Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
NCHI YA KWANZA DUNIANI KUHITAJI KUWA NA WANAHABARI WENYE LEVEL YA DIGRII NI Tanzania.
Katika hali kama maluweluwe ya sinto fahamika. Duniani kote tumekuwa tukipiga kelele kuwa Vyombo vya habari na habari iwe mhimili unaojitegemea ndani ya dola kama ilivyo bunge, mahakama na Executive, tumekuwa tukilalama kama waropokaji kwa kuwa majukumu yake ni mengi na mengine ni risk, huku tukitambua pia tunavuka nje ya mipaka kulingana na uzito wa habari.
Taaluma hii huwezi kulinganisha na taaluma kama ya madaktari au walimu, muda mwingi taaluma hii ni zaidi ya kujitolea. Unafanya kazi kubwa kuliko hata mshahara wako. Na ndio maana wale wanaokuwa na Digrii hutafta kazi zingine ili kuepuka suluba za kashikashi za hapa na kule.
Wanahabari wanapotengeneza habari mpaka kuja kukamilika, habari husika inapitia mikononi mwa wanahabari wasio punguwa 6, anaanza anayetafta habari, anawasilisha ofisini, anayeipokea anaipitia kwanza kama imekaa sawa na kufanya marekebisho ikiwemo lugha, naye anaikabidhi kwa mwingine ambaye anaanza kuihariri ama kwa kuirefusha au kuipunguza kulingana na uzito wake, naye anakabidhi kwa yule atakaye sanifu picha itakayotumika kama kuna uhitaji, naye anaikabidhi kwa atakaye hariri kwa Mara ya mwisho na kuhitimishwa kwa yule atakaye uunda kichwa cha habari na hapo hufanyiwa pageloyout(kupangwa) na habari zote zikikamilika ndipo kiwandani huanza kuprinti. Huu ni mfano tu, japo majukumu ni mengi sana.
Na ndio maana jiulize vijana wengi wanapenda kuwa watangaziji tu ila hawapendi kuingia mtaani kutafta habari maana wanajua ni shughuli pevu. Hapo ndipo ujiulize huyo mwenye digrii ataingia kweli mtaani?
Ndio maana tuna Astashahada wanaotusaidia kutafta habari, ndio maana tuna Stashahada wanaotuboreshea habari na wakati mwingine nao kutafta habari, ndio maana tuna Shahada wanaotutaftia habari pia na kuhariri.
Kuna Waandishi Wazoefu wa siku nyingi ambao mwanahabari wa Leo mwenye Shahada bado anahitaji ujuzi wao. Taaluma ya habari ni kipaji nasio elimu ya darasani na ndio maana wenye Shahada wengi hukimbiaga kazi ya habari.
Kuna mambo ndani ya habari hayahitaji Digrii uliyosoma Bali uzoefu na maarifa. Na ndio wapo Waandishi hawana vyeti vya taaluma hiyo lakini wamejifunza ndani ya uandishi na kuwa na uzoefu mkubwa, kitu ambacho wizara husika ilipashwa kuwatunuku vyeti kupitia VETA ili wakidhi kigezo cha kuwa na cheti.
Unaposema lazima wanahabari wawe na Digrii inamaana unataka kupunguza watu WA kutafuta habari. Digrii sio sifa ya kuwa Mwanahabari. Bali Digrii ni sifa ya kuwa umesoma maswala ya habari lakini siokuyafanyia kazi.
Nashauri Mswada WA habari urekebishwe na kuundwa kanuni zitakazo wafanya hata wenye Cheti na Stashahada kuendelea na majukumu yao kama kawaida.
Deogratius Nalimi Kisandu
19 Jan 2017