Tanzania nchi yangu inavyokwenda kufiliska mchana kweupe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania nchi yangu inavyokwenda kufiliska mchana kweupe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vijijini Lawama, Apr 19, 2012.

 1. Vijijini Lawama

  Vijijini Lawama JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndg zangu, naskitika ninavyoona nchi yangu niloipenda inaenda kufilisika mchana kweupe chini ya kiongozi shupavu wa safari Ndg Kikwete. Tanzania hii hii leo nasikia imekpoa kila pahali kwenye mabenki na hata kwenye mifuko ya hifadhi za jamii ili angalau tu kulipa mishahara ya watumishi wake. Tanzania hii hii imekuwa kwa wakati sasa kuanzia robo ya pili ya mwaka wa fedha 2010/2011 ikilipa deni la taifa ambalo wachumi wa hazina walisema lilikuwa limeiva, leo hii tunaambiwa katika ripoti ya CAG deni la Tanzania limefikia Trilioni 14.4, je hili deni litaisha kulipwa lini? na hizi pesa zimeifanyia nini jamii ya kitanzania? Hapa panahitaji tafakuli ya hali ya juu. Je kwa miaka mitatu iliyobaki kwa huyu bwana Kikwete kumaliza muda wake tutakuwa mahali salama kwa huduma za jamii, Lecturer wangu mmoja alisafiri toka Uk kupitia Kenya kwenda Tanzania na kushangaa tofauti ya matumizi ya pesa kati ya Tanzania na Kenya ilivokuwa kubwa (kwa maana ya mfumko wa bei). Namnukuu '' YOU NEED TO BE RICH TO LIVE IN TANZANIA'' nami nikajiuliza inamaana watanzania sisi ni matajiri sana? swali jingine kama matajiri hilo deni tunalodaiwa na ambalo sasa linalipwa na Tanzania limetoka wapi?
   
Loading...