Tanzania, nchi ya vijipesa, vijisenti, na ubunge unaoleta umaskini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania, nchi ya vijipesa, vijisenti, na ubunge unaoleta umaskini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiwi, Mar 9, 2012.

 1. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Wanajamvi,

  Baada ya kumsikiliza Adam Kighoma Malima jioni hii, na kusikia akisema ana haki ya kutembea na vijipesa vyake takriban dola elfu nne na shilingi zaidi ya milioni moja taslimu, nikakumbuka usemi wa mzee wa vijisenti, pamoja na kauli ya Spika kuwa Ubunge ni kazi ya kifukara sana. Hivi kusema kweli ni watanzania wangapi wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku? Watanzania wangapi leo hii wanalala na njaa, na wale waliokula hawajui kama kesho watapata chakula? Ni watanzania wangapi hawamudu kupeleka watoto shuleni? Ni watanzania wangapi hawajui hata maji ya kunywa watayapata wapi? Kweli hawa ndio tunategemea watatufikiria sisi kama watanzania na kujali maslahi yetu? Ambao bado wamelala usingizini amkeni!!!

  Mungu Ibariki Tanzania!!!
   
 2. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Na leo ametuhakikishia mbele ya kadamnasi kuwa ana bunduki mbili, bastola na bunduki kubwa. What arrogance Honourable Mr. Deputy Minister!!! Huna haja ya kujikweza, kumbuka watanzania ndio waliokupa dhamana ya kufika hapo ulipo!

  Watanzania wenzangu huu uongozi wa awamu hii ni bomu, wameoza wote. Hakuna jinsi ya kuwasafisha. Ondoeni huu uozo, tunaangamia!!!
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  .
  Hawataki kujionyesha kwamba hawanazo. Lakini utawahurumia kwa jinsi wanavyokuwa wadogo kama piritoni wakiwa mbele ya nchi wafadhali wakiomba misaada. Wakiisha zipata ndio wanazitumbukiza kwenye mifuko yao tena bado zikiwa dollar hivyo hivyo na kuziita vijicent/vipesa kwenye uwanja wa kinamamapoa wa kibongo. Eti wawaone babkubwa. Mbongo noma kweli.
  .
   
 4. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  ....utajipa pressure bure!
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwani Watanzania hawajapata pressure bado? Hebu angalia nchi inavyoendeshwa na hao wenye vijipesa. Tatizo ni kuwa wengi tu hawajui kama wana pressure na wanaona hali ni kawaida tu...mpaka siku mtu anapodondoka.
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu anayeitwa mheshimiwa alikuwa na haja gani ya kutaja kwamba ana bunduki mbili? Je katika tukio hili la kuibiwa hizo bunduki zimemsaidia nini?

  Tiba
   
 7. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Kwake dola elfu 4 ni vijipesa. Ndo bongo hii.
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Yeah. Only in Tanzania ndio mahali mtu anaita kiasi hicho 'vijipesa'. Katika nchi zingine watu hawatembei na pesa nyingi kama hivyo, akitembea nazo kiasi hicho basi hushukiwa kuwa ni muuzaji unga au anafanya biashara haramu.
   
 9. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nimekaona hako kajamaa....
  Ulimbukeni ni tatizo la msingi kwa "viongozi" wetu.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Silaha zote hizo za nini? Yuko vitani?
   
 11. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama mtu anatembea na zaidi ya cash money 20Ml anasema ni vijipesa (pocket money), kumbe NI HALALI MADAKTARI WAGOME!
   
 12. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TANZANIA HAKUNA AMANI ni kutembea na masilaha lukuki kama wasomali!
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Anasema anaweza akapigiwa simu aende kwenye kikao cha gafla iraq au somalia so ni muhimu kutembea na passport pamoja na vijihela,kuhusu ak47 na 9mm amesema kwamba hua wanasafiri usiku maporini so ni muhimu kua na mavitu kama hayo,huyo dada aliyemlamba nampa big up!!
   
 14. d

  dmatemu JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 591
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  mkuu ndo hivyo bwana Bong inaliwa na wachache. Kwanza mi nawapongeza sana hao waliomliza Maliam yaani kama ningewafahamu, ningewapa hata bia moja moja kwa kuwapongeza. Maisha ya sasa magumu halafu we unatembea na US $4000 ndani ya nchi hii jamani ni haki? Hata kama ningekuwa mm ningekwiba tu hela hiyo maana najua ni mtaji tosha wa kuanzisha biashara na kuachana na umaskini. Hongereni wadada bado mkuu wa kaya tu
   
Loading...