Tanzania Nchi Yangu Nakupenda kwa Moyo Wote


MIXOLOGIST

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Messages
3,403
Likes
7,278
Points
280
MIXOLOGIST

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2016
3,403 7,278 280
Habari zenu wana jamii,

Wakati tunaingia kwenye msimu wa sikuu nimekaa nikatafakari maagizo ya mkuu wa nchi kuhusu kuzuia unanyasaji na udhalilishaji wa wamachinga na wachimbaji wadogo wadogo.

Baada ya kutafakari, kwanza nikajiuliza maswali yafuatayo:

1. Je wamachinga wanafikaje kwenye meneo ambalo siyo rasmi?
2. Je kwanini wanaachwa kuzagaa kwenye maeneo waliyovamia kwa muda mrefu?
3. Je ni jukumu la nani kuwazuia wasivamie na kufanya mazoea kwenye maeoneo yasiyo rasmi?
4. je kuvamia eneo lisilo rasmi na kufanya shughuli zako kwa muda mrefu bila ya kubugudhiwa kunaweza kuhalalisha uvamizi wako?
5. Je sheria ndogo ndogo za majiji na miji zinazo ratibu biashara ndogo ndogo zinasemaje kuhusu biashara za wamachinga?
6. Je katazo la Mh. Raisi lina uhalali wowote kisheria? (Legality of the orders of the President) , na
7. Je wahanga wa maamuzi ya Mh. Raisi wana fursa gani kisheria kupinga au kuzuia utekelezaji wa amri hiyo?

Pili, baada ya kuyawaza maswali hayo juu, nilitafakari haki na wajibu wa pande zote zinazo husika na tatizo hili nakujikuta najiuliza maswali mengine kama ifuatavyo:

1. Je haki ya wamachinga ni ipi?
2. Je wajibu wao kama raia ni upi?
3. Je haki za watendaji ni zipi?
4. je wajibu wa watendaji ni upi?
5. Je mgogoro kati ya watendaji na wamachinga ni wa kitaifa? na
6 Je kuna haja ya Mh Raisi kuingilia migogoro isiyo yakitaifa?

Mwisho kabisa nikatafakari haki na wajibu wa wizara ya nishati na madini na haki za wachimbaji wadogo na zile za wawekezaji wakubwa nako pia nikajiuliza maswali yafuatayo?
1. Je shughuli za kuchimba madini haziratibiwi na sheria?
2. Je ni nani mchimbaji mdogo?
3. Je ni kwa namna gani mchimbaji mdogo halali anaweza kutofautishwa na mchimbaji mdogo mvamizi?
4. Je mchimbaji mdogo haguswi na matakwa ya sheria za madini?
5. Ni zipi haki za mchimbaji mdogo?
6. Ni upi wajibu wa mchimbaji mdogo?
7. Ni zipi haki za muwekezaji mkubwa?
8. Ni upi wajibu wa muwekezaji mkubwa?
9. Je ni sahii kufuta leseni wa muwekezaji mkubwa bila ya kufanya uchunguzi wa kujua uhalali wake?
10. Je hakuna namna ya kuchochea uwekezaji wa pamoja kati ya wachimbaji wadogo na wawekezaji wakubwa?

Basi baada ya kukosa majibu ya maswahi hayo hapo juu nikaukumbuka mwimbo wangu pendwa

"Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote, nchi yangu Tanzania nakupenda kwa moyo wote"
 

Forum statistics

Threads 1,275,228
Members 490,947
Posts 30,536,206