Je, Tanzania bado ni nchi ya Amani?

Pole Asha,
Nakuona kama mgeni japo hujabisha hodi, ila nikutie moyo kuwa mada yako ni nzuri sana.
Mimi sina jibu kwa sasa ila nikuhakikishie kwamba hapa JF (jamii forum) utapata majibu.Mimi mwenyewe nimesaidiwa sana hapa.Changia hoja za watu pia.
Kaa mkao wa kula Asha.

Asante exaud kwa ushauri japo mimi si mgeni sana.Nilijiunga hapa mwanzoni mwa mwaka huu lakini nikajikuta nabanwa sana na masomo mahali fulani.nikashindwa kuendelea hapa.Pia nikapoteza password mara kwa mara.
Sasa Mungu amenisaidia nimeshavaa JOHO la taaluma, kwa hiyo nitakuwa hapa jamii mara kwa mara.
Asante kwa kunitia moyo.
 
wapenzi wana jamii,
mimi binafsi sielewi kabisa dhana hii ya amani.
Watu huzungumzia amani lakini sijui uwepo wa amani unapimwaje.
Kwa mfano kisiasa mataifa mengi husema nchi ya tanzania ni nchi ya amani.
Hivi kipimo cha amani ni kipi?
Je amani sii kitu ambacho kiko ndani ya moyo wa mtu?amani huletwa na mungu au mazingira?
Mtu binafsi si ndo anapaswa kujua kama ana amani au la?
Au kipimo cha amani ni kipi?


tanzania hatuna amani ya kweli.
Kilichiopo ni ujinga, uwongo na uzandiki.
Hebu angalia maeneo ya north mara,
polisi na wananchi wanawindana ili wauane.. Je hiyo ni amani ya wapi?
Watu hawana tena imani na serikali yao, hawana pa kukimbilia na hawajui ni nani atakae wakomboa kutoka kwenye adha zao.
 
Hotuba ya waziri mkuu inasema Tanzania kua tuna amani mi nasema sisi hatuna amani sisi tuna utulivu unaoambatana na woga
 
Kwahiyo ikawa je baada ya amani. Yafaa mbele yake uandike TO BE CONTINURE Tungojee episod 2
 
Naomba wadau tujadili hili,Kama Tanzania tuna AMANI au ni WAOGA katika kudai haki zetu za msingi.
 
nchi ikipata uhuru ndio inaweza kudhaniwa ina amani. sisi hatujapata uhuru bado...
bali tumebadilisha wakoloni kutoka wazungu kuja weusi. tena hawa wamekuwa wabaya kuliko wazungu.
yaani hadharani na kweupe kabisaa wanadai wapewe posho 200000 + 50000 + 80000 = 330000 kwa siku nje ya mshahara.
wakati mtanzania anapewa mshahara 146000 kwa mwezi = 4867 kwa siku. je huo si unyonyaji? bila shaka ndiyo. sasa ndani ya
ukoloni amani itatoka wapi wakati kuna kunyonywa?
 
Kama alivyosema mdau hapo juu kwamba sisi hatuna amani kwa sababu bado tupo kwenye Ukoloni mweusi. Bahati mbaya wakoloni hawa ni ndugu na majirani zetu mitaani!
 
WanaJF,

Naomba kusahihishwa kama ntakuwa nimekosea, ninavyoamini mimi AMANI ndani ya Taifa letu imejengwa na Watawaliwa na si Watawala. Nasema hivyo kutokana na mambo mengi mabaya ikiwa ni pamoja na kukosekana umakini kwa watawala ambao wamewekwa madarakani lakini Watawaliwa (Watanzania ) tumekuwa wagumu wa kuhoji au kuandamana kudai haki kutendeka.

Mtakumbuka kejeli za viongozi wakuu mbalimbali ambazo zimewahi kutolewa na zingine zinaendelea kutolewa mfano: Kiongozi mmoja aliposhutumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia ndege ya serikali kwenda nayo jimboni kwake kwa shughuli binafsi akawajibu wananchi kwa kejeli sasa nyinyi mlitaka niende na uongo ? Mwingine aliwahi kusema Ndege ya Rais lazima inunuliwe hata kama Watanzania mtakula nyasi, kibaya zaidi ndege ilinunuliwa na ikawa tena ni mbovu; katika hilo hatukuweza kuhoji tena, Mwingine aliwambia Wananchi kama hawawezi kulipa hela ya kivuko shs. 200 basi wawe wanapiga mbizi, zipo kauli nyingi za maudhi kutoka kwa viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Amani ya nchi hii haijajengwa na watawala imejengwa na watawaliwa wenyewe kwa sababu ya uoga wa kuchukua maamuzi kwa watawaliwa

Uoga tulionao Watanzania tusipo badilika utatuletea hasara kubwa katika Taifa, hivi inakuwaje mambo makubwa yenye maslahi kwa Taifa kama vile mikataba tunayoingia na wawekezaji wa nje inakuwa siri ? Huduma muhimu za kibinadamu kama vile maji , afya , elimu zinakuwa ovyo lakini Watanzania hatuwezi kuhoji badala yake Wananchi wasiokuwa na uhakika hata wa kupata mlo kwa siku wanaombwa michango ya kuchangia elimu, afya nk. huku rasilimali za nchi yao zikiporwa kwa serikali kuingia mikataba yenye usiri ?

AMANI Iliyopo Tanzania haijawahi kujengwa na Watawala ila imejengwa na Watawaliwa wenyewe kwa sababu ya uoga wa kuhoji mambo dhidi ya watawala na kufanya maamuzi magumu kama vile kuandamana, kugomea baadhi ya mambo ili kuweza kusaidia kurekebisha mienendo ya watawala. Mawazo yangu naona pengine ni wakati muafaka wa kufikirisha akili zetu na tuanze kuwa na utamaduni wa kuhoji mambo na kulazimisha HAKI kutendeka, ikishindikana kuchukua hatua ya mabadiliko ya kiuongozi/Utawala
 
Sio amani bali ukondoo au unyumbu wa watz. Ulianza zamani sana. Wakati wa watemi na machifu, mtemi alikuwa anasafiri kwa kubebwa. Mtu alikuwa akijitoa kutoka km nyingi ili aje kumbeba chifu bila kuamrishwa. Au chifu kuonyesha mke walo ishara ya kumpenda na ww ukampeleka kwake ili amuoe. Wakoloni waliwapiga babu zetu viboko hawakulalamika na sana sana walikuwa wanasema aksante baada ya kupigwa viboko hamsa ishishirini. Wataliwa ndio wenye amani ktk miili yao.
 
Jana nilipata fursa ya kuongea na raia wa kigeni aliyepata fursa ya kuishi Tanzania kwa miaka miwili. Tuliongea mengi hasa mambo aliyoyaona na kuyapitia.

Baadae maongezi yetu yakaja kuhusu amani iliyopo Tanzania.

Jibu lake lilikuwa: 'Tanzania hakuna amani bali ni hofu waliyo nayo wananchi ndiyo inaonekana kama amani. Wananchi wanaogopa ghadhabu ya polisi, wakubwa na nguvu za dola ili wasidhurike zaidi.'
 
Mbona amani ipo vizuri tu.Na wanasiasa wako free sana. Miji yote mikubwa kwa midogo imetulia na wanafuraha tele. Tatizo ni ushabiki wa kisiasa ndio umetawala wakati huu wa kufukuzia uchaguzi wa 2015.
 
Kwa hiyo mliamuaje na huyo mamluki wako? Katuleteeni basi siraha za kupambana na hao mapolisi Kama mnavyodai kuwa ndio tunao waogopa!!!
 
Tangu aingie raisi wa sasa nchi haina amani yeye anaendesha umafia akiwa ikulu kwa kauli zake tu na matendo ya wanachama na viongozi wake wanayoyafanya na kasha yeye kuwapandisha vyeo inadhihirisha yeye ni mvuruga amani na ndio maana sasa kuna vita ya wazi kati ya wafudaji na wakulima huko tarime wana musoma wanaume wameamua kumaaliza wanawake ,wanawaua na hakuna anayekamatwa alibino wameisha, wanaoshabikia siasa za upinzani wanauawa utasema kuna amani amani gani serikali iko likizo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom