Tanzania nchi ya maajabu, 70% na zaidi inategemea kilimo na haina kiwanda cha mbolea,mbegu wala kutengeneza trekta

Eeeh ndiyo nawafahamu wanaitwa Pop Vriend wana bonge la kiwanda. Pia wapo wanaitwa Africasia wako Unga Limited eneo la viwanda, kuna pia wanaitwa Suba. Bado hatujataja Meru company ambao wana mashamba ya mbegu mpaka huko Kigoma! Huyu mleta mada amekurupuka!
Inawezekana anaishi nje ya nchi miaka mingi..
 
Kwani sekta binafsi imezuiwa kuyafanya haya unayoyaema na kuziba haya mapungufu? kwn hayo makampuni mnayoyasifia ni ya serikali za huko kwa mabeberu au ni ya watu binafsi? Wadanganyika nimewavulia kofia kwa kupenda kulalama!
 
Minjingu ni cha wachina? SEED co zinatoka Zambia?
Kuliko kutumia mbegu za Seed Co ya Tz, bora upande mahindi ya kienyeji. Hiyo mbolea ya Minjingu itakuwa inafanya vizuri huko kijijini kwako.
Nimeandika kwa kifupi sana, wakulima hasa wa ukanda wa kusini wataongezea zaidi.
 
Kuliko kutumia mbegu za Seed Co ya Tz, bora upande mahindi ya kienyeji. Hiyo mbolea ya Minjingu itakuwa inafanya vizuri huko kijijini kwako.
Nimeandika kwa kifupi sana, wakulima hasa wa ukanda wa kusini wataongezea zaidi.
Sisi wakulima Lindi imetuulia korosho zetu
 
Dj Shibobo toka umekuwa mkulima akili imekaa sawa, enzi za UDj Pamodzi ulikuwa chawa wa CCM kindakindaki.
 
Mama D, kiwanda hiki kilimapata kasheshe kubwa mara tu JPM alipoingia madarakani awamu ya 5. Mifuko tu ya ku-pack hiyo mbolea ilikuwa ilichapishwa nchi jirani!! Kwa taarifa, kiwanda hiki kinafanya repackaging! Hakizalishi mbolea!!
Acha basi upotoshaji? Minjingu wanazalisha mbolea asilia yenye virutubisho vya phosphorus, ni mbole ya kupanda kama ilivyo TSP na DAP. Karasinga alikuwa anachakachua kwa kuweka hiyo mbolea kwenye mifuko ya Kenya ili ionekane imetoka Kenya na siyo kwamba alikuwa ana repackage! Hii ilikuwa hujuma kwa nchi!
 
Ona sasa mmemfanya mtoa kakimbia
Sasa yeye anakuja bila data sisi tumfanyeje sasa? Hawa ndio wanatufanya wapinzani waonekane mazwazwa kumbe wana akili timamu kabisa!! Kila kitu majitu yamezoea kubeza tu bila kufanya utafiti wa kutosha! Na kweli amelikimbia bandiko lake!!
 
mkuu tafadhali iondoe bangi hapo ...psychedelic drug ...Dawa yenye tiba nyingi Sana kiafya mkuu..
Huyo ana sonona...ana stress za maisha na kupandishiwa vifurushi ...dawa Ni kumpuuza ..
Response ya mama d nimeipenda.

Ni vyema Sana post zinapoaandaliwa humu ziwe zinafanyiwa uchunguzi wa kina na wahusika..
Mbegu na mbolea Tz zipo zinazalishwa Ila Tatizo Ni Bei....
Unakuta huyo mfokaji na Mtoa mada hata propagation and spacing ya mahindi hajui ..
Tumpuuze tuu.
nimekuelewa naona ana sonona
lkn hakuna kitu kinaniuma mtu kuja utokako na kuanza kutukana Mama zetu ili hali yeye kazaliwa na mwanamke, ule ugomvi niliununua nilitaka auhamishie kwangu.
Mambo ya mbegu wala maduka yanayouza mchicha hayafahamuu anasema unatoka nje. Basi yameisha
 
Sasa yeye anakuja bila data sisi tumfanyeje sasa? Hawa ndio wanatufanya wapinzani waonekane mazwazwa kumbe wana akili timamu kabisa!! Kila kitu majitu yamezoea kubeza tu bila kufanya utafiti wa kutosha! Na kweli amelikimbia bandiko lake!!
Nimecheka aisee
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom