakati kuna wananchi ambao mlo wa siku hawapati na wengine wanasaza na kutupa(unawezaje kuwa na jamii yenye amani wakati wengi wanashinda na njaa wakati wachache wameshiba na kusaza?
  • Hii ni nchi ambayo viongozi wangependa waheshimiwe kwa kutowatendea haki raia wao.Heshima itoke wapi wakati raia wanapoteza maisha kwa makosa ya serikali(mfano vifo vya mabomu mbagala na g'mboto na vifo vya Arusha)
  • Hii ni nchi pekee ambapo haki haipatikani mahakamani,mwizi wa kuku anahukumiwa kifungo lakini anayeua na kuibia taifa anaachiwa huru
  • Wafanyakazi,waalimu,madaktari na wanafunzi hawapati haki yao ya msingi mfano mishahara mizuri na mikopo ya masomo kwa madai ya ukosefu wa fedha lakini fedha zinaweza kupatikana za kuwalipa matapeli wa nishati
  • Nchi ina kila aina ya raslimali lakini raia wake wengi ni maskini wa kutupwa,nchi inazidiwa kimaendeleo na nchi ambazo hazina raslimali na tumezikomboa kutokana na migogoro ya kivita,angalia majirani zetu wote wametuzidi kwa kila kitu
  • Nchi haina cha kujivunia zaidi ya woga wa amani,hamna shirika la ndege la kujivunia,hamna reli ya kujivunia,hamna bandari ya kujivunia hamna chochote cha kujivunia,hata mlima wetu wa kili ulishajulikana hauko kwetu,mbuga zetu nzuri zinawanufaisha wachache,hata madini yetu hatuyaoni(wameuziwa wageni)
  • Watanzania walio wengi hawajui kinachoendelea nchini mwao,angalau wa mijini wameanza kuamka
  • Nchi hii watu wake wamebaki kushabikia maendeleo ya wenzetu,utakuta watanzania wanashabikia mipira ya nje au vitu vizuri vya wenzetu maana sisi vya kwetu hatuna(hata vingozi wetu wako radhi waende kutibiwa au kutembea nje maana kwetu tuna nini?)
  • Nchi imejaa jamii inayoamini ushirikina kwenye ngazi zote kuanzia viongozi hadi jamii(angalia maalbino walivyo uawa,pia fika bagamoyo uambiwe ambavyo viongozi wetu wanahudhuria kwa waganga wa kienyeji
  • Siasa za nchi zimebaki kuwa za kishabiki zisizo na tija kwa mtanzania,hata akitokea kiongozi makini anaonekana adui au tishio kwa wenzake hata wakubwa zake
  • Mtanzania wa chini ameachwa kujijua mwenyewe na matokeo yake watu wamekuwa desperate kutatua matatizo yao kwa njia yoyote ndio maana hata akitokea mtu akasema anaweza kuwaondolea matatizo yao basi wanaamini,yawe matatizo ya kifedha au maradhi(mfano DECI ya matapeli au sasa babu wa loliondo na tiba yake),haya yote yanatokea wakati nchi ina uongozi uliochaguliwa na hawa hawa maskini(wameachwa wajitatulie matatizo yao)
  • Inapofika mbwa mwoga akafukuzwa sana ili auwawe mwishoni huwa anabadilika ghafla na kumshambulia anayemfukuza.Hili ni angalizo kwa watawala kwani jamii hii itakapochoka(na imeshachoka),itaigeukia mamlaka husika na kudai haki yake kwa nguvu zote
  • Maangalizo kama haya yamejaa kwenye vyombo vya habari makini lakini hayasikilizwi au kufanyiwa kazi,hata vyombo vya dini vimeongea sana
  • Ikumbukwe kuwa maskini akinyanyasika sana mwishoni huwa anamwachia mungu amtatulie matatizo yake na hii ndipo ilipofikia nchi hii(tukumbuke mungu huwa anamjibu mja wake kwa njia za ajabu na za ukweli hivyo iko siku)
   
 2. Wed

  Wed JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Mkuu nakuunga mkono. Umaskini, Ujinga, Magonjwa, Kukosa elimu, na serikali kushindwa kutatua matatizo yao, yote haya yanachangia watu kujikita kwenye kutafuta majibu rahisi kwa matatizo mazito.

  Wananchi wamekata tamaa. Yote haya yanatonana na Mdudu CCM kupekecha akili zao !! Tunachopaswa kufanya ni kutoa elimu kwa mtu mmoja baada ya mwingine ili tuninasue kwenye haya makucha ya CCM ! Mimi hii kazi naifanya kila siku. Naamini nawe unauwezo wa kuifanya pale ulipo.
   
 3. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mbona umesahau haya:
  Ni nchi ya 1 afrika ambayo ndege ya raisi wake inauwezo wa kuruka non-stop mpaka USA, tehe tehe usiniulize kama USA nayo ni sehemu ya Tz nami nisije uliza kama hiyo ndege inamsaidiaje mkulima wa Gambushi ambaye hana barabara ya kupitishia pamba yake,
  Ni nchi ya 1 afrika kuwa na mjengo wa waheshimiwa wa gharama kubwa na kifahari kuliko yote, tehe tehe, wah wanauchapa usingizi ipasavyo wakimulikwa na vyombo vya habari wanasema walikuwa wanasali au sijui kutafakari, ili hali vitu vingi vikiwa wazi. Tafadahli usiniulize zile sheria kandamizi zinashughulikiwaje na hilo jengo, rejea ripoti ya Nyalali,
  Ni nchi pekee duniani yenye Tanzanite, lakini nenda makao makuu ya Wilaya ambako tanzanite inachimbwa -Olkursmet/Simanjiro kama utakuta bomba la maji safi na salama au basi hata hospitali ya hadhi ya Wilaya
  Ni nchi yenye mlima mrefu afrika ambao unanufainshi nchi nyingine ktk mapato ya utalii;
  Ni nchi ya 1 afrika ambayo rasilimali zake za madini zina mchango wa chini kabisa kiuchumi.

  Nilikuwa napita tu, waweza ongezea unayoyafahamu kwani orodha ni ndefu.
   
 4. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Maneno yako yamenichoma najisikia kama kulipua mabarauti magogoni :crying:
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nchi ya ajabu sana!
   
 6. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,053
  Likes Received: 293
  Trophy Points: 180
  Mnazidi kunitia hasira na kapu langu la Dagaamchele wamenidodea na umeme hapa kwa Mpemba hakuna. Nitaweka wapi hili kapu walau wasioze ili kesho niuze tena. Na hii simu ninayotumia kutuma ujumbe huu inaniashiria kuisha chaji ya betri..oops Imezima!!..
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  UVCCM wakikusikia nadhani watayatafakari.
   
 8. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  This is a Kingdom of blinds whereby one eyed man is a king
   
 9. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  Kinachosikitisha sana ni pale ambapo mambo yanafanyika hovyo hovyo tu na watawala wanakaa kimya kama vile wanawaongoza vipofu au viziwi.Hata wanapotokea watu wakasema au kulalamika basi wao huchukuliwa kama maadui wa dola au amani ya nchi.Hivi kweli nchi hii itaendelea kwa mtindo huu??mbona hawa viongozi hawaoni hata angalau uchungu kwa hawa maskini ambao wanawapa kura kila wakati?hivi kweli we kiongozi unajisikiaje unapokuwa unaishi kwenye nyumba nzuri Dar es salaam wakati kule wilayani ulikotoka watu wako wanakula majani alafu we unaenda kuwaomba kura na kuwasahau?zile barabara za kuingilia kijijini kwako hazipitiki na wala umeme na maji hamna,we waona sawa kula raha dar es salaam kweli?ifike mahali watu wamwogope mungu jamani!!!hivi anapotokea mtu akayazungumzia haya matatizo ya jamii hadharani(hata kama wa chama pinzani)hivi huyu anawezaje kuwa adui wa amani au maendeleo?
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nchi ya Mazuzu wasioweza kusimamisha ujambazi wa uporaji wa rasilimari za nchi
   
 11. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Nderingosha you have said. All are facts!

  Hili ni rinchi lililo laaniwa kwa kila kitu. Hakuna kitu cha kujivunia hata kimoja. Napenda kuchangia japo kidogo kwenye baadhi ya maeneo k.m:
  1. UMEME: Kwanini kila mwaka umeme wetu ni wa dharura? Mbona wenzetu kama Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi n.k. hatusikii wananunua umeme wa DOWANS,IPTL,RICHMOND,SONGAS na upuuzi mwingine kama huo? Je,ina maana kwao hakuna ukame? Majibu ya maswali haya ni kuwa NCHI HII IMEJAA INATAWALIWA NA MAFISADI.
  2. NDEGE: Kwa nchi zote za EA zikiwemo nchi ndogo kama Rwanda na Burundi zina MASHIRIKA YA NDEGE. Kenya Airways,Uganda Airways,Rwanda Airways,Burundi Airways ni mashirika ya ndege ya nchi husika na hatujasikia yanatetereka wala KUBINAFSIHWA kama AIR TANZANIA! Je,wenzetu wanatumiia uchawi gani kuendesha Mashirika yao ya Ndege?
  3. RELI: Tumebinafsisha RELI YETU(TRC) kwa Wahindi wa na kuunda TRL ambayo tayari imeshafilisiwa na huyu mwekezaji uchwara wa Kihindi anayejiita RITES. Hakika hawa wahindi wamethibitisha kuwa ni MATAPELI wa kutupwa na si wawekezaji. Think about RELI iliyojengwa na mkoloni wa Kijerumani kwa gharama kubwa kama kichocheo cha maendeleo kwa kurahisisha usafiri wa raia na bidhaa za Biashara na Chakula leo hii imetelekezwa, haina mwenyewe.
  4. MADINI: Nianze na Tanzanite, madini pekee DUNIANI yanayopatikana Tanzania. Lakini ajabu ni kwamba kumbukumbu(records) zinaonyesha kuwa TANZANITE inauzwa/kusafirishwa nje kwa mauzo na nchi za KENYA,SOUTH AFRIKA na INDIA!! Sijui serikali ya CCM inafanya kazi gani. Yaani kuachia wageni waje wavune madini,wayapeleke kwao,waya process na wayasafirishe nje ya nchi zao kana kwamba yametoka kwao. Huu hakika ni UJUHA WA KUTUPWA. Hii haliko kwenye madini ya Tanzanite peke yake,nenda kwenye DHAHABU,ALMASI,KITO n.k. mwendo ni uleule. TUNAJUA KUNA NDEGE ZA WAWEKEZAJI KWENYE MIGODI YA KAHAMA,GEITA,RESOLUTE HUWA ZINARUKA KILA SIKU NA MADINI YA MABILIONI YA PESA KWENDA MAKWAO NA BAADAYE KUYAUZA KAMA YAMETOKA KWENYE NCHI ZAO ILHALI YAMETOKA TZ!!!Hakika haya mambo yanatia kichefuchefu.
  5. UTALII: Nianze na Mlima mrefu kuliko yote Afrika,The Kilimanjaro;inaaminika ukienda ulaya baadahi ya nchi wanajua kuwa MLIMA KILIMANJARO UPO Kenya!!!Watalii wanachulkuliwa na KENYA AIRWAYS moja kwa moja mpaka Nairobi baadaye wanachukuliwa na magari ya kitalii ya Wakenya wanaletwa mpakani mwa Kenya na Tanzo,wanatembezwa na kuonyeshwa mlima Kilimanjaro ukiwa Tanzania lakini wakidanganywa kuwa upo Kenya. Kweli hii ni nchi ya MAJUHA WA CCM!
  6. BANDARI : Ukifika kwenye Bandari zetu kuu kuanzia Dar,Tanga, Mtwara hakuna kinachofanyika cha kimaendeleo. DAR imekodishwa kwa kina TICTS ambao ndiyo wana-control kila kitu kwenye Bandari hii- WIZI MTUPU. Inaaminika wao wanapata fedha nyingi kuliko wanayopata Serikali! Wameweka TARRIFS kubwa kubwa ili wapate faida haraka na kwa misingi hiyo Wafanyabiashara wengi wanakwepa kupitishia mizigo yao kwenye Bandari zetu na wanakimbilia Bandari kama za Mombasa-Kenya na SA.
  7. MBUGA ZA WANYAMA: Tanzania tuna Mbuga za wanyama nyingi sana na tuna wanyama ambao ni rare species(wanapatikana TZ tu). Lakini ajau ni kuwa Mbuga na Wanyama hawa hazitusaidii Watanzania, badala yake zinawanufaisha WAGENI ambao baadhi wamenunua vitalu na kuvifanya mali yao. Hawa jamaa wame-camp huko mbugani kazi yao ni kuwinda hawa wanyama na kuwasafirisha kwa ndege kwenda makwao. Wamefanya Tanzania kuwa ni shamba la Bibi. We unaingia unavuna,unakula na unaondoka zako na hakuna mtu wa kukuuliza. Hizi ni SERA ZA CCM yaani CHAMA CHA MAJAMBAZI au CHUKUA CHAKO MAPEMA!
  Haya ni machache tu ya baadhi ya mambo yanayo udhi sana kwenye nchi hii kiasi cha kuifanya IONEKANA NI NCHI ISIYOKUWA NA WATAWALA MAKINI CHINI YA UONGOZI WA CHAMA TWAWALA-CCM.

  Bado hatujagusia udhaifu kwenye sekta nyeti kama za Elimu,Afya,Uchumi,Siasa safi na Uongozi bora.Mfamo mdogo tu; fikiria juu ya BABU WA LOLIONDO. Kwamba viongozi na serikali yote wamemwona BABU kama vile ni MKOMBOZI NA SULUHU YA MAMBO YOTE KUANZIA MAGONJWA MPAKA UCHUMI. Hakika hii ni aibu kwa nchi hii!

  Ndiyo maana tunasema TANZANIA YA SASA INAHITAJI MABADILIKO YA PEOPLES POWER ili tuweze kubadilisha kabisa MFUMO WA UTAWALA kutoka CHAMA CHA MAFISADI(CCM) kwenda UTAWALA MPYA WA CDM(CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO) na ndipo Watanzania watakapoanza kuona FAIDA NA MAANA YA KUWA NA RASLIMALI HIZI KUBWA KUBWA K.M. MADINI,WANYAMA,MILIMA,n.k. TULIZOJALIWA NA MWENYE ENZI MUNGU.

  Wasalaam.
   
 12. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,751
  Likes Received: 6,022
  Trophy Points: 280
  Naunga mkona hoja. Kwenye list ya ongeza na haya ambayo ni ya kipekee duniani/Afrika na yanapatikana Tanzania:

  9. MIFUGO: Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo. Hii ilitegemewa Tanzania iwe miongoni mwa mataifa yanayozalisha bidhaa bora kabisa (original) za ngozi duniani. Ingeongeza ajira, pato la taifa, kufahamika kimataifa, n.k. Lakini wapi! TUMELAANIWA?

  10. MAZIWA VICTORIA NA TANGANYIKA: Ziwa Victoria ni la pili kwa ukubwa duniani na 51% iko Tanzania (43% - Uganda, 6% - Kenya) na ni chanzo kikuu cha Mto Nile - mto ambao ni wa kinabii. Ziwa Tanganyika; kwanza limechukua jina la nchi yetu halafu ni la pili kwa kina kirefu duniani na likiwa refu zaidi (kwa marefu). Lakini wapi! TUMELAANIWA?

  11. MLIMA KILIMANJARO: Ni mrefu zaidi Afrika na pekee uliofunikwa kwa theluji ukiwa kwenye tropics; jirani kabisa na Ikweta. Lakini wapi! TUMELAANIWA?

  12. MIPAKA NA NCHI NYINGINE: Tanzania ni kati ya nchi zilizo na majirni wengi zaidi duniani - fursa za kiuchumi hizo! Tumepakana na nchi nane: Msumbiji, Malawi, Zambia, DRC, Burundi, Rwanda, Uganda, na Kenya. Mashariki kuna bahari. Lakini wapi! TUMELAANIWA?

  13. MADINI YA VITO: Tanzania ni kati ya nchi zenye utajiri ulipindukia wa madini ya vito na metali nzito - Almasi, dhahabu, Tanzanite, ruby, chuma, uranium, n.k. Lakini wapi! TUMELAANIWA?

  14: KILIMO:
  Tanzania ni nchi ambayo kila zao linalolimwa duniani linastawi pia Tanzania. Kuna kipindi tuliwa kuongoza kwa katani na karafuu. Tanzania inongoza kwa korosho na pia iko juu sana hata kwa ndizi (nadhani tupo kumi bora) bila kutaja kahawa, pamba, chai, n.k. Lakini wapi! TUMELAANIWA?

  ... n.k. n.k. listi inaweza kuwa ndefu upendavyo ... ukiongeza na AMANI NA UTULIVU.


   
Loading...